Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-32

ILIPOISHIA
Pia hata maiti yake haikuvalishwa nguo ya kawaida, ilivishwa sanda ya kawaida, yalikuwa maagizo ya mganga ili wachawi wasimle nyama.
Misa ya mazishi ilifanyika kisha kumuaga marehemu na kusababisha vilio kwa watu waliomfahamu Ambakisye na tabia yake ya upole kwa kuwajali wakubwa na wadogo. Matayarisho yote yalikwenda vizuri, muda ulipofika waliubeba mwili na kuupeleka makaburini huku akina mama wakimsindikiza kwa vilio.
SASA ENDELEA...


Mama Ambakisye ilibidi ashikiliwe kutokana na kukosa nguvu na maumivu makali ya moyo kutokana na kumpoteza mwanaye kipenzi. Japokuwa upande mmoja alimlaumu mumewe kwa kiburi chake cha kulazimisha mambo, bado alimuona hata jirani yake naye hakutakiwa kuchukua uamuzi wa hasira kumuua mtoto wake bila sababu, japokuwa hakujua nani aliyemuua Atuganile.
Watu walimshika hadi makaburini ambako walimuweka chini ya mti na kumpepea baada ya kuonekana akihema kwa shida huku presha ikimpanda kutokana na kulia sana.
Baada ya jeneza kuwekwa pembeni ya kaburi, padri alisogea kuliombea kaburi na mwili wa marehemu kisha aliomba mwili uingizwe kaburini.
Ilikuwa tofauti na imani za Kikristo ya kuzikwa kwenye jeneza, mwili wa Ambakisye uliteremshwa kaburini chini kukiwa na watu wanne ili kuupokea.
Walianza kuingia watu kaburini akiwemo mzee Amangise ambaye aliingia kaburini amzike mwanaye. Mganga aliyekuwa amesimama karibu na kaburi, machale yalicheza na kupiga kelele kumuomba Amangise asiingie kaburini.
"Itakuwaje nisimzike mwanangu?" Mzee Amangise alimshangaa mganga.
"Nina maana yangu, acha wazike wengine, utajua baadaye."
Mzee Amangise alitoka ndani ya kaburi shingo upande na kusimama pembeni. Mganga alisimama na kuwaeleza wazikaji wasizike kwanza, nao walifanya hivyo. Alitoa kitu mfukoni na kukiminya na kuanza kuzungumza kama anakemea pepo kwa muda huku jasho likimtoka.
Haukupita muda, alitokea bundi na kuelekea alipokuwa amelazwa mke wa Amangise akipepewa, lakini alipokaribia aliganda kama amefungwa kamba, watu wote waliokuwa eneo lile walitimua mbio na kumuacha mke wa Amangise peke yake.
Mganga alizidi kuzungumza huku akiminya alichokuwa amekishika hadi kikapasuka kama bomu.
Ajabu baada ya kupasuka bundi aliyekuwa akienda kwa mke wa Amangise naye alipasuka vipandevipande. Watu wote walishtuka na kuzidi kuyaona maajabu kwenye mazishi ya wiki ile.
"Hivi watu wana faida gani kushiriki uchawi? Nawaambia kila mmoja akitoka hapa akaache uchawi kama si hivyo nitawaumbua. Nawajua wengine tupo hapa mnashangaa lakini ndiyo michezo yenu. Sasa hivi mmewaingiza mpaka watoto wenu kila kona uchawi unanuka.
"Mji huu si salama tena, narudia, wote wenye mchezo huu mkachome tunguri zenu na kuacha tabia ya kuwatesa watu bila sababu," mganga alisema kama mtu aliyepandisha mashetani.
Baada ya kusema vile alitulia kwa muda kisha alisema kwa sauti yake ya kawaida:
"Mnaweza kuzika."
"Vipi naweza kuingia?" Mzee Amangise aliuliza.
"Mzee wangu nayapenda maisha yako na mkeo, yule bundi ilikuwa safari ya mkeo angemgusa tu naye tungemzika kesho. Nina sababu ya kukuambia usiingie kama unataka uzikwe na mwanao basi ingia umzike."
"Mmh! Basi waendelee."
Wazikaji walipoanza kuzika walishtuka kuona kitu kikianguka ndani ya kaburi, walipoangalia waliona joka kubwa lililokuwa likivuja damu. Walipiga kelele na kutoka nje ya kaburi kwa kujirusha nje. Lakini mganga aliwaeleza wamtoe kwa vile wamemuwahi alikuwa ametumwa kufanya ubaya kama yule bundi.
"Nyoka aliyetumwa amekufa."
Baada ya kumtoa nyoka aliyekuwa amekufa ambaye alikuwa ametapakaa damu kama alikuwa wakiogelea kwenye mto wa damu, zoezi la mazishi liliendelea vizuri bila tatizo lolote.
Baada ya msiba mganga aliomba kuzungumza tena.
"Wazee wangu, kijijini kwetu kumekuwa na michezo mingi ambayo watu wengi hawaioni kwa macho ya kawaida.
"Nimekuwa nikiyaona kwa macho lakini nilikaa kimya, wapo niliowafuata kuwaeleza waache mchezo huo na walipokaidi amri yangu wanajua nini niliwafanya.
"Sasa leo kwa mara ya kwanza nalisema hili kwa sauti kubwa, wote wenye tabia ya kishirikina waachane na tabia hiyo mara moja.
"Hii inasababisha waganga sasa hivi badala ya kutibu tunaroga kutokana na matatizo ya kijinga tu ambayo ni ya ujirani ya kuzungumza na kuyamaliza.
"Wengi mmekuwa mkikimbilia Malawi kuwaumiza wenzenu, nasema kuanzia leo uwe mwanzo na mwisho. Narudia kusisitiza najua kuna watu wana masikio ya kenge, hawasikii mpaka watokwe damu masikioni, wachawi wote mnaombwa kuacha mara moja na mkitoka hapa mkatupe tunguri.
"Najua wapo wanaowanyooshea vidole wenzenu na kuonekana wema hata kwenye nyumba za ibada. Hao ndiyo wanaokaa mbele lakini ni watu wabaya sana, wamewaweka wenzao misukule. Sasa mkitoka hapa mkaiachie misukule la sivyo nitawaumbueni.
"Kuna mtu kafanya mchezo wake majibu yake yatapatikana kuanzia usiku huu na mwengine kiyama chenu kinakuja.
"Samahanini kwa usumbufu wa kuwaweka makaburini baada ya kuzika ila anayeona natania, siku hiyo sitataka msamaha wa mtu. Najua wapo wachawi wanaotaka kunijaribu, nawakaribisha ila kila atakayekuja kwangu hatarudi, mtazika wiki nzima na kila nyumba itakuwa na kilio," alisema kwa kujiamini, tofauti na waganga wengi kuwa watu wazima lakini yule alikuwa kijana mdogo wa miaka kumi na saba au kumi na nane ambaye alionekana kujiamini kupita kiasi.
Wakati huo Andendekisye na mganga wake walikuwa wakisubiri majibu ya kombora walilolituma. Walisubiri majibu kutoka makaburini kwa watu ambao wangerudi na jibu la kilichotokea. Baada ya kusubiri kwa muda waliona watu wakitoka makaburini, walijawa na hamu ya kutaka kujua nini kimejiri huko.
Alibahatika kumpata mmoja wa watu waliokuwa wakitoka mazishini kwa kuvizia ili watu wengine wasijue anamuuliza nini.
"Vipi unatoka makaburini?"
"Ndiyo."
"Vipi za huko?"
"Mmh! Nzuri kiasi."
"Kwa nini unasema hivyo?" Andendekisye moyo wake ulianza kufurahi kwa kuamini walichokikusudia kimetimia."
"Tumezika katika wakati mgumu sana."
"Hakukuwa na tukio lolote?"
"Mmh! Mwaka huu mbona kijiji kimefanywa cha majanga ya uchawi."


