Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

ILIPOISHIA :
“Hebu subiri , ” alisema na kuziba sehemu ya
kuzungumzia na kumgeukia Mage .
“Eti Mage mwili wa Colin umepelekwa hospitali
gani?”
“Mama sijasema amekufa ila watu wanafikiria
hivyo, ” Mage alimgeuka mama yake .
“Sasa kapelekwa wapi ?”
SASA ENDELEA .. .
“Mama mwambie amekimbizwa Muhimbili, ila
usimwambie yupo kwenye hali gani mengine
atayajua hukohuko mwenyewe.” Baada ya
kuzungumza na mwanaye aliachia sehemu ya
kuzungumzia na kuzungumza na mama Colin.
“Anasema baada ya ajali wasamaria wema
wamewapeleka Muhimbili.”
“Wanasema hali yake ipo vipi ?”
“Hawajajua kwa vile amebebwa na kuingizwa
kwenye gari na kuwahishwa hospitali.”
“Na ..na. . Cecy ?”
“Sijajua hebu subiri ... Eti Cecy alikuwepo ?
Alimuuliza mwanaye.
“Ndiyo.”
‘‘Ndiyo walikuwa pamoja .”
“Na ..nashukuru dada .”
“Nami nakuja huko .”
“Sawa tutakutana .”
Baada ya kukata mama Mage alinyanyuka
kuelekea chumbani kuchukua funguo ya gari,
baada ya kuchukua alitoka nje na Mage alitoka
kumfuata mama yake waliingia kwenye gari na
kutoka kuelekea Muhimbili. Muda wote Mage
alikuwa akilia kitu kilichomfanya mama yake
kuingilia kati .
“Unasema hajafa unalia nini mbona unamchuria
mwenzio. ”
“Mama inauma Colin ndiye lilikuwa tumaini
langu mwisho.”
“Muombee basi apone. ”
“Yaani Mungu asikie dua yangu, Colin apone
lakini mchumba wake afe .”
“Wee mtoto roho gani hiyo?”
“Mama wakipona wote sina changu . ”
“Hebu achana na mawazo, ” mama Mage
alisema huku akikanyaga mafuta kuwahi
hospitali.
Mama Colin baada ya kuzipata taarifa zile
alimpitia mama Cecy aliyekuwa hana taarifa
zozote kwa kujua mwanaye alikwenda mazoezi
asubuhi na mpenzi wake . Naye alishtuka lakini
mama Colin alimpa moyo wafike hospitali ili
wajue kipi kinaendelea japokuwa hakujua
watoto wao wapo kwenye hali gani.
Walijikuta wakifika pamoja na Mage na mama
yake, waliongozana wote mapokezi kuulizia
taarifa za wagonjwa wao . Waliambiwa wote
wamekimbizwa chumba cha wagonjwa
mahututi kwa vile hali zao si nzuri . Walikwenda
kuonana na mganga mkuu , aliwakaribisha
ofisini kwake.
“Ndiyo wazazi wangu kwanza poleni sana .”
“Mmh ! Hatujapoa kwani hatujui hali za watoto
wetu,” alijibu mama Colin .
Dokta Bukos kwanza alitulia kama anasoma
taarifa kwenye karatasi kutafuta neno la
kuwaeleza ili wasipagawe kutokana na hali za
wagonjwa wao. Baada ya kutulia kwa muda
alinyanyua uso wake na kusema kwa sauti ya
upole.
“Wazazi wangu hali za wagonjwa si mbaya
wala nzuri sana lakini bado tunapigania maisha
yao .”
“Lakini baba mtu mpaka kuletwa chumba cha
wagonjwa mahututi lazima hali yake ni mbaya
sana?” aliuliza mama Colin .
“Ni kweli , chumba hicho ni kwa ajili ya
uangalizi wa karibu kwa mgojwa.”
“Kwani hali zao zikoje?” aliuliza mama Cecy .
“Bado kwa vile wameletwa hawajitambui hivyo
kwanza tunashughulika na suala la kurudisha
ufahamu kisha tutajua tufanye kitu gani. ”
“Mbona nilisikia wamekufa ?” Mage aliropoka .
“Si kweli , kama wangekuwa wamekufa wodini
tumewapeleka kufanya nini ?” daktari alijibu
kwa ukali kidogo.
“Wee Mage acha kuropoka ,” mama yake
alimkanya.
“Jamani naomba kuzungumza na wahusika wa
wagonjwa wengine msubiri nje ,” daktari
alisema.
Mage na mama yake walitoka nje na kubakia
mama Colin na Cecy, baada ya kubakia wawili
dokta alitaka kujua uhusiano wa waliobakia na
wagonjwa. Wote walijitambulisha .
“Basi wazazi wangu ajali waliyopata ilikuwa
mbaya sana , majeraha si makubwa sana lakini
inaonesha wamejigonga kwenye kitu kigumu
wakati gari likipata ajali hivyo kusababisha
mtikisiko wa ubongo uliopelekea kupoteza
fahamu . Lakini tunahangaika ili kurudisha
fahamu zao .”
“Zitachukua muda gani kurudi?” mama Cecy
aliuliza.
“Hatuwezi kujua ubongo umecheza kiasi gani ,
lakini msiwe na wasiwasi hii ni hali ya kawaida
kwenye ajali za namna hii,” dokta aliwapa
moyo .
“Tunaweza kwenda kuwaona ?” aliuliza mama
Cecy.
“Kwa leo bado kuna baadhi ya mambo
tunashughulika nayo kuanzia kesho mna nafasi
ya kuja kuwaona. ”
“Sawa .”
Mama Colin na mama Cecy walitoka ofisini kwa
mganga mkuu na kukutana na Mage na mama
yake wakiwasubiri , walipotoka waliwauliza.
“Vipi wanasemaje ?” Mage alikuwa wa kwanza
kuuliza.
“Bado wapo chini ya uangalizi maalumu ,” alijibu
mama Colin .
“Hatuwezi kuwaona ?” mama Mage aliuliza .
“Kwa leo haiwezekani.”
“Mmh ! Basi watakuwa wana hali mbaya sana ,”
Mage alisema.
“Anayejua ni dokta , sisi hatujui kwa vile
hatujawaona, ” alijibu mama Colin ambaye
alionesha kuchoshwa na maswali ya Mage .
“Jamani hatuna cha kufanya maombi yetu yote
yawe kwa watoto wetu ili Mungu awaepushe
na matatizo yaliyo mbele yao ,” alisema mama
Mage .
“Ni kweli dada yangu ,” alisema mama Cecy
ambaye muda wote alikuwa kimya kutokana na
mshtuko alioupata kwa ajali ya watoto wao.
Walikubaliana kurudi nyumbani mpaka kesho
ambayo wangerudi kuwaona , mama Mage
aliwashauri wote waongozane nyumbani kwa
mama Colin kufanya maombi ya pamoja ili
Mungu awaepushe na matatizo yale.
Waliongozana wote hadi nyumbani kwa mama
Colin ambako walifanya maombi ya pamoja
yaliyoongozwa na mama Mage .
 
Mkuu hebu endelea kidogo hadithi hii ina muda haijaendelezwa.
 
Wakili wa Moyo-36



ILIPOISHIA:
“Colin nasema hivi, kila usemalo ni kweli tupu na una haki yoyote ya kufanya lakini kumbuka penzi halilazimishwi, nina imani umenielewa, kuwa mstaarabu tuachane kwa usalama.”
SASA ENDELEA…


Mage alinyanyuka na kumsogelea Colin aliyekuwa ameinama akilia na kumpigapiga mgongoni.

“Sweet naomba usilie mwanaume kaumbwa kukabiliana na matatizo, hili ni moja wapo.”

Colin alinyanyuka kama mbogo na kumsukuma Mage aliyeanguka chini huku akibwata.

“Muongo mkubwa, mnafiki unanipaka mafuta kwa mgongo wa chupa, eti sweet.”

“Huwezi amini Colin nakupenda sana japo Hans nampenda zaidi, nipo tayari kulipa gharama zote za maandalizi ya harusi yetu pia hata kulipa gharama zozote ili kuhakikisha nawe unakuwa na mke atakayeziba pengo langu.”

Mage pamoja na kusukumwa, hakukasirika akaamka pale chini, Colin hakumjibu neno lolote zaidi ya kuinama huku akilia.

Mage alimshika mkono na kumnyanyua, alimtazama kwa macho yaliyojaa machozi na kusema kwa sauti ya chini.

“Colin nisamehe sana siwezi kuwa mnafiki mapenzi nayajua, nipe ruksa mpenzi wangu. Nilikuja huku ili tupate muda wa kulizumgumza hili, sikutaka tulizungumze juujuu. Nakupenda lakini sitaki nikutese kwa kukunyanyasa kimapenzi kwa vile mapenzi nayajua yanavyoumiza.”

Colin alitulia huku akimtazama Mage aliyekuwa akitia huruma, alijiona mjinga kulazimisha mapenzi. Alikohoa kidogo na kusema:

“Sawa nimekuelewa.”

“Nashukuru.”

“Kuna la zaidi?” Colin alimuuliza Mage.

“Hakuna.”

“Tunaweza kuondoka.”

Walichukua vitu vyao na kuelekea nje kwenye gari ili warudi mjini.
***
Cecy baada ya kutoka twisheni, alisimama chini ya mti kuagana na shoga yake huku wakijikumbusha baadhi ya mada walizopewa wakasome nyumbani. Alikuwa amepiga hatua kubwa katika kusoma na kuandika hata kuzungumza lugha ya Kingereza baada ya kusoma kwa uchungu mkubwa.

Siku zote aliamini kumkosa Colin kulitokana na kukosa elimu, kwake umaskini hakuuona sababu kama angekuwa na elimu yake ambayo hata mama Colin angeiheshimu.

Toka aanze kusoma alionekana ndiye mwanafunzi aliyetaka kujua lugha, kuisoma, kuiandika na kuizungumza.

Japokuwa hakukijua sana Kiingereza lakini aliweza kumsikia mtu na kumuelewa hata kumjibu mawili matatu, ile ilimpa kiburi cha kuzungumza muda wote hata alipokosea hakujisikia vibaya kwa vile alielekezwa. Baada ya kujadiliana na shoga yake, alisogea mbele kuelekea njia ya kwao japo palikuwa mbali kidogo lakini hakujali umbali ule kutembea kwa miguu kwa vile alikuwa akitafuta kitu.

Siku zote aliingia darasa la mchana kwa vile asubuhi alikuwa akienda kwenye biashara zake.

Ada ya mwanzo alitumia fedha aliyoachiwa na Colin siku aliyompeleka kwao na kuwaacha kwenye mataa kwa ahadi tamu ya kuyabadili maisha yao. Alikumbatia daftari lake na kutembea taratibu kukifuata kichochoro cha kuingilia njia ya mkato. Aliangalia saa yake, ilimuonesha ni saa kumi na moja na nusu jioni.

Alishtushwa na sauti ya gari aina ya Nisan Patrol New Model jeupe lililosimama nyuma yake, alipogeuka aliona msichana akiteremka kwenye gari huku akibwata kwa sauti kuonesha anazozana na mtu ndani aliye ndani ya gari.

Alipomuangalia aligundua ni Mage, mwanamke aliyezima ndoto zake za kuwa mke wa Colin. Alisimama nyuma ya mti kumuangalia, alimsikia akisema kwa sauti:

“Wewe mtu gani unayelazimisha mapenzi, nimekueleza ninaye ninayempenda hutaki kunielewa. Naomba uteremke kwenye gari langu, siwezi kutembea na mtu asiyeelewa. Sasa hiyo elimu uliyosoma inakusaidia nini ikiwa hutambui nini maana ya upendo?

