Hakuna kitu kizuri kama familia nzuri

Hakuna kitu kizuri kama familia nzuri

Shukrani kwa mada nzuri.
Familia ndio msingi wa mambo mengi mazuri na mabaya ktk jamii/taifa.
 
Hapana, ila nina rafiki na pia nina ndugu ambao wako na wenza wao wa toka utotoni! Ni full furaha na familia zao, kuna familia ukiiangalia kama ina furaha au huzuni unajua.
mimi nilikuwaga "kipofu", nilipendwa sana na mdada mmoja rafiki wa utotoni, sikuona mapenzi yake sababu ya upofu tu! Sasa hivi majuto ni mjikuu ila maisha lazima yaendelee!!
Its never too late. Tengeneza hapo hapo ulipo. Kujuta hakutoisaidia familia yako.
 
Hii una maana kuishi kwa maandiko. Hilo liko wazi.

Mimi nazungumzia matukio, ukikosea kuoa watu hawasemi ni mipango ya Mungu watasema hukumshirikisha Mungu as if wale wote ambao mambo yao au ndoa zao zinayumba hawamjui wala kuomba Mungu, ukipatia kuoa ni mipango ya Mungu! Kwahio mambo mazuri Mungu ndio anapanga ila mabaya sio Mungu anapanga tunajipangia wenyewe. Kwanini Mungu kwa uwezo wake asituamuru tufanye mema siku zote?!
Yaweza ikawa vyote viwili, kutomshirikisha Mungu, na pia kuelekeza machaguzi kwa kutumia akili zako za kuzaliwa na hapo ile nguvu inayotoka Principality ndo inachukua nafasi kuvuruga machaguzi bora.

Kiujumla, kwenye kuchagua mwenza ndo changamoto kweli kweli, unaweza ukafunga ndoa na mtu ambaye humfeel kabisa kumbe Mungu amekupa huyo akiwa na lengo nyote wawili msipotee na mwisho wa siku unajikuta kumbe ni mwenza wako kabisa, ipo hii sana tu.

Yote kwa yote ni kushukuru tu hata kama ni mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimpata mtu sahihi utainjoi sana familia bora na yenye furaha!
Kwa uchunguzi wangu mdogo usio rasmi nimetambua kuwa wale ambao Mungu huwakutanisha toka wakiwa mashuleni yaani udogoni wanaishi kwa amani sana!
Wachache wanaokutana ukubwani, nao huishi maisha yenye familia ya furaha!!
Kuna watatu nawafahamu walikutania msingi na sekondari ila maisha yao ya ndoa ni tafrani kuliko hata hiyo tafrani yenyewe.
Kweli msingi mzuri wa mahusiano ya wanandoa ndio utakaojenga Ndoa na familia bora,lakini sio lazima msingi huo uwe ulianzia utotoni.
 
shangazi yangu ndo anavomfanyia mumewe..mme analala kivyake kisa tuu jamaa amestaafu na hana kazi..hata papuchi hapewi tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu ndo watu kama hao ambao nawashangaa kwamba ina maana yeye furaha na amani ya familia haina maana kwao??

Anapofanya hivyo na kuona kabisa kuwa familia haina raha anakuwa anajisikiaje??

Too bad mkuu shangazi yako anachokifanya sio fair hata kidogo aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole kwa kutotambua upendo aliokuwa nao rafiki yako wa utotoni,japo kama ulivyosema life has to go on no matter what,ila I just hope hukumwonesha some kind of dharau like kuona sio wa type yako maanake hiyo inaongeza maumivu hata zaidi
Yawezekana hata angemuoa huyo rafiki yake wa utotoni leo angekuwa na majuto mengine kwasababu tu Hana apreciation ya kile alichonacho. Angeanza "oooh ningejua nisingeoa mwanamke alonipenda mimi maana mimi sikumpenda, now sifurahii mapenzi yetu"

Maana hata huyo alonaye alimchagua mwenyewe, na aliona ndio chagua sahihi kwakwe. Atafute tu ni wapi alikosea then arekebishe hapo hapo maana kitu bora siku zote ni kile usichokuwa nacho.
 
Aisse hii ngumu kumeza jamani sasa sisi ambao tumeham hama sana tushapotezana na marafiki wetu wa utototni itakuwaje jamani?????
Kumbe majibu unayo.
[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
Mungu haombwi mkate akatoa kitumbua mkuu,tama yako ni nzuri sana endelea kuomba itimizwe bila kusahau na wewe unaplay part ya kuja kuwa mshiriki bora kabisa wa familia yako

Hakuna kitu kizuri kama familia nzuri mkuu
 
Tukumbuke KILA MTU ANAPENDA FURAHA MAISHANI. Na usidhani kwamba kila familia inaweza kukupa faraja katika wakati wako mgumu. Wanaume tumekuwa wahanga sana katika hili hasa pale mambo yanapoyumba mpaka kipato kupungua. Utajuta.

