Haji Manara kaacha ndara (ndala) mbele ya John Heche

Haji Manara kaacha ndara (ndala) mbele ya John Heche

Kuna swali moja ameulizwa heche kuwa nchi nyingi za kiafrika zimeingiza Serikali za pinzani lakini hakuna chochote kilichobalika je wao wataweza vipi,naona heche mwenyewe hakulijibu kwa usahihi.
 
Hehe na hao watangazaji wametofautiana katika kiwango cha kufahamu mambo,Heche anawazidi katika kufahamu mambo mengi zaidi yao lazima Manara na wenzake wangeonekana hovyo.

Waandishi wamebobea katika masuala ya mpira na udaku unampeleka kuhoji issue za politics lazima atafeli tu.

Ni sahihi Kabisa.
 
Aiseeh!

Haji Manara ni muongeaji mzuri Sana. Na mwenye uwezo mkubwa hasa akikutana na watu wajingawajinga, wenye uelewa Mdogo.

Umaarufu na nguvu yake kuu ya kuongea ipo kwenye udhaifu wa wanaomsikiliza na anaokutana nao head by head. Wengi amewatoa nishai kwa sababu zifuatazo;

1. Haji Manara ni muongeaji mno mwenye uswahili ndani yake
Kwenye uongeaji wake hutumia mbinu ya maneno ya shombo na vikejeli vya hapa na pale Jambo ambalo huwafanya opponents wake kupoteza mhimili kwani wanakuwa too emotional au wanapoteza kujiamini.

2. Pili, Manara hutumia mbinu ya Victims na kujifanya mhanga ila yeye akikushambulia anakuja full. Hii inawafanya anaopambana nao wawe wamefungwa mikono. Kwani hawajiachii moja kwa moja.

3. Haji Manara hutumia mbinu ya kujifanya mtoto mjini na mtu mwenye connection ndefu. Hii huwatisha opponents wake wengi.
Kwani wengi huogopa watoto wa mjini.

Katika mechi ambazo Haji Manara kazicheza amepoteza Mechi Mbili tuu.
Mechi ya Kwanza ni Ile Aliyocheza na Jerry Muro. Ambapo Jerry yeye alifunguka na kurusha missile huku akikataa kufungwa mikono.
Hapa Manara aliacha Ndala( ndara) akaishia kulalamika na mashabiki na waamuzi waliingilia kati wakimtetea.

Jana Haji kama kawaida Yake akiwa na uzoefu Mkubwa wa mapambano ya kupepeta mdomo, kupangua hoja, kujenga hoja, kushusha vimondo na kejeli za hapa na pale.
Akiwa na uhakika na KAZI yake.

Manara hakuamini alipojikuta katika Hali ngumu dhidi ya Opponent wake John Heche.

John Heche alikuwa akiyajibu maswali na hoja za Manara kwa namna ambayo Manara mwenye hakuitarajia licha ya mbinu alizotumia Manara kama kawaida yake kumjaza Na kumpandisha Heche Sukari.
Lakini Heche alikuwa Mtulivu mwenye kujua nini anatakiwa kufanya kwa watu wa karba ya Manara.

Hatimaye Manara alijikuta akiacha ndara na akiondoka na ONYO kuwa HUKU USIJE yaani kwa vijana wa Chadema ni kumfuata Mamba kwenye kina kirefu.

Siri kuu ya kupambana na Vijana wa Chadema unapokuwa nao kwenye mahojiano;

1. Epuka Uchawa.
2. Ongea Ukweli.
Kwa sababu ukiongea ukweli automatic utaonekana uko smart.

3. Kama kuna sehemu serikali inakosea usikatae sema ni kweli. Lakini elezea namna serikali inavyohangaika kupambana na kukosea kwake huku nawe ukitoa maoni ya jinsi ya kurekebisha.

