Hadithi ya umslopagaas

Hadithi ya umslopagaas

tukatambua ya kuwa mto ulikuwa chini ya ardhi, na sasa umetokea tena, nao unapita katikati ya magenge marefu kadiri ya futi elfu mbili kwenda juu.

Juu sana tuliona mbingu ni nyeupe, lakini hapo tulipo ni nusu giza, kama katika chumba kilichofungwa milango na madirisha wakati wa mchana. Inaendelea ilipoishia...

Kando ya maji palikuwa na ukingo upana wa yadi saba au nane wenye mawe yaliyoviringana kwa kusukumwa na maji.

Basi, tulikusudia kuteremka hapa ili tupumzike kidogo baada ya hatari zote zilizotupata, na kuvinyoosha viungo vyetu.

Mahali hapa palikuwa pa kutisha sana, lakini panafaa kupumzikia katika hatari na vitisho vya mto, na kutupa nafasi ya kupanga vizuri vitu vilivyomo mtumbwini.

Basi, tulichagua mahali, tukaupweleza mtumbwi kwa shida, kisha tukateremka katika mawe yale.
Bwana Good alishuka ukingoni kwanza, akasema kwa sauti kubwa, ‘’Lo, ama mahali hapa pabaya mno! Panatosha kumtia mtu kifafa,’’ akacheka.

Mara ile sauti kubwa ilikariri maneno yake, ikayazidisha mara nyingi sana. ‘’Kifafa ho!ho!ho!- Kifafa ho!ho!ho!’’ na sauti nyingine ikaitikia juu sana katika genge, ‘’Kifafa! Kifafa! Kifafa!’’ na sauti ilifuata, sauti ikachanganyika pamoja na sauti ya kucheka, mpaka mahali pote palilia, kisha ikatulia tena ghafla kama ilivyoanza.

Umslopogaas akasema kwa utulivu, ‘’Ah! Naona ya kuwa mashetani wako hapa, na kweli mahali hapa paonekana kama ni mahali pa mashetani.’’ Nilijaribu kueleza ya kuwa sauti zile tulizozisikia ni mwangwi tu, lakini hakusadiki.

Akasema, ‘’La mimi naweza kuutambua mwangwi niusikiapo. Mmoja ulikaa karibu na nyumba yangu huko katika nchi ya Umla na vijana wa kike walizoea kuongea nao. Lakini kama huu ni mwangwi, basi ule wa kwetu ulikuwa mtoto wa mwangwi tu! La, la, ni mashetani.

Lakini hata hivi naona si mashetani kitu,’’ akanusa tumbako, ‘’wanaweza kukariri maneno ya mtu, lakini hawawezi kusema maneno yao wenyewe, tena, hawathubutu kujionyesha’’. Akanyamaza, kama kwamba anawadharau mashetani hao.

Baada ya hayo tuliongea kwa sauti ya kunong’ona, maana tulichukizwa kusikia kila neno tunalolisema linatupwa huko na huko kama mpira katika mchezo.

Lakini hata sauti za kunong’ona zilitambaa katika magenge kama sauti za siri, mpaka zilipofifia kama mivumo ya upepo.

Mara tulipotua juu ya mawe yale, tuliyaosha na kuyaganga majeraha yetu ya kuunguzwa moto kadiri tulivyoweza.

Tulikuwa na mafuta kidogo kwa taa yetu, kwa hivi hatukuweza kuyatumia kuyatibu majeraha yetu, basi, tulimnyonyoa bata mmoja, tukatumia mafuta ya kidari chake, yakatufaa sana.

Kisha, tuliviweka vitu vyetu vizuri katika mtumbwi, tukaanza kula, nasi tulikuwa na njaa sana ya chakula, maana tulikuwa tumezirai kwa muda wa saa nyingi, na sasa ilipata saa sita.

Basi, tulikaa tukaanza kula nyama baridi, lakini tulikuwa dhaifu tukataka tutapika, tena, vichwa vilituuma kwa ajili ya taabu za usiku.

Halafu kidogo. Niligeuka nitazame nyuma yangu, nimevutwaa na sauti niliyosikia kama kwamba kitu kinatambaa juu ya mawe, nikaona kaa mkubwa sana wa maji baridi amekaa juu ya mwamba. Alikuwa mkubwa sana kama bata watano kiasi cha bata wakawaida.

Mnyama huyu wa kuchukiza alikuwa na macho yaliyotokeza, yakawa kama yananiangalia, tena, alikuwa na mikono mirefu na magando makubwa sana.

Basi, hapo wanyama wengi kama huyo walitoka kila upande, labda walivutwa na harufu ya chakula, wakatoka nyuma ya mawe na katika matundu ya mwamba.

Wengine walitukaribia sana. Mara ile mmoja alimuuma Bwana Good kwa nguvu sana, akalia kwa sauti kubwa, kisha kwa mara nyingine tena mwangwi uliirudiarudia sauti ile.

Umslopogaas alilitwaa shoka lake akamvunja Yule kaa, na mara ile Yule kaa alilia kwa sauti kubwa, na mwangwi uliirudisha sauti yake iliyo chukiza sana. Mara akaanza kutoa povu kinywani, na wengi wengine wakaja kutoka kila mahali.

Wale walipoona ya kuwa mwenzao ameumia, walimrukia wakaanza kumraruararua kwa magando yao makubwa, wakavitia vipande vya nyama yake vinywani mwao.

Basi, tulishika vitu vyovyote tulivyoweza kupata, tukaanza kupigana nao. Walizidi kujazana tele, wakatoa harufu mbaya sana.

Kila tulipomuua mmoja, wenziwe walimrukia wakamraruararua na huku akitoa povu kinywani mwake tena kila walipopata nafasi walituuma na sisi pia, wakajaribu kuiba chakula chetu.

Mmoja mkubwa sana alimrukia bata mmoja tuliyemnyonyoa, akajaribu kumchukua, na mara ile wengi sana walijitupa juu yake wakaanza kulialia na kutoa povu vinywani wakaila nyama yake na huku wakiraruana pia.

Basi, hapa Bwana Good akasema, ‘’Haraka tuondoke hapa au kweli tutashikwa na wazimu.’’

Basi, tuliusukuma mtumbwi wetu ambao ulizungukwa na wanyama hao wengi sana, tukaushusha mtoni, tukaingia ndani, tukatoka pale tukawaacha wanyama hao wanalialia na kutoa povu linalo nuka vibaya.

Umslopogaas akasema, ‘’Wale ni mashetani wa mahali hapa.’’ Na sisi tulielekea kuyakubali maneno yake.

Sir Henry akasema, ‘’Na sasa tutafanya nini?’’ Nikajibu, ‘’Tuache mtumbwi uchukuliwe na maji tu.’’ Basi, tukauacha uchukuliwe tangu mchana hata jioni, wala hatuna habari kuwa usiku unaingia kwa sababu ya giza la mahali hapo, mpaka Bwana Good alipoonyesha juu tukaona nyota angani.

Basi, kwa kuwa hatuna la kufanya, tulikaa tukiiangalia ile nyota, na mara ilitoweka, na giza likazidi tena, tukaanza kusikia muungurumo wa maji tena, nikaguna nikasema, ‘’Tumeingia chini ya ardhi tena.’’ Nikaangaza taa.

Ndiyo, bila shaka, tumekwisha ingia chini tena tukaweza kuona mwamba wa juu ya mto. Basi usiku mwingine wa hatari na hofu ukaanza.

Sitaweza kuyaeleza mambo yaliyotokea tutachoshana tu, basi, yatosha kusema ya kuwa ilipopata karibu na saa sita ya usiku, tulipiga mwamba uliotokeza katikati ya mto, tukawa karibu kupinduka na kutoswa majini.

Lakini tuliwahi kuutoa mtumbwi na kuendelea tena. Basi, hivi saa zilipita mpaka karibu na saa tisa.

Sir Henry na Bwana Good walikuwa wamelala, wamechoka kabisa, na Umslopogaas akawa amekaa mbele ameshika pondo, na mimi, nilikuwa nikiuongoza mtumbwi.

Mara nilimsikia Umslopogaas anatoa sauti, na mara ile nilisikia sauti ya kucharuka kama kwamba kitu kinapenya katika matawi ya miti, nikaona ya kuwa mtumbwi wetu unapenya kwa nguvu katika miti na matawi yanayotambaa.

Kisha, nikaona upepo mzuri unaupepea uso wangu, nikajua kuwa tumetoka tena katika chini ya ardhi na sasa tunaelea juu ya maji wazi.

Sikuweza kuona kitu kwa macho yangu kwa sababu ya giza la usiku, lakini nilifurahi kuona tumekwisha toka katika mto ule wa kutisha. Basi, nilikaa nikivuta hewa nzuri katika mapafu yangu, nikayangoja mapambazuko kwa saburi nilivyoweza.
 
Walete mkuu!! We zishushe tu hata tatu
 
Hapa matumaini ya uhai yanaanza kupatikana. Tiririka tupo pamoja.
 
Na humu msimulizi mkuu ni Makumazahn wakati nasoma hiki kitabu miongo miwili na nusu iliyopita nilikuwa nadhania ni vitu vya uhalisia teh.
Yaah mzee allan ndio msimulizi mkuu wa mtunzi kama waonavyo wily gamba na musiba au beny mtobwa na joram kiango. Ukiisoma vyote viwili yaani version ya kiingereza na ya kiswahili utapata ladha tofauti ingawa napenda sana cha kiswahili maana mikwara yake inasomeka uzuri. Pia ukipata audio ya kingereza pia msimuliaje alijitahidi kuelezea kwa kuteka hadhra
 
SURA YA KUMI NA MOJA

Kwa muda wa saa nzima nilikaa tu nikiyangojea mapambazuko, na huku Umslopogaas pia alikuwa ameshikwa na usingizi.

Nikakaa mpaka upande wa mashariki ukageuka rangi ya kijivu, na ukungu ukatambaa juu ya uso wa maji kama vivuli vya mapambazuko yaliyo kwisha sahauliwa zamani, Ulikuwa unaotoka katika kitanda chake cha maji kuliamkia jua.

Kisha, rangi ya kijivu iligeuka ya manjano, na ya manjano ikageuka nyekundu.

Kisha, miali mizuri ya nuru ilitoka katika mbingu za mashariki, na sasa katikati yake dalili za mapambazuko zikaja mbio kama mishale, zikatawanya ukungu na vivuli na kuvigusa vilele vya milima ya mbali katika mwendo wake wa kuruka toka mlima mpaka mlima.

Ndipo milango ya dhahabu ikafunguliwa mbinguni na jua lenyewe likachomoza kwa utukufu na sherehe na uzuri na mng’ao wa mikuki mingi, likaufunika usiku kwa nuru na mwangaza, kukawa kweupe.

Mpaka sasa sikuweza kuona kitu ila mbingu zenye rangi ya samawati, maana ukungu mnene ulitanda juu ya uso wa maji, kama kwamba uso wake wote ulikuwa umefunikwa kwa utando wa pamba.

Lakini kidogo kidogo jua lilikunywa ukungu, ndipo nilipoona ya kuwa tunaelea juu ya ziwa kubwa la maji maangavu, ambalo kingo zake hazionekani.

Nyuma yetu kadiri ya maili kumi hivi, milima mirefu sana ilitanda upeo wa macho, ikafanya namna ya ukuta uliolizuia ziwa lile, nami sina shaka ya kuwa mto ule uliotuchukua unatoka mahali katika ukuta ule wa milima.

Na kwa hakika nilithibitisha habari hizi baadaye, na nguvu za mwendo wa mto ule zilikuwa dhahiri. Maana hata sasa mtumbwi wetu ulikuwa ukipelekwa mbele kwa nguvu za maji.

Halafu kidogo wenzangu waliamka, wakafurahi mno walipoona kuwa tumetoka katika mto ule wa kutisha, na sasa tuko chini ya mbingu za samawati tena.

Ndipo tulipochangamka tukaanza kuongea na kufikiri shauri la kufanya, tukakusudia kuutafuta ukingo wa ziwa, maana tuna njaa sana, wala hatuna kitu cha kula isipokuwa vipande vichache vya nyama kavu.

Tulikuwa tumepoteza chakula chote kilivyoliwa na wale kaa wa kuchukiza. Basi, sasa shida nyingine ikazuka.

Hatujui bado ukingo wa ziwa u wapi, maana hatuwezi kuona kitu ila utando mkubwa wa maji maangavu yenye rangi ya samawati na milima ile tulikotokea.

Lakini tuliona ndege maji wengine wanaruka toka upande wa kushoto, tukabahatisha ya kuwa wanatoka mahali pao kando ya ziwa wanapokula chakula ili wakashinde ziwani mchana, na kwa hivi tulielekea upande huo, tukaanza kupiga kafi.

Baada ya kupita kitambo, upepo ulianza kuvuma kwa nguvu na kutupeleka huko tulipotaka kuendeea.

Basi, tulitengeneza tanga kwa blanketi na mti, tukapelekwa mbele vizuri. Kisha, tulikula vile vipande vya nyama kavu vilivyosalia, tukanywa maji matamu ya ziwani, tukatia moto viko vyetu, tukangojea mambo yatakayotokea.

Tulipokuwa tumekwenda muda wa saa moja, Bwana Good ambaye alikuwa akitazama huko na huko kwa darubini, akasema kuwa anaweza kuona nchi kavu, akaeleza kwa kuwa jinsi rangi ya maji inavyobadilika inaonyesha kuwa tunakaribia mlango wa kuingilia mtoni.

Halafu kidogo tukaona kuba kubwa lenye rangi ya dhahabu linatokeza katika ukungu, na mara ile Bwana Good akatoa habari kubwa zaidi, yaani anaweza kuona mashua ndogo yenye tanga inatujia.

Habari hii, ambayo tuliweza kuihakikisha kwa macho yetu baadaye kidogo, ilitutatiza sana, yaani kufikiri kuwa wenyeji wa ziwa hii lisilojulikana wanajua jinsi ya kuendesha mashua kwa matanga.

Baada ya kupita muda kidogo ilikuwa dhahiri ya kuwa watu wale waliomo katika mashua wamekwisha tuona. Kwa muda kidogo walisita kama kwamba wanaona shaka, kisha, mashua ilitujia mbio mnoo.

Katika muda wa dakika kumi ilikuwa imekwisha tukaribia, na sasa ni mwendo wa yadi mia moja tu kutoka mtumbwi wetu, tukaona si mtumbwi ila ni mashua ndogo nzuri iliyoundwa kwa mbao, nayo ina tanga.

Lakini mara macho yetu yalivutwa kuwatazama waliomo ndani yake, ni mwanaume na mwanamke, nao rangi yao ni nyeupe, tulitazamana kwa ushangao tukifikiri macho yetu yamedanganyika, lakini sivyo, bila shaka ni kweli, hawakuwa weupe kama sisi, lakini hata hivyo si weusi.

Basi, kumbe, habari zile tulizozisikia zilikuwa kweli kabisa, nasi tumeongozwa kwa njia ya ajabu kuligundua lile taifa la watu weupe.

