KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Moja ya mada muhimu sana toka kwako, na kiujumla hapa JF.Naunga mkono jitihada za kuifungua nchi, ila sikubaliani na approach inayotumika katika kufanya hivyo.
Ni kweli tunahitaji wawekezaji , ni kweli tunahitaji ajira lakini namna tunavyowatafuta na kushirikiana nao sioni hiyo faida inayosemekena itapatikana.
Tunaweka mazingira mazuri ya uwekezaji ndio , at the expense ya kurisk rasilimali zetu lakini tunachokipata hakilingani na risk yenyewe.
Hizo Multinational Corporations ni wazoefu wa kufanya investments katika developing countries, wanajua namna ya kufanya ili kupata faida.
Wanajua udhaifu wa watendaji na viongozi wa developing countries, na pia wana wataalam lukuki wa namna ya kukwepa kodi , hivyo naamini kabisa kuwa hatutaambulia chochote. Historia ni shahidi na tumeona namna Accacia ilivyotufanya over the years.
Moja ya mambo ambayo wawekezaji hao wanayataka ni upatikanaji kwa urahisi kwa Work Permit.
Sasa kama tunataka watanzania wafaidike na hizo ajira sioni namna gani watafaidika nazo kama wageni nao watafurika kupigania hizo nafasi.
Hao wawekezaji ndio hulalamika kuwa watanzania hawaajiriki kwakua ni wezi, hivyo wanapenda kutoa wafanyakazi nje ya nchi sasa kama watanzania ni wezi, kwanini wageni wanapewa nafasi ya kuwekeza katika nchi ya wezi.
Kwakweli sijawahi kuona nchi ikipata maendeleo kwa njia ya uwekezaji wa Taifa jingine.
Kwa Mfano Rais wa Taifa kubwa kabisa lenye uchumi mkubwa marekani , Bwn Trump katika kipindi cha miaka mi nne alisafiri mara 19 tu katika nchi 24 duniani, sasa Rais wetu kwa miezi sita tu anazo safari zaidi ya 6 unaweza ona miaka yake 10 itakua na safari si chini ya mia na zaidi.
Tunapenda nchi yetu iendelee na ifunguke lakini tujadiliane na kuangalia ni namna gani tunaweza kufanya hivyo na tukanufaika, ila binafsi sioni kama kusafiri sana nje ya nchi ndio suluhu, na pia sioni sana kama Foreign Direct Investment ni suluhu tosha.
Nawasilisha.
Imewasilishwa vizuri, bila mihemko na unazi uliozoeleka toka kwako.
Lakini kidogo inachanganya. Unazungumzia "ziara" au "uwekezaji" (kufungua nchi)?
Uwekezaji toka nje ni muhimu, ninakubaliana kabisa na hilo, lakini kama ulivyoeleza, "ufunguaji wa nchi unafanyika kimakosa", kama ulivyoeleza, kwa vile tunafungua tu huku tukiwa hatuna uwezo wa kumiliki huo ufunguzi. Tunajiachia tu waje wafanye, huku sisi tukiwa tupotupo tu, wakati hatujui lolote. Huu ni upumbavu.
Jambo ambalo nami ningependa kulikazia hapa ni hii dhana potofu kabisa aliyo nayo Samia ya kudhani kwamba Tanzania itaendelea kwa vile watu wanakuja kuwekeza hapa bila ya mipango maalum. Hili litakuwa ni jalala la uchafu.
Maendeleo ya nchi hii yanawategemea waTanzania wenyewe kuyaleta. Juhudi kubwa zaidi zingeelekezwa huko kwa wananchi wenyewe. Wawekezaji muhimu kabisa katika maendeleo ya nchi hii ni waTanzania wenyewe.
Mama hili kalitupa mbali kabisa, anachojua yeye ni "kufungua tu nchi."
Mafuta ya kula, kwa mfano ya Alizeti, nayo mpaka tusubiri wawekezaji waje hapa ndio tuweze kutosheleza mahitaji yetu? Mifano ya aina hii ipo tele, na katika yote hiyo, hatuhitaji hata miaka mitano kujitegemea wenyewe katika mahitaji ya vitu hivyo na kuuza nje.
Tunafanya nini na elimu yetu, ili hao wawekezaji wanapokuja hapa tunafuzu kupata teknologia yao ambayo itabaki hapa hapa sisi tukiitumia kwa manufaa yetu.
Kuna hizi nyimbo zinaimbwa kila mara kwamba ni lazima wawepo waTanzania wanaoandaliwa kuchukua nafasi za wageni baada ya muda maalum. Huyu mama anajua kinachofanyika huko? Ameweka msisitizo wowote na ufuatiliaji kujua kuwa hili jambio muhimu linatimizwa? Yeye kazi kubwa aliyofanya hadi sasa ni "kufungua nchi tu", bila kujua anaifungua tupate faida ipi. Haandai mazingira ya kufaidika na ufunguzi huo.
Mama Samia ni lazima abadili mwelekeo, anakotupeleka siko kabisa.