Hakuna watu wanaopenda kujisifu kama wacheza drafti

Draft niulizeni Mimi acheni mambo ya porojo hapa, Mwalimu wangu marehem juma mchafu bingwa wa Tanzania, achana na mangwelele huyu bwana ni bingwa mstaafu aliumwa mpaka akachanganyikiwa baada ya kumpeleka muhimbili akaambiwa ugonjwa anaoumwa ni anawaza hesabu kubwa sana akitaka kupona aache huu mchezo ndo mwanzo wa kustaafu mabao,aka mabauna.sasa hivi kuna mtoto mmoja anatamba huko tz anaitwa Ronaldo juzi kachukua ubingwa wa Tanzania mashindano yalifanyika moshi lakini naapa nikija bongo lazima nipige nae maana huku niliko nimeuwa wote mabingwa wote now wananiita magufuli kutokana na hii makitu, ukifika Dodoma kijiwe cha Saba saba utakuta kuna dogo anaitwa Serengeti, ukienda pale meriwa kuna mtu anaitwa gandu keke, pale chan'gombe kuna mtu wa kuitwa dogo janja ukifika mambo pouwa kuna mtu hatari sana wakuitwa kwata mwizi au kamata Mwizi huyo mtu ni hatari sana ukifika chadulu unakutana na jamaa wa kuitwa nduli huyu bwana ana roho mbaya kuliko ya amini dadaa, pale mbagala zakhiem kuna mtu wa kuitwa adinan ukija morogoro kuna mtu wa kuitwa chatanda pale juwata lakini timu yake ipo chamwino, dah uzi unikumbusha mbali jinsi nilivyokuwa nasafirishwa Mikoa mbali mbali kwa ajili ya hiyo kit. Daah ngoja niishie hapa maana nina mengi ya kuandika kuna siku ntaleta kisa cha kupigwa kipapai cha macho nilipovamia kijiji kimoja turiani huko cha kuitwa chogoari. Ramadan Kareem

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika eneo unaweza kukuta watu wanajisifu basi ni wacheza drafti.

Ukifika kijiwe cha wacheza drafti kwa mara ya kwanza kama hujawahi kufika basi unaweza kukimbia ukijua hawa watu ni wauaji wakubwa maan hutaacha kusikia kauli kama nakuua, hili umekufa, usinichezee mimi mtu mbaya sana, mimi sio mtu wa kuchezea, hili huponi, hili sikuachi nakuua, yaani kwenye drafti kila mtu ni mbaya.

Binafsi napenda drafti, hua nikitoka kazini mapema nikafika maeneo ya nyumbani lazima nende kwenye vijiwe vya drafti nikafunge watu,pamoja na kua mimi sio mtaalam sana ila ukiingia kwenye 18 nakuua, huponi.

Mimi sio mtu mzuri kabisa kwenye drafti.

Wale wapenda drafti tupeane majina ya madrafti magumu kwenye play store niwe nacheza kuchangamsha akili.

Nakumbuka nikiwa form one niliwahi kumfunga bingwa wa kijiwe kwa ambae alikua anawapanga watu kama nyanya, hakuamini wakaenda kunishtaki home kua nimekalia draft sisomi, hiii ni baada ya mimi kudhalilisha wazee wa kijiweni😂😂.
[/QUOTE
Ni kweli aiseer
 
Ok Mkapa yule alikua mchezaji wa Yanga? sema Kama anajua mwambie aende manyanya hapo au Mbagala kizuiani au mtoni kwa Azizi Ally au Popobawa manzese hizo ndio club maarufu za mabingwa wa mabingwa tunaotambulika na huo mchezo Tanzania...akienda manyanya game collage atapata wapinzani sio huko nyumbani...
yah mkuu..umetisha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heavyweight wa draft Tanzania hawazidi kumi Mangwelele,Shaban katoto,Ronaldo,Nduli ndulaima,Noel,Aman Siri Mchunguzi,Kwatamwizi,Simba Dom,Simba Keko ,Dogo janja,Ali baka wa Moshi na Rama wa Arusha...Issa Mamba bingwa wa tege kumi Tanzania kama haupo hapo hatukutambui...

Ebhana niko dar mbagala nipo karibu na kijiwe gani cha mabingw niende kujifunza draft niwe moto


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom