Hakuna mkate mgumu mbele ya chai (Falsafa ya Deus Seif na Abubakari Alawi inavyoendelea kukivuruga Chama cha Walimu Tanzania)

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Leo hii tarehe 16 Machi 2023 Wapiga dili Deus Seif na Abubakari Alawi wamefanikisha kuzuia mambo kadhaa kufanyika kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania.

Kama ambavyo tumebainisha hapo awali juu ya dhamira yao ya kurudi madarakani na kuendelea kufanya ubadhirifu ndani ya chama cha walimu huku wakiwafaidisha baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, ni wazi kuwa kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa maandiko yetu utagundua namna ambavyo mafisadi hao wameshindwa kuzuia uchu wao wa fedha za walimu kiasi cha kufanya kila linalowezekana kuhujumu na kuathiri maamuzi yote yanaowahusu kwenye vyombo mbalimbali vya serikali.

Katika hukumu iliyotolewa leo tarehe 16 Machi 2023. Mahakama Kuu kanda ya Dodoma imezuia mkutano mkuu wa CWT kugusa baadhi ya maeneo yakiwemo uchaguzi wa Katibu Mkuu, makamu wa rais na nafasi ya mweka hazina.

Huu ni mwendelezo wa kujaribu kuwasafisha mafisadi waliokwisha kuhukumiwa hapo awali ambao rufaa dhidi ya hukumu zao Jamhuri ilishindwa na kuonekana si kitu hivyo kuidhalilisha serikali. Swali la kujiuliza, Je Deus Seif na Abubakari Alawi ni akina nani mpaka waipelekeshe Jamhuri na kuidhalilisha TAKUKURU kiasi hiki? Wana chai ya aina gani kiwango cha mkate wowote kutokuhimili?

Wana nguvu kiwango gani hata kuathiri uchaguzi kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania? Wana nguvu kiasi gani kiasi cha kupingana na maamuzi ya mkutano mkuu uliowavua madaraka na uwanachama kutokana na ubadhirifu wao na matumizi mabaya ya madaraka?

Cha kujiuliza ni kwamba gharama ya wajumbe zaidi ya 1000 kwenda na kurudi Tanga na kwa idadi ya siku wanazotumia ni kwa nini haionekani kwamba chama kinahujumiwa? Yani hawa jamaa wanacheza na pesa za walimu kiasi cha kulipa vyombo vya habari kupotosha umma na kusherehekea ushindi wao dhidi ya Jamhuri.

Siku wanachama wa CWT watakapojua haki zao, watakapojua nguvu zao na watakapojua maadui zao na namna fedha zao zinavyofanyiwa ufisadi wataweka mipango sahihi ya kuendeleza chama chao.

Wanasiasa na baadhi ya viongozi wa Serikali wamekigeuza chama cha walimu kama mtaji wao. Hata hiki kinachoendelea leo hii kuna ushawishi wao mkubwa. Na ushahidi usio na shaka tunao.

Kuna siku inakuja tutaweka hadharani kila kitu na umma utawatambua. Kila kitu tunacho na vielelezo tunavyo. Maandiko haya ni kama bendera nyekundu ya kuwaonya waache mara moja hujuma zao la sivyo kila mwalimu mwenye fedha yake ndani ya chama ataona waziwazi namna fedha yake ilivyokuwa ikichezewa na namna ambavyo mafisadi hao bado wanahisi wana haki ya kuendelea kuzitafuna fedha hizo kiasi cha kuendelea kung’ang’ania kurudi madarakani na kudharau nguvu ya umma kwa kiwango hiki. Tutaendelea kuuambia umma wa walimu, chama cha walimu na watanzania kwa ujumla mpaka pale ambapo mafisadi hawa watakoma na kuheshimu fedha za walimu.

Kila hatua ya kudhoofisha nguvu ya umma inayofanywa na mafisadi hawa itafungua ukurasa mpya wa mapambano dhidi ya uhuni uonaofanywa na watu wachache wasio na woga wala haya.

Mbinu za Deus Seif na Abubakari Alawi na wote walio nyuma yao ambao baadhi yao tumekwisha kuwabainisha zimefika mwisho.
 
Kwann hiki chama kisifutwe tu kila siku mnatulalamikia hapa futeni mjiunge hata vicoba shubamit ningekuwa mwalimu ningeenda mahakamani kuomba hiki chama kifutwe
 
Back
Top Bottom