“Nasema teremka la sivyo nitakuachia gari niondoke zangu.”

Baada ya muda, Cecy alishtuka kumuona mwanaume aliyekuwa akiambiwa vile ni Colin, baada ya kuteremka kwenye gari kinyonge, alisogea pembeni na kusimama bila kujua nyuma yake yupo Cecy.

Cecy roho ilimuuma kuona mtu ampendaye anadhalilishwa vile. Colin alitokwa na machozi kitu kilichozidi kumuumiza moyo Cecy na kushangaa watu ambao muda si mrefu walitegemea kufunga ndoa lakini ajabu mwanamke anatoa maneno makali kama yale ya kumdhalilisha mumewe mtarajiwa.

Alitulia aione sinema ile inaishaje kwa kujificha nyuma ya mti ili wasimjue, baada ya muda alisikia sauti ya Colin.

“Mage pamoja na hayo lakini kumbuka ...



Itaendelea............

Duh hatar
 
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Walikubaliana kurudi nyumbani mpaka kesho ambayo wangerudi kuwaona, mama Mage aliwashauri wote waongozane nyumbani kwa mama Colin kufanya maombi ya pamoja ili Mungu awaepushe na matatizo yale.
Waliongozana wote hadi nyumbani kwa mama Colin ambako walifanya maombi ya pamoja yaliyoongozwa na mama Mage.
SASA ENDELEA...

Walipiga magoti na kushikana mikono kisha mama Mage alishusha maombi.
"Baba Mungu tumepiga magoti mbele yako, tunajua hakuna chochote chini na juu ya jua kiwezacho kufanyika bali kwa idhini yako.

Baba Mungu lisilowezekana kwa mwanadamu kwako linawezekana, lililo zito kwa mwanadamu kwako ni jepesi. Eeh, Baba tunaomba uwaepushe watoto wetu na matatizo mazito kama ulivyoweza kumuepusha mwanao mpendwa pale msalabani.
Kama ulivyoweza kumponya Ayubu na maradhi ya ajabu ambayo alipona kupitia uweza wako. Baba Mungu unaweza kumponya aliye mahututi, unaweza kumfufua aliyekufa, kwako wewe hakuna kinachoshindikana.
Baba waponye wenetu ambao hatujui hali zao ni wewe pekee mwenye uwezo wa kuugeuza usiku ukawa mchana basi yaondoe maradhi milini mwao wape afya njema.
Baba vunja pepo wa maumivu, vunja pepo wa mauti, vunja pepo wa maradhi kwa jina la mwanao Yesu Kristo aliyehai. Amen."

"Ameni," waliitikia pamoja.
Baada ya maombi walinyanyuka na kukaa kwenye makochi, kwa vile hawakuwa na la kuzungumza mpaka siku ya pili watakapokwenda kuwaona wagonjwa wao. Mama Mage na mwanaye waliaga na kuondoka kurudi nyumbani na kuwaacha mama Colin na Cecy wakiwa wamekaa kila mmoja akiwaza lake.
***
Siku ya pili alfajiri walikutana wote Hospitali ya Muhimbili kwa vile daktari alikuwa hajafika ilibidi wamsubiri hadi saa moja asubuhi alipofika, alipowaona aliwaeleza wasubiri ili afike wodini kwanza.
Dokta Bukos baada ya kuwazungukia wagonjwa wote na kuchukua taarifa kutoka kwa daktari wa zamu, aliwafuata kwenda kuwaona wagonjwa wao.

Waliingia mmojammoja kutokana na taratibu za kuingia Chumba cha Maalum cha Wagonjwa Mahututi (ICU). Colin alikuwa akipumulia mashine akiwa amelala bila kutikisika. Lakini Dokta Bukos aliwaeleza kuwa kidogo ameanza kupata fahamu kwa misuli ya mwili kuanza kufanya kazi taratibu japokuwa hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya kulala vilevile walivyomkuta.
Katika chumba kingine, Cecy naye alikuwa vilevile amejilaza akitumia mashine ya kupumulia, yeye alionekana ufahamu bado kabisa japokuwa mapigo ya moyo dokta alisema yapo mbali sana. Lakini aliwaomba wazidishe kumuomba Mungu na si kulia.
WIKI MOJA BAADAYE...
Baada ya wiki moja hali ya Colin iliimarika kidogo kwa kuweza kutambua watu japokuwa bado alikuwa hawezi kuzungumza kwa haraka kwa kutafuta maneno.
Cecy hali yake ilikuwa bado mbaya pamoja na mwili kuanza kurudisha hisia bado alikuwa akiendelea kutumia mashine za kumsaidia kupumua.

Walijikuta katika wakati mgumu baada ya hali ya Cecy kuonekana kuchelewa kuimarika.
Mganga mkuu aliomba kama wana uwezo basi Cecy apelekwe India kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuamini uwezo wa madaktari wa Tanzania uliishia pale kuweza kuuamsha mwili lakini hali ilikuwa bado tofauti na Colin ambaye aliweza kula hata kufanyishwa mazoezi japokuwa alikuwa akizungumza kwa shida.

Madaktari waliwahakikisha kuwa ndani ya wiki nyingine hali itaimarika zaidi na kuweza kuanza mazoezi ya peke yake. Fedha iliyokuwa ikitakiwa kwa ajili ya matibabu na nauli ya Cecy na msaidizi wake ilikuwa kubwa ambayo mama Cecy hakuwa nayo.
Kwa hali ya mgonjwa ilivyokuwa ikionekana, mama Colin aliamini kabisa Cecy hawezi kupona hivyo kutoa kiasi hicho cha fedha ni sawa na kuzitupa.
Mama Cecy alikuwa radhi kuuza nyumba ili tu mwanaye akatibiwe, lakini mama Colin alimshauri asisumbuke kwa vile wagonjwa wa aina ile huwa hawaponi hivyo heri asiipoteze nyumba kwani Cecy akifa hatakuwa na sehemu ya kukaa.

Mama Cecy alikuwa radhi kulala nje lakini ajue hatima ya hali ya mwanaye.
Ili kujitoa kwenye lawama, alichangia shilingi milioni tano katika milioni ishirini na tano zilizotakiwa.
Mama Cecy alitafuta dalali wa kuiuza nyumba kwa bei ya kutupa ili tu mwanaye akatibiwe India kama kufa basi afe akijua alikuwa akipigania maisha yake.

Wiki ile ndiyo ilikuwa wiki ya malipo ya Cecy kutoka katika kampuni ya jarida la Ebony ambayo iliingiza kwenye akaunti ya Cecy.Pia walifunga safari hadi Tanzania kuonana na Cecy kwa ajili ya kumpiga picha zingine kwa ajili ya matoleo mengine. Jarida lililotoka na picha ya Cecy ilisababisha jarida livunje rekodi ya mauzo ya kampuni ile tangu ianzishwe.
Uongozi wa kampuni ile ulipanga kumpa mkataba mnono wa muda mrefu zaidi pia kumfunga asitumike kwenye majarida mengine.Walipofika walitaka kuonana na meneja wake ambaye ni mchumba wake, Colin, mmiliki wa kampuni ya Urembo.
Taarifa walizopata ziliwashtuwa sana kusikia Cecy na mchumba wake walipata ajali mbaya na wapo mahututi hospitali. Walikwenda kuwaona wagonjwa.Colin alionekana hajambo lakini Cecy bado hali yake ilikuwa tata, walionana na mganga mkuu na kutaka kujua nini hatma ya mgonjwa kwa siku alizokaa hospitali.
Aliwaeleza hatua walizochukua tangu mwanzo kwa wagonjwa wote na kufanikiwa kwa mmoja na sehemu walipokwama na kuhitaji msaada wa matibabu zaidi kwa mmoja nje ya nchi.
Itaendelea wiki ijayo.
 
daa sasa kuna uwezekano wa bi Cesy kupona ila mapenz mh..let karma decide
 
Hapo sasa
no one knows the future, ila nahisi cecy atapona na colin atachukua mda mrefu kupona
 
Wanamkatisha tamaa ma cecy kama vile wao wataishi milele
 
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Walikubaliana kurudi nyumbani mpaka kesho
ambayo wangerudi kuwaona, mama Mage
aliwashauri wote waongozane nyumbani kwa mama
Colin kufanya maombi ya pamoja ili Mungu
awaepushe na matatizo yale.
Waliongozana wote hadi nyumbani kwa mama Colin
ambako walifanya maombi ya pamoja
yaliyoongozwa na mama Mage.
SASA ENDELEA...
Walipiga magoti na kushikana mikono kisha mama
Mage alishusha maombi.
“Baba Mungu tumepiga magoti mbele yako, tunajua
hakuna chochote chini na juu ya jua kiwezacho
kufanyika bali kwa idhini yako.
Baba Mungu lisilowezekana kwa mwanadamu
kwako linawezekana, lililo zito kwa mwanadamu
kwako ni jepesi. Eeh, Baba tunaomba uwaepushe
watoto wetu na matatizo mazito kama ulivyoweza
kumuepusha mwanao mpendwa pale msalabani.
Kama ulivyoweza kumponya Ayubu na maradhi ya
ajabu ambayo alipona kupitia uweza wako. Baba
Mungu unaweza kumponya aliye mahututi, unaweza
kumfufua aliyekufa, kwako wewe hakuna
kinachoshindikana.
Baba waponye wenetu ambao hatujui hali zao ni
wewe pekee mwenye uwezo wa kuugeuza usiku
ukawa mchana basi yaondoe maradhi milini mwao
wape afya njema.
Baba vunja pepo wa maumivu, vunja pepo wa
mauti, vunja pepo wa maradhi kwa jina la mwanao
Yesu Kristo aliyehai. Amen.”
“Ameni,” waliitikia pamoja.
Baada ya maombi walinyanyuka na kukaa kwenye
makochi, kwa vile hawakuwa na la kuzungumza
mpaka siku ya pili watakapokwenda kuwaona
wagonjwa wao. Mama Mage na mwanaye waliaga
na kuondoka kurudi nyumbani na kuwaacha mama
Colin na Cecy wakiwa wamekaa kila mmoja
akiwaza lake.
***
Siku ya pili alfajiri walikutana wote Hospitali ya
Muhimbili kwa vile daktari alikuwa hajafika ilibidi
wamsubiri hadi saa moja asubuhi alipofika,
alipowaona aliwaeleza wasubiri ili afike wodini
kwanza.
Dokta Bukos baada ya kuwazungukia wagonjwa
wote na kuchukua taarifa kutoka kwa daktari wa
zamu, aliwafuata kwenda kuwaona wagonjwa wao.
Waliingia mmojammoja kutokana na taratibu za
kuingia Chumba cha Maalum cha Wagonjwa
Mahututi (ICU). Colin alikuwa akipumulia mashine
akiwa amelala bila kutikisika. Lakini Dokta Bukos
aliwaeleza kuwa kidogo ameanza kupata fahamu
kwa misuli ya mwili kuanza kufanya kazi taratibu
japokuwa hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya
kulala vilevile walivyomkuta.
Katika chumba kingine, Cecy naye alikuwa vilevile
amejilaza akitumia mashine ya kupumulia, yeye
alionekana ufahamu bado kabisa japokuwa mapigo
ya moyo dokta alisema yapo mbali sana. Lakini
aliwaomba wazidishe kumuomba Mungu na si kulia.
WIKI MOJA BAADAYE...
Baada ya wiki moja hali ya Colin iliimarika kidogo
kwa kuweza kutambua watu japokuwa bado alikuwa
hawezi kuzungumza kwa haraka kwa kutafuta
maneno.
Cecy hali yake ilikuwa bado mbaya pamoja na mwili
kuanza kurudisha hisia bado alikuwa akiendelea
kutumia mashine za kumsaidia kupumua.
Walijikuta katika wakati mgumu baada ya hali ya
Cecy kuonekana kuchelewa kuimarika.
Mganga mkuu aliomba kama wana uwezo basi
Cecy apelekwe India kwa ajili ya matibabu zaidi
baada ya kuamini uwezo wa madaktari wa Tanzania
uliishia pale kuweza kuuamsha mwili lakini hali
ilikuwa bado tofauti na Colin ambaye aliweza kula
hata kufanyishwa mazoezi japokuwa alikuwa
akizungumza kwa shida.
Madaktari waliwahakikisha kuwa ndani ya wiki
nyingine hali itaimarika zaidi na kuweza kuanza
mazoezi ya peke yake. Fedha iliyokuwa ikitakiwa
kwa ajili ya matibabu na nauli ya Cecy na msaidizi
wake ilikuwa kubwa ambayo mama Cecy hakuwa
nayo.
Kwa hali ya mgonjwa ilivyokuwa ikionekana, mama
Colin aliamini kabisa Cecy hawezi kupona hivyo
kutoa kiasi hicho cha fedha ni sawa na kuzitupa.
Mama Cecy alikuwa radhi kuuza nyumba ili tu
mwanaye akatibiwe, lakini mama Colin alimshauri
asisumbuke kwa vile wagonjwa wa aina ile huwa
hawaponi hivyo heri asiipoteze nyumba kwani Cecy
akifa hatakuwa na sehemu ya kukaa.
Mama Cecy alikuwa radhi kulala nje lakini ajue
hatima ya hali ya mwanaye.
Ili kujitoa kwenye lawama, alichangia shilingi milioni
tano katika milioni ishirini na tano zilizotakiwa.
Mama Cecy alitafuta dalali wa kuiuza nyumba kwa
bei ya kutupa ili tu mwanaye akatibiwe India kama
kufa basi afe akijua alikuwa akipigania maisha yake.
Wiki ile ndiyo ilikuwa wiki ya malipo ya Cecy kutoka
katika kampuni ya jarida la Ebony ambayo iliingiza
kwenye akaunti ya Cecy.Pia walifunga safari hadi
Tanzania kuonana na Cecy kwa ajili ya kumpiga
picha zingine kwa ajili ya matoleo mengine. Jarida
lililotoka na picha ya Cecy ilisababisha jarida livunje
rekodi ya mauzo ya kampuni ile tangu ianzishwe.
Uongozi wa kampuni ile ulipanga kumpa mkataba
mnono wa muda mrefu zaidi pia kumfunga
asitumike kwenye majarida mengine.Walipofika
walitaka kuonana na meneja wake ambaye ni
mchumba wake, Colin, mmiliki wa kampuni ya
Urembo.
Taarifa walizopata ziliwashtuwa sana kusikia Cecy
na mchumba wake walipata ajali mbaya na wapo
mahututi hospitali. Walikwenda kuwaona
wagonjwa.Colin alionekana hajambo lakini Cecy
bado hali yake ilikuwa tata, walionana na mganga
mkuu na kutaka kujua nini hatma ya mgonjwa kwa
siku alizokaa hospitali.
Aliwaeleza hatua walizochukua tangu mwanzo kwa
wagonjwa wote na kufanikiwa kwa mmoja na
sehemu walipokwama na kuhitaji msaada wa
matibabu zaidi kwa mmoja nje ya nchi.
Itaendelea wiki ijayo.
 
Back
Top Bottom