Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

Hadithi ya kusisimua: Vita ya wachawi

HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-15

ILIPOISHIA:
“Sasa fanya hivi nitakupitia kwenu ili twende tukamchimbe bibi Tumwambile, nina senti kidogo najua atakubali kutueleza.”
“Sawa, basi mi nitakusubiri, muda mzuri jioni, nitakuwa nimemaliza kazi.”
SASA ENDELEA...


“
Poa.”
Walikubalia amweleze baba yake ili wajue atamsaidia vipi pia ampitie jioni waende kwa bibi Tumwambilile wakajue matatizo yao yanatokana na nini. Kwa vile Atuganile hakutaka wazazi wa mpenzi wake wamuone alitokea dirishani na kwenda kumsubiri Ambakisye kwa mbele.
Baadaye Ambakisye alitoka na kumfuata njiani na kumsindikiza lakini mama ya Ambakisye aliwaona kwa mbali wakisindikizana na kumwambia mumewe.
“Baba Amba.”
“Unasemaje?”
“Umemuona mwanao kumbe alikuwa na mwanamke wake.”
“Kapitia wapi?”
“Hata najua.”
“Umewaona wapi?”
“Si walee,” alimuonesha Ambakisye aliyekuwa akimsindikiza mpenzi wake kwa mbali.
“Mmh! Kazi ipo ndiyo maana hakushtuka sana tulipompa taarifa ya kupotea kwa mpenzi wake.”
“Nina wasiwasi hata mwanetu anahusika na mpango huu, yaani hakutoa hata chozi ndiyo kwanza yupo na mpenzi wake.”
“Kule kuonesha ameumizwa na tukio lile na kufikia hatua ya kutaka kupambana, kumbe muongo mkubwa.”
“Kama ni hivyo basi vita yetu itakuwa ngumu.”
“Wee fuatilia kwa mtu wako ili tujue tatizo lipo wapi?”
“Lazima nifanye hivyo.”
“Kabla ya kulipua hakikisha Amba hahusiki tusijelia mikono kichwani.”
“Lazima nifanye hivyo.”
Wakati huo Ambakisye alikuwa akirudi kutoka kumsindikiza mpenzi wake. Alipofika karibu, wazazi wake walibadilisha mada ili asijue walikuwa wakizungumza nini.
“Baba,” Ambakisye alimwita baba yake.
“Unasemaje?”
“Samahani njoo chumbani kwangu mara moja.”
Baba yake bila kusema kitu alinyanyuka na kumfuata mwanaye chumbani, walipoingia Ambakisye alimueleza baba yake tatizo lililojitokea jana usiku na muda mfupi. Baba yake alishtuka kidogo na kumuuliza:
“Hali kama hii imewahi kutokea mara ngapi?”
“Ndiyo mara ya kwanza kibaya hata sehemu za siri zinasinyaa.”
“Eti?” baba yake alishtuka.
“Ndiyo baba hali hii imenitisha, kitu cha ajabu imejitokeza kwa wakati mmoja usiku wa jana ilianza kwangu kisha mwenzangu kutoka ujauzito kitu ambacho kinanitisha.”
“Inawezekana kabisa familia ya mpenzi wako inahusika.”
“Baba hebu kwanza angalia tatizo langu mbona mnapenda kuwashutumu kila kitu?” Ambakisye alisema kwa jazba kidogo.
“Hebu teremsha nguo zako nione.”
Ambakisye aliteremsha kaptura aliyokuwa amevaa na nguo ya ndani na kumuonesha baba yake ambaye alishtuka kuona mambo yapo vile.
“He! Hili ni tatizo.”
“Vaa twende mtoni.”
Ambakisye alivaa nguo zake na kwenda mtoni ambako watu walikuwa wakitumia kuoga. Kauli ya baba yake ilimfanya kujiuliza amegundua nini mpaka kumweleza waende mtoni, hakujua wanakwenda kufanya nini. Njiani mzee Amangise alichuma majani na kuendelea na safari yao.
Walipofika mtoni walitafuta sehemu iliyokuwa imejificha, baada ya kufika sehemu hiyo ambayo ilikuwa na miti mingi, alimwambia mwanaye atoe nguo zote kama anataka kuoga.
Ambakisye alifanya kama alivyoelezwa na baba yake, alitoa nguo zote na kusubiri kuona baba yake anataka kufanya nini.
Mzee Amangise alichukua majani mabichi aliyochuma njiani na kuyafikicha kisha aliyazungusha sehemu za siri za mwanaye na kumwambia aingie ndani ya maji.
Baada ya kuingia ndani ya maji, baba yake aliangalia sehemu za siri za mwanaye. Hali aliyoiona ilimshtua sana na kumuuliza mwanaye akiwa bado yumo ndani ya maji.
“Amba hali hii imekuanza lini?”
“Baba si nimekuambia jana usiku.”
“Hapana ugonjwa huu huwa wa kuzaliwa si wa kuugua ukubwani kama ungeugua ukubwani kwa dawa niliyokufunga ingeonesha ni tatizo la kutibika, lakini kwa hali hii inaonesha kabisa hata tufanye nini huwezi kupona.”
“Baba kwani naumwa ugonjwa gani?”Ambakisye alishtuka.
“Ugonjwa wa kukosa nguvu za kiume wa kuzaliwa.”
“Hapana baba, siwezi kuugua ugonjwa huo kwa vile ni jana usiku tu wala sina muda mrefu.”
“Hebu toka ndani ya maji.”
Ambakisye alitoka ndani ya maji na kuvaa nguo zake, alijikuta akikosa raha kwa maneno ya baba yake. Ilibidi apate ukweli wa tatizo lake kwa kumuuliza baba yake.
“Baba una maanisha ugonjwa huu hauponi?”
“Watu wanaokuwa hivyo huwa hawaponi, huu ni wa kuzaliwa nao kwako nashangaa kusema ni jana na kuwa katika hali hii. Mmh! Nimeishajua, naona sasa wananichezea baada ya kumchukua kichawi mchumba wako sasa wamekugeukia mwenyewe.”
“Kina nani?”
“Kwani waliondoka siku ya kikao wakisema tutawaona wao kina nani?”
“Una maanisha familia ya kina Atu?”
“Ndiyo, walisema watakukomoa naona wametimiza azma yao.”
“Huenda basi nao wamelipa kisasi cha Atuganile kutolewa ujauzito.”
“Wala hiyo siyo sababu hebu tupitie kwa Mwakasanga tukaangalie tatizo nini.”
Walikubaliana kupitia kwa Mwakasanga mtaalamu wa tiba za jadi, walipofika waliingia ndani ili wamweleze tatizo lao.
“Karibuni, naona leo baba na mwanaye mmenitembelea?”
“Ndiyo ndugu yangu.”
“Mbona nyuso zenu zinaonesha kuna tatizo?”“Ni kweli.”


