Hakuna Mlipa Kodi anayependa kodi! Serikali na wananchi wajue hili

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Watanzania wengi walikuwa wanafikiri kodi ni kitu cha watu wengine! Sasa ndiyo wanajua ni lazima kulipa kodi. Zile risiti ambazo tulikuwa hatuziombi ni pesa ambazo serikali imekosa na sasa tunalipa wote.

Wale machinga ambao mlikuwa mnawashangilia wauze bila kodi sasa ndiyo mnajua kwamba wasikolipa wale utalipa wewe maana ni lazima mtu alipe.

Lakini vilevile zile shangingi na magari ya kifahari pesa ndizo zinatoka hivi. Uchungu sasa mnajua tuache kulalamika sana
 
Watanzania wengi walikuwa wanafikiri kodi ni kitu cha watu wengine! Sasa ndiyo wanajua ni lazima kulipa kodi. Zile risiti ambazo tulikuwa hatuziombi ni pesa ambazo serikali imekosa na sasa tunalipa wote. Wali machinga ambao mlikuwa mnawashangilia wauze bila kodi sasa ndiyo mnajua kwamba wasikolipa wale utalipa wewe maana ni lazima mtu alipe. Lakini vilevile zile shangingi na magari ya kifahari pesa ndizo zinatoka hivi. Uchungu sasa mnajua tuache kulalamika sana
Tuache kulalamika,sawa unatupa vyanzo vipi vya mapato ili tuweze kuchangia tozo hizo.
 
Kodi halali inalipwa saaana tu lkn kodi magumashi atalipa nani labda Chanzo Cha Matatizo coz wanajuana.
 
Kodi itapendwa kama wote tukifika Muhimbili tutapokelewa kama binadamu wenzetu wanaoshuka kwenye ma Vieite wanavopaparikiwa!

Dawa zote zitolewe dirisha la Pharmacy sio kuelekezana Pharmacy za mtaa wa pili kwa kigezo kwamba dawa ilioandikwa haipo kwahio kanunue pale!

Ukienda polisi hulazimiki kuhonga hela ya mafuta ili watoe gari kumkamata mhalifu wako!

Hulazimiki kwenda stationery ya jirani ya kituo kutoa copy ya loss report na kulipishwa kuitengeneza online sababu ukifanya mwenyewe process haikamiliki!

Wabunge watozwe 30% ya mapato yao kama kodi ya uzalendo kila mwezi bila kupepesa macho! Gari watembelee zisizozidi 2500cc watachagua wenyewe ila engine ya gari isizidi ukubwa huo!

Mawaziri walipwe mshahara mmoja kulingana na current tittle! Kama ni mbunge aliyetuliwa kuwa waziri mbali na posho, mshahara wa ubunge asilipwe ichangie kodi ya uzalendo. Atapokea mshahara wa waziri tu.Gari ya waziri isiwe na zaidi ya 3000cc of engine!

Magari ya kifahari iwe mwiko, gari za kutembelea viongozi zisizidi 150M sababu ziko tax exempted!

Haya yakiweza kutimizwa kwa usahihi ndipo mje na ngonjera za kodi za wazalendo!
 
Tuache kulalamika,sawa unatupa vyanzo vipi vya mapato ili tuweze kuchangia tozo hizo.

Yaani wamaume au mwanamke kijana unasubiri kupewa kila kitu. Kwani kazi ya serikali ni kukupa vyanzo? Kuna misitu kibao ipo ya kulima, kuna bahari na maziwa yenye samaki kuna wateja kibao wa kilimo wewe unasubiri upewe vyanzo utasubiri sana. Kama huna pesa za kutuma au kupokea pesa usiwenazo hasa kama huingizi kipato chochote. Usi subiri serikali hawaja kuzaa kazi yao ni kujenga miundo mbinu na kuwezesha kwenye elimu lakini uvivu wa mtu ni lazima tuamke
 
Kodi itapendwa kama wote tukifika Muhimbili tutapokelewa kama binadamu wenzetu wanaoshuka kwenye ma Vieite wanavopaparikiwa!

Dawa zote zitolewe dirisha la Pharmacy sio kuelekezana Pharmacy za mtaa wa pili kwa kigezo kwamba dawa ilioandikwa haipo kwahio kanunue pale!

Ukienda polisi hulazimiki kuhonga hela ya mafuta ili watoe gari kumkamata mhalifu wako!

Hulazimiki kwenda stationery ya jirani ya kituo kutoa copy ya loss report na kulipishwa kuitengeneza online sababu ukifanya mwenyewe process haikamiliki!

Wabunge watozwe 30% ya mapato yao kama kodi ya uzalendo kila mwezi bila kupepesa macho! Gari watembelee zisizozidi 2500cc watachagua wenyewe ila engine ya gari isizidi ukubwa huo!

Mawaziri walipwe mshahara mmoja kulingana na current tittle! Kama ni mbunge aliyetuliwa kuwa waziri mbali na posho, mshahara wa ubunge asilipwe ichangie kodi ya uzalendo. Gari ya waziri isiwe na zaidi ya 3000cc of engine!

