Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
wachawi-jpg.167682


TUMESHUHUDIA Wachawi wakiwatesa watu wasio na hatia hata kuanzisha vita na waganga wa jadi ambao hujitolea kuwasaidia waliowaroga kuwaondolea mateso mazito kutokana na kutupiwa uchawi ambao huwatesa katika maisha yao yote. Tumeshuhudiwa

vifo vya ghafla vya watu na baadaye kusikika wameonekana sehemu fulani wakiwa hai au wamegeuzwa msukule.

Wachawi siku zote wamekuwa na umoja katika mambo yao ikiwa na kujenga chama cha pamoja chenye nguvu huku kila mwanachama akichangia mtu mmoja ambaye huwa kitoweo chao. Pia wamekuwa wakishirikiana katika kumsaidia mwenzao anapoingiliwa na nguvu za kiroho au za dawa za jadi kuhakikisha wanapambana nao mpaka tone la mwisho la damu yao.

Lakini nao huingia vitani baada ya mmoja kuonekana anajifanya anajua au kuingilia kazi ya mwenzake au mmoja kutaka kumpima mwenzake. Hapo hutokea vita kubwa ambayo hugawa makundi kwa kila moja kusaidia upande wake ndipo panapokuwa hakuna cha kumsalia mtume.

Mapenzi ya watu wawili yamefanya Vijiji vya Ibungu, Mbako, Kilasilo mpaka Isaki katika Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kuingia katika vita kubwa ya kichawi kwa maeneo hayo kuoneshana ubabe. Hukuwepo malaika wako alikuwepo. TEREMKA NAYO.

Pamoja na mvua kali ya radi kuendelea kunyesha, Ambakisye na Atuganile hawakutoka porini walijificha chini ya mti kwa vile muafaka ulikuwa bado haujapatikana. Mvua iliendelea kunyesha na radi za kutisha zilipiga, Atuganile aliendelea kulia machozi ambayo hayakuonekana kutokana na kusafishwa na mvua.

"Ambakisye mpenzi wangu, hebu jifikirie wazazi wangu hawatanielewa kabisa."

"Atu unajua kabisa tatizo lipo wapi, mimi kama mimi sina uamuzi wowote, nimewaeleza lakini wamekataa."

"Umewaeleza na hali yangu?"

"Nimewaeleza lakini wamekataa kwa vile tayari walikuwa wameisha nitafutia mwanamke wa kuoa."

"Ambakisye nilikueleza mapema kuhusu hili na ulinikubalia lakini leo unanigeuka?"

"Atu siyo mimi ni wazazi wangu ndiyo walioamua hivyo, siwezi kwenda kinyume nao."

"Na hii hali nifanyeje?" Atuganile alisema huku akionesha tumbo lake lililokuwa na ujauzito wa miezi mnne wakati huo mvua ilikuwa ikiendelea kuwalowesha chapachapa .

"Basi tuitoe."

"Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya ujinga wa wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako hata wazazi

wangu wanajua wewe ndiye mume wangu, unafikiri watapokeaje taarifa hii. Nimewaficha toka uliponieleza, nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu.

Ukinipa (Like) nitaendelea sehemu ya pili kazi kwenu.

 

Attachments

  • wachawi.jpg
    wachawi.jpg
    10.4 KB · Views: 3,654
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI - 02

vita-jpg.167725



ILIPOISHIA : “Basi tuitoe.” “Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya ujinga wa wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho, kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako, hata wazazi wangu wanajua wewe ndiye mume wangu.
Unafikiri watapokeaje taarifa hii? Nimewaficha tangu uliponieleza nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu. SASA ENDELEA…

“ Ambakisye wazazi wangu nawajua vizuri, nikiwaeleza wanaweza kukufanya kitu kibaya, hebu kaa na wazazi wako waeleze kuwa mimi ndiye chaguo lako na haupo tayari kumuoa mwanamke mwingine!” “Hawezi kukubali kwa vile tayari wameshapeleka posa, kilichobakia ni ndoa tu.”

“Amba wazazi wako wasijejilaumu kwa uamuzi wao wa kikatili nikitoka hapa naenda kuwaeleza wazazi wangu, naogopa watakachokifanya kwa vile hawatakubali. Nataka kukuhakikishia hutamuoa huyo mwanamke.” “Sina jinsi kawaeleze litakalotokea watakuwa wamelitaka.”

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, giza nalo lilikuwa limeanza kuingia. Ambakisye na Atuganile ambao walikwenda porini tangu asubuhi ili kulijadili jambo lile ambalo lilimuumiza sana Atuganile.