Itaendelea Kesho tena....
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-16

ILIPOISHIA:
Walikubaliana kupitia kwa Mwakasanga mtaalam wa tiba za jadi, walipofika waliingia ndani ili wamweleze tatizo lao.
"Karibuni, naona leo baba na mwanaye mmenitembelea?"
"Ndiyo ndugu yangu."
"Mbona nyuso zenu zinaonesha kuna tatizo?"
"Ni kweli."
SASA ENDELEA...


Baada ya kusema vile Mwakasanga aliangalia juu akiwa ameshika mkono kidevuni kwa muda na kucheka kidogo kisha aliuliza:
"Mmh! Mlikuwa mnasemaje?"
"Nina imani umeona kila kitu."
"Ndiyo, mlikuwa mnatakaje?"
"Umsaidie mwanangu pia kumjua aliyefanya hivi."
"Waswahili wana usemi wao kuwa moto mkubwa ulianza cheche."
"Unamaanisha nini?"
"Unajua vizuri kwa hiyo vita mnayoitafuta haitakuwa na mshindi zaidi ya kubakisha magofu ya miji yenu."
"Vita na nani?"
"Mzee Amanyisye we' mtu mzima unajua ulichokifanya na ndicho ulichofanyiwa."
"Kwa maana hiyo wamelipa kisasi?"
"Walaa hawajalipa ila wanajipanga kulipa kisasi ila kilichotokea ulipiga wakapiga kila aliyepiga amefanikiwa kutimiza alichokikusudia bila waliotumwa kujua wanaharibu."
"Nimekuelewa, sasa utanisaidia vipi?"
"Wewe ndiye mwenye uwezo wa kumaliza tatizo kwa kwenda kwa mwenzio ili muombane samahani bila hivyo nakuapia hakuna mshindi. Mnaweza kuona mlifanya kidogo ndicho kilichompoteza mchumba wa mwanao. Kama nilivyokwisha kusema mwanzo wa moto mkubwa ni cheche na ninavyokwambia tayari moto umeishaanza kuchoma pori sijui nani atapona."
"Sasa utanisaidiaje?"
"Unatakiwa kwanza usafishwe kwa vile sasa hivi umechafuka kila nitakachokufanyia hakitakusaidia. Siku zote nguo nyeupe inataka mwili msafi."
"Mmh! Sawa, na huyu?"
"Nitakupa dawa atumie kwa siku tatu ikishindikana itabidi nimtibu kichawi."
"Sawa."
Walikubaliana kupanga siku ya mzee Amanyisye kupelekwa mzimuni kutubu aliyoyafanya ili aweze kupewa tiba. Ambakisye alipewa dawa ya unga ya kunywa na kuelezwa atumie kwa siku tatu kisha arudi. Alichukua dawa na kuondoka na baba yake aliyeamini amemjua mbaya wake hivyo ni kuingia vitani kuwasambaratisha.
Wakiwa njiani wanarudi nyumbani, Ambakisye alikuwa na mawazo mengi juu ya kauli za mganga zilizoonesha familia zote mbili zilipigana makombora, moja akiwa amelibeba yeye bila kujua ambalo liliwalipua wenyewe. Alipanga akitoka hapo akambane Atuganile amweleze alipewa nini na wazazi wake kumpelekea bila yeye kujua.
Pia hakutaka kukaa kimya alimgeukia baba yake na kumuuliza:
"Baba kumbe dawa uliyonipa ndiyo iliyotoa ujauzito wa mpenzi wangu?"
"Nani kakwambia?"
"Si Mwakasanga amesema."
"Ulimsikia amesema mimi nilikupa dawa ya kutoa ujauzito?" mzee Amanyisye alikuwa mkali kidogo.
"Hata ukisema kwa ukali baba mmenikosea, hivi nisipopona nitakufa mgumba wakati tayari nilikuwa na mtoto wangu?" Ambakisye alimuuliza baba yake kwa uchungu.
"Ambakisye aliyozungumza mganga ni mengine kabisa hayahusiani na matatizo yenu," baba yake alipinda ukweli.
"Sawa ukweli utajulikana tu muda si mrefu."
"Nimekukataza kujishughulisha na mambo ya waganga unaweza kuambiwa adui ni baba au mama yako ili tu kutugombanisha."
"Sawa baba nimekuelewa," Ambakisye alikubali shingo upande.
Walipofika nyumbani baba yake alimhimiza kunywa dawa aliyopewa na mganga na kumuomba tatizo lake liwe siri yao mpaka walimalize pia hata mpenzi wake asimweleze kinachoendelea upande wao. Ambakisye alimkubalia lakini kichwani alikuwa anawaza tofauti.
Baada ya kunywa dawa aliachana na baba yake na kujipumzisha kusubiri jioni atakapokwenda na mpenzi wake kwa bibi Tumwambilile. Alijilaza kitandani lakini mawazo yake yalikuwa mbali kuhusiana na tatizo lake pia kutoka ujauzito wa mpenzi wake.
Aliamini cheche za moto zilizoteketeza msitu zilizosemwa na mganga ni baba yake.
Lakini aliamini yote atayajua akienda kwa bibi Tumwambilile kwa kumbana na kumuahidi zawadi nzuri.
****
Jioni kama walivyokubaliana na mpenzi wake alimpitia kwao na kwenda kumsubiri kwa mbele. Kwa vile macho ya Atuganile muda wote yalikuwa barabarani alipomuona mpenzi wake akipita alimuacha apite kisha alimfuata kwa kumziba machoni kwa kutokea nyuma yake.
Ambakisye alimvutia kwa mbele ya kumkumbatia, kila mmoja alionesha furaha kwa mwenzake kutokana na kushibana mioyoni mwao.
"Za muda?" Atuganile alimuuliza mpenzi wake.
"Mmh! Kiasi namshukuru Mungu."
"Vipi, baba alisemaje?"
"Mmh! Alishtuka sana, alinipeleka mpaka mtoni kunipima kwani hakuamini kusikia tatizo langu lilianza jana usiku. Amesema tatizo lile ni la kuzaliwa nalo anashangaa mimi kulipata jana."
"Kwa hiyo amesema tatizo lako linapona?"
"Ndiyo nimeanza kutumia dawa leo."
"Mungu atakusaidia mpenzi wangu."
"Asante, Eti Atu, wazazi wako walikupa nini uniletee bila wewe kujua madhara yake?"
"Kitu gani?" Atuganile alishtushwa na swali la mpenzi wake.
"Sasa mimi nitajuaje ukiwa ulikibeba wewe."
"Mmh! Kwani ndiyo sababu ya tatizo lako?" Atuganile alishangaa swali la mpenzi wake ambalo lilimtisha na kuamini kama atajulikana yeye ndiye anayehusika hivyo lazima penzi lao lingevunjika.
"Ndiyo," alijibu kwa kutojiamini huku vidole vikiwa mdomoni.
"Basi ndiyo iliyonimaliza."

"Mungu wangu! Basi watakuwa wamenidanganya."
"Kina nani?"
"Wazazi wangu."
"Wamekudanganya kivipi?"
"Waliniambia ni dawa ya kufanya usiniache, kama ni kweli naomba usiniache mpenzi wangu."
Kauli ya Atuganile ilirudi katika agizo alilopewa Ambakisye na wazazi wake ambalo halikuwa tofauti. Kutumia uongo kama ule alimuua mwanaye bila kujua basi ndivyo ulivyoumizwa na yeye. Kwa hiyo hakuona sababu ya kulaumu kwa vile alifanya bila kufahamu.
"Atu, siwezi kukulaumu najua tatizo lipo wapi," Ambakisye alimtoa hofu mpenzi wake.
"Najuta mpenzi wangu kukubali kitu nisichokijua," Atuganile alisema huku akilia kilio cha majuto.
Ambakisye alimbembeleza mpenzi wake na kumuomba waendelee na safari yao ya kwenda kumuona bibi Tumwambilile.

Je, watakapofika kwa bibi huyo kitajiri nini? Fuatilia Kesho...............
 
We mzizimkavu najua we ni Brazilian pole kwakipigo ila nakushauri toa kitabu Upo fit mwanangu god bless u.
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-17

ILIPOISHIA:
"Najuta mpenzi wangu kukubali kitu nisichokijua," Atuganile alisema huku akilia kilio cha majuto.
Ambakisye alimbembeleza mpenzi wake na kumuomba waendelee na safari yao ya kwenda kumuona bibi Tumwambilile.

SASA ENDELEA...

