Haiwezekani Air Tanzania iwe na ndege inayotoza Tsh. 100,000/- kwa safari za ndani?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,591
4,279
Hivi haiwezekani ATC iwe na ndege ambayo kwa mfano itacharge shs 100,000/- kwa safari za ndani ya nchi na iwe maalum kwa viwanja vyenye abiria wa kujaza ndege.
Mfano: Mwanza, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma (hata mara 4 kwa siku).

Mbadala wake, waruhusu mabasi yatembee usiku; namaanisha yaanze safari kati ya saa kumi na mbili jioni (18h00) na saa mbili (20h00) jioni hivi; Ili yafike yanakokwenda Asubuhi. Ile ya kuanza safari sijui saa kumi na moja alfajiri (05h00) haisaidii sana, labda kwa kama 15% tu

Ukweli tunapoteza muda mwingi sana barabarani. Chukua mabasi 500 yanatembea mchana kutwa. Ina maana kuna karibia 25,000 hawafanyi kazi mchana kutwa.
 
Dar to Kigoma nauri iwe laki moja labda kwa usafiri huu
FB_IMG_1686736922692.jpg
 
Laki 1 ni only Dar to Znz…

Arusha to Dar laki 1 famchezo nini 😂

Wacha tusafiri na bus usiku… kesho naijaribu safari ya usiku.
Kesho unajaribu safari ya kwenda wapi? Sasahivi ni mikoa mingapi ina safari za usiku? Nimesikia mwanza tu
 
Laki 1 ni only Dar to Znz…

Arusha to Dar laki 1 famchezo nini 😂

Wacha tusafiri na bus usiku… kesho naijaribu safari ya usiku.

Ndege ya kawaida ya Abiria 170 inaweza kufanya safari 6 kwa siku (mchana) ambapo ikicharge shs 100,000 inaweza kupata angalau shs 80,000,000 kwa siku. Wangetuambia pia na gharama za uendeshaji kwa siku ukizingatia mafuta ya ndege ni bei poa kuliko ya magari ili tuone kweli haiwalipi
Kwa sasa kwenye hizo route kuu wameweka route chache sana kwa kuwa watu hawafiki bei hivyo ndege hazijai; Hata najiuliza madege yote hayo yamenunuliwa yapo wapi.....
 
Hivi haiwezekani ATC iwe na ndege ambayo kwa mfano itacharge shs 100,000/- kwa safari za ndani ya nchi na iwe maalum kwa viwanja vyenye abiria wa kujaza ndege.

Mfano: Mwanza, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma (hata mara 4 kwa siku).

Mbadala wake, waruhusu mabasi yatembee usiku; ili yafike yanakokwenda asubuhi.

Ukweli tunapoteza muda mwingi sana barabarani.

Chukua mabasi 500 yanatembea mchana kutwa. Ina maana kuna karibia 25,000 hawafanyi kazi mchana kutwa.
Fast jet waliweza hawa wengine wanashindwaje!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom