Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-30

IILIPOISHIA:Mganga hakutaka maiti ilale kwani ingemletea picha mbaya kwa wateja wengine, ilibidi kaburi lichimbwe usiku uleule na watu watatu kwa kupokezana mganga msaidizi wake na Amangise mwenyewe kwa vile wagonjwa waliokuwepo walikuwa wanawake watupu.
SASA ENDELEA...

IJapokuwa Andendekisye alikuwa na uchungu wa kifo cha mkewe lakini alilazimishwa na mganga kusaidia kazi ya kuchimba kaburi kisha waliuchukua mwili wa mke wa Andendekisye na kwenda kuuzika watu watatu usiku uleule. Baada ya kuzika walirudi nyumbani kwa mganga ambaye kichwa kilimuuma kwa kilichotokea, toka aanze uganga hakuwahi kutokewa na kitu kama kile.
Alipofika kilingeni kwake aliangalia rada zake, ajabu kila alipoangali ilikuja sura yake kuonesha ndiyo iliyofanya vile. Kila njia alitumia ili aone nani aliyefanya vile hakukuwa na jibu lingine zaidi ya kujiona yeye kuwa ndiye mhusika wa kifo cha mke wa Andendekisye.
Baada ya kuchemka alimwambia Andendekisye:
"Inaonekana jirani yako makombora ya mbali hayamuwezi nitaondoka na wewe mpaka kwako nikatege bomu langu karibu. Hawezi kunichezea akili sijawahi kuchezewa akili, naapa nikimshindwa naacha uganga."
"Yaani siamini kama ukishindwa nitakwenda popote ili nimtie adabu hawezi kunitia hasara mara mbili," Andendekisye alisema kwa uchungu.
"Tunaondoka muda huu ili mchana itukute Tanzania natega vyangu baada ya majibu naondoka usiku kurudi kwangu."
"Yaani nipo radhi kutumia kiasi chochote cha fedha hata kuuza shamba langu lote ili nimtie adabu."
"Wala hutaingia hasara yoyote majibu utayapata leo hii hii kama yeye anajua hivi sisi tunajua vile. Sijawahi kushindwa na kitu chochote, wachawi wote wanajua mimi ni nani. Kama kombora la mbali limemkosa sasa vita naihamishia Tanzania, kitu nitakachomfanya hakitasahaulika katika midomo kijijini Ibungu na vitongoji vyake na Tanzania nzima."
"Nataka pigo limalize mpaka kizazi chake chote hata kama kuna ndugu zake hakikisha unafagia mpaka sisimizi anayemuhusu.""Hiyo kazi ndogo, hata jengo analoishi litageuka kichunguu, amenichokoza huwa sichezewi, mimi ndiye mchawi niliyeogopwa mpaka na shetani," mganga alijitapa kwa hasira.
Baada ya mganga kuchukua makombora ya maangamizi, waliondoka alifajiri ile na kuacha wagonjwa chini ya wasaidizi wao huku akiwaeleza atarudi usiku wa siku ile ili kuendeleza tiba zao na kama kuna mmoja atakuwa bado hajapata nafuu japokuwa aliamini dawa aliyowapa ilikuwa ni nzuri, wamuongezee dozi.
Walipanda magari mpaka mpakani na kuvuka mpaka hadi Tanzania na kupitia baikeli yake mpaka Ibungu ambako walifika saa saba mchana wakati huo watu walikuwa katika maandalizi ya mazishi ya Ambakisye. Alipofika alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake na kuingia ndani.
"Mkuu taarifa wanazika saa kumi jioni," Andendekisye alimweleza mganga baada ya kudodosa habari za kijijini.
"Basi kazi itaishia makaburini wote watarudi na pumzi lakini si Amangise na mkewe, hilo kombora ni moja ya silaha, huzitumia kwa nadra hasa kwa watu wenye kutaka kupimana nguvu na mimi."
"Yaani nikisikia wamekufa mbona nitafanya sherehe, nitachinja ng'ombe wawili."
"Hiyo kazi ndogo namaliza kazi yangu kachague hao ng'ombe kabisa."
"Hilo halina tabu, yaani mpaka sasa nashindwa kulia kwa kifo cha mke wangu kipenzi, naona kama bado nipo ndotoni na asubuhi nikiamka naona kama zamelala pembeni yangu."
"Najua, lakini moyo wako wa kuvumilia unanipa nguvu ya kuifanya kazi vizuri."
"Nataka kilio changu kigeuke kicheko."
"Jioni haipo mbali."
"Sasa hivi sitasema kitu nasubiri majibu toka makaburi juu ya vifo cha Amangise na mkewe."
"Mmh! Sasa kazi ndiyo inaanza kabla hawajaenda makaburini. Nipatie unga, ungo na chungu."
Andendekisye alifanya vile haraka kwa kumletea mganga alivyoomba kisha alikaa pembeni. Mganga alifungua makombora yake na kutoa dawa aliyochanganya na unga na kipande cha ngozi ya chatu na kufunika kwa ungo.
Kisha alichukua dawa nyingine na kuchanganya na unga na kucha ya bundi na kuvifunika na chungu, walitoka nje na kuomba chungu kingine kipya.
"Nipatie kuku mwekundu."
Andendekisye aliingia bandani na kuchukua jogoo jekundu na kumpa mganga ambaye alimchukua na kumlisha hirizi ndogo kisha alimzika akiwa hai. Chungu alikichukua na kukiweka nyuma ya nyumba na kuomba kisu.
"Nichome tena kisu?" Andendekisye alishtuka.
"Hapana , kazi yote nafanya mimi kama bomu wacha linilipukie."
"Mmh! Hapo sawa, maana sasa hivi kisu nakiogopa sidhani kama nitachinja hata kuku katika maisha yangu kwani sasa hivi nikishika kisu nitakuwa kama namuua mke wangu."
"Ondoa wasi kazi yote nimeamua kuifanya mwenyewe wewe subiri majibu utajua huwa sibahatishi kwenye kazi yangu."Baada ya mganga kuchukua kisu na chungu kipya alikiweka nyuma ya nyumba na kukiweka kisu ndani ya chungu bila kitu chochote.
Kisha walirudi ndani na kumwambia Andendekisye. "Fungua kwenye chungu," alimwambia afunue chungu kilichowekwa dawa na kucha ya bundi.
Andendekisye alisogea kwenye chungu na kufungua, alishtuka na kusababisha kukidondosha chungu baada ya kumkuta bundi mkubwa ndani yake aliyetengenezwa na dawa alizochanganya mganga ambazo ziligeuka kuwa ndege huyo
"He!"
"Unashangaa nini?"
"Siamini."
"Kazi umeanza, hii ndiyo silaha itakayommaliza mke wa adui yako," mganga alisema huku akimtoa bundi na kumuweka pembeni kisha alimgeukia Andendekisye aliyekuwa bado amepigwa na butwaa baada ya kuona maajabu yale kwa mchanganyo wa dawa kutoa bundi.
"Hii nitafunua mwenyewe kwa vile unaweza kufa kwa mshtuko, utakachokiona usishtuke ni silaha za maangamizi."
"Kwani kuna nini?"
"Utaona tu."