Itaendelea wiki ijayo...
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-33

ILIPOISHIA:
Baada ya kusubiri kwa muda waliona watu wakitoka makaburini, walijawa na hamu ya kutaka kujua nini kimejiri huko.
Alibahatika kumpata mmoja wa watu waliokuwa wakitoka mazishini kwa kuvizia ili wengine wasijue anamuuliza nini.
"Vipi unatoka makaburini?"
"Ndiyo."
"Vipi za huko?"
"Mmh! Nzuri kiasi."
"Kwa nini unasema hivyo?" Andendekisye moyo wake ulianza kufurahi kwa kuamini walichokikusudia kimetimia."
"Tumezika katika wakati mgumu sana."
"Hakukuwa na tukio lolote?"
"Mmh! Mwaka huu mbona kijiji kimefanywa cha majanga ya uchawi."
SASA ENDELEA...


"Ehe!" Andendekisye alijiandaa kumsikiliza.
Alielezwa matukio yaliyotokea makaburini tukio la bundi kumfuata mke wa Amangise lakini kabla ya kumfikia mganga alifanya mambo yake na yule bundi kuganda kisha alipasuka vipandevipande kabla hajamfikia mkusudiwa.
Tukio lingine lilikuwa la nyoka aliyedondokea kaburini akiwa amekufa huku mwili wake wote kutapakaa damu kila kona kama alikuwa akiogelea kwenye dimbwi la damu.
"Duh!" Andendekisye alishtuka kusikia vile.
"Yaani kila kukicha kinazaliwa kituko kipya."
"Kwa hiyo Amangise na mkewe wanaendeleaje?"
"Kivipi, kwani walikuwa wakiumwa?"
"Hapana kutokana na tukio lile kipi kimewatokea?"
"Wapo salama, lakini inasemekana bila mganga basi Amangise na mkewe wangemfuata mtoto wao kuzimu."
"Umesikia tetesi watu wanasema nani anahusika na matukio yake?" Andendekisye alidodosa.
"Mmh! Kwa kweli kila mmoja anasema lake japo kuna watu wanakuhusisha wewe kutokana na kauli zako."
"Mi sihusiki bali siku ile nilisema kwa hasira," Andendekisye alijisafisha.
"Basi kauli yako imeumba, watu wote wanajua wewe ndiye uliyemuua Ambakisye na kutaka kuwaua Amangise na mkewe."
"Mbona hawasemi Amangise alivyomuua mwanangu?"
"Ni vigumu kujua kwa vile wewe ulijitapa mbele ya watu kuwa ulimuua Ambakisye sasa unafyeka ukoo mzima."
"Hakuna siwezi kufanya hivyo zile zilikuwa hasira."
"Watu wanasema mara ya kwanza ulipoondoka ghafla kabla ya kumzika mwanao ulienda kumtengeneza Ambakisye."
"Si kweli."
"Wewe unasema hivyo, lakini kila mmoja anajua wewe ndiye mhusika mkuu, pia tukio la leo linaambatana na wewe na mkeo kuondoka jana usiku baada ya mazishi ya mwanao. Inasemekana ulienda kuwamaliza Amangise na mkewe lakini mpango wako safari hii umefeli."
"Watakuwa wamenielewa vibaya, hakuna kitu kama hicho."
"Basi ndiyo hivyo kauli yako haijaondoka vichwani mwa watu."
"Kwa hiyo hakuna yeyote aliyeathirika na tukio lile?" Andendekisye alizidi kuchimbua.
"Wapo wachache waliochubuka wakati wa kumkimbia bundi na mmoja ameumia mkono wakati wa kumkimbia chatu aliyeangukia kaburini."
"Amangise hakuingia kaburini?"
"Ndiyo."
"Kwa nini hakumzika mwanaye si mnaona mnaniita mchawi wakati mchawi mnamuacha."
"Alikatazwa na mganga alisema akiingia angezikwa na mwanaye."
"Mmh! Huyu mganga anatoka nchi gani?" Andendekisye aliuliza macho yamemtoka pima.
"Walaa, wa hapahapa nchini."
"Haiwezekani lazima Amangise alisafiri mbali."
"Mbona mganga mwenyewe unamjua wa kijiji cha pili."
"Nani?"
"Si yule kijana aliyemrudisha mtoto wa Mwakasege."
"Yule si mganga alipanga ili kuvutia biashara yake nilichunguza na kuujua ukweli."
"Basi ndiye aliyefanya kazi ya kuokoa maisha ya Amangise na mkewe."
"Kama yule hana lolote yule kijana tapeli, mganga awe kijiji cha jirani?" Andendekisye aliendelea kubisha.
Andendekisye aliupinga uwezo wa mganga kwa yule kutokana na kuamini sana waganga wa kweli wapo Malawi na si Tanzania.
"Halafu mganga amesema kila mmoja anayejihusisha na ushirikina aache mara moja, wote tumeambiwa tukitoka makaburini tukachome tunguri zetu kama tunazo."
"Na wasipochoma?"
"Amesema kiama chao kinakuja cha watu kuumbuka hadharani."
"Anawatisha tu watu, hana jeuri hiyo."
"Wewee! Yule kijana anatisha, nina wasiwasi wachawi wa kijijini siku ya kuumbuka inakuja kwa atakayekaidi amri yake."
"Kama kweli basi ataanza kuumbuka Amangise na mkewe, maana wale wanatisha kwa uchawi."
"Basi wacha niwahi msibani watu wamepita muda."
"Hakuna tatizo tutaonana baadaye."
Andendekisye aliagana na mtu aliyempa taarifa ya makaburini na kumfanya kichwa kizidi kuchanganyikiwa alirudi ndani kwa mganga aliyekuwa akisubiri majibu ya kazi yake makaburini. Sura ya Andendekisye ilimshtua mganga na kutaka kujua kulikoni.
"Vipi?"
"Mambo mabaya."
"Mabaya kivipi?"
"Tumefeli tena."
"Muongo!"
"Kweli, hakuna cha bundi wala chatu."
"Kwani imekuwaje?"
Andendekisye alimweleza yaliyotokea makaburini ya kupasuka vipandevipande kwa bundi na kuokotwa kwa nyoka kaburini akiwa ametapakaa damu mwili mzima kama alikuwa akiogelea kwenye bahari ya damu.
"Mmh!" mganga aliguna baada ya kuona ngoma aliyokuwa akicheza si ya kitoto.
"Sasa tunafanyaje?"
"Yaani nazidi kukutana na vikwazo, sielewi nimekosea wapi, hebu twende nyuma ya nyumba tukaangalie bomu lingine. Siamini kama mtu ninayepambana naye ana uwezo mkubwa kama huo lazima kuna kitu nimekosea."
"Nasikia kuna kijana mmoja ndiye aliyezuia zoezi letu bila hivyo kazi ingekwenda vizuri."
"Hakuna kiumbe kinachoweza kuzuia kazi yangu, hebu tukaangalie ili niangalie nimekosea wapi. Wachawi walioshindikana hupiga saluti mbele yangu itakuwa mganga huyu kwanza anatoka wapi?"
"Kijiji cha jirani."
"Hapahapa Tanzania?"
"Ndiyo."
"Tanzania hakuna waganga, subiri nikamtie adabu."
Walizunguka nyuma ya nyumba kuangalia mtego mwingine unaonesha kitu gani.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua Kesho.........
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-33