*** Miaka mitatu nyuma katika Kijiji cha Ibungu katika Wilaya ya Ileje, Ambakisye na Atuganile walianzisha uhusiano wa kimapenzi ambao ulifahamika kwa familia zote mbili.
Lakini familia ya mzee Amangise anayotokea Ambakisye ilikuwa na chaguo lao lingine bila kumueleza mtoto wao.
Ila familia ya mzee Andendekisye anayotoka msichana Atuganile walijua kabisa mtoto wao ataolewa na

Ambakisye hata waliposikia mtoto wao mjamzito, hawakuwa na wasiwasi zaidi ya kujiandaa kwenda kwenye familia ya mzee Amangise kupanga jinsi ya watoto wao kuoana.
Atuganile, akiwa na furaha ya kupata ujauzito, alikwenda kwa mpenzi wake kumueleza hali yake ya ujauzito. Mwenzake alipokea taarifa hiyo kwa furaha na kumweleza kuwa atakwenda kuwaeleza wazazi wake ili wapange mipango ya ndoa yao.

Lakini ilikuwa tofauti kwa wazazi wa Ambakisye baada ya kuwaeleza hali ya mpenzi wake, alishangaa wazazi wake kumueleza habari nyingine kuwa wao tayari wamemchagulia mke ambaye muda huo walikuwa tayari wametoa posa na siku iliyokuwa inafuata ilikuwa ndiyo ya kwenda kujitambulisha.

Ambakisye alichanganyikiwa kutokana kauli ya wazazi wake na kuwaeleza kuwa mchumba wake tayari ni mjamzito. Lakini walimweleza kuwa hawawezi kubadili uamuzi kwa vile tayari walishatoa posa. “Wazazi wangu mbona mnanifanyia ukatili? Mnajua kabisa Atu ni mpenzi wangu na sasa hivi ana ujauzito wangu. Nitaieleza nini familia yao wakati niliwathibitishia kumuoa binti yao?”

“Imeanza lini mtoto kujitafutia mwanamke wa kuoa?” Wazazi wake walimuuliza. “Lakini wazazi wangu mnajua kila kitu, kwa nini mmefanya hivyo?” “Tumeshaamua jiandae na kesho asubuhi tuna safari ya Kilasilo ukweni kwenda kujitambulisha.” “Wazazi wangu japokuwa mimi ni mtoto wenu lakini hamkunitendea haki, mlitakiwa kunishirikisha kwanza.”

“Sisi wazazi ndiyo wenye haki kukutafutia mchumba kutoka katika familia bora si mke bora mke.” “Mmh! Sawa.” Ambakisye hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nao kwa shingo upande, lakini alijua ana kazi kubwa ya kumweleza mpenzi wake taarifa ile nzito itakayoujeruhi moyo wake. Siku ya pili alipelekwa Kijiji cha Kilasilo ukweni kutambulishwa kwa wazazi wa mchumba wake, mtoto wa familia ya mzee Ambokile.

Baada ya kufika huko Ambakisye alikutanishwa na mchumba wake aliyechaguliwa na wazazi wake. Alikuwa ni binti mzuri, lakini hakuwa chaguo lake kwa vile tayari alikuwa na mpango wa kuoana na Atuganile. Siku hiyo ilifanyika sherehe kubwa na kuchinjwa ng’ombe na pombe kunywewa kwa wingi.
Jioni walirudi kijiji kwao kwa ajili ya maandalizi ya harusi wa mtoto wao, Ambakisye hakulala pamoja na kwamba ulikuwa usiku mnene, alikwenda kwa mpenzi wake kumweleza kilichotokea siku ile. Alikuta familia ya mzee Andendekisye ilishalala.

Kwa vile chumba cha mpenzi wake alikijua alikwenda kugonga. Baada ya muda alisikia sauti ya Atu ikiuliza: “Nani?” “Mimi Amba.” “Ooh! Mpenzi wangu, leo ulienda wapi maana nilikutafuta sana,” Atu alisema huku akifungua mlango na kutoka nje.

“Nilitoka na wazee kidogo.” “Mmh! Umerudi saa ngapi?” “Hata dakika tano hazijakatika.” “Za huko?” “Nzuri, mbaya.” “Uzuri wake nini na ubaya wake nini?” “Uzuri tumekwanda salama tumerudi salama.” “Ubaya?” Atu alimuuliza huku akimtazama usoni akisaidiwa na mwanga wa mbalamwezi uliokuwa ukiwaka sana. “Ubaya wake, safari niliyopelekwa ilikuwa kwenda kuoneshwa mchumba.”