Nilitaka kupiga ukelele wa furaha nilipokumbuka ukuu wa ajabu ya jambo hili, tukapeana mikono, tukafurahi kwa sababu safari yetu imesitawi kupita tulivyoweza kutumaini.

Maisha yangu yote nilikuwa nimesikia tetesi tu ya habari za taifa hili la watu weupe wanaoishia katika milima ya ndani ya nchi hii kubwa, nikatamani kuwaona kwa macho yangu, mwenyewe na kuithibitisha habari na sasa nimekwisha waona nimetosheka kabisa.
 
Yule mwanaume aliyekuwa ndani ya mashua alikuwa ana umbo zuri, ila si zuri kupita kawaida ya wanadamu, na nywele zake ni nyeusi za singa, uso wake ni mng’avu na wa kipanga.

Alikuwa amevaa namna ya gwanda rangi ya kahawia na namna ya shuka, Fupi ya kitambaa kile kile miguu yake ilikuwa mitupu.

Katika mkono wake wa kuume na wa kushoto amevaa bangili nene za madini ya rangi ya manjano nikaikisia ni dhahabu.

Yule mwanamke alikuwa mzuri wa kupendeza, na macho yake ni makubwa, na nywele zake ni za kuviringana zenye rangi ya kahawia.

Mavazi yake ni ya kitambaa cha namna ile ile ya Yule mwanaume na baadaye nilipata kujua ya kuwa wanawake huvaa namna ya gwanda inayofika magotini.

Kisha kitambaa kirefu upana wake futi nne na urefu wake futi kumi na tano, kinachotandwa mwilini kwa mapindo ya kupendeza macho, na pindo lake lilitiwa rangi ya bluu au hudhurungi au rangi nyingine kulingana na cheo chake.

Vazi hilo hutupiwa begani na kuangukia mbele na mkono na ziwa la kuume huachwa wazi.

Mavazi hayo hupendeza sana hasa kama Yule aliyevaa ni kijana mzuri kama mwanamke huyu alivyokuwa.

Huko nyuma ilikuwa sisi tunawashangaa wao na wao pia wameshangaa zaidi kutuona sisi.

Yule mwanaume alikuwa kama kwamba ameduwaa kwa kuwa na hofu, na kwa muda alisita kuja karibu na mtumbwi wetu asiukaribie zaidi. Halafu kidogo alitukaribia, akaanza kutuita kwa maneno ya lugha yenye sauti nyororo ya kupendeza masikio, lakini hatukuweza kufahamu hata neno moja.

Basi tulimwita kwa Kiingereza na kwa lugha nyinginezo tulizozijua, lakini hakuweza kufahamu hata neno moja. Ikaonekana kwamba sauti zetu zinamtia ushangao zaidi.

Yule mwanamke alikuwa anatuangalia sana. Basi, alipoona kuwa hawezi kutufahamu aliigeuza mashua yake akaanza kuiendea ng’ambo ya ziwa, na mashua yake ilikwenda mbio kama mbayuwayu.

Nikasema, ‘’Ni dhahiri Yule mtu atarudi upesi pamoja na wenzake, basi afadhali tufanye shauri jinsi tutakavyo wapokea.’’

Sir Henry akasema, ‘’Mimi naona hakuna shauri ila jinsi wao watakavyo tupokea sisi’’
Bwana Good hakusema neno, ila alianza kushughulika na kutoa sanduku la chuma katika mizigo yetu.

Sir Henry akamuuliza, ‘’Je, unataka kufanya nini sasa?’’
Akajibu, ‘’Nataka kuvaa sasa. Je, wataka nionekane katika nchi mpya hali nimevaa nguo hizi?’’ Akaonyesha nguo zake jinsi zilivyokuwa zimechakaa na kuchafuka.

Basi, tulilishusha tanga, tukaoga ziwani tukarudi mtumbwini tena tumeburudishwa kabisa, tukakaa tukaota jua, na Bwana Good alilifungua sanduku lake akatoa nguo safi zake za kimanowari akazivaa.

Tulipomwona amevaa hivyo, sisi pia tuliona hamu ya kubadili nguo zetu, tukaanza kujitengeneza kadiri tulivyoweza, huku nyuma tulikuwa tunaikaribia ng’ambo ya ziwa polepole, maana mara tulipokwisha oga, tulilitweka tanga tena.

Baada ya saa moja na nusu tangu tulipoachana na Yule mtu, tuliona namna ya jahazi na mashua nyingi zinatoka mtoni au bandarini. Katika vyombo hivyo kimoja kilikuwa kikiendeshwa kwa makasia ishirini na manne, lakini vingi katika vile vingine viliendeshwa kwa matanga.

Tulipoangalia kwa darubini, tuliona ya kuwa kile chombo kinaendeshwa kwa makasia kinaonekana kama kwamba ni chombo cha serikali, maana mabaharia zake wote wamevaa mavazi ya namna moja na mwanaume mzee mwenye ndevu nyeupe ndefu alikuwa amesimama mbele juu ya sitaha kama ni mkubwa wa chombo, nae amevaa upanga kiunoni.

Ni dhahiri watu waliomo katika vyombo vingine wamevutwa kwa udadisi, nao walikuwa wanatujia upesi walivyoweza.

