Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Vijana wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam wameanzisha kampeni kubwa ya kutaka Freeman Mbowe achukue fomu kwa mara nyingine ya kugombea Uenyekiti CHADEMA.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu #MwambaTuvushe imeungwa mkono na maelfu ya watu ambao wanachanga pesa zao kwa kiwango cha kuanzia mia tano ili kutimiza shilingi milioni 1 ya kuchukulia fomu ya uenyekiti.

Vijana hao wa CHADEMA wameapa kumchukulia fomu na kuzijaza kisha kwenda kumlazimisha kiongozi huyo kuzitia sahihi na baada ya hapo wazirejeshe.

Vijana hao wameamua kuanza kampeni hiyo kabambe baada ya Tetesi kuvuma kwamba Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ameamua kutogombea tena nafasi hiyo.

Wafuasi hao wa CHADEMA wametishia kukesha nyumbani kwa Mwenyekiti huyo na kumzuia kwenda popote mpaka atakapokubali kusaini fomu hizo za kugombea Uenyekiti.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vincent Mashinji alipuliza rasmi kipenga cha uchaguzi mkuu juzi na kutangaza uchaguzi mkuu wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho utakuwa December 18.

=====
Michango ya wadau

Mbowe, mmoja kati ya 'principled leaders' tulionao sasa hivi Tanzania, lakini kaumizwa sana yeye kama kiongozi wa upinzani. Laiti hawa vijana wanaochangishana wangeonyesha moyo huo huo wa kuwa karibu na kiongozi wao wakati alipokuwa akiumizwa, pengine majaribu anayopitia sasa hivi yasingekuwa yanamkabili.

Ameharibiwa biashara, maksudi kabisa, mashamba na kubambikiwa kesi mbaya. Kawekwa ndani miezi kadhaa..., na kujionea uhalisia wa upweke unaoweza kumpata kiongozi. Katambua kwamba kuwa kiongozi unachukua dhamana ya watu unaowaongoza; lakini bila shaka hakujua kwamba watu hao hao wanaoonyesha mapenzi kwa kiongozi wao wakati wa raha, wanaweza kugeuka na kusahau kabisa kiongozi huyo anapopatwa na masaibu kutokana na juhudi za uongozi wake. Kiongozi anasahaulika na kutelekezwa. Bila shaka hili linamuuma sana hata kama hasemi.

Sasa anakabiliwa na kesi ya kupikwa, na pengine yeye kama kiongozi makini wa chama amekwishajua mitego iliyotegwa ili kukimaliza chama moja kwa moja.

Je, itasaidia kitu gani yeye kuchaguliwa kuendelea kuwa kiongozi wa chama kama amekwishaandaliwa kutokuwepo kwenye uwanja wa siasa? Huu ni udadisi, lakini hatuwezi kutotambua uwezekano wake.

Hao vijana wanaochangishana, wanaweza wakasema potelea mbali, bado wanataka kiongozi aongoze bila kujali yaliyopangwa na wenye mabavu. Kama hivyo ndivyo, basi wasiishie kuchangishana tu. Wawe tayari kusimama na kiongozi wao katika raha na katika majaribu yote yaliyoandaliwa juu yake. Hili litamtia nguvu yeye ya kuendelea kukitumikia chama akijua, kujitoa kwake kunatambuliwa na kuheshimiwa na anaowaongoza.
 
Ni jambo jema, lakini huyu ndugu ameumizwa sana na utawala kisa tu ni hicho cheo. Natamani angepumzika kupisha mwingine lakini huyu aliyetangaza nia nahisi harufu ya kijani. Hakuna jinsi, SISIEM waendelee kulala na viatu sharti Mbowe awe mwenyekiti, tena napendekeza hadi hapo atakapoona hawezi hata kutembea.
 
Watu Wana hofu na Mbowe... Mbona vyeo Ni majukumu mazito? Au Mbowe Ni kikwazo kwa wapinzani wake?...
 
Huu ni ubabe umetumika

Mbowe apunguze udkteta

Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
2019 Imeisha

-Soko la Korosho limeharibiwa -Ajira Sekta rasmi na sekta binafsi zimeshuka

-Hali ngumu ya Maisha Maradufu

-Uchaguzi Serikali za Mitaa Umeharibiwa

-Kuna Hatari kutokea Janga la Njaa Kanda ya Kati

-Katiba Inavunjwa na kubakwa Mchana wa Jua Kali

Hiyo ndiyo 2019
 
Back
Top Bottom