Hakika wanaume wenye tabia kama ya Messi tumebaki wachache sana

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,133
68,444
UNAAMBIWA Lionel MESSI hajawahi kumgusa mwanamke mwingine zaidi ya mkewe Antonela Roccuzzo aliyeanza naye mahusiano tangu utotoni huko Rosario, Argentina.

Mnamo 2017, Messi na Antonella walifunga ndoa iliyotajwa kama ‘ndoa ya karne’ na kujaaliwa watoto watatu Thiago, Mateo na Ciro.

Raccuzzo ambaye kwa sasa ni Mwanamitindo ana taaluma Udaktari wa meno na mawasiliano ya kijamii aliyosomea katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Rosario kabla ya kujitolea kumsaidia Messi na kuzingatia familia yao.

Kupitia taaluma yake ya Uanamitindo amefanya kazi na chapa maarufu kama Stella McCartney, Adidas, na hivi majuzi, Alo.

Messi anampenda sana mwanamke huyo mrembo amejitolea sana kwake kiasi kwamba hata hawagusi wanawake wengine. Inaelezwa Messi alitaka kuwa mchezaji bora wa soka duniani ili aweze kumhudumia Roccuzzo na kumpa maisha mazuri.

Walipofunga ndoa, mashabiki wengi wa kike walijaribu kujaribu kumshawishi. Shabiki mmoja Suzy Cortez (almaarufu Miss BumBum) alijichora tatoo ya Messi mwilini mwake na kujaribu kumtumia picha zake akiwa katika jezi yake lakini Messi alim-block mara moja.

Messi amekuwa katika muonekano usio wa kawaida anapokuwa karibu na Wanawake wengine katika picha akiibana mikono yake au hata kuiweka mifukoni kuliko kugusana au hata kuweka begani kwa mwanamke mwingine.

Messi hufanya hivyo kuepuka vyombo vya habari kupindisha picha hizo kwa njia isiyo sahihi na kufanya ionekane kuwa kuna kitu kinaendelea wakati hakipo.

Mwanamuziki Shakira alipiga naye picha lakini alijiweka mbali na kuweka wazi kuwa mambo ni ya kiplato kabisa. Hamwekei mikono mwanamke mwingine kwa sababu kwake, ukaribu wa kimwili unabaki kwa mke wake tu.

Messi ni mmoja wa wanaume wachache ambao huweka mipaka kwa wanawake ambao sio mke wake. Anataka kuishi maisha ya faragha na Roccuzzo na watoto wao, na anaweka wazi mara kwa mara kwamba ana upendo wake ni kwa mpenzi wake huyo wa tangu ujanani.

NB: Uhusiano wa kiplato (platonic relationship) ni ule ambao watu wawili wana uhusiano wa karibu lakini hawana uhusiano wa kimapenzi. (Dhana hii inatokana na mawazo ya mwanafalsafa wa kale Plato). Kwenye hili wanaume wengi tutafeli.

Wanawake yapi maoni yenu kwa aina hii ya wanaume wenye tabia ya kufanana na Messi?
Lionel-Messi-and-Antonela-Roccuzzo-smiling-shortly-after-the-couple-were-married-in-2017.jpg
GettyImages-1450128847.jpg
 
Hiyo ndio siri ya mafanikio yake,ameshajielewa bila ya hivyo kila kitu kingeyayuka,watu wengi huwa hawajui kuwa baraka mnapokuwa kwenye ndoa zinaweza kuja kupitia mmoja wenu hivyo kwenda kinyumme cha hapo kila kitu kitapotea...
Hakika upo sahihi kuna cha kujifunza kwenye namna messi anavyoishi licha ya kuwa na umaarufu ambao wengi huwazuzua.
 
Neno "tumebaki wachache" sijalipenda .

" Wanaume sisi ni waaminifu . "

Mwanaume akiwa hajatulia ujue lazima kuna tukio la kutisha alichezewa likamfanya apoteze Uaminifu .
Kwa experience yangu ni kweli, wanaume wengi tuna upendo( refer first love) ila matukio ya usaliti ndio yanatubadilisha kutokuwa waaminifu.
 
UNAAMBIWA Lionel MESSI hajawahi kumgusa mwanamke mwingine zaidi ya mkewe Antonela Roccuzzo aliyeanza naye mahusiano tangu utotoni huko Rosario, Argentina.

Mnamo 2017, Messi na Antonella walifunga ndoa iliyotajwa kama ‘ndoa ya karne’ na kujaaliwa watoto watatu Thiago, Mateo na Ciro.

Raccuzzo ambaye kwa sasa ni Mwanamitindo ana taaluma Udaktari wa meno na mawasiliano ya kijamii aliyosomea katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Rosario kabla ya kujitolea kumsaidia Messi na kuzingatia familia yao.

Kupitia taaluma yake ya Uanamitindo amefanya kazi na chapa maarufu kama Stella McCartney, Adidas, na hivi majuzi, Alo.

Messi anampenda sana mwanamke huyo mrembo amejitolea sana kwake kiasi kwamba hata hawagusi wanawake wengine. Inaelezwa Messi alitaka kuwa mchezaji bora wa soka duniani ili aweze kumhudumia Roccuzzo na kumpa maisha mazuri.

Walipofunga ndoa, mashabiki wengi wa kike walijaribu kujaribu kumshawishi. Shabiki mmoja Suzy Cortez (almaarufu Miss BumBum) alijichora tatoo ya Messi mwilini mwake na kujaribu kumtumia picha zake akiwa katika jezi yake lakini Messi alim-block mara moja.

Messi amekuwa katika muonekano usio wa kawaida anapokuwa karibu na Wanawake wengine katika picha akiibana mikono yake au hata kuiweka mifukoni kuliko kugusana au hata kuweka begani kwa mwanamke mwingine.

Messi hufanya hivyo kuepuka vyombo vya habari kupindisha picha hizo kwa njia isiyo sahihi na kufanya ionekane kuwa kuna kitu kinaendelea wakati hakipo.

Mwanamuziki Shakira alipiga naye picha lakini alijiweka mbali na kuweka wazi kuwa mambo ni ya kiplato kabisa. Hamwekei mikono mwanamke mwingine kwa sababu kwake, ukaribu wa kimwili unabaki kwa mke wake tu.

Messi ni mmoja wa wanaume wachache ambao huweka mipaka kwa wanawake ambao sio mke wake. Anataka kuishi maisha ya faragha na Roccuzzo na watoto wao, na anaweka wazi mara kwa mara kwamba ana upendo wake ni kwa mpenzi wake huyo wa tangu ujanani.

NB: Uhusiano wa kiplato (platonic relationship) ni ule ambao watu wawili wana uhusiano wa karibu lakini hawana uhusiano wa kimapenzi. (Dhana hii inatokana na mawazo ya mwanafalsafa wa kale Plato). Kwenye hili wanaume wengi tutafeli.

Wanawake yapi maoni yenu kwa aina hii ya wanaume wenye tabia ya kufanana na Messi?
View attachment 2740981View attachment 2740982
Hakuna anayeweza kuthibitisha maana ni siri yake mwenyewe
 
Back
Top Bottom