Nilisema, ‘’Sasa tutaona Je, watakuwa marafiki au watatumaliza?’’ Hapana aliyeweza kujibu swali hilo, tukaona shaka kwa jinsi Yule mzee mwenye upanga alivyoonekana kuwa mtu wa vita.

Ndipo Bwana Good alipoona kundi la viboko majini kadiri ya yadi mia mbili toka mahali tulipo, akasema kuwa labda ni shauri jema kuwaonyesha wenyeji wale nguvu zetu kwa kuwapiga viboko hawa, yaani ikiwezekana.

Kwa bahati mbaya, hata na sisi tuliona ni shauri jema, basi, tulitwaa bunduki zetu kubwa tukaanza kujiweka tayari. Walikuwapo viboko wanne, dume mkubwa mmoja jike mmoja na watoto wakubwa wawili.

Tuliwakaribia bila udhia, na wale wanyama wakubwa walikuwa kama hawashuku hatari, walizama na kuibuka tena mbali kidogo tu, na kwa hakika niliona ni ajabu jinsi walivyokuwa kama wamefugwa. Basi, vyombo vile vilipotukaribia kadiri ya yadi mia tano.
 
Sir Henry alianza, akampiga mtoto wa kiboko. Risasi ilimpata katikati ya jicho, ikapita katika kichwa chake ikamuua akazama na kuacha mstari mrefu wa damu majini.

Mara ile mimi nilimwelekezea Yule jike, na Bwana Good alijaribu kumpiga Yule dume.

Risasi yangu ilipiga, lakini haikumuua, na Yule kiboko alizama kwa kishindo kikubwa, akaibuka tena akinguruma na kutoa pumzi kwa nguvu, na kuyatia maji yaliyomzunguka rangi ya damu yake. Ndipo nilipompiga risasi nyingine nikamuua.

Lakini Bwana Good hana shabaha hata kidogo! Alikikosa kichwa cha Yule dume, na risasi yake ikampaza tu uso alipokuwa akipita.

Nilipoangalia baada ya kupiga ile risasi ya pili, niliona kuwa wale wenyeji hawana habari za bunduki, maana vishindo vyake na jinsi viboko wale walivyopigwa viliwajaza ushangao na fadhaa. Watu wengine walilia kwa sauti za hofu na wengine walianza kurudi nyuma haraka.

Hata Yule mzee mwenye upanga alikuwa kama kwamba ameduwaa na kuona hofu, akakisimamisha chombo chake.

Lakini hatukupata wasaa kutazama sana, maana mara ile Yule kiboko dume aliyekuwa amekasirika sana kwa ajili ya jeraha lililompata, aliibuka tena karibu nasi, akatutazama kwa ukali mno.

Sote tulipiga bunduki zetu, tukampiga huko na huko, akazama tena amejeruhiwa vibaya. Sasa udadisi ulikuwa umewashika wenyeji wale ukauondoa woga wao, na wengine walitukaribia zaidi, na miongoni mwao ni Yule mwanaume na mwanamke tuliowaona kwanza.

Hao walitukaribia sana. Mara ile Yule kiboko dume aliibuka karibu na mashua yao, akakifunua kinywa chake, akanguruma kwa ghadhabu, akaishambulia mashua yao.

Yule mwanamke akapiga yowe, na Yule mwanaume akajaribu kuipeleka mashua upande, asiweze. Basi, sasa kinywa kikubwa chekundu cha kiboko chenye meno yanayong’aa kiliiuma mashua ile ndogo, kikaimega kipande kikubwa cha ubavu wake, na kuipindua.

Basi, mashua ilizama, na watu wale walibaki wanatapatapa majini. Kabla hatujaweza kufanya jambo la kuwaokoa, Yule mnyama mkali aliibuka tena, akamshambuli kinywa wazi Yule mwanamke aliyekuwa akishindana na maji.

Mara kinywa chake kilipotaka kumuuma, nililenga bunduki yangu, nikapeleka risasi juu ya kichwa cha Yule mwanamke, ikaingia sawasawa kinywani mwa Yule kiboko.

Lo! Alipinduka, akaanza kuzunguka zunguka majini na huku anakoroma na kutoa damu nyingi puani, kabla hajajiweza tena, nilimpiga upande wa shingo, na risasi ikamuua.

Hakujimudu hata kujisogeza tena akazama pale pale. Sasa ikawa kazi ya kumwokoa Yule mwanamke, maana Yule mwanaume alikuwa ameogelea mpaka katika chombo kingine, tukamtoa katika maji tukamvutia katika mtumbwi wetu, na huku watu wanapiga kelele. Yule mwanamke alikuwa amechoka na kuogopa lakini hakuumia.

Huku nyuma vyombo vilikuwa vimesongana mahali pamoja, na wenyeji waliogopa sana, tukatambua kuwa wanashauriana.

Tulifikiri labda shauri lao litakuwa baya kwetu, kwa hivi tulizishika kafi zetu tukapiga kuwaendea mbele ili wasipate nafasi kulimaliza shauri lao.

Vyombo vingine vilirudi nyuma, na vingine vilikaa palepale, na kile cha Yule mzee kikaja kutulaki.

Halafu tukiwa karibu sana, nikaona ya kuwa ameshangaa kutuona namna tulivyo, tena anaona hofu kidogo. Alikuwa amevaa mavazi kama yale ya Yule mtu tuliyemwona kwanza, isipokuwa ngwanda lake ni la kitambaa cheupe chenye mapindo ya hudhurungi.

Bwana Good alivua kofia yake kumwamkia, akasema naye kwa Kiingereza, na Yule mzee aliviweka vidole viwili mdomoni mwake, tukafahamu ni namna yao ya kuamkia, kisha alianza kusema maneno kwa sauti nzuri laini.

Lakini tulifanya ishara kumjulisha ya kwamba maneno yake hatuwezi kuyafahamu. Basi, hapa hatukuweza kufanya neno, nami kwa kuwa niliona njaa nikafikiri nimjulishe hivi, nikakifungua kinywa changu nikakielekeza kidole, kisha ninalisugua tumbo langu.

Basi, Yule mzee alizifahamu ishara hizo, hapo akakielekeza kidole chake bandarini, na mtu mmoja katika chombo chake alitutupia kamba akatuashiria tuifungie mtumbwini mwetu, tukaifunga.

Basi chombo kile kikakivuta chetu kuiendea bandari kwa wepesi na vyombo vingine vilitufuatia.

Baada ya dakika ishirini tulifika mlangoni pa bandari, tukaona imejaa vyombo vilivyojaa watu waliokuja kutuangalia.

Tuliona ya kuwa watu wote ni wa namna ile ile, ila wengine ni weupe kupita wenzao. Basi baada ya kwenda mbele kidogo, mto ulipinda tukafanya sauti ya furaha na ya kushangaa, maana mbele yetu tuliona kwa mara ya kwanza mji wao ambao baadaye tuliambiwa unaitwa Milosis.

Mwendo upatao yadi mia tano tukafika kando ya mto, palikuwa na genge la miamba lililopanda ghafla kadiri ya futi mia mbili, na sehemu ya mbele ilitengenezwa iwe magadi ya vyombo.

Juu ya genge hilo palikuwa na jumba kubwa sana ambalo limejengwa kwa mawe ya namna ile ile ya miamba ya genge lile.

Jumba hilo lilikuwa limejengwa katika pande tatu za kiwanja chenye umbo la mraba, na upande wa nne wa kiwanja ulizibwa kwa ukuta mrefu wenye mlango mdogo tu wa kuingilia kiwanjani.

Baadaye tuligundua ya kuwa jumba hilo ni la malkia wawili wa nchi hii. Nyuma ya jumba, mji ulikuwa katika mwinuko wa mlima unaopanda taratibu mpaka juu yake, na huko palikuwa na jumba jingine la marumaru nyeupe lenye kuba ya dhahabu juu yake, ndilo kuba tuliloliona tulipokuwa tupo mbali bado.

Nyumba zote za mji zilijengwa kwa mawe mekundu isipokuwa jumba hilo, nazo zilikuwa zimepangwa kwa utaratibu na njia zake zilikuwa pana, nzuri.

Kadiri, tulivyoweza kuona, nyumba zote zilikuwa hazina ghorofa, na kila moja ilisimama peke yake imezungukwa na bustani.

Nyuma ya jumba la malkia, palikuwa na njia pana sana iliyopanda ule mwinuko kwa mwendo wa maili moja na nusu, mpaka kufikia kiwanja kilichokuwa mbele ya jumba lile la marumaru nyeupe lililosimama juu ya mlima.

Lakini mbele ya macho yetu tuliona kitu cha ajabu cha Milosis, ndiyo ngazi kuu ya kupandia genge mpaka jumbani kwa malkia, ambayo uzuri wake ulitushangaza sana.

Kutoka upande huu mpaka upande huu wa ngazi, ulikuwa uzio wa futi sitini na tano nayo ilikuwa imejengwa sehemu mbili; kila sehemu ilikuwa na vipandio mia moja na ishirini na tano, na kila kipandio kilikuwa cha mawe ukubwa wake inchi nane kwenda juu na futi tatu kwa upana.

Kweli ngazi hiyo ilikuwa kazi kubwa ya ustadi nasi tuliambiwa ya kuwa ngazi ilianzishwa zamani sana, ikaachwa mara nne kwa muda wa miaka mia nyingi kwa sababu wale waliojaribu kuijenga walishindwa, hata kijana mmoja jina lake Rademas alisema ya kuwa ataijenga, ama sivyo basi atakubali kutupwa chini toka juu ya lile genge; lakini akishinda, basi lazima apewe binti wa mfalme amwoe.

Alipewa muda wa miaka mitano kumaliza kazi zote na alipata majengo na watu wa kazi kadiri alivyotaka.

Mara tatu alijaribu kujenga lakini ngazi iliporomoka , hata mwishowe Yule kijana alitambua kuwa ameshindwa, alikusudia kujiua siku iliyofuata ile ilipoporomoka mara ya tano.

Lakini ilitokea usiku uleule alipokuwa amelala usingizini aliota ndoto na katika ndoto akaona mwanamke mzuri sana amekuja akamgusa pajini akayafunua macho yake, kumbe, aliona kama kazi zote zimekwisha.

Alioteshwa jinsi ya kuifanya, na kuzishinda shida zote alizokuwa nazo.

Basi, aliamka na mara ile alianza kufanya kazi kwa jinsi nyingine kabisa, na mwishowe alishinda, na siku ya mwisho ya miaka ile mitano aliyopewa alimwongoza binti wa mfalme kuipanda ngazi kuu ile mpaka katika jumba la juu.

Basi, baadaye aliurithi ufalme kwa haki ya mke wake akaanzisha ukoo wa wafalme wa huko, ukaitwa ‘’ukoo wa ngazi kuu.’’

Ndipo alipofanya ukumbusho wa kazi yake, akachora sanamu ya mawe ya yeye mwenyewe hali amelala usingizi akiota, na Yule mwanamke mzuri anamwinamia na kumgusa paji la uso. Akaisimamisha sanamu hiyo katika sebule kubwa ya jumba, nayo imo humo hata leo.
 
Sir Henry (inkubu )yeye ni mshiriki tu mtunzi anaitwa Richard haggard aliandika riwaya hii mwaka wa1885.
Sir Henry Rider Haggard, KBE, Kt (/ˈhæɡərd/; 22 June 1856 – 14 May 1925), known as H. Rider Haggard, was an English writer of adventure novels set in exotic locations, predominantly Africa, and a pioneer of the Lost World literary genre
 
tukatambua ya kuwa mto ulikuwa chini ya ardhi, na sasa umetokea tena, nao unapita katikati ya magenge marefu kadiri ya futi elfu mbili kwenda juu.

Juu sana tuliona mbingu ni nyeupe, lakini hapo tulipo ni nusu giza, kama katika chumba kilichofungwa milango na madirisha wakati wa mchana. Inaendelea ilipoishia...

Kando ya maji palikuwa na ukingo upana wa yadi saba au nane wenye mawe yaliyoviringana kwa kusukumwa na maji.

Basi, tulikusudia kuteremka hapa ili tupumzike kidogo baada ya hatari zote zilizotupata, na kuvinyoosha viungo vyetu.

Mahali hapa palikuwa pa kutisha sana, lakini panafaa kupumzikia katika hatari na vitisho vya mto, na kutupa nafasi ya kupanga vizuri vitu vilivyomo mtumbwini.

Basi, tulichagua mahali, tukaupweleza mtumbwi kwa shida, kisha tukateremka katika mawe yale.
Bwana Good alishuka ukingoni kwanza, akasema kwa sauti kubwa, ‘’Lo, ama mahali hapa pabaya mno! Panatosha kumtia mtu kifafa,’’ akacheka.

Mara ile sauti kubwa ilikariri maneno yake, ikayazidisha mara nyingi sana. ‘’Kifafa ho!ho!ho!- Kifafa ho!ho!ho!’’ na sauti nyingine ikaitikia juu sana katika genge, ‘’Kifafa! Kifafa! Kifafa!’’ na sauti ilifuata, sauti ikachanganyika pamoja na sauti ya kucheka, mpaka mahali pote palilia, kisha ikatulia tena ghafla kama ilivyoanza.

Umslopogaas akasema kwa utulivu, ‘’Ah! Naona ya kuwa mashetani wako hapa, na kweli mahali hapa paonekana kama ni mahali pa mashetani.’’ Nilijaribu kueleza ya kuwa sauti zile tulizozisikia ni mwangwi tu, lakini hakusadiki.

Akasema, ‘’La mimi naweza kuutambua mwangwi niusikiapo. Mmoja ulikaa karibu na nyumba yangu huko katika nchi ya Umla na vijana wa kike walizoea kuongea nao. Lakini kama huu ni mwangwi, basi ule wa kwetu ulikuwa mtoto wa mwangwi tu! La, la, ni mashetani.

Lakini hata hivi naona si mashetani kitu,’’ akanusa tumbako, ‘’wanaweza kukariri maneno ya mtu, lakini hawawezi kusema maneno yao wenyewe, tena, hawathubutu kujionyesha’’. Akanyamaza, kama kwamba anawadharau mashetani hao.

Baada ya hayo tuliongea kwa sauti ya kunong’ona, maana tulichukizwa kusikia kila neno tunalolisema linatupwa huko na huko kama mpira katika mchezo.

Lakini hata sauti za kunong’ona zilitambaa katika magenge kama sauti za siri, mpaka zilipofifia kama mivumo ya upepo.

Mara tulipotua juu ya mawe yale, tuliyaosha na kuyaganga majeraha yetu ya kuunguzwa moto kadiri tulivyoweza.

Tulikuwa na mafuta kidogo kwa taa yetu, kwa hivi hatukuweza kuyatumia kuyatibu majeraha yetu, basi, tulimnyonyoa bata mmoja, tukatumia mafuta ya kidari chake, yakatufaa sana.

Kisha, tuliviweka vitu vyetu vizuri katika mtumbwi, tukaanza kula, nasi tulikuwa na njaa sana ya chakula, maana tulikuwa tumezirai kwa muda wa saa nyingi, na sasa ilipata saa sita.

