Ni kweli mkuu lakini kunakuwa hakuna alternative nyingine zaidi ya kuonesha kuwa mwanaume yupo??
Au kuonesha katika namna nyingine??
Na unafikiri hata kama hamuhusishi watoto moja kwa moja, unafikiri watoto hawajui kusoma mazingira na kuona mabadiliko??
Unafikiri wanakuwa affected kiasi gani??
Na je ukiona hali inakuwa mbaya zaidi sio bora mkaachana kabisa kuliko kuendelea kuishi maisha ambayo hayapendezi??
Na mkuu dont take this as an attack simlaumu mtu aliye na shida ya familia naelewa hakuna asiyependa furaha nimetumia fursa hii kutukumbusha tu wote ambao tunaishi katika namna ambayo huenda ikawa kikwazo kwa familia zetu kuwa na furaha, kulewa wanawake wengi kuweka heshima bar kuwapa watu wengine kipaumbele badala ya familia kama kuna mtu ana hiyo tabia ni vyema akaacha kwa sababu ni kati ya viharibu furaha ya familia
Na sijabase upande mmoja maanake ni kwamba hata ikiwa mwanamke anatabia za kuvunja furaha ya familia mdomo mwingi kutojali majukumu yake kama mama kutomuheshimu mume wake yeye pia anapaswa kuchukua hatua coz familia ni ya watu wawili kama msingi na sio mtu mmoja mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app