Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,780
- 7,905
Kitendo cha Manara kuitisha Press Conference na kuizungumzia Yanga kwa Lugha za kushurutisha timu dhidi ya TFF na Rais wa TFF bila kuwepo msemaji wa Yanga Alikamwe, ni kuivunja heshima Yanga. Yanga ni taasisi yenye heshima nchini ikijihusisha na Soka na bidhaa za soka, lakini kitendo alichokifanya Manara ni kama kuigombanisha Yanga na TFF, malalamiko ya Manara yanaonekana yanalenga moja kwa moja Uongozi wa Rais wa TFF. Hapa nchini hakuna Timu kubwa kuliko Shirikisho la Moira wa miguu la Tanzania, kitendo cha Manara kutaka Yanga iweze kuishurutisha TFF ni kuvunja miiko ya soka nchini.
Manara kabla ya kutoka Simba alitifuana vikali na viongozi wa Simba ikiwemo Barbra Gonzales aliyewahi kuwa CEO wa Simba, mitandaoni palichafuka sana kiasi cha kupelekea Haji Manara kuachishwa/Kuacha kazi Simba na kupokelewa Yanga, ambapo ndani ya sakata hilo TFF walimfungia Haji Manara kuacha kujihusisha na mpira kwa muda uliopangwa. Haji Manara baada ya kuamia Yanga alisikika voice notes akimkashifu Rais wa Yanga "Engineer Hersi" pamoja na aliyewahi kuwa kocha wa Yanga ndugu "Gamondi" kuwa ni watu wabaya sana, na akazungumza maneno mengi mabaya dhidi yao ambapo baadae mambo yaliisha juu kwa juu.
Jana haji manara tena karudia kosa la kuitisha press conference na kuzungumza timu ya Yanga kwa kuichafua TFF na uongozi kwa jumla kana kwamba katumwa na timu au nyuma yake wapo watu au ni shida ya kukubaliana na hali ya kuwa muda wa kutumikia soka kama msemaji umeisha. Video hiyo hapo chini,
View: https://youtu.be/7zJwAv6EPHs?si=Iywzb280GQjNM7DP