HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-41
ILIPOISHIA:
Hakuamini kijana mdogo kama yule kumuumbua lakini alimshukuru kwa huruma yake. Usiku wa siku ile baadhi ya
wazee wenye imani ya kishirikina waliona wameumbuliwa walikodi vijana wa kijiji kile kumuhamisha kinguvu yule
mganga usiku uleule walihakikisha wanamtoa nje ya mji wa Kyela na kumwambia akirudi wanamuua.
Zoezi lile lilifanyika kwa siri hakuna aliyejua huku nyuma nyumba yake ikatiwa moto.
SASA ENDELEA...
Andendekisye baada ya kuumbuliwa japokuwa alisamehe, bado aliona sehemu ile si salama tena kwake kwa kuamini kila mmoja atamnyooshea kidole kwa yote yaliyotokea.Aliuza kila kilicho chake na kuhama mji wa Kyela na kuhamia sehemu nyingine ambayo hakutaka mtu yeyote ajue amekwenda wapi. Huo ukawa mwanzo na mwisho wa habari zake.
Lakini jirani yake Amangise yeye hakwenda popote, alibakia huku akiwa mwana kondoo aliyerudi zizini kwa kuokoka na mkewe. Lakini baada ya miaka miwili Amangise alifariki baada ya kupooza upande mmoja. Baada ya mazishi yaliyosimamiwa na kanisa, mke wa Amangise alichukuliwa na ndugu zake waliokuwa wakiishi sehemu iliyoitwa Ipinda.
Siku zote katika maisha yake alihubiri watu wamtegemee Mungu na si mwanadamu, pia kutumia busara kwa jambo lolote zito kwa kumtanguliza Mungu mbele. Kutokana na busara zake za kiutu uzima, kila majirani walipogombana alitumiwa kusuluhisha kwa kutumia kisa chake cha kweli mpaka naye mauti yalipomchukua na kuacha ushuhuda huu unaomaliza kuusoma leo.
Nashukuru wote tuliosafiri pamoja kwenye mkasa huu toka mwanzo mpaka mwisho, nina imani kuna kitu mmejifunza. Hakuna ategemewaye chini ya jua zaidi ya Mungu, hakuna amani kwa ncha ya upanga bali maelewano.
Dunia nzima watu wengi wamepoteza maisha na wataendelea kupoteza maisha kwa kutumia ubabe kuliko mazungumzo.
Muombe akupe busara na hekima na kumtanguliza yeye katika kila kitu hakika moyo wako siku zote utakuwa na amani. Siku zote
amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa. Mganga hutibu anayeteswa na si kuua au kuchukia maendeleo ya mwenzako ni uchawi. Mpende jirani yako kama nafsi yako amani itatawala milele, zingatia na kufanyia kazi, asante. Kwa kuacha shughuli zenu kunifuatilia Hadithi hii ya ajabu.
MWISHO THE END.