ILIPOISHIA:
Baada ya kusubiri kwa muda waliona watu wakitoka makaburini, walijawa na hamu ya kutaka kujua nini kimejiri huko.
Alibahatika kumpata mmoja wa watu waliokuwa wakitoka mazishini kwa kuvizia ili wengine wasijue anamuuliza nini.
“Vipi unatoka makaburini?”
“Ndiyo.”
“Vipi za huko?”

“Mmh! Nzuri kiasi.”
“Kwa nini unasema hivyo?” Andendekisye moyo wake ulianza kufurahi kwa kuamini walichokikusudia kimetimia.”
“Tumezika katika wakati mgumu sana.”
“Hakukuwa na tukio lolote?”
“Mmh! Mwaka huu mbona kijiji kimefanywa cha majanga ya uchawi.”
SASA ENDELEA...


“Ehe!” Andendekisye alijiandaa kumsikiliza.
Alielezwa matukio yaliyotokea makaburini tukio la bundi kumfuata mke wa Amangise lakini kabla ya kumfikia mganga alifanya mambo yake na yule bundi kuganda kisha alipasuka vipandevipande kabla hajamfikia mkusudiwa.

Tukio lingine lilikuwa la nyoka aliyedondokea kaburini akiwa amekufa huku mwili wake wote kutapakaa damu kila kona kama alikuwa akiogelea kwenye dimbwi la damu.
“Duh!” Andendekisye alishtuka kusikia vile.
“Yaani kila kukicha kinazaliwa kituko kipya.”
“Kwa hiyo Amangise na mkewe wanaendeleaje?”
“Kivipi, kwani walikuwa wakiumwa?”

“Hapana kutokana na tukio lile kipi kimewatokea?”
“Wapo salama, lakini inasemekana bila mganga basi Amangise na mkewe wangemfuata mtoto wao kuzimu.”
“Umesikia tetesi watu wanasema nani anahusika na matukio yake?” Andendekisye alidodosa.
“Mmh! Kwa kweli kila mmoja anasema lake japo kuna watu wanakuhusisha wewe kutokana na kauli zako.”

“Mi sihusiki bali siku ile nilisema kwa hasira,” Andendekisye alijisafisha.
“Basi kauli yako imeumba, watu wote wanajua wewe ndiye uliyemuua Ambakisye na kutaka kuwaua Amangise na mkewe.”
“Mbona hawasemi Amangise alivyomuua mwanangu?”
“Ni vigumu kujua kwa vile wewe ulijitapa mbele ya watu kuwa ulimuua Ambakisye sasa unafyeka ukoo mzima.”

“Hakuna siwezi kufanya hivyo zile zilikuwa hasira.”
“Watu wanasema mara ya kwanza ulipoondoka ghafla kabla ya kumzika mwanao ulienda kumtengeneza Ambakisye.”
“Si kweli.”

“Wewe unasema hivyo, lakini kila mmoja anajua wewe ndiye mhusika mkuu, pia tukio la leo linaambatana na wewe na mkeo kuondoka jana usiku baada ya mazishi ya mwanao. Inasemekana ulienda kuwamaliza Amangise na mkewe lakini mpango wako safari hii umefeli.”
“Watakuwa wamenielewa vibaya, hakuna kitu kama hicho.”

“Basi ndiyo hivyo kauli yako haijaondoka vichwani mwa watu.”
“Kwa hiyo hakuna yeyote aliyeathirika na tukio lile?” Andendekisye alizidi kuchimbua.
“Wapo wachache waliochubuka wakati wa kumkimbia bundi na mmoja ameumia mkono wakati wa kumkimbia chatu aliyeangukia kaburini.”
“Amangise hakuingia kaburini?”
“Ndiyo.”

“Kwa nini hakumzika mwanaye si mnaona mnaniita mchawi wakati mchawi mnamuacha.”
“Alikatazwa na mganga alisema akiingia angezikwa na mwanaye.”
“Mmh! Huyu mganga anatoka nchi gani?” Andendekisye aliuliza macho yamemtoka pima.
“Walaa, wa hapahapa nchini.”

“Haiwezekani lazima Amangise alisafiri mbali.”
“Mbona mganga mwenyewe unamjua wa kijiji cha pili.”
“Nani?”

“Si yule kijana aliyemrudisha mtoto wa Mwakasege.”
“Yule si mganga alipanga ili kuvutia biashara yake nilichunguza na kuujua ukweli.”
“Basi ndiye aliyefanya kazi ya kuokoa maisha ya Amangise na mkewe.”
“Kama yule hana lolote yule kijana tapeli, mganga awe kijiji cha jirani?” Andendekisye aliendelea kubisha.

Andendekisye aliupinga uwezo wa mganga kwa yule kutokana na kuamini sana waganga wa kweli wapo Malawi na si Tanzania.
“Halafu mganga amesema kila mmoja anayejihusisha na ushirikina aache mara moja, wote tumeambiwa tukitoka makaburini tukachome tunguri zetu kama tunazo.”
“Na wasipochoma?”

“Amesema kiama chao kinakuja cha watu kuumbuka hadharani.”
“Anawatisha tu watu, hana jeuri hiyo.”
“Wewee! Yule kijana anatisha, nina wasiwasi wachawi wa kijijini siku ya kuumbuka inakuja kwa atakayekaidi amri yake.”

“Kama kweli basi ataanza kuumbuka Amangise na mkewe, maana wale wanatisha kwa uchawi.”
“Basi wacha niwahi msibani watu wamepita muda.”
“Hakuna tatizo tutaonana baadaye.”
Andendekisye aliagana na mtu aliyempa taarifa ya makaburini na kumfanya kichwa kizidi kuchanganyikiwa alirudi ndani kwa mganga aliyekuwa akisubiri majibu ya kazi yake makaburini. Sura ya Andendekisye ilimshtua mganga na kutaka kujua kulikoni.
“Vipi?”

“Mambo mabaya.”
“Mabaya kivipi?”
“Tumefeli tena.”
“Muongo!”
“Kweli, hakuna cha bundi wala chatu.”
“Kwani imekuwaje?”

Andendekisye alimweleza yaliyotokea makaburini ya kupasuka vipandevipande kwa bundi na kuokotwa kwa nyoka kaburini akiwa ametapakaa damu mwili mzima kama alikuwa akiogelea kwenye bahari ya damu.
“Mmh!” mganga aliguna baada ya kuona ngoma aliyokuwa akicheza si ya kitoto.
“Sasa tunafanyaje?”
“Yaani nazidi kukutana na vikwazo, sielewi nimekosea wapi, hebu twende nyuma ya nyumba tukaangalie bomu lingine. Siamini kama mtu ninayepambana naye ana uwezo mkubwa kama huo lazima kuna kitu nimekosea.”

“Nasikia kuna kijana mmoja ndiye aliyezuia zoezi letu bila hivyo kazi ingekwenda vizuri.”
“Hakuna kiumbe kinachoweza kuzuia kazi yangu, hebu tukaangalie ili niangalie nimekosea wapi. Wachawi walioshindikana hupiga saluti mbele yangu itakuwa mganga huyu kwanza anatoka wapi?”
“Kijiji cha jirani.”
“Hapahapa Tanzania?”
“Ndiyo.”

“Tanzania hakuna waganga, subiri nikamtie adabu.”
Walizunguka nyuma ya nyumba kuangalia mtego mwingine unaonesha kitu gani.


Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua Kesho.........

mkuu mzizi mkavu njoo basi uendeleze tunakungoja huku kaka
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-34

ILIPOISHIA:
"Hakuna kiumbe kinachoweza kuzuia kazi yangu, hebu tukaangalie ili niangalie nimekosea wapi. Wachawi walioshindikana hupiga saluti mbele yangu itakuwa mganga huyu kwanza anatoka wapi?"
"Kijiji cha jirani."
"Hapahapa Tanzania?"
"Ndiyo."
"Tanzania hakuna waganga, subiri nikamtie adabu."
Walizunguka nyuma ya nyumba kuangalia mtego mwingine unaonesha kitu gani.

SASA ENDELEA...