Basi, tulikaa tukaanza kula nyama baridi, lakini tulikuwa dhaifu tukataka tutapika, tena, vichwa vilituuma kwa ajili ya taabu za usiku.

Halafu kidogo. Niligeuka nitazame nyuma yangu, nimevutwaa na sauti niliyosikia kama kwamba kitu kinatambaa juu ya mawe, nikaona kaa mkubwa sana wa maji baridi amekaa juu ya mwamba. Alikuwa mkubwa sana kama bata watano kiasi cha bata wakawaida.

Mnyama huyu wa kuchukiza alikuwa na macho yaliyotokeza, yakawa kama yananiangalia, tena, alikuwa na mikono mirefu na magando makubwa sana.

Basi, hapo wanyama wengi kama huyo walitoka kila upande, labda walivutwa na harufu ya chakula, wakatoka nyuma ya mawe na katika matundu ya mwamba.

Wengine walitukaribia sana. Mara ile mmoja alimuuma Bwana Good kwa nguvu sana, akalia kwa sauti kubwa, kisha kwa mara nyingine tena mwangwi uliirudiarudia sauti ile.

Umslopogaas alilitwaa shoka lake akamvunja Yule kaa, na mara ile Yule kaa alilia kwa sauti kubwa, na mwangwi uliirudisha sauti yake iliyo chukiza sana. Mara akaanza kutoa povu kinywani, na wengi wengine wakaja kutoka kila mahali.

Wale walipoona ya kuwa mwenzao ameumia, walimrukia wakaanza kumraruararua kwa magando yao makubwa, wakavitia vipande vya nyama yake vinywani mwao.

Basi, tulishika vitu vyovyote tulivyoweza kupata, tukaanza kupigana nao. Walizidi kujazana tele, wakatoa harufu mbaya sana.

Kila tulipomuua mmoja, wenziwe walimrukia wakamraruararua na huku akitoa povu kinywani mwake tena kila walipopata nafasi walituuma na sisi pia, wakajaribu kuiba chakula chetu.

Mmoja mkubwa sana alimrukia bata mmoja tuliyemnyonyoa, akajaribu kumchukua, na mara ile wengi sana walijitupa juu yake wakaanza kulialia na kutoa povu vinywani wakaila nyama yake na huku wakiraruana pia.

Basi, hapa Bwana Good akasema, ‘’Haraka tuondoke hapa au kweli tutashikwa na wazimu.’’

Basi, tuliusukuma mtumbwi wetu ambao ulizungukwa na wanyama hao wengi sana, tukaushusha mtoni, tukaingia ndani, tukatoka pale tukawaacha wanyama hao wanalialia na kutoa povu linalo nuka vibaya.

Umslopogaas akasema, ‘’Wale ni mashetani wa mahali hapa.’’ Na sisi tulielekea kuyakubali maneno yake.

Sir Henry akasema, ‘’Na sasa tutafanya nini?’’ Nikajibu, ‘’Tuache mtumbwi uchukuliwe na maji tu.’’ Basi, tukauacha uchukuliwe tangu mchana hata jioni, wala hatuna habari kuwa usiku unaingia kwa sababu ya giza la mahali hapo, mpaka Bwana Good alipoonyesha juu tukaona nyota angani.

Basi, kwa kuwa hatuna la kufanya, tulikaa tukiiangalia ile nyota, na mara ilitoweka, na giza likazidi tena, tukaanza kusikia muungurumo wa maji tena, nikaguna nikasema, ‘’Tumeingia chini ya ardhi tena.’’ Nikaangaza taa.

Ndiyo, bila shaka, tumekwisha ingia chini tena tukaweza kuona mwamba wa juu ya mto. Basi usiku mwingine wa hatari na hofu ukaanza.

Sitaweza kuyaeleza mambo yaliyotokea tutachoshana tu, basi, yatosha kusema ya kuwa ilipopata karibu na saa sita ya usiku, tulipiga mwamba uliotokeza katikati ya mto, tukawa karibu kupinduka na kutoswa majini.

Lakini tuliwahi kuutoa mtumbwi na kuendelea tena. Basi, hivi saa zilipita mpaka karibu na saa tisa.

Sir Henry na Bwana Good walikuwa wamelala, wamechoka kabisa, na Umslopogaas akawa amekaa mbele ameshika pondo, na mimi, nilikuwa nikiuongoza mtumbwi.

Mara nilimsikia Umslopogaas anatoa sauti, na mara ile nilisikia sauti ya kucharuka kama kwamba kitu kinapenya katika matawi ya miti, nikaona ya kuwa mtumbwi wetu unapenya kwa nguvu katika miti na matawi yanayotambaa.

Kisha, nikaona upepo mzuri unaupepea uso wangu, nikajua kuwa tumetoka tena katika chini ya ardhi na sasa tunaelea juu ya maji wazi.

Sikuweza kuona kitu kwa macho yangu kwa sababu ya giza la usiku, lakini nilifurahi kuona tumekwisha toka katika mto ule wa kutisha. Basi, nilikaa nikivuta hewa nzuri katika mapafu yangu, nikayangoja mapambazuko kwa saburi nilivyoweza.
Taratiibu naitafuna. Big up sana mkuu blackstarline
 
Back
Top Bottom