“Mchumba! Hapo sijakuelewa unamaanisha nini?” Atu alimsikia lakini hakumuelewa. “Wazazi wangu wamenipeleka Kijiji cha Kilasilo kunitafutia mchumba.” Je, nini kitatokea? Usikose kuwa nasi siku ya kesho hapa



 

Attachments

  • vita.jpg
    vita.jpg
    78.5 KB · Views: 12,280


HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI -03


ILIPOISHIA:
VITA YA WACHAWI - 03
“Uzuri wake nini na ubaya wake nini?”
“Uzuri tumekwenda salama tumerudi salama.”“Ubaya?” Atu alimuuliza huku akimtazama usoni akisaidiwa na mwanga wa mwezi uliokuwa ukiwaka sana.
“Ubaya wake, safari niliyopelekwa ilikuwa kwenda kuoneshwa mchumba.”
“Mchumba! Hapo sijakuelewa una maanisha nini?” Atu alimsikia lakini hakumuelewa.
“Wazazi wangu wamenipeleka Kijiji cha Kilasilo kunitafutia mchumba.”

SASA ENDELEA…

“Wewe uliwaambiaje?”
“Niliwashangaa kwa vile wanajua wewe ni mchumba wangu.”
“Au hujawaeleza hali yangu?”
“Niliwaeleza lakini waling’ang’ania uamuzi wao.”
“Mmh! Amba hili siwezi kuwaeleza mapema wazazi wangu, naomba ukakae tena na wazazi wako uwaeleze mimi na hali hii nitaolewa na nani?”
“Acha nijaribu lakini nina kazi kubwa.”
“Jaribu nina imani watakuelewa.”
“Haya mpenzi wangu usiku mwema.”
Baada ya Ambakisye kuondoka Atuganile alibakia amesimama mlangoni akiwa haamini taarifa zile, alijiuliza Ambakisye alikuwa akimtania au nini! Baada ya kupigwa sana na baridi alirudi ndani na kujilaza. Bado usingizi ulikuwa mbali kwa mawazo, alitoka nje kwenda kumuuliza Ambakisye alichokisema ni kweli au anamtania.
Pamoja na hali ya usiku ilikuwa imetulia lakini muda ule ilikuwa ikitisha kutokana na wazazi wa watoto pale kijijini waliwakataza watoto wao kutembea usiku.
Pamoja na woga wa Atu lakini asingelala mpaka apate ukweli wa maneno ya Ambakisye alichomueleza ni kweli au anamtania. Upepo wa usiku ulivuma kuongeza ukali wa baridi, alitembea huku mapigo ya moyo yakiwa juu. Kila aliposikia sauti tofauti aligeuka kuangalia nyuma huku akiongeza mwendo.
Alifika nyumbani kwao Ambakisye, alikuta wazazi wake hawajalala lakini wamo ndani kutokana na kusikia wakiongea. Alinyata kusogea katika chumba cha mpenzi wake na kugonga dirisha huku akiita “Amba…Amba.” Ambakisye alishtuka kusikia sauti ya mpenzi wake.
“Atu!” alishtuka.
“Abee.”
“Vipi mbona tena huku?”
“Amba bado sijaelewa.”
“Hujaelewa nini mpenzi wangu?”
“Uliyosema ni kweli au unanitania?”
“Atu ni kweli kabisa siwezi kukutania.”
“Mmh! Sawa.”
Atuganile alisema huku akigeuka kuelekea kwao huku akilia, Ambakisye alitoka na kumfuata kumbembeleza.
“Atu usilie, si umenipa kazi ya kuzungumza na wazazi wangu basi tusubiri.”
“Basi naomba asubuhi uzungumze nao ili saa nne nipate jibu.”
“Sawa.”
Ambakisye alimsindikiza mpenzi wake mpaka kwao na kurudi kulala.
***
Hakukuwa na mabadiliko yoyote toka kwa wazazi wa Ambakisye zaidi ya kusimamia msimamo wao. Atuganile siku ya tatu alimpitia mpenzi wake kwao asubuhi sana na kwenda naye porini ili wakayazungumze kwa kina. Baada ya kufika porini ambako waliingia ndani sana wakiamini watakuwa peke yao.
Wakiwa katikati ya mazungumzo wingu zito lilianza kutanda kitu kilichofanya Ambakisye amweleze Atuganile warudi kijijini.
“Atu wingu linaonesha mvua kubwa inashuka tuondoke mpenzi wangu.”
“Amba kwani mvua ikishuka kuna nini?”
“Inaweza kuwa kubwa na kutudhuru.”
“Kifo cha kunyeshewa na mvua si kikubwa kama familia yako ilivyoupasua moyo wangu bila ganzi.”
“Kwa hiyo?”
“Hata kama wazazi wako wameamua lakini nataka msimamo wako wewe juu yangu?” Atuganile alimkazia macho Ambakisye.
“Mimi nakupenda wewe.”
“Upo tayari kusema hivyo kwa wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Huwezi kuamini toka siku ile sijaieleza familia yangu, najua kwa jambo kama hili lazima tutajenga uadui mkubwa ambao unaweza kuleta maafa makubwa,” Atuganile alimtahadharisha Ambakisye.
“Hata mimi najua, lakini wazazi wangu wanajifanya wameweka pamba masikioni.”
Mvua ilianza kuteremka na kuwafanya wasogee chini ya mti mkubwa kujikinga japokuwa wasingeizuia kutokana na kasi yale iliyoteremka nayo. Atuganile pamoja na woga wa mvua lakini katika kuyatetea maumivu ya moyo wake hakuogopa kitu. Waliendelea kulowa huku radi na miungurumo mikubwa ikiendelea kulindima angani.
Kutokana na mvua kuwa kali iliyoambatana na upepo baadhi ya miti ilianza kukatika na kuzidi kuwatia hofu ya kutoka eneo lile salama.
“Amba, achana na mvua hebu niangalie upande wangu nitasimama wapi, wazazi wangu watapokea vipi habari za kushtua kama hizi?” Atuganile alisema kwa sauti ya kilio.
“Kwa kweli wazazi wangu hata mimi hawakunitendea haki.”
“Ambakisye hebu jifikirie mara mbili mpenzi wangu wazazi wangu nawajua mimi naogopa kutokea matatizo mazito hasa kwako mpenzi wangu.”
“Atu, unajua kabisa tatizo lipo wapi, mimi kama mimi sina uamuzi wowote, nimewaeleza lakini wamekataa.”
“Umewaeleza na hali niliyonayo kwa sasa?”
“Nimewaeleza lakini wamekataa kwa vile tayari walikuwa wameishanitafutia mwanamke wa kuoa.”
“Ambakisye nilikueleza mapema kuhusu hili na ulinihakikishia utanioa lakini leo unanigeuka?”
“Atu siyo mimi ni wazazi wangu ndiyo walioamua hivyo siwezi kwenda kinyume.”
“Na hii hali nitafanyaje?” Atuganile alisema huku akionesha tumbo lake lililokuwa na ujauzito wa miezi minne wakati huo mvua ilikuwa ikiendelea kuwalowesha chapachapa .
“Basi tuitoe.”
“Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako wazazi wangu wanajua wewe ndiye mume wangu unafikiri watapokeaje taarifa hii. Nimewaficha toka uliponieleza nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu.

