Halahala usimle kuku na mayai yake!

Halahala usimle kuku na mayai yake!

tatizo kila kimoja kila ladha yake, ukila kuku hamu ya mayai iko palepale wala si suala la ulafi, tatizo roho kutamani ladha tofauti tofauti....
kuku ana ladha yake, mayai hali kadhalika, haya mambo ni magumu Ruta labda upate msaada wa Mungu kuyakabili!:becky:

muhanga Muumba anachukia walafi ambao hawatosheki na alichowapa...............
 
Last edited by a moderator:
Wataalamu wanasema Haina Chenga wala Haina Kuremba Ruta!

Ndallo Mayai yanatosha kabisa.....................hayana chenga au kuremba.....................na huyu kuku sanasana atakuachia laana uanze kuchechemea au hata kusuasua.............................majuto huwa ni mjukuu.........
 
Last edited by a moderator:
Mhhhh! Haya bana Ruta. Mie nakulaga omelette na scramble eggs.

 
Last edited by a moderator:
Tena Imany John umenikumbusha hiki kipindi cha sikukuu........kuku wengi wanachinjwa na mayai yanaliwa haifai kabisa............waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaache huo upuuuuuuuuuuuuuuuuuzi

Jamaa yangu unakoelekea siku hizi kwenye haya masuala si kuzuri! Sidhani kuwa itachukua siku nyingi kabla hatujasikia kuwa umeng'ang'aniana na mtu Temeke.
 
Acha kujivunia aibu yako
Acha kula kuku na watoto
Acha kuku, kula mayai tu
Acha ubabaishaji wako
Acha, nasema wacha kabisa!
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Visingizio vyako nimevikataa kabisa
Katu siafiki huo utetezi wako
Kamwe sitabariki uzandiki huo
Eti yote ni halali yako pia!
Nani kakudanganya hivyo?
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Ukitaka maisha marefu, usimle kuku
Ukitaka amani, usimuibe kuku wa watu!
Ukitaka heshima, tafuna yai lake tu!
Ukitaka jina, mwache akutagie mengine
Ukitaka suluhu, mnusuru kuku akutagie
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Wanaokula kuku na mayai yake wamelaaniwa
Wasiomwonea huruma kuku ni walafi hao tu
Wasiomjali kuku wamejikosesha mayai yake
Wasiomlinda kuku kututoka kabla ya siku zao!
Wanaoabudu matumbo yao humeza kila kitu!
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Waliomtafuna kuku na mayai yake ni wafu!
Kama bado wako hai basi wanasuasua tu!
Kama wako barabarani basi wanachechemea tu!
Kama hawachechemei basi wanameza tunguri tu!
Kama hawamezi ndunga basi ni teja wa mengineyo!
Halahala usimle kuku na mayai yake!

Alas! sasa kati ya kuku na yai kilichoanza kipi?
 
Mhhhh! Haya bana Ruta. Mie nakulaga omelette na scramble eggs.

BAK recipes zake hazina shida mradi kaa mbali na kuku ili aendelee kukutagia mengine mengi..........kitunze kikitunze.............
 
Last edited by a moderator:
Jamaa yangu unakoelekea siku hizi kwenye haya masuala si kuzuri! Sidhani kuwa itachukua siku nyingi kabla hatujasikia kuwa umeng'ang'aniana na mtu Temeke.

Mtoboasiri mking'ang'aniana si ndiyo swai.................muwe wote hata na milele ijayo?
 
Back
Top Bottom