Hakuna maisha baada ya kifo(no life after death)

Hakuna maisha baada ya kifo(no life after death)

Ila tu kuna tabiri nyingi sana kwenye vitabu vitakatifu kuhusu kuibuka kwa watu kama wewe.
Hao walikua wanawapanga tu,
Coz walijua watapingwa so wakitokea wenye akili zao wachache waki challenge hivyo vitabu mbumbumbu wengi wataona utabir umekamilika so wanafunga akili zao,its mind game as simpo as that.
 
Mkuu,Watu hawataki kufungua bongo zao...hata huwa hawataki kujiuliza dini walizoletewa zinawagawa au zinaleta umoja..?

Dini ipi ni ya kweli..?

Mimi kama nazaliwa katika dini ya mzazi na kuishi nayo je ni ninakosa gani kama nikihukumiwa huko mwisho kwamba dini yangu (wazazi)haikuwa sahihi..?
And most of us tumekua na dini zetu kwa sababu ya wazazi wetu na si utashi wetu
 
So kama ungekuta wazazi wako wanaabudu sanamu la Posta na wewe ungekua hivyo usingesikia la bible wala Quran(namaanisha most of the people)
 
Kama mimea,wanyama,wadudu hufa na kupotea hata sisi binadamu ni hivyo hivyo usiumize kichwa kuwaza maisha baada ya kifo,ukishakufa ndo umekufa hakuna cha peponi,wala motoni,wala kufufuka tena kama pombe kunywa ipasavyo,ukifa ndo nitoleee
Kama ngono fanya upendavyo, ukifa ndo imetoka hakunamaisha baada ya kifo.
Hizo data umezipata wapi au ndo umelala ukaamka ukaamua kutoa haya? We jipe Moyo tu lakini mda kidogo utajua kama yapo au hayapo... Vuta subira tu...
 
Mkuu hicho ni kibri na angalia usije kuangamia soon. Kibri ni kibaya sana Hasa unapofanikiwa kimaisha. Naona maisha yamekulevya vya kutosha.
 
Hakuna moto wamilele, izo ni propaganda tu za kuwafanya wanadamu wawe waoga na waishi vizuri

kunamwanafalsafa mmoja alisema,dini ni moja ya kueneza UKOLONI

naludia tena hakuna maisha baada ya kifo
Wewe unajuaje kwamba hamna maisha baada ya kifo? Ulishakufa na kufufuka?
 
Ngoja nimalizie sala yangu ya asubuhi nitarudi kuchangia
 
Ukifa unazaliwa tena sehemu nyingine katika namna nyingine ili ufaidi maisha mengine
 
Basi IMANI NI KUWA NA HAKIKA ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Ni hakika ya mambo yanayongojewa kudhihirika, ni hakika ya mambo ambayo hayajadhihirika bado, kwamba yatadhihirika. Kama wewe imani yako haikuruhusu kula nyama basi usimuhukumu yule ambaye imani yake inaruhusu kula nyama.
Kwahiyo Afande Kirusi hiyo ni IMANI YAKO.
 
Hakuna moto wamilele, izo ni propaganda tu za kuwafanya wanadamu wawe waoga na waishi vizuri

kunamwanafalsafa mmoja alisema,dini ni moja ya kueneza UKOLONI

naludia tena hakuna maisha baada ya kifo
Dini zilikuepo kabla hata ya mkoloni, babu zetu walikua na imani nawalikua wanaomba kwa imani, ndio maana ilikua alfajiri wakiamka wanasema asante aliyefanya tukaliona jua na jioni pia likizama wanashukuru kwa kuimaliza siku, na wengine kwenye miti mikubwa na mawe nk..
 
wewe uliwahi kufa ukafufuka? ni marufuku kuzungumzia kitu usichoweza kudhibitisha KWA HIYO JIBU LIWE HATUJUI KAMA KUNA MAISHA BAADA YA KUFA.au subiri ufe utuletee mrejesho
 
So kama ungekuta wazazi wako wanaabudu sanamu la Posta na wewe ungekua hivyo usingesikia la bible wala Quran(namaanisha most of the people)
Ndio,ipo hivyo kwa walio wengi hapa Tz.

Kuna kijana mmoja "Muslim" nilimuuliza,hivi ungekuwa umezaliwa familia ya kikristo leo hii ungekuwa mkristo...?

Akasita kwanza kunijibu,ila baadaye alikuja kuthibitisha kitu ambacho mwenyewe huwa nakubali kuwa ni vigumu sana na kuachana, kutoka katika ufuasi wa dini...alinijibu hata kama angezaliwa katika familia ya kikrsito anaamini angebadili huko mbeleni na kuwa Muslim.

Kwakweli si rahisi kutoka katika dini kama hutaki kujiuliza maswali na kuchangamsha ubongo wako.

Maisha baada ya kifo ni hadithi tu.
 
Kama mimea,wanyama,wadudu hufa na kupotea hata sisi binadamu ni hivyo hivyo usiumize kichwa kuwaza maisha baada ya kifo,ukishakufa ndo umekufa hakuna cha peponi,wala motoni,wala kufufuka tena kama pombe kunywa ipasavyo,ukifa ndo nitoleee
Kama ngono fanya upendavyo, ukifa ndo imetoka hakunamaisha baada ya kifo.
Inaonyesha wewe ni Mpinga Kristo, maana Yesu Kristo mwenyewe alitufundisha kuwa kuna Maisha mengine baada ya haya.
 
Hakuna maisha baada ya kifo!

Ukifa unaoza hadi kufikia kuwa udongo kamili
 
Bora kuamini alaf usikute, kuliko kutoamini alaf ukute kuna Maisha...
 
Back
Top Bottom