Hakuna uhusiano wowote kati ya demokrasia na maendeleo

Waliokimbia Ulaya kwenda Marekani na kusaidiana kuutoa utawala wa Waingereza Marekani walitaka demokrasia. Wameweza kuweka kuepuka taratibu za uonevu walizoziacha Ulaya za Wafalme mafashist na walipata maendeleo.
 
Sehemu kubwa ya Africa imetawaliwa bila demokrasia kuwa muda mrefu lakini Africa ndio bara maskini zaidi duniani.
No! Hapana! Umasikini wa Afrika haukutokana na ukosefu au kutokuwepo kwa demokrasia BALI umetokana na WIZI, UPORAJI NA UNYONYAJI ULIOKITHIRI wa mali na rasilimali za Afrika by hao Wazungu na Wasia kwa kutumia nia nyingi nyingi ikiwa ni pamoja na mikataba ya kinyonyaji dhidi ya akina Chief Kimweri na wenzao ZAMA ZA KALE.

Leo kuna wizi wa wazi wazi wa rasilimali zetu ikiwa ni pamoja na madini yetu (almasi, dhahabu, shaba, chuma, tanzanite na mengineyo), mali asili ikiwa ni pamoja na mbao za thamani sana kama mninga au mitiki na mengineyo na hata wanyama wetu ZAMA ZA LEO! Na kwa karibuni na hata sasa ni kwa kutumia misaada wanayotupa. Say wanakopesha $1.0bi/= lakini at the end of the day unaishia kulipa hata say $2. 0bi/=! Kwani utalipa riba, service charges kwa ajili ya huo mkopo, na zaidi ya hayo, utalipa mishahara na migharama mingine mingi kwa ajili ya "wataalamu" wanao ambatana na huo mkopo! Achilia mbali kuwa utanunua hata vifaa vingine vya hiyo miradi kutoka kwao kwa bei za KURUKA! Kwa njia hiyo mipesa inarudi kwa hao waliotukopesha!

Chunguzeni mikopo hii mtaona kuwa kuna njia nyingi za kinyonyaji na wizi ndani yake na hivyo kuufanya huo mkopo au hata msaada usiwe na manufaa kwetu na hivyo kuzidi kutufanya kuwa masikini! Kuna mtu mmoja aliwahi kusema "mikopo inatufanya tuzidi KUSIKINIKA na watoa mikopo na wazidi KUTAJIRIKA!
 
Kuhusu case ya kariakoo ni suala la vipaumbele tu ukiimarisha soko la kariakoo kwa hizi billion 34 inawezekana sana zikakupa miradi mingi sana ya maji pindi maboresho yake yakikamilika!!
Kwa hesabu nzuri kama hizo mkuu pengine tungekuwa tumeshamaliza matatizo kama hayo ya maji kwa siku nyingi tu, sema ndio hivyo hakuna mipango kama hiyo.
 
Kwa taarifa yako hiyo Libya ingeweza kuwa na maendeleo bila hata udictaror. Na hata sasa imevurugika kwakuwa yeye Gadaffi alilazimisha kukaa madarakani kwa shuruti wakati tayari watu walikuwa wamemchoka. Na hata hivyo hiyo Libya pamoja na kwamba haiko stable, bado ina uchumi mzuri kuliko sisi wenye amani ya hofu.
Jibu rahisi ni kusema tu kwamba maendeleo hayaletwi na udikteta wala demokrasia, kwa sababu hapo kama Libya ingekuwa inaongozwa kidemokrasia basi maendeleo yake yangehusishwa na hiyo demokrasia.
 