Walikubaliana kuondoka kwenda kwa bibi kwa kupitia kilabuni kwa Mwangibile kununua chimpumu ya lita mbili na kwenda nayo.
Walikwenda hadi kwa bibi Tumwambilile, walipofika walikuta hakuna mtu ila mlango upo wazi na katikati ya mlango kulikuwa na paka mweusi.
Kwa vile Atuganile alikuwa amepazoea pale, walipofika alimwita kwa sauti ya juu huku akiingia ndani na kumuacha Ambakisye nje.
"Bibiiii Tumwa."
Alimpita yule paka mweusi mlangoni na kuingia mpaka ndani na kuendelea kuita mpaka chumbani lakini hakukuwa na jibu la mtu, ilibidi atoke nje alipokuwa amesimama mpenzi wake na kumuita kwa sauti ya kukata tamaa.
"Mmh! Hayupo."
"Sasa atakuwa amekwenda wapi?"
"Hata najua, lakini mlango upo wazi inaonesha hayupo mbali."
"Basi tumsubiri."
"Mmh! Labda yupo nyuma ya nyumba."
"Kamuangalie."
Atuganile alizunguka nyuma ya nyumba ya bibi Tumwambilile lakini vilevile hakumuona, alirudi na kumueleza mpenzi wake.
"Hata nyuma ya nyumba hayupo."
"Basi tumsubiri lazima atakuwa karibu."
Walisogea pembeni kwenye gogo na kukaa kumsubiri bibi Tumwambilile, paka aliyekuwa mlangoni alitoka alipokuwa amesimama na kuzunguka nyuma ya nyumba.
Baada ya dakika moja alitokea bibi Tumwambilile nyuma ya nyumba akiwa amejifunga kaniki nyeusi mabega nje.
"Wajukuu zangu karibuni."
Kwanza walishtuka kwa vile muda mfupi hakukuwa na mtu, kisha waliitikia kwa pamoja.
"Asante bibi shikamoo."
"Marahaba, karibuni wapenzi."
"Asante."
"Nakuja," alisema huku akiingia ndani.
Baada ya kuingia ndani walijikuta wakitazamana na kila mmoja alinyanyua mabega juu. Baada ya muda alitoka bibi Tumwambilile akiwa amebadili nguo na kujifunga kitenge na kingine kujitanda juu. Alikaa kwenye kizingiti cha nyumba yake na kuwafanya Atuganile na mpenzi wake wasogee kwa kubeba kipande cha gogo cha kukalia.
"Karibuni wapenzi leo naona mpo pamoja," bibi alisema huku akiachia tabasamu la kizee.
"Asante bibi," waliitikia kwa pamoja.
"Leo jua litawaka usiku Ambakisye kuja kwangu."
"Hapana bibi, huwa napita lakini sikuoni.
"Mmh! Kuna kipi kimewaleta jioni?"
"Bibi kama tulivyozungumza nimeona leo nije na mwenzangu."
"Tulizungumza nini?"
"Kuhusu matatizo yetu."
"Kwani nilikuambiaje?"
"Ulisema nisiyachimbue sana kwa vile tumeshapona."
"Kipi kimebadilika?"
"Hali ya mwenzangu ndiyo bado inatuchanganya."
"Nilikuambia nini kuhusu tatizo lake?"
"Ile dawa niliyopewa na mama hakutumia alisema mpaka azungumze na baba yake, jioni tulipokutana alinieleza walienda kwa Mwakasanga," Atuganile alijisahau kuwa alimwambia mpenzi wake kapewa na bibi Tumwambilile.
"Yule mganga?" bibi Tumwambilile aliuliza.
"Ndiyo."
"Ehe."
"Basi kule sijui walielezwa nini na kupewa dawa nyingine ambayo kaanza kuitumia leo, kaambiwa baada ya siku tatu arudi kujua anaendeleaje. Ameniomba nije kwako ili utusaidie tujue tatizo lipo wapi."
"Sasa mbona unamuongelea kama yeye hana mdomo," bibi Tumwambilile alimgeukia Atuganile aliyeongea kwa niaba ya mpenzi wake.
"Amba hebu mwambie bibi ili atusaidie."
"Bibi nafikiri hakuna nitakachosema tofauti na aliyoyasema mpenzi wangu. Ni kweli bibi hali yangu ni mbaya na inaonekana kabisa matatizo yetu wazazi wetu wanahusika kwa asilimia kubwa kwa kutupa dawa kwa kutudanganya matokeo yake imekuwa madhara kwetu.
"Bibi nina imani wewe ni msaada mkubwa kwetu hebu tupe ukweli wa tatizo hili, japo hupendi tuchimbue lakini mambo mengi yapo wazi kwa vile kuna siri kubwa kwa wazazi wetu."
"Kwani mlipokwenda kwa Mwakasanga alisemaje?"
"Alimwambia baba kuwa alipiga naye kapigwa."
"Alipiga nini na kapigwa nini?"
"Inaonekana kutoka kwa ujauzito wa Atu, ulitoka katika familia yangu na mimi ndiye niliyemuua mwanangu bila kujua. Na hii hali niliyonayo inatoka katika familia ya mpenzi wangu naye aliniuliza bila kujua kama hali hii itanitokea. Pia alimuuliza kama ilikuwa wanalipa kisasi alijibiwa kuwa upande wa pili ndiyo wanajiandaa kulipa kisasi sasa sijui kisasi cha nini na kisasi gani.
Alimwambia kuwa vita ya familia mbili haitapata mshindi zaidi ya kubakisha magofu, suluhu ni familia mbili kukaa chini kumaliza tofauti zake. Kwa hiyo bibi naomba msaada wako."
"Msaada upi?"
"Kwanza kupata ukweli ya ninayowaza juu ya wazazi wetu, kipi kilipigwa toka pande zote. Na mwisho naomba kama yote ninayo yawaza yapo sawa basi wewe ndiyo usimame katikati kuiokoa vita ambayo naamini haina mshindi zaidi ya kufa wote."


Itaendelea kesho............
 
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-17

ILIPOISHIA:
“Najuta mpenzi wangu kukubali kitu nisichokijua,” Atuganile alisema huku akilia kilio cha majuto.
Ambakisye alimbembeleza mpenzi wake na kumuomba waendelee na safari yao ya kwenda kumuona bibi Tumwambilile.
SASA ENDELEA...


Walikubaliana kuondoka kwenda kwa bibi kwa kupitia kilabuni kwa Mwangibile kununua chimpumu ya lita mbili na kwenda nayo.

Walikwenda hadi kwa bibi Tumwambilile, walipofika walikuta hakuna mtu ila mlango upo wazi na katikati ya mlango kulikuwa na paka mweusi.
Kwa vile Atuganile alikuwa amepazoea pale, walipofika alimwita kwa sauti ya juu huku akiingia ndani na kumuacha Ambakisye nje.
“Bibiiii Tumwa.”