Haya yakiweza kutimizwa kwa usahihi ndipo mje na ngonjera za kodi za wazalendo!

umechelewa kulalamika ungetakiwa kuomba risiti ili serikali iwe na pesa. Machinga hawalipi kodi ulitegemea pesa itoke wapi wakati wananchi wengi hawafanyi kazi na kuna vichaka vya mashamba serikali inaagiza mafuta, sukari na hata kuna samaki za china watu wavivu na hii itasaidia sana
 
Watanzania wengi walikuwa wanafikiri kodi ni kitu cha watu wengine! Sasa ndiyo wanajua ni lazima kulipa kodi. Zile risiti ambazo tulikuwa hatuziombi ni pesa ambazo serikali imekosa na sasa tunalipa wote. Wali machinga ambao mlikuwa mnawashangilia wauze bila kodi sasa ndiyo mnajua kwamba wasikolipa wale utalipa wewe maana ni lazima mtu alipe. Lakini vilevile zile shangingi na magari ya kifahari pesa ndizo zinatoka hivi. Uchungu sasa mnajua tuache kulalamika sana

1. Kwani wabunge, Mawaziri na wale vigogo wengine wanalipa kodi?
2. Vipi wale wabunge 19 wasio na vyama nao tunawalipa tokea kwenye zile kodi tunazokamuliwa?
3. Vipi zile pesa CAG anataarifu hatuishi kupigwa huko BOT TPA na kote serikalini? Source ni huku kukamuliwa kodi?
4. Vipi haya makampuni yanayozalisha hasara? Hiyo pesa ni hiyo hiyo tunayokamuliwa?
5. Nk

Huu uzalendo unaoasa kuwa hakuna apendaye kulipa kodi haya umeyazingatia?
 
Tuache kulalamika,sawa unatupa vyanzo vipi vya mapato ili tuweze kuchangia tozo hizo.

Mkuu vyanzo mbona lukuki:

IMG_20210716_182538_628.jpg
 
Kingine ni tuweze kumpa kisago kiongozi yoyote ambae atathibitika kuwa amefanya ufisadi wa kutisha😅
 
Kodi itapendwa kama wote tukifika Muhimbili tutapokelewa kama binadamu wenzetu wanaoshuka kwenye ma Vieite wanavopaparikiwa!

Dawa zote zitolewe dirisha la Pharmacy sio kuelekezana Pharmacy za mtaa wa pili kwa kigezo kwamba dawa ilioandikwa haipo kwahio kanunue pale!

Ukienda polisi hulazimiki kuhonga hela ya mafuta ili watoe gari kumkamata mhalifu wako!

Hulazimiki kwenda stationery ya jirani ya kituo kutoa copy ya loss report na kulipishwa kuitengeneza online sababu ukifanya mwenyewe process haikamiliki!

Wabunge watozwe 30% ya mapato yao kama kodi ya uzalendo kila mwezi bila kupepesa macho! Gari watembelee zisizozidi 2500cc watachagua wenyewe ila engine ya gari isizidi ukubwa huo!

Mawaziri walipwe mshahara mmoja kulingana na current tittle! Kama ni mbunge aliyetuliwa kuwa waziri mbali na posho, mshahara wa ubunge asilipwe ichangie kodi ya uzalendo. Atapokea mshahara wa waziri tu.Gari ya waziri isiwe na zaidi ya 3000cc of engine!

Magari ya kifahari iwe mwiko, gari za kutembelea viongozi zisizidi 150M sababu ziko tax exempted!

Haya yakiweza kutimizwa kwa usahihi ndipo mje na ngonjera za kodi za wazalendo!
ivi mawazir wanalipwa mara mbili kama m'bunge tena kama waziri?
 
Watanzania wengi walikuwa wanafikiri kodi ni kitu cha watu wengine! Sasa ndiyo wanajua ni lazima kulipa kodi. Zile risiti ambazo tulikuwa hatuziombi ni pesa ambazo serikali imekosa na sasa tunalipa wote. Wale machinga ambao mlikuwa mnawashangilia wauze bila kodi sasa ndiyo mnajua kwamba wasikolipa wale utalipa wewe maana ni lazima mtu alipe. Lakini vilevile zile shangingi na magari ya kifahari pesa ndizo zinatoka hivi. Uchungu sasa mnajua tuache kulalamika sana
Wee kilaza hizo tozo za simu ni kodi au unyang'anyi wa serikali kwa wananchi!
 
Sasa kauli ni kuwa uonevu sasa basi,tunataka matumizi bora ya kodi.bila unevu.

Iko hivi:

1. Asiyelipa kodi anatapanya huku unilaterally:

IMG_20210716_183804_119.jpg

2. Anayetozwa tozo za uzalendo huyu hapa:

IMG_20210716_183826_638.jpg

Inakuingia akilini?

Kimsingi kama kukiwa na matumizi mazuri yenye uwajibikaji, kodi ingepungua na haya ya uzalendo wala yasingekuwapo.

Habari ndiyo hiyo.
 
Iko hivi:

1. Asiyelipa kodi anatapanya huku unilaterally:

View attachment 1856112

2. Anayetozwa tozo za uzalendo huyu hapa:

View attachment 1856113

Inakuingia akilini?

Kimsingi kama kukiwa na matumizi mazuri yenye uwajibikaji, kodi ingepungua na haya ya uzalendo wala yasingekuwapo.

Habari ndiyo hiyo.
Uzuri ni kuwa hawa sioni kama wanaonewa,ila wanakubali kwa hiyari yao kuwa waimba mapambio au kuimbishwa mapambio tena kwa sauti kuu huku wakidhulumiwa na kuporwa haki zao za msingi,hata wanaojitokeza kuwasaidia wanaona hawana maana.
 
Back
Top Bottom