Hakuna namna naweza kuwashtaki Vodacom Tanzania kwa kuchelewesha muamala!?

JITU BANDIA

JF-Expert Member
Feb 5, 2023
2,679
6,019
Wakuu, hivi kisheria hii imekaaje!? Kuna uwezekano wa kuwafungulia shauri mahakanani hawa watoa Huduma kama Vodacom Tanzania kwa tatizo la kuchelewesha muamala wangu wa MUHIMU!?

Haya makampuni yamekuwa yakifanya kazi kwa mazoea sana... na kufanya wanachojisikia...

Hivi hakuna sheria ya wajibu wa mtoa Huduma kwa mteja!?

Na je vipi kama amekiuka huo wajibu. Nini kinafanyika!?

Wajuvi wa sheria tusaidiane kwa hili. Hii imekuwa kero aisee
 
1. Kwanza ni kuwaambia kampuni yako (i.e tigo, voda au azam) ili muelezane vizuri

2. Mkishindwana hapo utaweka malalamiko yako mtandaoni TCRA ( https://emrejesho.gov.go.tz/chagua_...6EMX74XYFJZf9NV6nrjnzNiHgtt6Iqhlm6VYeXW2vhplQ )

3. Kama hapo suala lako likishindwa kusuluhishwa inabidi ulipeleke kwenye kamati ya malalamiko ya TCRA.

4. Kama haujaridhika na maamuzi ya Kamati ya TCRA, basi utapeleka shauri lako/malalamiko yako Fair Competition Commision (FCC)
 
Wakuu, hivi kisheria hii imekaaje!? Kuna uwezekano wa kuwafungulia shauri mahakanani hawa watoa Huduma kama @Vodacom Tanzania kwa tatizo la kuchelewesha muamala wangu wa MUHIMU!?

1. Huo muamala wako ulikuwa ni kati ya mtandao wa Voda na kampuni nyingine au Voda-Voda?

2. Je, umechunguza na kujiridhisha vya kutosha kwamba tatizo lilikiwa ni mtandao wa Voda na sio ama kifaa ulichokitumia au sababu nyinginezo?
 
Mimi nafikiria kuwashtaki sababu natumia laini yao ya kasi internet muda mrefu sasa,toka juzi vifurushi vyao vya kasi internet avipatikani ukiwapigia wanakuambia wako kwenye marekebisho watavirudisha muda si mrefu na ikiwa nimelipia wiki hii kifurushi cha elfu 70
 
Back
Top Bottom