Wanaume wenye tabia ya kuingilia maugomvi ya wanawake zenu kwa kuwasaidia "kusutana" mnakera

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Za weekend?

Hivi mwanaume timamu kabisa mke wako kagombana huko na wanawake wenzake halafu wewe unaenda kuingilia ugomvi na kuanza kusutana na wanawake?

Kwanza mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kurushiana maneno na mtoto wa kike? Mpenzi wako akiudhiwa huko na marafiki zake wewe msaada unaoweza kumpatia ni kwenda na wewe kusutana?

Hapo ndio unaonesha Manhood yako? Ndio mkitoka hapo akuambie "safi sana mpenzi wangu umewasuta mpaka wamekoma"? Ndio sifa mnazoziona za maana siku hizi?

Leo nimepita mahali nikakuta kuna ugomvi wa watu wanatoleana maneno(kusutana). Mnaweza mkafikiri ni wanawake eh? HAPANA! ni mwanaume tena mume wa mtu kaenda kumsaidia mke wake kusutana na Bi dada mmoja ambaye anauza duka hapo.

Karibia kila mtu aliyekuwa anashuhudia lile alisikitika sana na kuona aibu kwa ile misuto mwanaume tena mume wa mtu aliyokuwa anaitoa.

Wanaume wenye hizi tabia badilikeni mnakera na kuaibisha sana. Tafuteni hela mpenzi wako akigombana huko mnaenda police na sio unaenda kumsaidia kusutana.

Acheni kujitoa uwanaume wenu kwa vitu vya ajabu. Wanawake kwa wanawake kugombana ni kawaida ila kisicho kawaida ni mwanaume kuingilia ugomvi na kusutana.

Mwanaume unayesutana na mwanamke au hata kutupia maneno wanaume wenzako unajishusha sana. Unadhalilisha nguvu ya manhood iliyowekwa ndani yako. Mwanaume pesa maneno maneno tuachieni sisi wanawake.
 
Kingine ni kwamba wanaume wengi siku hizi ndo wanaongoza kwa umbea. Sijui ni kuchoka kuwa wanaume wanatamani wawe wanawake au ni nini.

Mwanaume kuwa mbea mbea pia haipendezi kabisa. Unakuta mwanaume na yeye hataki kupitwa na jambo. Ana maumbea kama yote na anaona ni sawa.
 
Binadamu yeyote ni mbea, inategemea ni mada gani zinamvutia....

Nadharia ya kwamba wanaume sio wambea mmekaririshwa tu, ni gender stereotype.

Wanaume wakiongelea wacheza mpira sio umbea, ila wanawake wakiongelea mambo yanayowahusu kama vicoba ni umbea. Si unaona?
 
Za weekend?

Hivi mwanaume timamu kabisa mke wako kagombana huko na wanawake wenzake halafu wewe unaenda kuingilia ugomvi na kuanza kusutana na wanawake?

Kwanza mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kurushiana maneno na mtoto wa kike? Mpenzi wako akiudhiwa huko na marafiki zake wewe msaada unaoweza kumpatia ni kwenda na wewe kusutana? Hapo ndio unaonesha Manhood yako? Ndio mkitoka hapo akuambie "safi sana mpenzi wangu umewasuta mpaka wamekoma"? Ndio sifa mnazoziona za maana siku hizi?

Itakuwa version ile ya wapaka makeup, watoboa pua, na masikio,wavaa vikuku hasa huko daslam sie huku kijijini tunashinda shambani huo muda wa umbea na kusutana twatoa wapi.
 
bodaboda na madalali wa mtahani hao acha kabisa unaweza kuta wanajua habari zako kuliko hata wewe unavyojua.
 
Binadamu yeyote ni mbea, inategemea ni mada gani zinamvutia....

Nadharia ya kwamba wanaume sio wambea mmekaririshwa tu, ni gender stereotype.

Wanaume wakiongelea wacheza mpira sio umbea, ila wanawake wakiongelea mambo yanayowahusu kama vicoba ni umbea. Si unaona?
Mpira sio umbea. kujadili mpira sio umbea. Umbea mbona upo wazi kabisa?
 
Itakuwa version ile ya wapaka makeup, watoboa pua, na masikio,wavaa vikuku hasa huko daslam sie huku kijijini tunashinda shambani huo muda wa umbea na kusutana twatoa wapi.
Wengine unakuta hata hawajatoboa masikio wala hawapaki make up ila ni ujinga tu kudhani kusutana na maadui wa mpenzi wake ndio uwanaume. Ukimuoana unaweza sema mwanaume ndio huyu sasa, ngoja umkute kwenye misutano utasikitika.
 
Za weekend?

Hivi mwanaume timamu kabisa mke wako kagombana huko na wanawake wenzake halafu wewe unaenda kuingilia ugomvi na kuanza kusutana na wanawake?

Kwanza mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kurushiana maneno na mtoto wa kike? Mpenzi wako akiudhiwa huko na marafiki zake wewe msaada unaoweza kumpatia ni kwenda na wewe kusutana? Hapo ndio unaonesha Manhood yako? Ndio mkitoka hapo akuambie "safi sana mpenzi wangu umewasuta mpaka wamekoma"? Ndio sifa mnazoziona za maana siku hizi?

Leo nimepita mahali nikakuta kuna ugomvi wa watu wanatoleana maneno(kusutana). Mnaweza mkafikiri ni wanawake eh? HAPANA! ni mwanaume tena mume wa mtu kaenda kumsaidia mke wake kusutana na Bi dada mmoja ambaye anauza duka hapo.

Karibia kila mtu aliyekuwa anashuhudia lile alisikitika sana na kuona aibu kwa ile misuto mwanaume tena mume wa mtu aliyokuwa anaitoa.

Wanaume wenye hizi tabia badilikeni mnakera na kuaibisha sana. Tafuteni hela mpenzi wako akigombana huko mnaenda police na sio unaenda kumsaidia kusutana.
Acheni kujitoa uwanaume wenu kwa vitu vya ajabu. Wanawake kwa wanawake kugombana ni kawaida ila kisicho kawaida ni mwanaume kuingilia ugomvi na kusutana.

Mwanaume unayesutana na mwanamke au hata kutupia maneno wanaume wenzako unajishusha sana. Unadhalilisha nguvu ya manhood iliyowekwa ndani yako. Mwanaume pesa maneno maneno tuachieni sisi wanawake.
Palina unasemaje nisiwe nakusaidia au yetu hayawahusu😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom