Hakuna watu wanaopenda kujisifu kama wacheza drafti

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Katika eneo unaweza kukuta watu wanajisifu basi ni wacheza drafti.

Ukifika kijiwe cha wacheza drafti kwa mara ya kwanza kama hujawahi kufika basi unaweza kukimbia ukijua hawa watu ni wauaji wakubwa maan hutaacha kusikia kauli kama nakuua, hili umekufa, usinichezee mimi mtu mbaya sana, mimi sio mtu wa kuchezea, hili huponi, hili sikuachi nakuua, yaani kwenye drafti kila mtu ni mbaya.

Binafsi napenda drafti, hua nikitoka kazini mapema nikafika maeneo ya nyumbani lazima nende kwenye vijiwe vya drafti nikafunge watu,pamoja na kua mimi sio mtaalam sana ila ukiingia kwenye 18 nakuua, huponi.

Mimi sio mtu mzuri kabisa kwenye drafti.

Wale wapenda drafti tupeane majina ya madrafti magumu kwenye play store niwe nacheza kuchangamsha akili.

Nakumbuka nikiwa form one niliwahi kumfunga bingwa wa kijiwe kwa ambae alikua anawapanga watu kama nyanya, hakuamini wakaenda kunishtaki home kua nimekalia draft sisomi, hiii ni baada ya mimi kudhalilisha wazee wa kijiweni😂😂.
 
Toka utotoni mchezo huu ulifanya nikafinywa na mama mzazi.. naupenda Sana
Kuna njemba walikuwa wanacheza karata Kila siku nikawaambia mkilijua draft mtaziona karata si lolote! wakabisha.. siku ya siku nikawashawishi tukatengeneza draft mambo yakawiva ikawa Kuna njemba moja haijui kabisa ikafundishwa mpk ikajua mpk aliemfundisha akawa nae hamfungi mwanafunzi wake akaanza kumtambia.. baadae jamaa akaamia kwangu akizani mi hazi zake,alichezea kichapo Kila siku hata moja alikuwa hapitishi!!,baada ya kukubali mi mkuu kwake nikaanza kumfundisha ujuzi wa draft mwishowe akaweza siku anabahatisha kunifunga moja alifurahi kinyama.. tukawa tunaendelea kucheza mpk akajua vyema na maneno ya kwenye draft yakawa yanamtoka! ha ha ha nilikasirika ila siku muonyesha hasira zangu.. ila nikamuambia nakupa siku tatu hapitishi hata goli moja akabisha.. siku ya kwanza hakunifunga yapili pia na yatatu! mpk alinyoosha maelezo akanyanyua mikono juu kusalimu amri😂😂 sahivi nimemuacha anasumbua mtaa mpk mwenyewe anajishangaa draft limekuwa Kama kilevi kwake..
 
"Nilipewa mke na ng'ombe wawili juu kwakuwa nilienda kijiji flan nkapiga kijiji chote,nikisukuma hii kete ujue umekwisha"...ni moja ya vitisho alipenda kutoa jamaa wangu Kitimbe wa Kitimbe pale alipoona ushindi unakaribia kwa upande wake!!!!


"Nilifunga watu wote katika treni yani tokea Treni inaanza safar pale Mpanda hadi kufika Dar es salaam mimi nilikuwa napiga tuu watu, treni ilipofika dsm nilisusiwa na draft lenyewe afu wewe paka wa kihindi ndio unisumbue".....Huu ulikuwa mkwala wa jamaa yangu aliejiita Mkuu wa kituo! ilikuwa ukisikia huu mkwala ujue kashaona upenyo wa kwenda kingi!!!

"Huu mchezo ulifanya mi nishikiwe panga pale kigoma, nilipiga mji mzima mwishowe wakataka kunikata mapanga, leo hapa lazima niue mtu"......Hii ilikuwa ni kauli ya bwana Mgoma kufa pale alipoona ushindi upo upande wake

"Mimi ndio mzigua mwenye roho mbaya kuliko wote,natega mbele na nyuma... bao limeisha hili sasa sijui utatoa nyuma au mbele".......Hapa ilkuwa ukisikia hivi uju Mzigua kashatega bao kotekote


"Bana nikubane legeza tuondoke".....Jamaa yangu Chimulenga pale Tabora mjini alipenda kusema hivi ni ilikuwa akisema hivi bhas ujue kashakubana vibaya mno na ukijifanya kum'bania njia ya kuingi kingi bhas ujue bao linaisha hapohapo


Nimekumbuka mbali sana aisee
 
Ni mchezo mzuri unawaunganisha watu wa rika zote na hauna gharama kabisa unapunguza mambo mengi Sana ...Mimi nacheza ila vijana waneanzisha TEGE yaani wakuanzishia kete mbovu ili ufungwe maana watu washameza copy za pandu na sumu ya pandu au Samba mpya na za zamani hawafungiki...
 
Ni mchezo mzuri unawaunganisha watu wa rika zote na hauna gharama kabisa unapunguza mambo mengi Sana ...Mimi nacheza ila vijana waneanzisha TEGE yaani wakuanzishia kete mbovu ili ufungwe maana watu washameza copy za pandu na sumu ya pandu au Samba mpya na za zamani hawafungiki...
Mkuu kuna kundi la Mziki Mbeya mjini miaka ya 2005 walikuwa wanaitwa Isanga Family. Ulikuwa unawafahamu
 
Back
Top Bottom