Unapoona familia sio nzuri na haina furaha, kuna vitu vingi sn katikati, hasa vinavyowahusu baba na mama wa familia husika.

Kukosa urafiki, wivu, tamaa, kununa nuna, visasi, hasira, mwanamke kutaka kumcontrol mwanaume, kufichaficha siri, dharau, etc, ni kati ya mambo mengine mengi yanayosababisha familia nyingi kukosa furaha.

Kuna wanawake wengine (sio wote), wanashindwa kucontrol ulimi wao, hasa TONE, wanapoongea na wanaume, na muda mwingine kushindwa kutofautisha tone anayotumia akiwa anaongea na mume wake na housegal. Hili huleta magomvi mengi sn.

Wanaume hatupendi kuwa controlled na mwanamke, so inapoonekana kuna chembechembe hizo, lazima tutaonesha ubabe wa kiaina. So amani itatoweka kimtindo.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kawaida lawama kwa wanawake!!

Hivi nyie jukumu lenu haswa katika familia zenu zaidi ya kutoa pesa huwa ni nini haswa? Maana mara nyingi matatizo ya ndoa zenu huwa mnawatupia wake zenu as if nyie ni malaika vile!!

It takes two to tangle, kabla haujaanza kumnyooshea kidole mwenzio hebu tathmini wewe una mchango gani ktk kupotea kwa hiyo furaha ya ndoa/familia yenu?
 
Yawezekana hata angemuoa huyo rafiki yake wa utotoni leo angekuwa na majuto mengine kwasababu tu Hana apreciation ya kile alichonacho. Angeanza "oooh ningejua nisingeoa mwanamke alonipenda mimi maana mimi sikumpenda, now sifurahii mapenzi yetu"

Maana hata huyo alonaye alimchagua mwenyewe, na aliona ndio chagua sahihi kwakwe. Atafute tu ni wapi alikosea then arekebishe hapo hapo maana kitu bora siku zote ni kile usichokuwa nacho.
Yeah sure mkuu kwa hiyo badala ya kujutia ni vyema mtu akaangalia the way forward na kutafuta furaha inayomstahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah sure mkuu kwa hiyo badala ya kujutia ni vyema mtu akaangalia the way forward na kutafuta furaha inayomstahili

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, na ukute years back alikuwa anajisifia kwa kuchagua haswaaa. Atafute tu ni wapi waliharibu watengeneze tu, kuanza majuto ni mwanzo wa kutafuta mianya ya michepuko na ndipo atakapoivuruga zaidi familia yake.
Wanawake nao huwa hawabadiliki tu from no where, lazima kuna tatizo mahali. Washughulike na familia waliyo nayo, wasiwaze familia wasizokuwa nazo. Furaha yako unaitengeneza mwenyewe.

Wasimsahau na Mungu(kama ni waamini)
 
Yote hayo sababu ni kutovunja ukimya wanandoa mnapokuwa marafiki hamtaona haya kuambiana ukweli pindi mmoja wapo anapokosea.binafsi Mr wangu atakuwa rafiki yangu mkuu.
Inategemea na huyo mr wako utakae mpata malezi alio LELEWA na tabia yake kiujumla ....hakuna mwanamke asie penda kumfanya mmewe kama rafiki namba moja ...lakini ndio hivyo unajikuta unaolewa na mwanaume ambae anaona marafiki wa nje ni bora kuliko wewe mkewe. .kila la kheri .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli Mama la 2 watu wanabadilika, ndo hao naojiuliza wanakuwa wamepatwa na nini?? Hawaoni tena umuhimu wa familia zao kama mwanzoni? Maisha ya familia yanakuwa yamewakinai?? Inaumiza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu huwa hawabadiliki tu bila sababu, lazima kuna sababu.

Lakini kwa yeyote mwenye utashi na anatambua umuhimu wa familia yake. Kamwe hawezi kuruhusu sababu zozote zile ziingilie furaha ya familia yake. Iwe ni marafiki, pombe,pesa nk. Maana kwake familia kwanza.
 
kuna wengine baba na mama kila mtu analala chumba chake,ila baba anahudumia familia kama kawaida,hiyo nayo sijui ni familia bora ama
Baba anahudumiaje familia sasa? Maana familia ni pamoja na huyo mkewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom