Shukran kwa kupata fursa ya kutoa mchangowangu;
1.Fikiria namba yoyote katika kichwa chako,kisha ijumlishe namba hiyo kwa tano (5),Jumlisha tena kwa nne (4),Jumla tena kwa tatu (3),baada ya kupata jawabu Sasa waweza toa kwa namba ya awali uliyofikiria kwa kichwa chako.
Jibu lake ni 12.
2.Sasa fikiria Tatizo linalokusumbua,kisha jumlisha furaha,pia jumlisha matumaini,kisha malizia kwa kujumilisha na Suluhisho.lipige teke tatizo linalokusumbua.
Sasa umebaki na Furaha,Matumaini na Suluhisho.
3.Fikiria tena kitu/jambo linalokufanya uwe na huzuni Maishani,kisha ondoa hofu, ondoa woga wa maisha yajayo,ondoa woga wa maisha baada ya kifo,ondoa woga wa vita,matetemeko na kuangamizwa kwa ulimwengu.Sasa huna ulichobakizi cha kukuogofya,Umebaki bila woga wowote.
4.Fikiria tena kama mtu aliyezaliwa karne ya kwanza akimsubiri mwana wa adamu aje kuangamiza dunia/ulimwengu,Jumlisha karne tano,jumlisha tena karne tano, jumlisha karne tano pia jumlisha karne tano, sasa ni karne 20 hivyo na bado ulimwengu haujaangamizwa wala kuja kwa yule,Sasa hunaulichobakiza zaiidi ya kuanzia kutumia ubongo wako vilivyo-kisawa-sawa.
5.Fikiria tena watu waliopata kuishi hapo kabla, 99% walishakufa na wengine washasahaulikia.
Kwanini uogope kifo kisicho epukika.
Ndugu zangu wapendwa hakuna Maisha baada ya kifo,Chapa kazi sana,Fanya dunia iwe mahala salama pakuishi.