Je, ni nini hicho, fuatilia jumapil ijayo.
 
Jamani hizi hadithi zinapatikana katika global publisher, yeyote anayetaka muendelezo wa hadithi hii na nyingine na aingie katika Google
 
Jamani hizi hadithi zinapatikana katika global publisher, yeyote anayetaka muendelezo wa hadithi hii na nyingine na aingie katika Google

Nashukuru mkuu,nimegoogle nimeiona.Kwakifupi alipofunua mganga akatokea chatu.
 
PC yake imekufa function ya kucopy na kupaste coz kule global anapocopy imefika episode 32.
 
[h=1]VITA YA WACHAWI-31[/h]

ILIPOISHIA:
"He!"
"Unashangaa nini?"
"Siamini."
"Kazi umeanza, hii ndiyo silaha itakayommaliza mke wa adui yako," mganga alisema huku akimtoa bundi na kumuweka pembeni kisha alimgeukia Andendekisye aliyekuwa bado amepigwa na butwaa baada ya kuona maajabu yale kwa mchanganyo wa dawa kutoa bundi.
"Hii nitafunua mwenyewe kwa vile unaweza kufa kwa mshtuko, utakachokiona usishtuke ni silaha za maangamizi."
"Kwani kuna nini?"
"Utaona tu."
SASA ENDELEA...
Mganga alisogea kwenye ungo na kufungua, Andendekisye kidogo atimue mbio baada ya kutoka chatu mkubwa.
"He!" alishtuka."
"Usishangae kazi ndo' kwanza imeanza, hili kombora litammaliza adui yako akiingia kaburini tu atakutana na hii kitu inamgonga bila watu kujua kisha inapotea."
"Mmh! Kweli unatisha, na hivi vingine?"
"Zote ni zana za maangamizi, hii ya kuku kuzikwa nayo itakuwa na kazi hukohuko makaburini kwani, kama la nyoka litashindwa basi hii itafanya azikwe akiwa hai."
"Azikwe akiwa hai! Kivipi?" Andendekisye alishtuka.
"Wakati wameinama kuzima kuna dongo litaanguka na kuwafukia wote."
"Mmh! Na ya chungu?"
"Ni kama tuliyotumia Matipa sasa hii ni dijitali kila kitu kitajiendesha chenyewe tukikuta damu tujue kazi imekwisha."
"Mmh! Sawa."
"Basi ngoja nitege tusubiri majibu."
"Sawa."
Mganga aliingia kwenye kazi ya kutega mabomu kwa kuwachukua bundi na chatu ambao aliwaweka sehemu moja na kuwafunika na shuka nyekundu kisha alichukua dawa na kunyunyizia juu huku akisema maneno yake baada ya sekunde chache vitu vile vilitoweka na kumfanya Andendekisye azidi kuchanganyikiwa na mambo ya mganga akiamini kiama cha Amangise kimefika.
"Vimeenda wapi?" Andendekisye aliuliza macho yamemtoka pima.
"Vimekwenda kufanya kazi iliyonileta Tanzania huwa sitaki mchezo kwenye kazi zangu, majibu utayapata jioni."Baada ya zoezi lile waliendelea na mambo mengine huku wakisubiri majibu kwenye mazishi ya Ambakisye.
KIJIJINI IBUNGU
Kama kawaida wanakijiji walikusanyika katika nyumba ya mzee Amangise kwa ajili ya kumsindikiza kijana wao Ambakisye aliyeondoka bado mbichi. Katika vitu vilivyokuwa tofauti siku ile ni mazishi ya Ambakisye kuzikwa kama muislamu bila sanduku na kaburi lake kuwekewa mwana ndani.
Pia hata maiti yake haikuvalishwa nguo ya kawaida ilivishwa sanda ya kawaida, yalikuwa maagizo ya mganga ili wachawi wasimle nyama. Baada ya misa ya mazishi kufanyika kisha kumuaga marehemu na kusababisha vilio kwa watu waliomfahamu Ambakisye na tabia yake ya upole kwa kuwajali wakubwa na wadogo.
Matayarisho yote yalikwenda vizuri muda ulipofika waliubeba mwili na kuupeleka makaburini huku wakina mama wakimsindikiza kwa vilio.

HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-31

Itaendelea Jumapili ijayo.................

Back
Top Bottom