Hali ilivyokuwa katika Jiji la Dar wakati vijana CHADEMA wakimchukulia fomu Mbowe

Ccm ni nawakubali na wataendelea kukaa madarakani milele. Mi sielewi kwamba viongozi wa upinzani nao wanatekeleza mikakati ya Ccm au nao hawaelewi plan za Ccm. Hapa Ccm wamepiga bao ni wachache sana wataelewa huu mchezo
 
Ccm ni nawakubali na wataendelea kukaa madarakani milele. Mi sielewi kwamba viongozi wa upinzani nao wanatekeleza mikakati ya Ccm au nao hawaelewi plan za Ccm. Hapa Ccm wamepiga bao ni wachache sana wataelewa huu mchezo
Kwa hiyo nyie wanaCCM mmelewa mchezo siyo? Basi sawa
 
Eti watu ambao hawana hata kitanda cha kulalia wanaenda kumchukulia Bilionea Mbowe fomu ya unyekiti inayouzwa milioni moja!

Unakuta huyo anayeongea dining room yake iko kwa mama lishe (Mama nitilie)!

Hii nchi ina ujinga, Usanii na vituko vya kitoto sana!
Huwa unatapatapa mpaka unatia kinyaa
 
Mimi ndo huwa nachukia siasa za tanzania.au za afrika zina upuuzi mwingi sana kuliko akili.

Mbowe kwani hataki uenyekiti? Kama hataki mnamchukulia ili iweje?akija sema hakupenda mlimsukumia tu akajikuta ni mwenyekiti?

Kama ana taka si aende kwa uwazi tu akachukue?
Waangalie hawa vijana kwa umakini miezi kadhaa ijayo watakuja hapa na pale kumnanga mbowe kwa maneno ya kebehi huku wakiunga mkono juhudi.

Badala ya kuchangishana pesa za kusaidia wenye wagonjwa na maradhi wanachangishana kwa mambo ya hovyo.subirini si si nyingi sana.
Mi hizi sarakasi nilizing'amua mapema, uchaguzi ujao wataenda wamama wajawazito kumchukulia form
 
Ni kitu gani ambacho Mbowe amenyunyuzia hawa wanachama wenzake wa CHADEMA kila siku wanamtaka yeye tu?
 
Mi hizi sarakasi nilizing'amua mapema, uchaguzi ujao wataenda wamama wajawazito kumchukulia form
Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
 
Hata yule mkurugenzi wa ile coperative bank alikuwa awalipa baadhi ya shareholders ili wamlilie kuwa anafaa kuendelea kuwa CEO, hivyo hiyo michezo ya watu wa huko tulisha izoea
Pole sana
 
Nakumbuka wakati Makundi ya watu walipokua wanaenda kumuomba Lowasa agombee nikacheka Sana.
Mimi siafiki kiongozi yeyote kukaa muda mrefu madarakani kwasababu yoyote ile.
Sidhani Kama nchi au chama kinaweza kuwa na mtu mmoja tu anaeweza kuongoza..
 
Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
Mi siwashwi na chochote ila nasikitishwa kuona kwamba vijana wa Tanzania wana uwezo mdogo sana wa kupambanua mambo bila kujali viwango vyao vya elimu. Yaani hakuna tofauti ya msomi na asiesoma kama mimi
 
Ni nderemo. Ndivyo tunavyoweza kusema wakati makundi ya vijana yalivyofurika makao makuu ya CHADEMA kumchukulia fomu Mwenyekiti anayemaliza muda waje Freeman Mbowe ili agombee tena nafasi hiyo.

Mratibu wa zoezi la kuchangia kumchukulia fomu Mbowe Bwana Daniel Naftali Ngogo amesema pesa zimetumwa nyingi kupita kiasi na lengo la shilingi milioni 1 limevuka kwa mbali.Mpaka leo kabla ya kuchukua fomu zimechangwa shilingi milioni 5 na laki 6 Taslimu.Ngogo amesema katika orodha ya michango kiasi cha chini kilichotumwa ni shilingi 150 na kiwango cha juu ni shilingi laki 2

Tazama video chini jinsi ilivyokuwa

View attachment 1272250
View attachment 1272251
Foolish
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom