Hali ilivyokuwa katika Jiji la Dar wakati vijana CHADEMA wakimchukulia fomu Mbowe

Hongera kwa nia zenu na mapenzi yenu.
Sasa nasi wana CCM tukitafuta watu million 2, waka sign , kuomba mheshimiwa Raisi abadilishe katiba na aendelee kugombania uraisi zaidi ya mihula miwili, jee mtatuona tunakosea.

Atabadili ya ccm
 
Kamanda Mbowe ni tosha hasa kipindi hiki cha dhoruba.
Songa mbele makamanda taifa linahitaji ukombozi kwenye makucha ya mabeberu weusi CCM!!
 
Zumbukuku hili Sasa hapo wamechanga ili wabadili katiba?
Hongera kwa nia zenu na mapenzi yenu.
Sasa nasi wana CCM tukitafuta watu million 2, waka sign , kuomba mheshimiwa Raisi abadilishe katiba na aendelee kugombania uraisi zaidi ya mihula miwili, jee mtatuona tunakosea.
 
si muumini wa vyama..ila nadhan kuzidi mshikilia mbowe kama mwenyekiti ni kupoteza karata ya kulaumu Magufuri kuibaka demokrasia..najaribu fikiri tu nje ya box
Lakini pia watapoteza karata ya iwapo chama cha mapinduzi 2025 kitaporidhia mh.rais kuendelea kwa kipindi kingine cha miaka kumi hadi 2035 kwa kuungwa mkono na wananchi kupitia kura ya maoni 2024.
 
Tuna Imani kamanda hatawaangusha Watanzania
...mbowe kuendelea kutengeneza maigizo ya kupendwa ili awanie tena uongozi sio demokrasia ndani ya chama baada ya uchaguzi ndani ya chama atatengeneza ufa mkubwa sana matokeo yake chama kitakua kimenunua ajenda ya ulafi wa madaraka kama kilivyonunua ajenda ya ufisadi baada ya ujio wa lowasa....mbowe kafanya mambo mengi sana ya kukumbukwa kama mwanasiasa aliekivusha chama katika vipindi vigumu ilitosha kuilinda history yake nzuri awaachie wengine wakiongoze kifikie hatua yakuongoza nchi...wapo vijana wengi kama mh. Heche lisu lema mnyika wenje nk wenye uwezo wa kuongoza katika nafasi ya mwenyekiti lakini kwanini kila mda tuamonishwe hakuna kiongozi kama mbowe kwaiyo chama kinategemea akili ya mtu mmoja? Kama tunashindwa kuwaandaa vijana kuongoza chama tukipewa nchi tutaweza kuwa na mawaziri kweli? Kama kwenye kuongoza chama mnasema hawawezi je huo ubunge wao wanaumudu vipi?....kwa upuuzi huu tz hakuna upinzani wa kweli wote ni wajasiliama wamejivika mwamvuli wa siasa..kwenye madaraka ndo utajua hakuna cha ccm wala chadema wote ni kapu moja wanawaza matumbo yao
 
Vijana wa Chadema wamemchangia Mwenyekiti wa chama chao mh Mbowe kiasi cha sh 5,600,000 ili zimsaidie kuchukua fomu na kufanya kampeni kwa ajili ya kutetea nafasi yake.

Vijana hao waliokusanyika mtaa wa Ufipa yalipo makao makuu ya Chadema wakiwa wamevalia sare za chama chao wamesema kwa sasa hakuna mtu yoyote aliyejitolea kwa hali na mali kuitumikia Chadema zaidi ya Mbowe.

Wamesema Mbowe ni mwamba anayeweza kuwavusha katika safari yao ya kuelekea Ikulu mwakani yaani 2020

Source TBC habari!
 
Back
Top Bottom