Alimpita yule paka mweusi mlangoni na kuingia mpaka ndani na kuendelea kuita mpaka chumbani lakini hakukuwa na jibu la mtu, ilibidi atoke nje alipokuwa amesimama mpenzi wake na kumuita kwa sauti ya kukata tamaa.
“Mmh! Hayupo.”

“Sasa atakuwa amekwenda wapi?”
“Hata najua, lakini mlango upo wazi inaonesha hayupo mbali.”
“Basi tumsubiri.”
“Mmh! Labda yupo nyuma ya nyumba.”
“Kamuangalie.”

Atuganile alizunguka nyuma ya nyumba ya bibi Tumwambilile lakini vilevile hakumuona, alirudi na kumueleza mpenzi wake.
“Hata nyuma ya nyumba hayupo.”
“Basi tumsubiri lazima atakuwa karibu.”

Walisogea pembeni kwenye gogo na kukaa kumsubiri bibi Tumwambilile, paka aliyekuwa mlangoni alitoka alipokuwa amesimama na kuzunguka nyuma ya nyumba.
Baada ya dakika moja alitokea bibi Tumwambilile nyuma ya nyumba akiwa amejifunga kaniki nyeusi mabega nje.

“Wajukuu zangu karibuni.”
Kwanza walishtuka kwa vile muda mfupi hakukuwa na mtu, kisha waliitikia kwa pamoja.
“Asante bibi shikamoo.”
“Marahaba, karibuni wapenzi.”
“Asante.”

“Nakuja,” alisema huku akiingia ndani.
Baada ya kuingia ndani walijikuta wakitazamana na kila mmoja alinyanyua mabega juu. Baada ya muda alitoka bibi Tumwambilile akiwa amebadili nguo na kujifunga kitenge na kingine kujitanda juu. Alikaa kwenye kizingiti cha nyumba yake na kuwafanya Atuganile na mpenzi wake wasogee kwa kubeba kipande cha gogo cha kukalia.

“Karibuni wapenzi leo naona mpo pamoja,” bibi alisema huku akiachia tabasamu la kizee.
“Asante bibi,” waliitikia kwa pamoja.
“Leo jua litawaka usiku Ambakisye kuja kwangu.”
“Hapana bibi, huwa napita lakini sikuoni.

“Mmh! Kuna kipi kimewaleta jioni?”
“Bibi kama tulivyozungumza nimeona leo nije na mwenzangu.”
“Tulizungumza nini?”
“Kuhusu matatizo yetu.”
“Kwani nilikuambiaje?”

“Ulisema nisiyachimbue sana kwa vile tumeshapona.”
“Kipi kimebadilika?”
“Hali ya mwenzangu ndiyo bado inatuchanganya.”
“Nilikuambia nini kuhusu tatizo lake?”

“Ile dawa niliyopewa na mama hakutumia alisema mpaka azungumze na baba yake, jioni tulipokutana alinieleza walienda kwa Mwakasanga,” Atuganile alijisahau kuwa alimwambia mpenzi wake kapewa na bibi Tumwambilile.
“Yule mganga?” bibi Tumwambilile aliuliza.
“Ndiyo.”
“Ehe.”

“Basi kule sijui walielezwa nini na kupewa dawa nyingine ambayo kaanza kuitumia leo, kaambiwa baada ya siku tatu arudi kujua anaendeleaje. Ameniomba nije kwako ili utusaidie tujue tatizo lipo wapi.”
“Sasa mbona unamuongelea kama yeye hana mdomo,” bibi Tumwambilile alimgeukia Atuganile aliyeongea kwa niaba ya mpenzi wake.
“Amba hebu mwambie bibi ili atusaidie.”

“Bibi nafikiri hakuna nitakachosema tofauti na aliyoyasema mpenzi wangu. Ni kweli bibi hali yangu ni mbaya na inaonekana kabisa matatizo yetu wazazi wetu wanahusika kwa asilimia kubwa kwa kutupa dawa kwa kutudanganya matokeo yake imekuwa madhara kwetu.
“Bibi nina imani wewe ni msaada mkubwa kwetu hebu tupe ukweli wa tatizo hili, japo hupendi tuchimbue lakini mambo mengi yapo wazi kwa vile kuna siri kubwa kwa wazazi wetu.”
“Kwani mlipokwenda kwa Mwakasanga alisemaje?”
“Alimwambia baba kuwa alipiga naye kapigwa.”
“Alipiga nini na kapigwa nini?”

