Jiji la Dar kurindima leo wakati Freeman Mbowe akikabidhiwa fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ni asubuhi Tulivu ya siku ya Jumatatu huku jiji la Dar likiwa katika pilikapilika za kawaida kwa watu wake.Kwa wazungu wanaita Blue Monday.

Kwa upande wa kisiasa ni Jumatatu ya kitofauti kabisa ambapo Maelfu ya vijana wa Chadema wanatarajiwa kulitikisa jiji watakapoelekea ofisi ya Chadema Kinondoni kwa lengo la kumchukulia fomu za kugombea Uenyekiti Freeman Aikael Mbowe ambaye anatizamwa na watanzania kama mwanasiasa jabali wa upinzani asiyenunulika.

Wakizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari kwa nyakati tofauti waratibu wa zoezi la kuchangisha fedha za kumchukulia fomu Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake wamekiri taratibu zote zimekamilika.

Mmoja wa waratibu hao Twaha Mwaipaya amesema tayari michango imetimia shilingi milioni moja ambayo ni gharama ya fomu.

Hata hivyo Mwapaiya amesema zoezi la kukusanya michango halitakoma kwani kiasi kitakachozidi atakabidhiwa Mhe Mbowe ili akitumie kwa ajili ya kuwafikia wajumbe kuomba kura.

Mratibu huyo amesema tayari magari yameandaliwa katika majimbo yote ya Dar es Salaam ambapo wanachama wote watakaribishwa kwenda kushuhudia zoezi la kuchukua fomu na kwenda kumkabidhi Mhe Mbowe.

Safari ya kwenda kumchukulia fomu itaanza saa 3 kamili asubuhi hii kutoka majimbo yote kumi ya mkoa wa DSM

Naye Daniel Naftali Ngogo ambaye pia ni mmoja wa waratibu wa vijana katika zoezi hili alisema vijana wanaona kwa sasa Freeman Mbowe ndiye mtu pekee anayeweza kuendelea kuongoza chama hiki.

*Molemo Media* inatarajiwa kutoa Live coverage wakati wa zoezi la kuchukua na kukabidhi fomu kuanzia saa 3 asubuhi.
 

Attachments

  • Screenshot_20191125-151419_Facebook.jpg
    Screenshot_20191125-151419_Facebook.jpg
    171 KB · Views: 1
  • Vijana-wa-Chadema-waliojitokeza-leo-Habari-za-Chadema-Facebook.mp4
    685.7 KB
"Mbowe Mwansiasa jabali hanunuliki" Mleta Uzi.

Alie isaliti Kamati kuu ya wajumbe wa chadema 2015 kwa kuhongwa pesa na yule fisadi wa nywere nyeupe Ni Nan Kama siyo Mbowe? Je huko siyo kununulika?

Tukiacha tu na ushabiki Mbowe Ni Mwanasiasa mzuri kweli lakini anaependa Sana pesa hata Benard Membe Anaweza Akamununua tu 2020 akampa kiti Cha kugombea urais Kupitia tiketi ya Chadema..

Huyu jamaa ananunulika kirahisi mnoo kuliko Mwanasiasa yeyote kwasababu Anapenda pesa Sana.
 
Zilipendwa zama za kudanganywa, saizi tubataka Maendeleo. Hivi gamuonagi hata soni za kiutu kudanganya wakati nnajuaga
 
Mr Tyang,
Nawashauri vijana wa Lumumba mtafute hoja nyingine. Hizi hoja uchwara zinawadharaulisha sana
 
Back
Top Bottom