Itaendelea kesho wakati kama huu
 
VITA YA WACHAWI-4
ILIPOISHIA:

"Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako, wazazi wangu wanajua wewe ndiye mume wangu, unafikiri watapokeaje taarifa hii? Nimewaficha tangu uliponieleza, nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu.
SASA ENDELEA…


"Ambakisye wazazi wangu nawajua, nikiwaeleza wanaweza kukufanya kitu kibaya, hebu kaa na wazazi wako waeleze kuwa mimi ndiye chaguo lako."

"Hawezi kukubali kwa vile tayari wameshapeleka posa, kilichobakia ni ndoa tu."
"Amba wazazi wako wasije kujilaumu kwa uamuzi wao wa kikatili, nikitoka hapa naenda kuwaeleza wazazi wangu."
"Sina jinsi, kawaeleze."

Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, giza nalo lilikuwa limeanza kuingia. Ambakisye na Atuganile walirudi kijijini, wakati huo mvua zilikuwa zimebaki za rasharasha.
***
Atuganile alirudi nyumbani kwao huku macho yamemvimba kwa kilio, alipofika nyumbani alimkuta mama yake yupo nje, baada ya kumsalimia aliingia ndani moja kwa moja chumbani kwake. Mama yake alishtuka na kuacha kazi zake na kumfuata, alipoingia chumbani alishangaa kumkuta mwanaye amekaa chini kichwa amekilaza kitandani mikono kichwani.

Kitendo kile kilimshtua sana mwanaye, kurudi amelowa, tena akiwa amechelewa bila kujua siku ile alikwenda wapi, japokuwa hawakuwa na wasiwasi kwa kujua yupo na mpenzi wake Ambakisye.
"Atu," alimwita kwa sauti iliyomshtua mwanaye ambaye alikimbiza mkono kwenye macho kufuta machozi.
"Abee mama," alijitahidi kuitika vizuri lakini sauti ilionesha alikuwa akilia.
"Kuna nini mwanangu, kwanza umeondoka alfajiri umerudi umenyeshewa na mvua, umefikia kulia, kuna nini?"
"Mama, hata sijui nikueleze nini unielewe."
"Niambie tu mwanangu nitakuelewa tu."

Atuganile alimueleza mama yake yote aliyoelezwa na mpenzi wake juu ya wazazi wa Ambakisye kumtafutia mtoto wao mchumba mwingine. Kauli ile ilimshtua mama yake na kutaka ufafanuzi zaidi.
"Wamemtafutia mwanamke mwingine, ulikataa kuolewa?"
"Hapana, anasema hata yeye alikuwa hajui kitu."
"Yeye kasemaje?"
"Japokuwa hakuafiki kitendo cha wazazi wake lakini hawezi kupinga."
"Na hali hiyo?" Alimuuuliza kuhusu ujauzito.
"Amenishauri niitoe."
"Akaja na mahala, usosye ulwanda? Ikulonda mwisukulu gwangu afwe?" (Hana akili, utoe mimba, anataka mkujukuu wangu afe?)
"Unasema wamesema wazazi wake?"
"Anatutania."
"Kweli mama, Jumapili walikwenda kutambulishwa ukweni."
"Mmh! Sawa, tuachie kazi hiyo naona hawatujui."
"Lakini mama msimfanye Ambakisye kama John."
"Wao si wamekuona hufai, basi tutaoneshana kazi."

(John ni mvulana aliyeanza naye mapenzi, lakini alikwenda jijini Dar na kupata mwanamke mwingine na kumuoa, alipoulizwa alionesha dharau. Haukuchukua mwaka, alipata ajali mbaya akiwa na familia yake iliyochukua maisha yao, ikiwa mkono wa wazazi wa Atuganile.) Mwanzo wa mapenzi kabla ya kumkubali alitaka kuhakikishiwa kuolewa.

Ambakisye alimhakikishia kumuoa ndipo Atuganile alipomkubali na penzi lao lilijulikana kijijini kwa kila mmoja kuamini wawili hao wataoana. Kukataliwa kwa Atuganile kulimchanganya sana na kuwa na wasiwasi na uamuzi wa familia kwa kuamini maisha na mpenzi wake yatakuwa hatiani.

Mama Atuganile alikwenda kwa mumewe aliyekuwa akirekebisha banda la nyumba sehemu iliyokuwa ikivuja mchana. Alimuomba waingie ndani, mzee Andendekisye aliingia ndani kumsikiliza mkewe, kwa vile nguo zilikuwa zimelowa maji alisimama wima kumsikiliza.

"Unasemaje mama Atu?"
"Leo familia ya Amangise imenikata maini," alisema akishika mkono kiunoni.
"Kuna nini?"
Alimueleza yote aliyoelezwa na mwanaye, baada ya kumsikiliza alisema:
"Aliyesema hayo ni wazazi au Ambakisye?" Alimuuliza mkewe.
"Ambakisye lakini yamesemwa na wazazi wake."
"Kwa vile kesho tulipanga kwenda kwao kwa ajili ya kuzungumzia hali ya mwenetu, nina imani kila kitu kitajulikana."
"Naona wamenisahau, nitaisambaratisha familia yote, nyumba ibakie gofu."
"Usiwe na haraka ya kufanya lolote, yote tutajua kesho."
"Yaani nilivyokasirika, Ambakisye jua la kesho asingeliona."
"Usiwe na pupa, twende kwanza tukawasikilize."
"Yaani bila wewe sijui ingekuwaje?" Mama Atuganile alisema huku akitweta.

Mama Atuganile jazba ilikuwa juu, siku zote mumewe alimshusha bila hivyo uamuzi wake huwa mbaya. Hata kifo cha John hakumshirikisha mumewe, alifanya mwenyewe, jibu lilikuwa baada ya tukio ndipo alipoielezea familia yake kuwa yeye ndiye aliyetenda.

Baada ya kukubaliana, alirudi chumbani kwa binti yake na kumueleza asiwaze sana kwani kesho wanakwenda kusikiliza kauli ya familia ya mzee Amangise.
****
Siku ya pili, mzee Andendekisye na mkewe walikwenda nyumbani kwao Ambakisye, walipofika walipokelewa vizuri. Kama zilivyo mila na desturi, walikaribishwa pombe ya chimpumu kwenye kopo kubwa la plastiki la lita moja.
"Jamani karibuni sana."
"Asante."

Baada ya kunywa kidogo, hawakutaka kupoteza muda, walisema kilichowapeleka pale.
"Jamani si wakaaji sana, kuna jambo limetuleta," alisema mzee Andendekisye.
"Ndiyo, jambo gani?" Aliuliza mzee Amangise.
"Nina imani unajua uhusiano wa vijana wetu wawili, Ambakisye na Atuganile."
"Ndiyo."
"Jana usiku kaja binti yetu kutueleza jambo ambalo kwa kweli limetushtua sana."
Je nini kitatokea?

tukutane siku ya kesho jioni.
 
Sasa hapa ina maana familiya zote mbili ni Wachawi.