“Inaonekana kutoka kwa ujauzito wa Atu, ulitoka katika familia yangu na mimi ndiye niliyemuua mwanangu bila kujua. Na hii hali niliyonayo inatoka katika familia ya mpenzi wangu naye aliniuliza bila kujua kama hali hii itanitokea. Pia alimuuliza kama ilikuwa wanalipa kisasi alijibiwa kuwa upande wa pili ndiyo wanajiandaa kulipa kisasi sasa sijui kisasi cha nini na kisasi gani.
Alimwambia kuwa vita ya familia mbili haitapata mshindi zaidi ya kubakisha magofu, suluhu ni familia mbili kukaa chini kumaliza tofauti zake. Kwa hiyo bibi naomba msaada wako.”
“Msaada upi?”

“Kwanza kupata ukweli ya ninayowaza juu ya wazazi wetu, kipi kilipigwa toka pande zote. Na mwisho naomba kama yote ninayo yawaza yapo sawa basi wewe ndiyo usimame katikati kuiokoa vita ambayo naamini haina mshindi zaidi ya kufa wote.”

Itaendelea kesho............

Raha ya utamu uchelewe kuupata kma hivi yan kma unautoa vile alaf unaubania...yan burudan... safi sana mzizimkavu...
 
  • Thanks
Reactions: MZK
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-18

ILIPOISHIA:
“Atuganile leo umetukosea heshima kutuita wachawi,” mama yake alikuja juu.
“Mama ninyi wachawi tena wabaya na mnajipanga kumuadhibu mpenzi wangu kosa lake nini?
SASA ENDELEA...