Makaburini baada ya mganga kutoa onyo kwa wachawi wote aliondoka na watu walikwenda kuzika na walirudi msibani. Alipofika kwa Amangise aliongeza nguvu kwenye dawa alizoweka kutokana na kuona uzito wa kazi ulivyokuwa na vita iliyokuwa bado inaendelea. Baada ya kumaliza kazi yake alizungumza chemba na Amangise na mkewe.
"Nina imani kazi imekwisha, ninataka kuwaeleza vita yenu ni kubwa, kama nisingekuwa mjuzi wa mambo haya tulikuwa tunawazika kesho mtu na mkewe. Uchawi uliotumiwa ni mkubwa sana. Nyoka yule alitumwa kuja kukumaliza ukiwa kaburini ungemuona wewe tu baada ya kukuuma angetoweka hakuna mtu mwingine angemuona.
Kama angekuuma kusingekuwa na dawa ungekauka muda uleule na yule bundi alitumwa kuja kwa mkeo angemgusa tu basi angepata mshtuko ambao ulikuwa ndiyo safari yake, lakini nimewahi. Kuna makombora mawili nimeyazima hukohuko yalipokuwa majibu ya kazi yangu mtayasikia kama si usiku basi kesho.
"Kuna kitu nataka mkifanye usiku huu, nikitoka hapa tunguri zote mzitoe ndani na kuzitia moto na wala usijihusishe tena na mambo ya kishirikina. Mkimfanyia mtu ubaya wowote ujue unawarudia wenyewe. Wiki ijayo nitakuwa na kazi ya kukomesha uchawi kijiji hiki na ninyi mkiendelea kuuficha uchawi shauri yenu," mganga alitoa onyo.
"Tumekusikia, tunakuahidi kuachana na kila ovu madhara yake tumeyaona," Amangise alimuahidi mganga."Sasa baba, tutaweza kwenda kanisani kweli?" mke wa Amangise aliuliza.
"Kanisani mwende kwa vile mtakuwa watu wema ambao mtamuogopa Mungu na si kuingilia kazi ya Mungu kuua na kutesa."
"Basi tunakuahidi kuwa viumbe wapya."
"Mimi nimemaliza kama mnanifurahisha ili niondoke kitakachowatokea naomba msinishirikishe."
"Nakuahidi kusimamia kila kitu kuteketeza kila kitu," mama Ambakisye alimuahidi mganga.
Baada ya mganga kuyasema yake aliondoka kurudi nyumbani kwake na kuwaacha watu wakiwa msibani huku watu wakiwa makundimakundi kuzungumzia matukio ya wiki ile. Kuna mtu alisema alimuona Andendekisye mchana ule akielekea kwake akiwa na mgeni wa kiume.
Wapo waliojiuliza mkewe kamwacha wapi, lakini wapo waliofikiria labda alimpeleka kwao. Wanaomfahamu walipinga kwa kusema mkewe hakuwa na ndugu baada ya kufiwa na wazazi wake pia Andendekisye alikuwa hapatani na ndugu zake hivyo maisha yake yote hakuwahi kumuona akienda kusalimia ndugu zake.
Wapo walioamini huenda alikwenda kwa mganga kutokana na kauli yake na aliyeongozana naye huenda ndiye mganga lakini ajabu mkewe hakuonekana na kujiuliza mkewe yupo wapi. Kwa vile yalikuwa hayawahusu waligeukia kauli ya mganga kuhusu watu kuteketeza tunguri zao.
"Unajua yule kijana anatakiwa kudhibitiwa kwa vile anaweza kuwaumbua watu wazima."
"Atadhibitiwa vipi, lakini si amesema watu waharibu tunguri zao kila aliyekuwa nazo kabla siku ya kuwaumbua watu."
"Watu wengine familia zetu zinafanya hivyo si mwanzo wa kuumbuka."
"Hakuna jinsi ni kukubaliana naye bila hivyo aibu inakuja."
"Anatakiwa kudhibitiwa kabla ya siku hiyo."
"Mmh! Mnafikiri mtafanyaje?"
"Tutamfuata na kumuomba asitishe zoezi lake."
Wazee waliweka mikakati ya kumdhibiti mganga kabla siku ya kuwaumbua watu haijafika. Walipanga kumfuata kwake na kumuomba aachane na zoezi lile ambalo lingeleta picha mbaya kijijini.
***
Andendekisye na mganga wake walizunguka nyuma ya nyumba kuangalia chungu kitupu kilichowekewa kisu kina matokeo gani. Mganga alishangaa kukuta chungu kipo vilevile kama alivyokiacha. Alirudi ndani na kuchukua dawa ya unga na kwenda kuiweka kwenye chungu na damu kidogo ya kuku huku akisema:
"Hawezi kuzuia nguvu zangu, ngoja nimtie adabu."
Baada ya kuweka dawa na damu kidogo kwenye chungu alitulia kwa muda hali ilikuwa ileile. Alikitoa kisu kwenye chungu na kusema maneno yake kisha alikichoma kwa nguvu ndani ya chungu na kutulia kwa muda kisha alifumbua macho kuangalia kwenye chungu kumetokea nini.
Ghafla ndani ya chungu kulitoka damu iliyoruka kama mtu aliyekata kwa ghafla na kumpata usoni ambayo ilimuingia machoni. Aliachia kisu na kujifuta damu iliyomrukia usoni na kuingia machoni ambayo iliwasha kama pilipili. Baada ya kujifuta alifumbua macho lakini hakuweza kuona kitu zaidi ya macho kuendelea kuwasha.
"Andendekisye sasa ni saa ngapi?"
"Saa kumi na mbili jioni."
"Kuna giza?"
"Hakuna kwani vipi?"
"Kama mchana mbona sioni?"
"Labda damu imekuingia machoni jisafishe."
"Ndiyo tena inaniwasha kama pilipili."
"Nikuletee maji."
"Niletee tena fanya haraka macho yanauma kama kuna kaa la moto."
Andendekisye alikimbilia maji ndani na kumuacha mganga akijilazimisha kuangalia lakini kila alivyofumbua macho yaliongeza kuwasha. Baada ya kuletewa maji aliyaosha macho lakini hakukuwa na mabadiliko zaidi ya kuanza kuvimba mpaka mishipa ya kichwa kusimama.
"Mungu wangu sijui nini hii mbona naumbuka mtoto wa Msioka."
"Sasa itakuwaje?" Andendekisye aliuliza huku ameshika kichwa.
"Hata sijui macho yananiuma kama kidonda nakufa najiona."
"Sasa umekosea wapi?"
"Siwezi kujua, bora angeniua kuliko kunitia upofu nitarudije nyumbani nitawezaje kufanya kazi zangu mbona majanga?"


Itaendelea Siku ya alkhamisi.........
 
Leo nimeinjoi sana, MziziMkavu angalia naweusijekuwa mchawi maana hizi hadithi duh......!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-35

ILIPOISHIA...
Andendekisye alikimbilia maji ndani na kumuacha mganga akijilazimisha kuangalia lakini kila alivyofumbua macho yaliongeza kuwasha. Baada ya kuletewa maji aliyaosha macho lakini hakukuwa na mabadiliko zaidi ya kuanza kuvimba mpaka mishipa ya kichwa kusimama.
"Mungu wangu sijui nini hii mbona naumbuka mjukuu wa Msioka."
"Sasa itakuwaje?" Andendekisye aliuliza huku ameshika kichwa.
"Hata sijui macho yananiuma kama kidonda nakufa najiona."
"Sasa umekosea wapi?"
"Siwezi kujua, bora angeniua kuliko kunitia upofu nitarudije nyumbani, nitawezaje kufanya kazi zangu mbona majanga?"
SASA ENDELEA...


"Sasa hebu niambie nifanye kitu gani ili nikusaidie?"
"Mtafute mwanamke anayenyonyesha mtoto aje anikamulie maziwa machoni."
"Ngoja nijaribu."
Andendekisye alitoka nyumbani kwake bila kujua atampata wapi mwanamke anayenyonyesha. Alitembea kama mwenda wazimu, hata watu wake wa karibu aliwapita bila kuwasemesha, alionekana mtu aliyepagawa, akizungumza peke yake huku akilitaja jina la Amangise, akijipiga mikono kifuani kwa nguvu akiapa kumtia adabu kwa gharama yoyote.
Kutokana na kuchanganyikiwa na tukio lililompata mganga aliyekuwa akimtegemea, alijikuta akifika kijiji cha Mbako bila kujua. Alishtuka baada ya kuulizwa na mtu anakwenda wapi ndipo alipogeuza kurudi kijijini kwake. Wakati huo giza lilikuwa limeingia. Njia nzima alirudi akiwa amepagawa na kujiuliza mganga amefanya nini au na yeye ndiyo yamemkuta kama ya mkewe.
Katika kumjua mganga hakuwahi kumwona akilia kama mtoto kama siku ile, alijiuliza kama kweli mganga amepofuka atafanya nini na atawezaje kumrudisha kwao.
Alifika nyumbani kwake saa tatu za usiku na kukuta mganga bado ameshikilia macho huku akilia kwa uchungu.
Alipowasha taa alishtuka kuona macho ya mganga yakivuja damu, aliamini kwa hali ile alikuwa ameumbuka ataieleza nini jamiii ambayo inaamini kabisa yeye ni mchawi aliyehusika na vifo vya baadhi ya watu pale kijijini kikiwemo cha Ambakisye mtoto wa adui yake.
"Andendekisye nakufa naomba msaada wako," mganga alilalamika huku akigaragara chini.
"Nikusaidie nini maana nimechanganyikiwa?" Andendekisye hakujua afanye nini?"
"Hujapata mwanamke anayenyonyesha?"
"Yaani hata sijui nitampata wapi?"
"Huna majirani?"
"Ninao lakini nawaogopa wataniuliza nina shida gani na maziwa yao wakati sasa hivi kijiji kizima kinajua mimi mchawi."
"Kwa hiyo upo tayari kuniona nakufa, Andendekisye kumbuka nimetoka mbali kwa ajili yako."
"Ni kweli lakini sina ujanja."
"Kwani huyo mganga anakaa wapi?"
"Kijiji cha jirani."
"Naomba chondechonde kaniombee msamaha ili niepukane na adha hii, naumia mwenzio macho kama kuna mtu anayakata kwa ndani."
"Hii ni ajabu, ndiyo maana damu zinatoka kwa wingi."
"Mungu wangu natoka damu?" mganga alishtuka.
"Ndiyo."
"Nakufa mimi mjukuu wa Msioka."
"Ngoja basi niwahi kwenda kwa mganga sijui kama atakubali."
"Mbembeleze bila hivyo naamini siwezi kufika asubuhi lazima nitakufa."
"Sawa."
Andendekisye alipitia baiskeli na kuwahi kwa mganga ambaye aliamini ndiye aliyefanya mchezo ule. Alipiga pedeli kwa nguvu ili kuwahi, alichukua dakika 17 kufika. Alipofika alimkukuta akiwa amekaa uani kwake akizungumza na wateja wake waliokuwa wakipata tiba.
Kutokana na kasi aliyoingia nayo, alijikuta akifunga breki ya nguvu na kusababisha kupiga mwereka. Wote walishangaa jinsi alivyoingia na kupiga mwereka. Andendekisye aliponyanyuka hakujali baiskeli alikwenda moja kwa moja mbele ya mganga na kupiga magoti kuomba msaada.
"Mganga naomba msaada wako hali ni mbaya."
"Sina msaada, wewe si kiburi kaendelee na bado kiama chako kinakuja."
"Ha..ha..pana, sina jeuri yoyote kwako."
"Si umekuja na mganga toka Malawi, sasa kaloge tena baada kumpoteza mkeo sasa ni zamu yako endelea kushindana na wenye nguvu. Umeua wengi lakini nilikaa kimya hata hili bila kufuatwa na jirani yako ningekaa pembeni mmalizane.
"Nilitoa onyo mapema kuhusu mtu anayetaka kupima maji kwa kidole sasa subiri kiama chenu kinakuja.
"Na kamwambie mganga wako akijitia kujua utamrudisha maiti, mimi si mchawi bali mganga wa kutibu watu, sasa huyo mchawi mwenzako mwambie akifanya utani atarudishwa kwao maiti."
"Najua nimefanya makosa mengi kwa ubishi wangu lakini naomba msaada wako."
"Umekuja kunijaribu?"
"Ha..ha..pana."
"Unataka msaada gani wewe mwanga?"
"Mganga wangu macho yamepofuka."

Itaendelea Jumapili usikose kuwa pamoja na mimi.........
 
Leo nimeinjoi sana, MziziMkavu angalia naweusijekuwa mchawi maana hizi hadithi duh......!!!!!!
Liati kungelikuwa kuna uchawi wa kupata Pesa ningelikuwa mimi pia Mchawi lakini hakuna uchawi wa Mtu kuwa Tajiri kuna faida gani kujifunza Uchawi wa kuwadhuru watu? Ndugu mbalu
 
Last edited by a moderator:
Liati kungelikuwa kuna uchawi wa kupata Pesa ningelikuwa mimi pia Mchawi lakini hakuna uchawi wa Mtu kuwa Tajiri kuna faida gani kujifunza Uchawi wa kuwadhuru watu? Ndugu mbalu

Usemayo ni kweli kabisa Mkuu, akili za hawa jamaa zinawatosha wao tu.
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-36

ILIPOISHIA:
"Najua nimefanya makosa mengi kwa ubishi wangu lakini naomba msaada wako."
"Umekuja kunijaribu?"
"Ha..ha..pana."
"Unataka msaada gani wewe mwanga?"
"Mganga wangu macho yamepofuka."
SASA ENDELEA...


"Si umpeleke hospitali?"
"Si ungonjwa wa hospitali anateseka macho yanatoka damu."
"Kwani kafanya nini?"
"Alikuwa anatengeneza dawa ghafla akasema haoni."
"Dawa ya nini?"
"Ilikuwa ya matatizo yangu."
"Ukisema kweli nitakusaidia kama husemi ukweli naomba uondoke kabla hajakukuta yaliyomkuta mchawi mwenzako."
"Alikuwa akinitengenezea dawa baada ya matatizo ya nyumbani kwangu."
"Nani kamuua mkeo?"
"Si..si..jui."
"Sikiliza Andendekisye mimi ni mdogo sana kiumri lakini nafahamu mengi ya kidunia kuliko wewe. Sasa kama umekuja kunijaribu naomba uondoke mara moja."
"Nashindwa kusema kwa vile linanihusu."
"Basi mimi sina msaada wowote mpeleke Malawi atapona."
"Naomba unisaidie kijana wangu, nimeishaumbuka, nakuahidi kufanya yote uliyosema makaburini ya kuachana na mambo ya ushirikina."
"Ukinijibu maswali yangu vizuri nitakusaidia lakini ukinidanganya naomba unanze kuondoka baada ya mwenzio kupofuka macho wewe utapata ukurutu mwili mzima."
"Nitayajibu."
"Nani kamuua Ambakisye mtoto wa Andendekisye."
"Mimi."
"Kwa nini?"
"Kwa vile baba yake alimuua mwanangu."
"Amangise hakumuua mtoto wako bali kajiua mwenyewe."
"Una maana gani?"
"Ni kisasi cha aliyemuua ambaye ni mchumba wa Ambakisye akishirikiana na bibi Tumwambilile ndiyo maana vifo vyao vilifanana na vya muda mmoja. Kwa vile huna busara na tamaa ya mchawi wako akamuua asiye na kosa."
"Nilikuwa sijui."
"Nani kamuua mkeo?"
"Mimi."
"Nani alituma nyoka na bundi makaburini?"
"Mimi."
"Kwa sababu gani?"
"Nilikuwa sijui, nilitaka kulipa kisasi cha kuuliwa mwanangu."
"Kwa nini mganga amepofuka?"
"Kuna mtego mwingine baada ya bundi na nyoka kufeli alitengeneza bomu analolitegemea ndilo lililomlipukia."
"Sasa msaada wangu kuondoa maumivu ya macho lakini macho ndiyo amekuwa kipofu kweli hata pona tena mpaka anakufa."
"Na..naomba hata hiyo kwani anateseka sana."
Mganga alikwenda ndani na kumletea dawa ambayo alimweleza akachanganye na maziwa mabichi na kumnawisha uso maumivu yote yataondoka.
"Nashukuru."
"Ukifanya ujanja wowote tusilaumiane."
"Nakuahidi sitafanya chochote kibaya nimegundua makosa yangu."
"Basi wahi kumpatia tiba mganga wako."
Andendekisye alipanda baiskeli kuwahi nyumbani kumpatia tiba mganga ambaye alikuwa akilia kama mtoto kutokana na maumivu makali ya macho. Alipofika alikimbilia kwenye zizi na kumkamua ng'ombe mwenye kunyonyesha kisha alichukua maziwa na kuichanganya na dawa na kumnawisha mganga baada ya sekunde chache macho alitulia na kumfanya mganga kupitiwa usingizi mzito baada ya kuteseka kwa muda mrefu kwa maumivu ya macho.
***
Siku ya pili baadhi ya wazee walikwenda kumwona mganga kumweleza wanachotaka akifanye. Baada ya kufika aliwakaribisha kama wazazi wake na kuwasikiliza.
"Karibuni wazee wangu."
"Asante za toka jana?"
"Namshukuru Mungu."
"Kijana tumekuwa na shida moja ambayo tunataka tuzungumze."
"Hakuna tatizo, mna shida gani?"
"Kutokana na kauli uliyotoa jana makaburini kuhusu ushirikina tunaomba zoezi hilo ulisitishe."
"Mpaka lini?"
"Siyo mpaka lini bali lisimamame kabisa."
"Kwa sababu gani?"
"Unajua kijiji chochote hakikosi mila na destuli hivyo unachotaka kukifanya ni kutaka kukiumbua kijiji."
"Kwani nani ataumbuka kama huhusiki?"
"Hata kama tunahusika sisi kama wazee wa kijiji tunaomba uachane na zoezi hilo mara moja."
"Wazee wangu nimewasikia lakini ninachotaka kukifanya siyo mimi ni vitu vyangu vilivyomo kichwani mwangu ndivyo vimenituma hivyo lazima nitimize nilichoagizwa nikiacha nitaadhibiwa mimi."
"Kafanyie sehemu nyingine bila hivyo tutakufukuza kijiji hiki."
"Najua uwezo huo mnao lakini katu sitabadilia ninachotaka kukifanya, najua wote uliokuja mnaishi kwa ushirikina sikutaka kukuumbueni wakati mnaingia. Wewe mzee ndani mwako kuna misukule saba miwili ni watoto wa jirani yako mnayesali naye kanisa moja, uongo?" Mzee aliyeulizwa alibakia kukapua macho.
"Na wewe mkeo anauza pombe akiwa uchi na upawa anaotumia ni kiganja cha mtu na wewe ili kuongeza wateja, unajua ndiyo maana umekuja kuzima. Na wewe umemuua jirani yako kwa wivu kwa vile analima sana lakini hakuna mtu anayejua. Kwa vile mmekuja wenyewe mkitoka hapa yote niliyowaeleza kwa siri mkayaache mara moja atakayebisha kiama chake kinakuja," mganga alisema kwa kujiamini tofauti na umri na umbile lake dogo.
"Kijana tunakuapia hutafanikiwa kufanya hivyo kabla ya wiki tutakuwa tumekuhamisha," wazee walimpiga mkwara.
"Hakuna tatizo lakini mmechelewa lazima mtaumbuka."
Wazee waliondoka kwa hasira huku wakijipanga kumkwamisha kufanya mkutano wake wa kuwaumbua wachawi.
Usiku wakati Andendekisye alipokuwa amelala alimuota mkewe akiwa amemshikia kisu akitaka kumuua huku akimwambia na yeye lazima afe kwa vile alimuua bila sababu. Alishtuka usingizini lakini ajabu bado alimuona live mkewe amemshikia kisu, alikurupuka na kutoka nje lakini alimfuata na kuamua kutimua mbio kuokoa maisha yake.

Itaendelea Alkhamisi ijayo..........
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-37

ILIPOISHIA:
Usiku wakati Andendekisye alipokuwa amelala alimuota mkewe akiwa amemshikia kisu akitaka kumuua huku akimwambia na yeye lazima afe kwa vile alimuua bila sababu. Alishtuka usingizini lakini ajabu bado alimuona live mkewe amemshikia kisu, alikurupuka na kutoka nje, lakini alimfuata na kuamua kutimua mbio kuokoa maisha yake.
SASA ENDELEA...


Alishangaa nje alimkuta Ambakisye mtoto wa jirani yake aliyemuua pia na kijana mmoja aliyekataa kumuoa binti yake na kumuua. Wote walikuwa nje kila mtu kashika silaha yake na kuanza kumfukuza.
Alikimbia usiku kucha kuokoa maisha yake na kusababisha kujijeruhi kila alipoanguka.
Asubuhi watu walimuona kama mwenda wazimu kila alipotulia alishtuka na kuanza kutimua mbio huku akisema mke wangu usiniue na alipoanguka chini alipiga magoti kuomba msamaha huku akisema kuwa alimuua mke wake kwa bahati mbaya.
Kauli ya Andendekisye ilifanya watu wajue kumbe mkewe naye alimuua mwenyewe, kuna kipindi alikimbia mpaka akapoteza uwezo wa kupumua na kupoteza fahamu. Taarifa ile ilimfikia mganga ambaye aliamini kabisa kupitia Andendekisye ndiyo siku ya kuwaumbua wachawi.
Alibeba zana zake za kazi na kwenda mjini ambako alikuta Andendekisye amezungukwa na watu huku wengine wakitaka apelekwe hospitali lakini wengine walitaka aachwe afie mbali kwa vile alimuua Ambakiksye na mkewe kwa roho mbaya yake.
Wapo waliotaka kumtia moto lakini wazee wa kijiji waliingilia kati, bahati nzuri mganga alifika eneo la tukio na kuwafanya watu waliomzunguka kumpisha ili afanye mambo yake. Aliwaomba vijana wambebe mpaka uwanja wa mpira, walifanya vile wakati huo watu walikuwa wakikusanyika kujionea mganga anataka kufanya nini.
Baada ya kumfikisha Andendekisye aliyekuwa hajitambui, watu nao walikusanyika kama waliopigiwa mbiu ya mgambo baada ya kupashana kilichompata jirani yao ambaye alimuona ndiye mchawi wa kijijini. Baada ya vijana kumlaza chini, mganga aliandaa dawa zake kisha alisema kwa sauti ya juu.
"Jamani vijana wenzangu mnapajua nyumbani kwa Andendekisye?"
"Ndiyo," walijibu.
"Naomba mkamlete mtu mmoja mlemavu wa macho hapa."
Vijana wale walikimbia nyumbani kwa Andendekisye, walipofika walimkuta mtu mmoja amelala nje. Walipofika aliuliza kama Andendekisye amerudi huku akilaumu kuondoka bila kumuaga huku akijua mwenzake haoni na pia hajala tokea jana.
"Andendekisye kumbuka wewe ndiye umenisababishia balaa hili, bila wewe nisingekuwa hivi. Kibaya umeondoka ukijua kabisa sioni, sijala tokea jana hii ndiyo shukurani yako?" mganga aliuliza akiwa bado amejilaza chini.
"Mzee sisi tumetumwa na mganga tukupeleke uwanjani."
"Mganga gani?"
"Mganga mtoto."
"Ana shida gani na mimi?"
"Wewe twende utajua hukohuko."
"Kwani Andendekisye yupo wapi?"
"Naye yupo huko."
"Lakini mimi njaa inaniuma nipeni kwanza chakula."
"Utakula huko."
"Jamani mbona siwaelewi kila kitu mnasema huko."
"Sisi tumetumwa wala si wenyeji wa hapa."
"Haya twendeni."
Walimshika mkono na kwenda naye hadi uwanjani ambako kulikuwa kumejaa watu, wakati wote mganga alikuwa akifanya mambo yake bila kumshughulikia Andendekisye aliyekuwa bado amelala kama amekufa.
Baada ya kufika alisogezwa kwa mganga, vijana wale walimweleza jamaa ana njaa, ilibidi atafutiwe uji na viazi baada ya kushiba alisogezwa mbele ya mganga. Muda wote watu walikuwa kimya kutaka kujua kuna nini wakati huo wazee waliokwenda kwa mganga alishtuka kusikia mganga kajaza watu uwanja wa mpira akiwa na Andendekisye na mganga wake aliyeonekana kapofuka macho.
Walijifikiria kwenda polisi kuzuia anachotaka kukifanya lakini walijiuliza wataeleza azuiwe kwa sababu gani ikiwa serikali haitambui ushirikina, japo viongozi wake wanategemea nguvu za giza kutawala.
Baada ya kila kitu kukamilika mganga alimfanyia dawa Andendekisye aliyenyanyuka na kushangaa kuona umati wa watu na kumuuliza mganga.
"Nimefikaje hapa?"
"Tulia utajua tu kwa vile mwisho wa ubaya ni aibu."

Itaendelea Siku ya Jumapili musikonde basi.........
 
Back
Top Bottom