Waliokimbia Ulaya kwenda Marekani na kusaidiana kuutoa utawala wa Waingereza Marekani walitaka demokrasia. Wameweza kuweka kuepuka taratibu za uonevu walizoziacha Ulaya za Wafalme mafashist na walipata maendeleo.
Kujaribu kukopy ustaarabu wa ulaya na marekani na kuupest africa ni kujidanganya
 
Lakini umecopy ustaarabu wao wa kutumia gadgets na sasa hivi unapandisha threads JF.
Kukopy teknoloji ni sawa lakini kukopy mifumo ya kujiongoza no, ustaarabu africa bado sana!! Ndio maana hapa kwetu ni rahisi tu watu wakanunuliwa gongo na t-shirt wakati wa uchaguzi na mtu akapigiwa kura na watu wa namna hiyo halafu akashinda alafu washindi wanatoka na kulazimishwa kwamba demokrasia imekomaa tanzania!!
 
Udikteta unazaa maendeleo kwa kipindi gani ili tuupe muda?.
ni miongo sasa Africa ni chimbo la madikteta ila bado mnahamasishana kuchimba vyoo vya shimo hadi kesho kutwa.
Madicteta wanao pandikizwa ndio wanao shindwa kuleta maendeleo kutokana na miongozo wanayopewa na wanaowapa nguvu.

Dicteta anaetafutia nchiyake maendeleo halisi anauwezo wakufanikiwa kuendeleza nchi katika muda mfupi mfano libya.

Nchi za ulaya na marekani wanaendelea kwa spidi kilasiku sababu ya ukiukwaji mkubwa wa democrasia wanaoufanya katika nchi za wanyonge kwa kupora mali za wahusika na kuwawekea viongozi wanao kubaliana na dhuluma zao.
 
Kukopy teknoloji ni sawa lakini kukopy mifumo ya kujiongoza no, ustaarabu africa bado sana!! Ndio maana hapa kwetu ni rahisi tu watu wakanunuliwa gongo na t-shirt wakati wa uchaguzi na mtu akapigiwa kura na watu wa namna hiyo halafu akashinda alafu washindi wanatoka na kulazimishwa kwamba demokrasia imekomaa tanzania!!
Watu kama wewe ndiyo mnarudisha nyuma demokrasia . Ni wakati wa kutumia teknolojia kuwapa wananchi elimu ya uraia na kutambua haki zao na umuhimu wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Watu kama wewe ndiyo mnarudisha nyuma demokrasia . Ni wakati wa kutumia teknolojia kuwapa wananchi elimu ya uraia na kutambua haki zao na umuhimu wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
We jamaaa unachekesha sana hivi utatoa elimu gani ya uraia kwa mtu ambaye amepewa pombe ili ampigie mgombea fulani na pombe kanywa alafu uchaguzi unaofuata anafuatwa na kuambiwa kutakuwa na pombe tena!!
 
Mimi Nina mama namfahamu aliniacha hoi alipotembelewa na mjumbe wa ccm ili kuhakiki kadi yake ya chama yule mama akasema kwa namna huyu baba alivyonifuata hapa nyumbani na kunieleza vizuri sina sababu ya kumpigia kura mtu ambaye hata nyumbani kwangu hapajui
 
Watu kama wewe ndiyo mnarudisha nyuma demokrasia . Ni wakati wa kutumia teknolojia kuwapa wananchi elimu ya uraia na kutambua haki zao na umuhimu wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Asante sana mke wangu kwa huu ufafanuzi.
 
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/ viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.
Ingekuwa hivyo, Bara la Africa ndiyo lingekuwa tajiri zaidi duniani na Bara la Ulaya ndiyo masikini wa kutupwa
 
Ukitaka kujua faida au hasara ya demokrasia jaribu nyumbani kwako, kuwa mtemi waamulie kila kambo na usiruhusu hata mmoja kati ya mkeo ama watoto wanyenyue mdomo kukushauri kuhusu lolote lile pale nyumbani, kwa msingi kwamba wao as long as wanakula wanashiba, wanavaa, wanatibiwa vizuri na wanakwenda shule hakuna haja ya kukushauri kitu... afu pima baada ya miaka uone kama kutakuwa na maendeleo katika mji wako.
 
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/ viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.

Kwa hiyo mapendekezo yako ni kuwa mlio juu tuwaache tu huko huko muendelee kujilia vinono kwa raha zenu?
 
Back
Top Bottom