Huyu mzee Andende na mkewe ni uchawi gani huo wa kujitangaza........

Ama kweli Dunia imetawaliwa na UShirikina kila kona....... Kama ni mimi ni heri kufa kuliko kuoa Binti wa Mchawi, kwani hamuwezi kuwa na maendeleo yoyote, na hata watoto mtakaozaa wataliwa nyama kichawi tu......



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
nasubiri inoge inaonekana itakuwa kaliii balaa :thumbup::thumbup::thumbup::thumbup:😕
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-5

ILIPOISHIA:
Baada ya kunywa kidogo hawakutaka kupoteza muda walisema kilichowapeleka pale.
"Jamani si wakaaji sana kuna jambo limetuleta," alisema mzee Andendekisye.
"Ndiyo, jambo gani?" aliuliza mzee Amanyisye.
"Nina imani unajua uhusiano wa vijana wetu wawili, Ambakisye na Atuganile."
"Ndiyo."

"Jana usiku kaja binti yetu kutueleza jambo ambalo kwa kweli limetushtua sana."

SASA ENDELEA


"Jambo gani?"
"Kuwa Ambakisye anataka kuoa mwanamke mwingine."
"Ni kweli Ambakisye anataka kuoa mwanamke mwingine toka Kijiji cha Kilasilo."
"Sasa wazazi wenzetu kwa nini mmechukua hatua hiyo wakati mnajua uhusiano wa vijana wetu?" aliuliza mzee Andendekisye kwa sauti ya utulivu.
"Unajua mzazi humtafutia mtoto wa kiume mwanamke wa kuoa, na si kijana kutafuta mwenyewe. Sisi tuliishamtafutia mtoto wetu mwanamke wa kumuoa muda mrefu ilibakia kujitambulisha tu," alijibu mzee Amanyise.
"Kama mlijua hivyo kwa nini hukumkataza mwanao asimpotezee muda mtoto wetu?" mama Atuganile alimwuliza.
"Nilijua ni urafiki wa kawaida si wa kuwa mke na mume kwa vile sote tunajua mtoto wa kiume hutafutiwa mchumba na wazazi wake kama wakiwa hai," alijibu mama Ambakisye.
"Kwa hali ya mtoto wetu itakuwaje?" (akimaanisha ujauzito wa Atuganile)
"Hilo si juu yetu mwanenu alitakiwa kuwa makini kwa vile hatukuwa na makubaliano ya kumuoa."
"Kwa hiyo tutamfanyaje na mwanenu ndiyo kisha mharibu mtoto wetu?" mama Atuganile aliuliza.
"Kwa vile ujauzito ni wetu tutaulea akijifungua tutachukua mtoto."
"Kwa hiyo mmeamua kumuharibia binti yetu maisha?" mama Atuganile aliuliza huku mumewe akiwa kimya akitafakari majibu ya wazazi wenzao.
"Tumemuharibia kivipi?" mama Ambakisye aliuliza yakabaki majibizano ya kina mama.
"Nani atakayemuoa wakati wakijua amezaa na fulani tena wa kijiji hikihiki, lazima watamtia kasoro mtoto wetu kuwa amezalishwa na kutelekezwa na kuolewa binti wa mbali."
"Sisi hayatuhusu, kama hivyo tuutoe ujauzito kabla haujajulikana."
"Kweli hamna huruma mnataka kuniulia mjukuu wangu?" mama Atuganile alikuja juu.
"Si ili mtoto wetu apate mchumba," mama Ambakisye alijibu kwa mkato.
"Jamani tusije kulaumiana kama mumeamua kumharibia maisha mwanetu."
"Hilo mnajua nyie mlitakiwa kumkanya mtoto wenu kabla ya ndoa."
"Mmh! Sawa," mzee Andendekisye alinyanyuka kwa hasira na kumshika mkono mkewe na kuondoka huku akigonga meza iliyokuwa na pombe iliyosababisha kumwagika, hawakugeuka waliondoka huku wakizungumza kwa hasira.
***Atuganile aliyekuwa amebakia nyumbani akiwa na shauku ya majibu ya familia ya mpenzi wake kwa wazazi wake. Akiwa amekaa uani aliwaona wazazi wake wakirudi huku mikono ikirushwa juu kuonesha walipotoka hapakuwa na maelewano.
Moyo ulimuuma alijikuta akiwa na hamu ya kusikiliza kilichojiri walipokwenda. Baba yake alipofika alikaa chini hakuwa na hamu ya kukaa juu ya kigoda na kumuomba binti yake maji ya kunywa huku mkewe akiingia ndani.
Atuganile alikimbilia maji ndani na kumletea baba yake, baada ya kunywa alishusha pumzi ndefu kitu kilichomfanya binti yake kuuliza:
"Baba kuna usalama mtokako?"
"Wao si wanajifanya wajanja sasa hivi sitii neno lolote kwa mama yako nitamuacha afanye anavyotaka. Watakuja hapa wanalia nasi tutawajibu kama walivyotujibu."
"Lakini baba Ambakisye yeye hana tatizo ila wazazi wake," alimtetea mpenzi wake.
"Wao si wanafurahi hali uliyonayo basi tutaharibiana tupate hasara wote."
Atuganile alijua hasira za wazazi wake hasa kama baba yake amekubali kulipa kisasi hakuna msalie mtume. Kwake yeye mpenzi wake Ambakisye alikuwa bado anamuhitaji katika maisha yake hakutaka atendewe lolote baya. Wazo lake lilikuwa kumpoteza mwanamke anayetaka kuolewa ili nafasi yake ibakie palepale.
Lakini aliogopa kuwaambia wazazi wake kwa kuonekana anataka kumuhukumu asiye husika, alitaka mpango wake aupange kimyakimya na haraka kabla wazazi wake hawajamfanyia kitu kibaya mpenzi wake. Moyo wake ulikuwa kwenye wakati mgumu juu ya uamuzi wa wazazi wake hakujua wanataka kufanya kitu gani hasa waliposema kila mmoja apate hasara.
Alipanga jioni kwenda kwa bibi Tumwambilile ambaye alikuwa mtu maarufu sana pale kijijini ili amsaidie tatizo lake ikiwezekana azungumze na wazazi wake ili wasimfanye chochote mpenzi wake pia ampe msaada wa kuzuia ndoa ya mpenzi wake na mchumba aliyechaguliwa na wazazi wake.
Wakati yeye akiwaza hayo wazazi wa mpenzi wake nao walikuwa na mikakati yao, walimwita mtoto wao na kumuweka chini ili wapange mipango baada ya kuona upande wa pili umekuja juu.
"Mume wangu tuwe makini najua hawawezi kutuelewa, lazima kuna kitu watafanya kulipa kisasi."
"Mi siwaogopi wakileta mchezo nitafyeka ukoo mzima, wao si wananunua uchawi? Mimi ninao wa kurithi."
"Unajua nini?"
"Hata sijui."
"Wao kisingizio kikubwa si ujauzito wa mtoto wao! Basi dawa yao ni kuutoa, ile dawa na kutega itafaa tena tunampa Ambakisye akaitege."
"Atakubali?"
"Tutamdanganya atakubali tu kazi hiyo niachie mimi."
"Hebu kwanza mwite tuzungumze naye."
"Wee! Ambakisye," mama yake alimwita.
"Naam mama."
Ambakisye alikwenda kusimama mbele ya wazazi wake.
"Unajua wazazi wa mwenzako wameondoka hapa hawapo katika hali nzuri? Kuna dawa tutakupa uende ukaitege mlangoni kwa mpenzi wako."
"Ili?"
"Kwa vile wameondoka na hasira wanaweza kuutoa ujauzito wa mpenzi wako."

