Hakuna watu wanaopenda kujisifu kama wacheza drafti

Hakuna watu wanaopenda kujisifu kama wacheza drafti

s
Heavyweight wa draft Tanzania hawazidi kumi Mangwelele,Shaban katoto,Ronaldo,Nduli ndulaima,Noel,Aman Siri Mchunguzi,Kwatamwizi,Simba Dom,Simba Keko ,Dogo janja,Ali baka wa Moshi na Rama wa Arusha...Issa Mamba bingwa wa tege kumi Tanzania kama haupo hapo hatukutambui...
simba ana mwalimu wake anaitwa fyatuka mahisabati..huyo ni jini
 
Wewe utaishia pale kitanzini MR hufiki,kuna wazee wapo pale MR hotel kete wanasukuma kwa macho.
Akiona anaenda kingi utaskia john na mpira,john na mpira,anakwenda john kupeleka posa kapata mwali..
Akikufunga goal moja anakwambia nakupiga kamoja tu nna wake wengi nikikupiga viwili wake wenzako watakosa...
Yani kamoja kama nguruwe huwa hapigi vingi
Ukianza wewe kusukuma kete utaskia anayefata nani mmeniletea mporipori huyu ananishusha kiwango amefikaje hapa..
Ukisuma kete moja utaskia wewe uwe unakuja asubuhi kufanya mazoezi huu muda wa mafundi unataka kubakwa hapa

Huu mchezo hauhitaji watu wenye hasira kuitwa mchumba,baby,mke,mchepuko,mwanamwali,tanua nipite,maraya wewe
Aisee
 
Utasikia

''Leo lazima nichezee hayo makalio...tena utanifunulia mwenyewe, kunguru wewe

Au, ''leo nakupiga mpaka ukohoe mfupa''

Hapo jamaa anakaribia kupata ushindi
Kuna mtu nilishampiga ngumi ya uso...
na ndio ukawa mwanzo na mwisho kucheza hiyo michezo ya uswahilini....
 
Huu mchezo naupenda bt kila nikijfunza siwi mkali ktka kuwafunga watu .sijui nafeli wapi Alafu Huku ktaa watu wanacheza hadi ligi ya pesa
 
Draft lina njia zake tunaita copy master hizo and become the master kitakachobaki ni mbinu ndogo ndogo na mahesabu tu
Huu mchezo naupenda bt kila nikijfunza siwi mkali ktka kuwafunga watu .sijui nafeli wapi Alafu Huku ktaa watu wanacheza hadi ligi ya pesa
 
Mchezo wa draft una matokeo matatu, kuna
KUSHINDA,
KUSHINDWA NA
SALE.
Kiukweli mchezo huu unamfanya mtu kuwa MBISHI SANA.
 
Katika eneo unaweza kukuta watu wanajisifu basi ni wacheza drafti.

Ukifika kijiwe cha wacheza drafti kwa mara ya kwanza kama hujawahi kufika basi unaweza kukimbia ukijua hawa watu ni wauaji wakubwa maan hutaacha kusikia kauli kama nakuua, hili umekufa, usinichezee mimi mtu mbaya sana, mimi sio mtu wa kuchezea, hili huponi, hili sikuachi nakuua, yaani kwenye drafti kila mtu ni mbaya.

Binafsi napenda drafti, hua nikitoka kazini mapema nikafika maeneo ya nyumbani lazima nende kwenye vijiwe vya drafti nikafunge watu,pamoja na kua mimi sio mtaalam sana ila ukiingia kwenye 18 nakuua, huponi.

Mimi sio mtu mzuri kabisa kwenye drafti.

Wale wapenda drafti tupeane majina ya madrafti magumu kwenye play store niwe nacheza kuchangamsha akili.

Nakumbuka nikiwa form one niliwahi kumfunga bingwa wa kijiwe kwa ambae alikua anawapanga watu kama nyanya, hakuamini wakaenda kunishtaki home kua nimekalia draft sisomi, hiii ni baada ya mimi kudhalilisha wazee wa kijiweni[emoji23][emoji23].
Nilisha wahi kimpiga mzee wangu super. Nikiwa mdogo nikawa natamba kwa watu kua nimempiga mzee super, aisee ilikua mwanzo na mwisho draft kuonekana nyumbani, mzee alipiga marufuka akasema linachelewesha watu kufanya kazi.
 
pole sana kijana inaelekea shughuli yangu huijui . na kwa taarifa yako huo mkoa siyo mara ya kwanza mimi kuja na nimeshachua pesa za hao wazee mara nyingi tuu. wazeee wote wanaocheza pale mimi wananifahamu na nikifika tuuu lazima waniachie siti na ambaye huwa anajifanya jeuri kwangu huwa na mpatisha kindandi na kumwambia atafute sare mojaa tuu . ni mzee gani pale utakaenizuia nisichukue hiyo laki tano . wachezaji wote pale nawafahamu na ubovu wao naujua . kijani kama unataka kuniona njoo MR tarehe 5 siku wanayozindua hayo mashindano . watu tumezaliwa kuucheza huu mchezo .

Game imechezwa leo na mshindi wa kwanza ni Godfrey umeshapata taatifa zake eehhh😂😂watu wanasukuma kete hatari,ameramba kaki tano yake chap,mshindi wa pili laki2 na watatu laki1
 
Nilisha wahi kimpiga mzee wangu super. Nikiwa mdogo nikawa natamba kwa watu kua nimempiga mzee super, aisee ilikua mwanzo na mwisho draft kuonekana nyumbani, mzee alipiga marufuka akasema linachelewesha watu kufanya kazi.
Nimecheka balaaa😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom