WanaJF
Karibuni katika tukio la kihistoria la kumuomba na kumkabidhi fomu za kugombea Uenyekiti wa Chadema Taifa shujaa na mpambanaji asiyechoka Kamanda Freeman Aikael Mbowe.
Tukio hili linafanyika katika hoteli ya Protea Upanga jijini DSM.Itakumbukwa wazee kutoka sehemu mbalimbali nchini wameunganisha nguvu kumuomba Kamanda Mbowe kugombea nafasi hii.
Mpaka siku ya leo Kiongozi huyu anayejivunia mafanikio lukuki ndani ya Chadema alikuwa hajatangaza rasmi kama atatetea nafasi yake.Hali hii imewatia kiwewe wanachama kote nchini.
Updates...1
Mwenye shughuri ni mzee athumani yassini mzigo mapigo saba kutoka kigoma.
Kutakuwa na statement ya wazee wa Pwani walio amua kumsindikiza na kudhamini fomu ya mwenyekiti
Aidha kutakuwa na tamko la bawacha na tamko la vyuo vikuu kutoka kwa mwenyekiti Gango Kidela
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wameshafika ukumbuni kushuhudia tukio hili ili kuwajuza watanzania nchini kote.
Updates 2..
Kamanda wa Anga Shujaa Mpambanaji asiyechoka Freeman Mbowe anawasili hapa ukumbini.Ni shamrashamra kubwa sana zinatawala hapa ukumbini.Hakika ni hoihoi na nderemo kutoka kwa wazee na umati mkubwa wa wanachama uliofika hapa.
Itakumbukwa historia fupi ya Mzee Athumani mapigo saba ana miaka 20 ndani ya chadema
Wamesukumwa na jitihada za mwenyekiti kwenye kukijenga chama.Anataja mafanikio anasema tulikuwa na madiwani 40 leo wako zaidi ya 500
Anataja idadi ya wabunge walio anza na chadema hadi waliopo sasa.Mzee anasema amefungwa kwa ajili chadema, amelala nje kwa ajili ya chadema kutokana na kusakamwa na ccm
Anasema Mbowe ana historia na mageuzi ya nchi hii na hakuwahi kukubali kukata taama kwa kuwav anataka na amini kwenye mabadiliko
Sasa anafuata muwakilishi wa kinondoni Mama Esther Samanya
Anataja sababu
1. Hali ya chama ilivyo kuwa na kilivyo sasa ambapo kimefanya chaguzi kuanzia misingi, matawi, wilaya hadi mikoa ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya chama.
2. Utashi wa mwenyekiti kukikuza chama na kuwa mbunifu .
Sasa anatuata peter chacha muwakilishi wa wazee wa ilala.
Anasema wazee wa kigoma wametuwahi maana wao walitaka kumchukulia fomu kabla yao
Wanamfahamu mwenyekiti Mbowe tangu akiwa kijana kwenye chama mpaka hapa alopofikia sasa akikaribia uzee
"...Tuna upendo na tunamuamini sana mbowe na tunaamini atakipeleka chama hadi kuchukua dola" "..una watu wanao kipenda chama nyuma yako.. chapa kazi kamanda.."
Sasa wanafuata wa wazee wa Temeke.Waziri Mkumuna mwenyekiti wa wazee mkoa wa Temeke.
Anatoa shukrani kwa wazee wa kigoma hususani mzee mapigo saba kwa hatua walizo chukua
Anamuomba mwenyekiti apokee fomu na kutimiza malengo ya chama kuelekea kushika dola.Tanzania nzima ina ona kazi aliyofanya Mbowe
Anafuata muasisi wa chama wilaya ya temeke anawapongeza wazee wa kigoma, alikuwa miongoni mwa wazee 60 walioasisi chama hiki.Amemtaka kila mzee wa chadema kupeperusha bendera kwenye nyumba yake
Anafuata mzee kutoka Pwani Said Bakari Mazoea.Anasema Pwani yote inamuunga mkono Mbowe kwa kazi kubwa anayofanya.
Sasa anazungumza mwenyekiti wa bavicha kutoka Njombe.
Kwa niaba ya vijana anatambua mchango wa mh mbowe kutupeleka vijana nchi ya ahadi.Anatambua mchango wa waasisi kama kina mzee kimesera, kina mzee Athumani mapigo saba.
Anafuata mzee Peter Kimesera muasisi wa chama.
Tumeanza na watu 30 tukafanya mikutano 67. Wakati huo Mbowe akiwa kijana. Mbowe amepewa jina la Freeman ana wajibu wa kuwafanya watanzania kuwa Freeman.
Aliposhika chama akazindua chama upya, kuanzia mavazi mpaka aina ya siasa hadi hapa chama kilipo fikia.Kuanzia ongezeko la madiwani, wabunge na wanachama ni kutokana na mafanikio yaliyo fikiwa ndani ya chama
Sasa anafuata mratibu wa kanda ya Pwani.
Sisi waratibu tumekaa na kuamua hatma ya chama kwa kukuomba ugombee uwenyekiti.
Tunakuomba uchukue fomu uendelee kuwa mwenyekiti wetu
Sisi chadema ndio tuna mamlaka ya kichagua kiongozi wetu, msajali na mawakala wengine hawana mamlaka ya kuingilia mambo yetu.
Umejitolea mhanga, walitaka kukutoa roho soweto na bado hukuridi nyuma.
Updates 3...
Sasa anafuata Kamanda Mbowe.
1. Chadema imesheheni watu wenye vipawa na taaluma mbalimbali kwanini iwe mimi?
2. Sikukusudia kugombea uenyekiti wa chadema na kauli yangu niliitoa kwenye kamati kuu. Na niliwaambia tutafute mtu mwingine tunayemuamini lakini kamati kuu ikaja na azimio na ikakataa.
Kamanda Mbowe kwa heshima kubwa anakabidhiwa Fomu hapa huku ukumbi mzima ukizizima kwa hoihoi nderemo na vifijo.
Baadhi ya akina mama wanaangua kilio cha Furaha.
MWISHO