Hakuna Uuzwaji wa Ardhi Mkataba wa DP World na Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,907
945

MHE. ELIBARIKI KINGU - HAKUNA UUZWAJI WA ARDHI MKATABA WA DP WORLD NA TANZANIA

"Tukiwa kama wabunge tuna nafasi ya kusema vitu vinavyotoa muelekeo wa nchi. Mafanikio tunayoyazungumza ya Serikali ya awamu ya sita nyanja za Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa kwa dhati ya moyo niseme Waziri wa Fedha na Mipango umeitendea haki sana Serikali ya Awamu ya Sita katika masuala ya Sera" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Tunapoangalia hali ya Uchumi wa nchi za Afrika Mashariki, masuala ya Kupanda na kushuka kwa bei (Inflation), bei za vyakula na vifaa, Taifa la Tanzania ni imara katika Mataifa yote ya Afrika Mashariki. Katika haya tunakupongeza sana Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Rais anahangaika kutengeneza misingi ya kuleta kodi kwenye nchi, Uwekezaji unaozungumzwa, Rais akahakikisha tuache kukimbizana na mikopo, Taifa liwe na vyanzo vyake vya mapato. Rais amefanya Mipango, tunao watu wa DPWorld" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Kuna watu wanasema nchi imeuzwa, huu ni upotoshaji wa makusudi na lengo la kuchafua Umoja wa kitaifa. Mkataba wa Tanzania na Dubai haujumuishi kuuzwa kwa Ardhi ya Tanzania. Rais hawezi kuliuza hili Taifa na hafanyi maamuzi kwasababu ni Mzanzibar" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Wananchi na Viwanda wamekuwa wakilalamika, bei ambayo imekuwa ikitozwa kwenye vifaa vya elektroniki stempu imekuwa ni kubwa. Waziri muwaite wawekezaji mkae nao muwaombe washushe bei ili wananchi wawe na manufaa katika gharama zinazozungumzwa" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi
 

Attachments

  • mbunge-kingu.jpg
    mbunge-kingu.jpg
    47.8 KB · Views: 4
ukiona mwanasiasa anaongea 'Amani' , 'Umoja wa kitaifa" sijui nn.ujue hana hoja ni kutisha tu watu..anayevunja umoja wa kitaifa ni nani ? atajwe jina
 
Back
Top Bottom