4. Tafuta Makosa ya Chadema yataje ili kumfanya opponent wako atumie muda mwingi kujitetea katika Makosa. Kumbuka kujitetea katika Makosa ndio Uchawa wenyewe.
Hata hivyo Opponent wako pia anaweza kuku neutralise hoja yako kwa kukubali Makosa ili asitumie muda mwingi kujitetea.

Huku usije utaacha ndala athee!
Haji Manara si chochote si lolote
 
Mkuu Lisu ni moja ya watu ninaowakubali Sana lakini ninakuhakikishia kwenye Mahojiano Heche anautulivu Sana kuliko Lisu.

Lisu anaudhaifu wa hasira, Lisu anaudhaifu wa dharau Fulani hivi, ni rahisi kuonyesha dharau endapo utamuuliza swali chini ya kiwango na akashindwa kutoa majibu strong

Heche anauwezo wa kujidhibiti kuliko Lisu.

Sio rahisi Heche umkamate kwa Hotuba zake Kwa sababu anaweza kujizuia. Lakini kwa Lisu kumkamata ni rahisi Sana.

Kama ni kwenye Mpira.
Heche anacheza mpira kama Gaucho yaani hatumii nguvu au Kama Messi.
Wakati Lisu anacheza Mpira kama Ronaldo CR7 . Anatumia nguvu
sio kweli kwahili ninakua kushoto
 
Heche anautulivu mkubwa ambao Hata Lisu anatakiwa auige.
Lisu ni mzuri kwa kujua mambo mengi lakini ni rahisi kumjaza sukari akapoteamo kwa sababu lisu pia anahasira
Looh!

Yaani unamlinganisha mwalimu na mwanafunzi wake? Really?

Wewe hujuilizi, ni kwanini serikali imemtumia Lazarus Chakwera kumfuata mfungwa Tundu Lissu gerezani ili ku - negotiate naye ili inagalau mambo yao (serikali haramu) yawaendee vizuri??

Hii mimi nimeiona kwa Tanzania vs Tundu Lissu tu na kile tunachosoma ktk historia kati ya Serikali ya Makaburu wa South Africa vs Nelson Mandela..

Sijaona kwingine..

My point is:

Acha kumlinganisha John Heche na Tundu Lissu kwa sbb Heche ni mwanafunzi wa TL na anaendelea kujifunza kwake ndio maana ktk huu mwaka wote mwenyekiti wake akiwa gerezani, hakukubali kununulika ili kutunza heshima na utu wa mwenyekiti wake.

Uadilifu ni tabia ya Tundu Lissu na John Heche kaichukua hiyo na ndiyo pona pona ya CHADEMA kuwa kama CUF au NCCR MAGEUZI..!
 
Mkuu Lisu ni moja ya watu ninaowakubali Sana lakini ninakuhakikishia kwenye Mahojiano Heche anautulivu Sana kuliko Lisu.

Lisu anaudhaifu wa hasira, Lisu anaudhaifu wa dharau Fulani hivi, ni rahisi kuonyesha dharau endapo utamuuliza swali chini ya kiwango na akashindwa kutoa majibu strong

Heche anauwezo wa kujidhibiti kuliko Lisu.

Sio rahisi Heche umkamate kwa Hotuba zake Kwa sababu anaweza kujizuia. Lakini kwa Lisu kumkamata ni rahisi Sana.

Kama ni kwenye Mpira.
Heche anacheza mpira kama Gaucho yaani hatumii nguvu au Kama Messi.
Wakati Lisu anacheza Mpira kama Ronaldo CR7 . Anatumia nguvu
Lissu sio kwamba ana hasira, ile style ya kuongea kama jazba fulani ni hulka yake tu. Inaonekana kama panicking kwa sababu ule msemo wa "funika kombe mwanaharamu apite" Lissu umempiga chenga. Jamaa hata kama ni kitu kidogo tu kupotezea hawezi. Yeye nyeusi atasema hii nyeusi. Nyekundu atasema hii nyekundu
 
Back
Top Bottom