Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

Mage ananipa hasira malaya huyu ...........

Grand PA
 
ILIPOISHIA:
“Nashukuru sana mama, basi nikuache niwahi
nyumbani.”
“Hakuna tatizo msalimie mama yako.”
“Salamu zimefika.”
Mage aliagana na mama Colin na kurudi nyumbani
kwao huku dua zake zikiwa kwa Cecy asirudi hai ili
aichukue nafasi ambayo aliamini ilikuwa yake hapo
awali.
SASA ENDELEA...
Hakutaka kuyajutia maamuzi yake ya kuachana na
Colin na kurudiana na Hans kwani kwake ulikuwa
uamuzi sahihi ilitokea bahati mbaya ya kufungwa
maisha.
Moyoni mwake alikuwa tayari kumsubiri Hans hata
miaka kumi ili waoane lakini kifungo cha maisha
kilimvunja nguvu na kuamini mtu sahihi kwake
alikuwa Colin. Aliapa kumpigania Colin kwa nguvu
zote kumrudisha mikononi mwake hata kwa kutoa
uhai wa mtu. Alipofika nyumbani kwao alimweleza
mama yake kilichotokea na kumshtua sana.
“Mmh! Yamekuwa hayo unafikiri utafanyaje naona
kila kitu kimevurugika.”
“Lakini mama Colin kasema kesho niende
nikampeleke Colin hospitali.”
“Utampeleka vipi ikiwa hataki hata kukuona?”
“Mama yake kasema yeye anajua kila kitu
kinachotakiwa kufanyika na ameniahidi lazima
nitaolewa na mwanaye.”
“Mmh! Sawa kwa vile kasema mama yake lakini
maneno ya Colin yamenitisha kusema, eti yupo
tayari kufunga ndoa na maiti ya Cecy kuliko kuoa
mwanamke mwingine.”
“Mama au akili ya Colin imepata tatizo baada ya
kujigonga kwenye ajali?”
“Inawezekana maana ajali haikuwa ya kawaida.”
“Mmh! Inawezekana maana alivyonigeuka si
kawaida yake, mama Colin naamini ananipenda.”
“Au yule mtoto alimwendea Colin kwa Kalumanzira?”
“Inawezekana kabisa si bure ana urembo gani wa
kumfanya Colin atake kufunga ndoa na maiti yake.”
“Hata mimi naona, lazima nasi tuhangaike ili
kuhakikisha nafasi hiyo unaipata wewe.”
“Yaani huwezi kuamini sala zangu zote namuomba
Israel amtokee Cecy na kummaliza kabisa tufikirie
mambo mengine.”
“Duh! Kweli wewe kiboko, wenzio dua zao
wanaomba amani wewe shari.”
“Siku zote adui yako muombee matatizo.”
“Mmh! Haya.”
MUMBAY- INDIA
Katika hospitali ya Apolo katika mji wa Mumbay
nchini India madaktari waliendelea kuumiza vichwa
kutokana na ugonjwa wa Cecy ambao
uliwachanganya akili baada ya kuweza kufumbua
macho lakini mwili bado haukuwa na mawasiliano
kwa asilimia zote. Waliufanyia vipimo vyote na
kukaa jopo la madaktari bingwa kuchunguza Cecy
ana tatizo gani lililopelekea kuwa katika hali ile.
Hali iliyojitokeza ilikuwa tofauti na maelezo ya ajali
yake, walijikuta wakifikia uamuzi wa kumrudisha
Tanzania kwani waliamini hakutakuwa na
mabadiliko yoyote kwa muda mfupi. Matumaini ya
kupata nafuu yalikuwa asilimia ndogo sana kuliko
kupoteza maisha. Uhai wake waliamini
hautachukua muda mrefu kwa vile mawasiliano
hayakuwepo zaidi ya mapigo ya moyo yalienda
kawaida pia hata mapafu yalifanya kazi vizuri.
Kilichowashangaza kuweza kupita kwa chakula laini
na kufanyiwa kazi na kutoka kinyesi chepesi
ambacho alijisaidia bila habari. Mama yake alikuwa
na kazi ya kumgeuza na kumsafisha anapojisaidia
pia kumbadili ubavu ili kutoweka vidonda kwa kulalia
upande mmoja kwa muda mrefu.
Mama Cecy naye alikata tamaa ya mwanaye
kupona kutokana na kutotokea mabadiliko yoyote
makubwa zaidi ya kuweza kutazama na kula kitu
kilichokuwa kikitia matumaini kidogo.Baada ya jopo
la madaktari kukubaliana kumrudisha Tanzania,
kwa kuamini kwa kuwa Tanzania ataweza kupata
vitu viwili, moja kurikava taratibu akiwa nyumbani
hivyo kupunguza gharama. Pili hata akifa wasipate
gharama za kuusafirisha mwili wa marehemu.
Walimwita mama Cecy kumpa taarifa zile
walizokubaliana kuhusu mwanaye kurudishwa
Tanzania. Baada ya kuingia kwenye ofisi ya
madaktari bingwa alikaa kwenye kiti huku akiwa na
mkalimani daktari aliyeongozana naye.
“Mama Cecy, tumekuita hapa ili kukujulisha hatua
tuliyofikia, inaonesha ugonjwa wa mwanao
utachukua muda mrefu. Hivyo tumeamua
kumrudisha Tanzania ili uweze kumhudumia
nyumbani pia kupata msaada wa matibabu ya
kusaidia kuusisimua mwili.”
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
“Mmh! Sasa itakuwaje ikiwa hospitali
inayotegemewa mmeshindwa, mwanangu si ndiyo
anakwenda kufa?”
“Hapana si kufa bali huduma za muhimu tumejitahidi
kadri ya uwezo wetu, hatuwezi kuendelea kumweka
hospitali na kuongeza gharama wakati huduma
nyingine anaweza kuzipata akiwa hukohuko
Tanzania. Sisi kazi yetu kubwa tumemaliza kilicho
bakia ni kazi ya Mungu.”
“Mmh! Sawa.”
Mama Cecy alikubali kwa sauti ya kukata tamaa
kwani siku zote watu waliokwenda India hurudi
wamepona na ikishindikana basi mtu huyo huwa wa
kumzika. Aliamini ile ilikuwa kauli ya kumpa moyo
lakini siku za kuishi mwanaye zilikuwa
zinahesabika.
Itaendelea wiki ijayo Jumamosi.
 
Duh hi story toka Jana naisoma yani nimesitisha shughuli za bunge nipate uhondo aisee ni tamu balaa
Jamani ikiisha kabisaaa mnitag
Cc Khantwe (hujabanduka loh)
 
Last edited by a moderator:
Duh hi story toka Jana naisoma yani nimesitisha shughuli za bunge nipate uhondo aisee ni tamu balaa
Jamani ikiisha kabisaaa mnitag
Cc Khantwe (hujabanduka loh)

Hahahah....nipo hata sibanduki
 
Last edited by a moderator:
hii story nimeanza siku mbili zilizopita bigup sana wakuu mizambwa, bucho, daudi1, na mmary.
njooni muiendeleze au muuimzalizie
 
Back
Top Bottom