Natamani niwaone hao walimu cjawai kutana nao thou nimepita shule kadhaa, walimu wenzangu wengi wenye atleast visible life success ni wenye privilege kiasi mf wakuu wa shule.
Maana kwanza hawana muda wakukaa shule akiwa na makamu mzuri basi yeye kazini anakuja hata once a week au anakuja ana saini anasepa.
Hawa walikuwa/wanauwezo wa kutumia pesa ya shule na ya ziada na mishahara yao ikakaa.
Hizi case study zenu/zetu ziwe real ni walimu wangapi wanafikia hayo? Maana atleast kila staff ina watu(walimu) kumi na kuna uhakika ukatembelea shule 10 ukakuta wawili tu, nao sio maisha kusema maisha.
Eneo ninalokaa mie kuna chuo cha ualimu, sekondari 2 na shule za msingi 3 around kijiji kimoja na taasisi nyingine za serikali kama mbili hivi na chuo cha kilimo lkn ukitembelea madukani hapa center utakuta madaftari ya walimu ya madeni mpaka ya sembe 2kg, bado wanapigwa pesa kukopa mitaani kwa riba ya 50% yan laki kwa laki na nusu. Hawana jinsi wanakopa.
Sasa huwa najiuliza ina maana walimu tu ndio hawana akili ya kujiongeza ili kuongeza kipato? Ina maana ukienda fani nyingine kama kilimo, udaktari/nurse nk ambao tupo nao huku vijijini unakuwa na akili ya maisha?
Jibu linabaki ni hapana, ila ualimu sio kazi inayotoa malipo stahiki. Na marupurupu ya kujikimu.
Ngoja nikuoneshe yanayotokea huku vijijini, na walimu mnajifanya hamyaoni mnataka tusifiwe hapa wakati kazi hii haina malipo halisi.
Mwl anaeanza saizi daraja la IIIA, take home ni kama 270 kama sio chini ya hapa ila ipo maeneo hayo hayo. Huyu anaanza kazi pesa ya kujikimu anapewa laki na nusu, nyumba ya kupanga miezi sita inahtaji 240000/= hapa nimepigia anaanza na chumba cha elfu 40 kwa mwezi, wanaoanzia mijini kabisa ndio shida zaidi.
Anahtaji godoro la kuanzia, utakuta mahtaji yote kuanza kazi ni kama laki 5 minimum, alafu kapewa 150000/= tu bila shaka hii ataitumia kwa chakula tu nakununua sufuria na jiko la mkaa/mafuta na sahani wakati akisubiri mshahara wa kwanza, na pengine huwa hautoki kwa mwezi husika.
Mwishowe anaamua kukopa kwa mtu/ndg na jamaa au walimu aliowakuta ili maisha yaanze, (madeni yanaanza RASMI) sasa kila akifika mwisho wa mwezi anajikuta analipa deni anakosa pesa ya kula, hii trend inaendelea, mwisho anakuwa mwenyeji eneo husika anaanza kukopa madukani, hapo hajawai nunua chochote cha ziada ndani,hata kuchonga kitanda.
Miezi kadhaa badae anaona kujitoa katika tabu nikakope bank, anaenda kukopa bank, kwa mshahara wake anapata mil 4 ikikatwa anabaki na 3.8mil anarud nyumbani analipa madeni mpk inabaki karibu nusu.
Anaamua basi na yeye ni binadamu ananunua kitanda, labda na ka tv ka kichina ka 250000/= Familia za kiafrika nazo zipo nyuma, mama/baba anaomba pesa au mdogo mtu kafukuzwa ada, home hawana chakula anatuma kidogo, akiangalia balance kesha baki na laki 2
Mwisho wa mwezi salary inaanza kukatwa sasa hapokei 270000/= tena anapokea 190000/= hapa mdipo shida za walimu zinaanza.
Kesho anaingia vicoba (shida tu hiz) kesho yake finca, kesho kutwa blacc uko nako anakopa si zaidi ya laki 2 maana salary yake haina dhamana kubwa.
Kabla mkopo haujaisha bank inabdi atop up maana shida zinazidi na kazi kubwa ya ziada anauza bagia kwa wanaume anakomaa na tution ambazo siku hz pia hakuna, au anafungua kiduka cha elfu 50 ambacho kwa mzunguko wa alipo ni mdogo hapo anapambana na wazawa.
Walimu wengi waliopo vijijini wanajua shida ya wazawa huko hawataki kuona una biashara, wana kitu tunaita undewa, wivu wa kimasikini "atapataje mshahara alafu aje ashindane na sisi pia".
Walimu haya yote mnajua ila hamtaki kusema, wanawake ninyi mlioolewa mnakuwa supplied wala hamuoni, wengine walimu huku wa kike ni malaya (samahani kwa neno kali) ila wanafanya, wanatembea leo na diwani, kesho mtendaji, jioni afisa nanii wa hapa kijijini anaeonekana anaweza mpa walau tsh 10000 ya ziada.
So maisha ya umasikini inakuwa ni trend, walimu wamebaki kuwa walevi wengi wetu, stress anaingia darasani na yeboyebo, ananyonga baiskeli shati linanuka jasho anavaa siku 3
Walimu wenzangu haya yapo, mie nayaona kila siku, tupo wachache tuna mantain personality na heshima ya kutokuwa na madaftari ya madeni ya unga madukani lkn sio wote. Wengi wana dhiki
GOD SAVE TEACHERS