"Sasa kama watautoa si ndiyo itakuwa vizuri! Ili tumalize lawama zao."

Itaendelea wakati kama huu ..........
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-6

ILIPOISHIA:
"Kwa vile wameondoka na hasira wanaweza kuutoa ujauzito wa mpenzi wako."
"Sasa kama watautoa si ndiyo itakuwa vizuri! Ili tumalize lawama zao."
SASA ENDELEA


"Hapana sisi hatupo tayari kumpoteza mjukuu, tunataka kuhakikisha anazaliwa, we hupendi mtoto?"
"Napenda, mbona mwanzo ulinishauri nimwambie atoe?"
"Tulitaka kumpima tujue ana msimamo gani."
"Sasa kwa nini nisimuoe kabisa."
"Hebu kwanza fanya hili, mengine tuachie."
"Sawa wazazi wangu," Ambakisye alikubali akiwa na matumaini ya wazazi wake kubadili uamuzi kwa kujua umuhimu wa yeye kuwa na

mtoto.
"Lakini fanya mpenzi wako asijue."
"Hakuna tatizo."
Baada ya makubaliano, Ambakisye alijawa na furaha moyoni mwake kuomba mambo kama yanataka kunyooka. Alipanga kwenda usiku

nyumbani kwa mpenzi wake kuweka ile dawa huku akimpoza kuamini wazazi wake walikuwa na kitu wanataka kukifanya juu yao.
Jioni ya siku ile, Atuganile aliondoka kwao bila kuaga anakwenda wapi na kwenda kwa Bi Tumwambilile. Alipitia kwenye Klabu ya

Mwangibile na kununulia Chimpumu lita tano na kumpelekea. Bi Tumwambilile alimpokea.
"Jamani Atu karibu mke mwenzangu."
"Asante bibi."
"Vipi mbona jioni, kwema utokapo?"
"Kiasi."
"Kuna nini?"
"Bibi mbona una haraka hebu kunywa kwanza pombe kidogo nimekuletea ndipo tuongee."
"Niwekee kwenye kikopo changu kipo juu ya kichanja."
Atuganile alikwenda kwenye kichanja cha kuaminikia vyombo na kuchukua kikopo cha kunywea pombe na kumwekea kiasi na kumpa.
"Karibu bibi."
"Asante," Bi Tumwambilile alipiga funda ndefu kuonesha alikuwa na kiu na kuweka kopo chini kisha alifuta mdomo na kumgeukia

Atuganile.
"Mmh! Umenipatia kweli nilikuwa na kiu cha kufa mtu."
"Nilijua ndiyo maana nilipitia kwa mzee Mwangibile kukuchukulia najua kiu kitaisha." Na kweli, haya niambie mjukuu wangu una

tatizo gani."
Kabla ya kumueleza kilichompeleka pale, alimueleza kisa kizima cha yeye kukataliwa na familia ya mzee Amangise wakati akiwa

mjamzito. Baada ya kumsikiliza, alishusha pumzi ndefu na kubeba kopo lake na kunywa kupiga funda tatu na kuweka chini.
"Mmh! Sasa kwa nini wamefanya hivyo?"
"Wanasema wamempatia msichana mwingine kutoka Kijiji cha Kilasilo."
"Ina maana wasichana wa kijijini kwetu hawafai, mbona wanatutukanisha hivyo?"
"Yaani bibi hata siwaelewi, kibaya zaidi nina ujauzito wa Ambakisye sasa mimi nitaupeleka wapi?"
"Ulitaka kuutoa?"
"Hapana."
"Kwa hiyo wewe ulikuwa unatakaje?"
"Kwanza nilikuwa nataka umwambie mama asimfanye kitu chochote mpenzi wangu, pili nilikuwa nataka kumpoteza yule msichana

anayetaka kuolewa na Ambakisye ili niolewe mimi."
"Sawa vyote vinawezekana."
"Kwa hiyo unaniambiaje?"
"Jibu lako njoo uchukue kesho na jina la huyu mwanamke anayetaka kuolewa."
"Sawa."
"Tulichozungumza usimwambie mtu yoyote."
"Sawa bibi."
"Nikamwambie mama aje umwambie?"
"Hapana nitaonana naye tu, hilo lisikukuumize akili."
"Nitashukuru bibi."
"Nilitaka kusahau."
"Nini bibi?"
"Kuna kitu nataka nikutume."
"Kitu gani?"
"Ukiweza nenda Kijiji cha Kilasilo katika mto Kiwila wa sehemu watu wanao chota maji ya kufulia na kuoga ili uchukue maji

yake na majani ya pembeni uniletee."
"Sawa bibi nitafanya hivyo."
Atuganile aliagana na bibi Tumwambilile na kurudi nyumbani, kwa vile ulikuwa muda wa kuandaa chakula cha usiku, alifikia

jikoni bila kuwaeleza wazazi wake alikuwa amekwenda wapi. Alifanya kazi zake akipanga usiku aende kwa Ambakisye akaulizie

jina la mwanamke anayetaka kumuoa ili kesho ampelekee bibi Tumwambilile pia kumuomba amsindikize Kijiji cha Kilasilo.
****
Majira ya usiku baada ya chakula cha usiku, wazazi wa Atuganile walikuwa na kikao chao kujadili kulichotokea asubuhi.
"Kama hutaki nifanye hivyo tufanyeje?" mama Atuganile alimuuliza mumewe baada ya kumkatalia hatua aliyotaka kuichukua kwa

Ambakisye baada ya kumtia mimba binti yao na kugoma kumuoa.
"Basi tumfanye asiwe karibu tena na wanawake."
"Timtie kichaa."
"Hapana watajua ni sisi."
"Mbona hiyo adhabu ni ndogo kuliko uliyotaka kuitoa?"
"Tufanye isiyoendana na tukio la kumtia mimba mtoto wetu."
"Nilikueleza awe mbali na wanawake kwa kumuua nguvu za kiume."
"Tutafanyaje bila kumshirikisha Atu ambaye siamini kama atakubali."
"Tutatengeneza uongo kwamba akifanya hivyo basi mpenzi wake hawezi kumuacha. Kwa vile hatujaonesha kukemea kilichotokea

itakuwa njia rahisi ya kutimiza dhamira yetu."


Itaendelea tena


 
Back
Top Bottom