Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,339
- 3,674
Habarini wana MMU
Nimekuwa najiuliza sana ninapoona mwanaume au mwanamke akipuuzia family yake kabisa na kuishi aina ya maisha isiyo na mwelekeo au matumaini kabisa.
Mfano unakuta mwanaume pombe sana,wanawake sana washkaji sana kipaumbele wanapewa marafiki na family kupuuziwa kabisa,kuweka heshima baa huku nyumbani kutwa wanashindia ugali na michemsho(ile ya lazima sio ya hamu au afya)watoto wapo nyumbani hawana ada mama kachakaa kama ana miaka hamsini wakati ni kinda la miaka hata thelathini tu,wakati huo baba sio kwamba pesa haipo,pesa ipo ila haoni umuhimu wa kuitumia na family yake kwa njia nzuri kabisa
mambo kama haya hunifanya nijiulize maswali kadha wa kadha
Hivi watu wote wanaoishi maisha ya kupuuzia na kutojali familia hawaoni kuwa familia nzuri ni kitu kizuri na kinachoweza kukupa faraja hata katika wakati wako mgumu?
Tuseme famila nzuri wanazichukuliaje? wanaona zinaboa?
Sijui maoni ya wengine yamekaaje juu ya hili lakini binafsi naamini familia nzuri ndio kila kitu,ni familia nzuri inayoleta
Mtaa mzuri wenye amani
Taifa lenye watu wazuri
Maisha yenye tumaini na mpangilio
Napenda tukumbushane kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine tumejisahau na kupuuzia familia zetu tukae chini na kutafakri upya na kurekebisha pale ambapo tunaona panaharibu familia zetu
tukumbuke familia ndo kila kitu tena wakati unaenda unaweza kutamba sana wakati una nguvu nyingi za ujana unavutia kila mtu anakutaka lakini siku yote hayo yakiisha ndo familia inaanza kukumbukwa na wakati huo familia yako tayari imeshazoea maisha bila ya wewe na hivyo kujikuta unaishi maisha machungu ambayo hujawahi kuyafikiria
Wana MMU hakuna kitu kizuri kama familia nzuri tuzitunzeni tuzienzi tuzifurahie kikamili tuzijali,kamwe hatutawahi kujutia japo ya dunia mengi lakini yapo yanayoepukika.
Asanteni.