Nawaambia tumechoka kugeuzwa nyika kuumizwa kwa vita ya mafahari. Na pia nakuhakikishia Amba akifa mniue na mimi la sivyo watakufa wengi.”
“Unataka kutuua wazazi wako?” baba yake aliuliza.
“Muueni mpenzi wangu tumechoka kugeuzwa daraja la chuki zenu, hata kama nisingeolewa na Ambakisye kulikuwa na haja gani ya kumroga?”
“Atu, leo upo sawa au umekunywa pombe?” mama yake alishangazwa na ujasiri wa mwanaye.
“Kwani kuna neno gani hamkunielewa nimeliongea kilevi?”
“Nani kakuambia uongo huo?” mama yake aliuliza.
“Wazazi wangu nawaheshimu sana lakini kwa hili siwezi kukaa kimya kwa vile vita ya kichawi haina mshindi zaidi ya kubakia magofu tu. Kama mmechoka kuishi tuacheni sisi bado wadogo tuna hamu ya maisha. Kwani kila anayekupiga lazima umlipize ninyi si Wakiristo? Yesu aliwafundisha nini, ukipigwa shavu moja geuza na la pili, mbona hamfuati kila kitu lazima mlipe kisasi?”
Kauli ile iliwafanya wazazi wake wabaki kimya na kushangaa ujasiri wa mtoto wao na kujiuliza kautoa wapi pia aliyosema yote yalikuwa kweli. Ilibidi wawe wapole na mzee Andendekisye alimfuata mwanaye aliyekuwa akilia kwa uchungu na kumbembeleza.
“Basi mwanangu uliyosema tumekusikia na kutafanya kama unavyotaka, tulifanya vile kwa uchungu. Tusamehe sana hatukuwa na nia mbaya nawe ila kwa watu walio tudharau.”
“Baba naomba myamalize kwa vile vita yetu tunayeumia ni sisi watoto.”
“Sawa mama basi kapumzike kila kitu tutafanya kama unavyotaka.”
Atuganile huku akiendelea kulia aliondoka mbele ya wazazi wake huku moyo wake ukiwa mweupe huku akijiuliza mpenzi wake naye atazungumza nini na wazazi wake na watamuelewa vipi. Aliomba nao wawe tayari kukubali kosa na kujirudi ili tatizo liishe.
***
Ambakisye naye baada ya chakula cha usiku, aliwaita wazazi wake ambao walishangaa wito ule ulionesha una jambo zito moyoni mwake. Baada ya wote kukaa alianza kuzungumza.
“Wazazi wangu.”
“Ndiyo mzee.”
“Wazazi wangu toka nilipotoka tumboni kwa tumbo la mama yangu sijawahi kuwavunjia heshima.”
“Ni kweli, leo baba unataka kutuvunjia heshima?” mama yake alitania.
“Hapana na sitawahi ila nilitaka kuwauliza jambo moja.”
“Jambo gani?”
“Kuhusu ugomvi wenu na familia ya mzee Andendekisye nini hatima yake?”
“Mpaka atakapopatikana mshindi,” mzee Amangise alijibu kwa mkato.
“Sasa hii vita nani anayeumia kati yenu na sisi watoto?”
“Hiyo si juu yako, wewe ni mtoto sisi wazazi wako tunajua tunachokifanya.”
“Kwa hiyo mlipomuua mwanangu mlijua mnachokifanya, halafu kibaya mkanituma kumuua mwanangu bila kujua. Hivi ninyi ni wazazi wangu kweli mnaidhuru damu yangu? Nilitegemea ninyi ndiye wa kulea wanangu, kwa bahati mbaya kama Mungu akinichukua lakini kumbe ndiye maadui zangu wakubwa.
