ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA :
Mi kwangu naona kama ndiyo
unataka kuniongezea
umaskini, Cecy alijibu
kinyonge.
Vipi?
Hivi nikiwa huko tutakuwa
pamoja?
Hapana ila tutaonana mara
chache kwa vile utakuwa bize
na kazi yako ya kuizunguka
dunia kufanya maonesho .
Huoni kama nitakuwa
nimepata fedha zisizo na faida
kwangu.
SHUKA NAYO SASA . ..
Kivipi?
Colin wewe ni kila kitu
kwangu, niliapa kuwa mbali na
wewe ni pale mmoja wetu
akichukuliwa na umauti na si
vinginevyo.
Hilo tu, nitakuwa naonana na
wewe kila mara wala usihofu .
Colin nina wasiwasi nikiwa
mbali kuna vipanga watu
watakunyakuwa na mimi
kuichukia dunia, kukupata
nimetoka jasho la damu.
Furaha yangu ni kuwa karibu
yako na si kuingiza mamilioni
ya fedha.
Najua mpenzi unanipenda
lakini hili dili ni zaidi ya
mapenzi kwa vile
litayabadilisha maisha yako
sasa hivi una uwezo wa kujenga
gharofa Masaki au Kunduchi.
Colin mimi huko siendi na
hizo hela zao sizitaki .
Usifanye hivyo , ukilipoteza
utakuja kujuta maisha yako
yote.
Moyo wangu naujua hauna
shida ya mabilioni ya fedha bali
upendo toka kwako, pia naona
umekwenda kinyume na
makubaliano yetu.
Kivipi mpenzi?
Ulisema unataka kunifungulia
kampuni ili niwe nafanya
maonesho na si kwenda kufanya
kazi nje ya nchi.
Mpenzi, yaani dili ulilolipata ,
fedha utakayoipata kwa miaka
yote hiyo unaweza kukaa bila
kufanya kazi na kuishi maisha
ya juu .
Sina maana hiyo, uliniahidi
baada ya kumaliza masomo
unanioa sasa ahadi yetu ipo
wapi? Au ndiyo unanitoa
kijanja urudiane na Mage
baada ya mpenzi wake
kufungwa? Cecy alilia wivu .
Ahadi yetu ipo palepale, we
fanya kazi mwaka mmoja kisha
tunafunga ndoa ndipo nitajua
nitafanya nini.
Cecy mpenzi hujui tu kiasi
gani cha fedha utakacholipwa ,
ni wasichana wachache duniani
wenye bahati hii . Tukitaka
tufanye harusi itachukua muda
wakati mwezi ujao unatakiwa
Afrika Kusini kwa mazoezi ya
wiki mbili kabla ya kwenda
Ufaransa.
Kutokana na makubaliano, picha
za Jarida la Ebony watatumia za
kwenye onesho na zile
walizokupiga siku ile. Malipo
yako ya kwanza yataingia mwezi
ujao ya dola elfu mia mbili
arobaini (Sh 408 ,000 ,000 ) kwa
mwaka.
Baada ya mwaka malipo
yataongezeka na kuwa dola elfu
mia tatu ( Sh 510 , 000 ,000 ). Pia
utapata bonasi ya asilimia tano
kutokana na mauzo, huoni kwa
miaka miwili utakuwa mbali
mpenzi wangu kwa kutengeneza
dola elfu mia tano arobaini ( Sh
918 ,000 ,000 )?
Bado kampuni ya maonesho
itakulipa dola elfu mia tatu ( Sh.
510 ,000 ,000 ) kwa mwaka na
bonasi kila onesho la nchi
kubwa barani Ulaya na Amerika.
Unataka nini tena mpenzi
wangu, kipindi hiki, hebu ndoa
iweke pembeni tupige pesa .
Colin nakuona kama
unampigia mbuzi gitaa,
nakueleza kwa mara ya mwisho,
pesa inaweza kununua kitu
chochote chini ya jua lakini si
furaha ya moyo wa mtu , dawa
ya mtu ni mtu si kitu.
Mmh ! Sasa wewe ulikuwa
unatakaje?
Kwanza tuoane kisha tutajua
kama kwenda au kufanyia kazi
hapa lakini si kukaa mbali na
wewe .
Ulikuwa mtihani mzito kwa
Colin kutokana na msimamno
wa mpenzi na kuliona kama dili
lile litapeperuka kwani
walikuwa wapo nchini
wakisubiriwa kauli yao kwamba
ataanza lini kufanya kazi. Lakini
kwa Cecy alikuwa haelewi kitu .
Jioni ya siku ile Colin alikutana
na mama Cecy na kumuelezea
hatua waliyofikia na uamuzi wa
Cecy.
Mama nilikuwa naomba
umweleze mwenzangu akubali
kwanza kwenda kufanya kazi,
ndoa itafuata baadaye .
Mmh ! Nitajaribu kumweleza ,
nina imani atanielewa .
Yaani nitashukuru sana,
sijawahi kuona mwanamke
mwenye msimamo kama Cecy .
Kwa vile Cecy alikuwa
amekwenda kuoga aliporudi
alikaa pembeni ya mama yake
na kumuacha Colin aliyekuwa
amekaa kochi la peke yake.
Baada ya ukimya mfupi mama
Cecy aliuvunja ukimya ule .
Cecy mama.
Abee mama .
Nina imani leo Mungu
atuangazia maisha yetu ?
Ni kweli mama, lakini maisha
hayatakuwa na furaha bila
kutimiza ndoto yangu .
Najua una hamu ya kutimiza
ndoto yako , lakini kilichotokea
ni muhimu kwa wakati huu
ndoa yako ipo palepale .
Hilo nalijua , siku zote fimbo ya
mbali haiuwi nyoka, kama
nitaanza kazi naweza kukaa
hata miezi mitatu bila kumuona
Colin na wakati penzi langu
limenitoa jasho la damu.
Naweza kupata fedha lakini
nikapata jeraha lisilopona
mpaka nakufa na pengine
likawa ndiyo sababu ya kifo
changu.
Kwa nini unasema hivyo?
Mama kama unavyojua
mchumba wa Mage yupo ndani
na kesi yake ni nzito , kwa
habari za juujuu kweli
anahusika katika vifo vya mkewe
na mwanaye ili arudiane na
Mage . Kwa hiyo uwezekano wa
kutoka ni mdogo , huoni muda
huo nikiwa mbali na Colin
penzi linaweza kuzaliwa upya
na nafasi yangu kupotea.
Kama nilijitoa kwa ajili ya
Colin ifike wakati nimkose hizo
fedha zitakuwa na faida gani
kwangu. Nipo tayari kupoteza
hata fedha zilizojaa bahari
lakini si kumpoteza Colin , moyo
wangu ndiyo unaojua thamani
yake si yeyote.
Mama hujui kiasi gani niliumia
niliposikia Colin akioa lakini
machozi yangu hayakwenda
bure, Mungu alisikia kilio
changu na kunirudishia mpenzi
wangu mikononi mwangu na
kuamini haki ya mtu huwa
haipotei bali hucheleweshwa .
Sasa kama unafahamu hivyo
kwa nini una wasiwasi na
Mage ?
Mama, Golden chance never
came twise .
Hapo umeniacha feri una
maanisha nini?
Kwangu hii ni nafasi ya
dhahabu kamwe haijirudii mara
mbili.
Cecy nakuahidi wewe ndiye
mwanamke wa maisha yangu ,
nilivyofahamu thamani yako
ndani ya moyo wangu upengo
wangu uliongezeka mara dufu.
Itaendelea wiki ijayo .