wankuru nyankuru
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 491
- 763
Mimi ni muumini wa hili kanisa usharika wa Mbezi Louis, tokea nianze kusali nikiwa sunday school pale ni mwaka wa 18 sasa, katika vitu nlivyogundua ni kwamba haya makanisa hasa Kkkt yanaendeshwa kupitia sadaka za waumini yaani waumini wakisema wasitoe sadaka ndani ya miezi 3 tu hali ya viongozi ipo taabani
Usiposhiriki misa au kutoa Sadaka unaonekana mkosaji, ibada nzima ni michango tu kikapu kuanzia mwanzo hadi mwisho watu wanakamuliwa ni pesa kwenda mbele ila sijui kama wanajua hizo pesa zinapotokea ni wapi
Linapokuja swala la uchumi tunatakiwa tuwe kitu kimoja, kesho kama taifa tukiingia mikataba mibovu alafu kesho tukaja kuivunja nchi ikiingia kwenye madeni mazito haumii mtu mwingine tunaumia wote ndio haya matozo na kodi kubwa walizoweka huu ni mwanzo tu picha linakuja Viongozi wetu wa KKKT ikifika mahali mkaambiwa kuwa hatuna pesa sababu uchumi umeharibika muwe wasikivu maana ibada zenu ni kuomba pesa mwanzo mwisho, hajawajenga wachungaji na wainjilisti kujitegemea kiuchumi mmewajenga kuwakamua waumini kwenye kapu la sadaka.
Askofu Shoo unasema unabariki uwekezaji ni uwekezaji gani huo wa kijinga namna hii, unampa mtu Bandari kwa mkataba wa kudumu huo ni uwekezaji au uuzaji wa Bandari? Kesho akiingia kiongozi type ya Magufuli akauvunja mwishowe DP world wataenda mahakamani halafu tukidaiwa mabilioni ya pesa wanatuwekea Tozo na kodi kubwa tulipe wananchi, wananchi tukishapigika tukija makanisani mikono mitupu muwe waelewa maana kodi kubwa ni chanzo cha kufanya watu wafilisike.
Niwapongeze Roman kwa kuwa wakweli maana mmeona mbali, waumini wenu mnajua kabisa uchumi wao ukiyumba utaleta shida hadi kwenu ila uchumi ukinyooka hata kwa kanisa ni faida kubwa.