Mbunge Elibariki Kingu Ameishauri Serikali Kuiongezea Mkataba wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya SONGAS

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ELIBARIKI KINGU AMEISHAURI SERIKALI KUONGEZA MKATABA WA SONGAS

"Na kule wanakopita watu wa CHADEMA wanapiga propaganda kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako January (Wizara ya Nishati)" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"Nataka niwaombe wabunge wote tuendelee kumuunga mkono Mhe. January Makamba na Mama Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Nishati, tuendelee kuwashika mkono. Kazi wanayoifanya ni kubwa. Sisi kwenye Ilani tuliwatuma mtuwashie Umeme, Umeme unawaka unataka nisikusifie? - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

Wabunge mbalimbali wakati wakijadili Bajeti ya Wizara ya Nishati leo Jumatano Mei 31, 2023 bungeni jijini Dodoma wameitaka Serikali kuongeza mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme ya SONGAS. Mmoja wa wabunge ni Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi

"SONGAS inapaswa kuongezewa mkataba kwa sababu inafanya kazi nzuri ya kuzalisha Umeme wa uhakika na kulipunguzia mzigo Shirika la Umeme nchini (TANESCO). SONGAS ni mfano bora wa matokeo ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)" - Mhe. Elibariki Kingu, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi.

WhatsApp Image 2023-05-31 at 17.13.29.jpeg
 
Back
Top Bottom