Sasa nimefahamu ule moto uliosemwa unataka kuwaka na kuunguza kila kitu, cheche ni ninyi wazazi wangu, na bado mnataka kuendeleza vita ya nini ina faida gani kwenu. Basi tumieni miili yenu kuliko kutumia miili yetu katika mateso,” Ambakisye aliwapa makavu laivu wazazi wake.
“Ambakisye wewe mtoto mdogo hujui kitu, mchumba wako kauawa na familia ya mpenzi wako unaona kitu cha kawaida. Mimi ndiye Amangise Mwanambo huwa sirudi nyuma mtu akinianza lazima nimalize.” Mzee Amangise alijitapa.
“Mmh! Sasa nasema hivi chochote kitakacho mtokea mpenzi wangu au familia yao hakikisheni na mimi mnaniua kama si hivyo mimi ndiye nitakuwa adui yenu namba moja.”
“Acha vitisho vya kitoto, wewe mtoto utabakia kuwa mtoto.”
“Mimi si mtoto, hata haya matatizo yangu chanzo ni wewe kwa nini hawakukupiga wewe wananiumiza mimi kwa kiburi chako?”
“He! Amba una tatizo gani?”mama mtu alishtuka kauli za mwanaye.
“Mimi sasa hivi sina tofauti na mwanamke,” Ambakisye alisema kwa uchungu huku akilia.
”He! Umefanya nini?” mama yake alishtuka.
“Sehemu zangu zimekufa na yote sababu yenu.”
“Mungu wangu! Imeanza lini?”
“Siku ambayo wazazi wangu mlishiriki kumuua mwanangu.”
“Mmh!” maneno yalikuwa mazito.
“Wazazi wangu siamini, tena leo baba kaambiwa kuwa chanzo ni cheche na suluhu ni kuelewana na si nguvu za kichawi.”
“Unamuamini vipi mganga?” baba yake aliingilia kati.
“Basi naomba kuanzia leo mnitoe kwenye familia yenu nitahangaika kivyangu. Nina imani kwa nguvu za Mungu nitapona na nguvu zenu za kichawi zitashindwa. Kuanzia leo ukitaka kupigana na familia ya mzee Andendekisye tafuta ugomvi mwingine si kuhusu mimi.
Naomba nikinyanyua mguu wangu hapa nifuteni katika akili zenu, mkiweza kuniroga nirogeni nife lakini Mungu ataniongoza siku zote haki ya mtu haipotei.
“Pia nakuombeni nikifa msije kunizika hata kama nitaoza au nikiliwa na wadudu,” baada ya kusema vile aligeuka na kuelekea chumbani kwake na kuwaacha wazazi wake wakiwa wamepigwa bumbuwazi.
“Baba Amba umemsikia mwanao?”
“Mmh! Alipofikia sehemu inatisha, au amekunywa?”
“Kwani aliyosema kuna la uongo?”
Wakiwa katikati ya mazungumzo Ambakisye alitoka na begi lake, hali ile ilimfanya mama yake kukimbia mbio na kwenda kujitupa mbele ya mwanaye.“Amba mwanangu unataka kufanya nini, kwa nini
unachukua uamuzi mkubwa kama huo?”
“Nina imani mnaye mtoto mwingine naomba niwaache na maisha yenu nikifa Mungu atanisitiri.”
“Hapana baba usiondoke linazungumzika.”
“Kwani nikiondoka kuna mtakachopungukiwa, kama mateso ya vita yenu napata mimi, heri niondoke ili nife na Mungu wangu.”
“Ambakisye mwanangu ni hasira tu baba, nimekusikia mwanangu nipo tayari kuyafanya yote. Usiondoke tupo chini ya miguu yako,” mzee Amangise naye aliungana na mkewe kumuomba mtoto wao asiondoke.


Itaendelea kesho...
 
msimamo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku, ahsante mr. dry root
 
Back
Top Bottom