Hadithi: Wakili wa moyo

Hadithi: Wakili wa moyo

bucho tumeachwa solemba bana tumesubiri kama mtoto anavyosubiri pipi aise na mizambwa haonekani kutokea bana

Dawa nikumchukulia hatua za kisheria ili aweze kuja kumalizia hii shughuli aliyoiachia katikati. Nafikiri huu ni unyanyasaji mkubwa wa haki za binadamu. Nakuomba embu jaribu kuangalia kama kuna uwezekano wa kumfungulia kesi ili aamrishwe na mahakama kuendelea na hadithi hii. Tafadhali mkuu ikiwezekana unijulishe gharama za kesi hiyo ili tufanikishe zoezi hilo
 
Last edited by a moderator:
Kwa heshima na taadhima naomba niendeleze hii hadithi hadi mkuu mkuu mizambwa arudi. Kisha ataebdelea kutokea hapo.




ILIPOISHIA: Alitulia aione sinema ile inaishaje kwa kujificha nyuma ya mti ili wasimjue, baada ya muda alisikia sauti ya Colin: SASA ENDELEA… “Mage pamoja na hayo lakini kumbuka tumepanga nini mimi na wewe katika maisha yetu?” “Haihusu! Nimekwambia mapenzi siyo lazima,ninaye nimpendaye wewe nikuweke wapi?” “Mage...Mage.” “Jina langu,kwaheri.”

Mage alisema huku akielekea kwenye gari ili aondoke na kumuacha Colin aliyekuwa bado amesimama akilia. Kitendo kile kilimuumiza sana Cecy bila kujitambua alitoka nyuma ya mti na kwenda kumvamia Mage kwa nyuma na kuzivuta nywele zake na kuanza kumshushia kipigo. Colin alishtuka kumuona Cecy eneo lile na kujiuliza ametokea wapi,ilibidi amuwahi kumtoa juu ya Mage aliyekuwa akipiga kelele za maumivu. “Cecy muache.”

“Hawezi kukudhalilisha kiasi hicho kama umalaya wake apeleke mbele,” Cecy alisema huku akitweta kwa hasira akitaka kujitoa mikononi mwa Colin ili akamfunze adabu Mage. “Colin,have you sent this bastard to come and attack me?“ (Colin umemtuma chokoraa huyu aje anipige?) Mage alibadili lugha na kusema huku akisikilizia maumivu. “No baby! I’m also suprised as to where she came from!” (Hapana mpenzi! Hata mimi nashangaa sijui katokea wapi.) Colin alijitetea. “Colin,what type of a man who forces to be loved,what’s wrong with you? Let her go!” (Colin wewe ni mwanaume wa aina gani unang’ang’aniza mapenzi,una kasoro gani, mwacha aende) Cecy safari hii naye alivunja yai na kumfanya Colin abaki mdomo wazi.

“Colin thank you,stay with that bastard whom you sent to beat me.” (Colin asante, baki na huyo chokoraa uliyemtuma kunipiga) Mage alisema huku akielekea kwenye gari. Colin aliyekuwa amemshika Cecy ili asiendelee kumuadhibu Mage,alimuachia na kumfuata Mage kumuomba msamaha. “Please Maggie,excuse me,don’t be so cruel to me.” (Tafadhali Mage,samahani,rudisha moyo nyuma usinifanyie ukatili huo.)

Alipopiga hatua ili amfuate Mage kwenye gari,Cecy alimfuata na kumzuia kwenda kuomba msamaha. “Colin...Colin... why do you cling to her,how good is her; do you love her for her richnes or behaviour? (Colin... Colin... unamng’ang’ania ana sifa gani,unampendea utajiri au tabia?) Colin alijitahidi kujitoa mikononi mwa Cecy lakini alikamatwa madhubuti. Wakati huo Mage alikuwa ameingia kwenye gari na kutupa nje begi la Colin na kuondoa gari kwa kasi huku akimuacha Colin akilisindikiza kwa macho. Baada ya gari kupotea machoni alitulia huku machozi yakiziba macho.

Cecy roho ilimuuma kuona mtu ampendaye akitokwa machozi kwa ajili ya kulilia penzi lisilokuwepo. “Colin,mbegu ya penzi humea kwenye moyo wenye rutuba ya mapenzi,kwa nini unalazimisha kupanda mbegu yako kwenye mawe? Kwa nini unakuwa kenge asiyetaka kuelewa. Mshukuru Mungu msichana wa watu amekuwa mkweli mapema,” Cecy alisema kwa sauti ya kilio iliyomshtua Colin na kurudisha macho kwake.

Pamoja na yote yaliyomtokea,alishangazwa na ujasiri wa Cecy,msichana aliyeonesha kuumizwa na kitendo cha kudhalilishwa na Mage. Kingine nina uwezo wa kuzungumza Kingereza kwa ufasaha mkubwa. Pia kuonekana binti mwenye mvuto kutokana na mavazi na muonekano. “Cecy,” alimwita kwa sauti ya upole. “Abee.” “Kwanza samahani.” “Ya nini Colin?” “Najua nimekudhalilisha kwa kitendo changu cha kumlilia Mage.” “Colin siwezi kukulaumu kwa vile ile ni haki yako japo sijui sababu ya yeye kukudhalilisha kiasi kile ikiwa kila kitu kipo katika hatua za mwisho,kilichobaki ni ndoa tu.” “Mage amerudiana na bwana’ke wa zamani na kuamua kuvunja uchumba wetu.” “Kama amekueleza ukweli sasa unamng’angania wa nini?”

“Cecy ni ghafla sana,heri kungekuwa na tatizo,kanifuata nyumbani juzi na kunipeleka Bagamoyo,niliamini ana mapenzi yake ya dhati kwangu lakini baada ya kukaa siku mbili za furaha,ya tatu alinieleza kitu ambacho kimenichanganya sana.” “Colin ulikuwa unampenda Mage mapenzi ya dhati au tamaa ya macho?” Cecy alimuuliza akiwa amemkazia macho. “Mapenzi ya dhati.”

“Muongo! Umempenda kwa shinikizo la mama yako,kama amejitoa kwa hiyari yake, huoni hii ni nafasi ya kuipanda mbegu yako sehemu sahihi ambayo utaotesha mti wenye kivuli na matunda matamu?” “Cecy kwanza unatoka wapi muda huu?” “Shule.” “Hongera.” “Siwezi kusema asante.” “Kwa nini?” “Mpaka ufute machozi yangu.” Colin alitoa kitambaa mfukoni ili amfute Cecy machozi lakini alishikwa mkono na kumfanya aulize: “Vipi Cecy mbona unanishika mkono?” “Si machozi haya Colin.”

“Machozi gani Cecy?” Colin alishtuka. “Ya moyoni,nimeumizwa sana pia nimedhalilishwa sana juu ya penzi lako, lakini Mungu si mnafiki,leo amekudhihirishia mbele ya macho yangu kuwa mke uliyechaguliwa mara ya pili, hakuwa mke sahihi bali lilikuwa penzi la kuigiza.

Colin mimi ndiye mkeo uliyechaguliwa na Mungu. Nifute machozi yangu kwa kufunga ndoa na mimi si kwa kitambaa cha mkononi bali cha moyoni,” Cecy alisema kwa sauti iliyojaa hisia kali za mapenzi. “Cecy nimekuelewa,naomba unipe muda.” “Muda wa nini wakati nafasi yangu imerudi tena nikiishuhudia si kwa kuhadithiwa na mtu.” “Nimekuelewa,niache kwanza nifike nyumbani,kumbuka toka juzi sipo nyumbani na ninarudi na taarifa hizo sijajua mama atazipokeaje?” “Mmh! Sawa,ila pole kwa yote yaliyokukuta.” “Nashukuru.” “Colin naomba nikusindikize mpaka kwenu,” Cecy alimwambia Colin huku akiuchezea mkono wake. “Hapana,si unamjua mama,atapata la kusema.” ”Nimekuelewa mpenzi.” Colin alitoa hela mfukoni bila kuzihesabu na kumpatia Cecy,alizipokea na kushukuru kwa kupiga magoti kitu kilichomshtua Colin na kuona tofauti yake na Mage. Siku zote Cecy alikuwa msichana mtiifu ambaye mwanzo alikuwa chaguo la mama yake baadaye alimgeuka baada ya kumuona Mage. Waliagana,kila mmoja akakodi gari mpaka kwao. **** Mage,baada ya kuachana na Colin aliendesha gari kwa kasi huku moyo ukimuuma kwa kitendo chake cha kikatili alichomfanyia mtu aliyeonesha mapenzi mazito kwake na aliyemkabidhi moyo wake mzimamzima kutokana na kumuamini. Aliyakumbuka maneno yaliyokuwa kwenye picha kubwa chumbani kwa Colin,moja lilisema: ASANTE MUNGU KWA KUNIPA MKE MWEMA na lingine MAGE

NAKUPENDA ZAIDI YA KUPENDA. Mage alijikuta akilia na kufanya machozi kuziba macho,alisimamisha gari pembeni na kuendelea kulia kilio cha kwikwi. Aliisikia sauti ya Colin ikisema: “Mage uamuzi uliochukua ni kuupasua moyo wangu bila ganzi,naomba urudishe moyo nyuma,mpenzi wangu bora ungeninyang’anya kila kitu katika mwili wangu na kuniachia moyo wako ni muhimu kuliko chochote duniani,japokuwa nipo nawe kwa muda mfupi,lakini nimekuzoea sana.” Itaendelea
 
ILIPOISHIA:

“Mage uamuzi uliochukua ni kuupasua moyo wangu bila ganzi, naomba urudishe moyo nyuma, mpenzi wangu bora ungeninyang’anya kila kitu katika mwili wangu na kuniachia moyo wako, ni muhimu kuliko chochote duniani. Japokuwa nipo nawe kwa muda mfupi, lakini nimekuzoea sana.” TWENDE KAZI…

Sauti ile ilimfanya apaze sauti na kusema: “Colin nisamehe sana,najua jinsi gani nilivyokuumiza,najua mapenzi yanavyojeruhi moyo wa mtu. Colin nisamehe sina jinsi,nilikupenda lakini Hans ni pumzi yangu,siwezi kuiacha nafasi adimu aliyonirudishia.” Mage aliongea kwa sauti kama anazungumza na Colin,aliinamia usukani na kuendelea kulia. Uchungu ulimjaa moyoni kila alivyomfikiria Colin jinsi alivyokuwa akimbembeleza na kutokata tamaa ya kukubaliana na ukweli kwamba,penzi limekwisha.

Aliamini asingeweza kuendesha gari kwa hali aliyokuwa nayo kwani hata nguvu zilikuwa zimemuisha kwa ajili ya uchungu uliomjaa moyoni. Aliwaza kumpigia Brenda ili aje amchukue. Wazo lile hakukubaliana nalo kwa vile siku ile alitaka kwanza kuonana na Hans ili amueleze kilichojiri ndipo aende nyumbani.

Aliamua kumpigia Hans,alichukua simu ili ampigie,ilibidi afute machozi kwanza kuziona ‘kiipadi’. Alitafuta jina la Hans na kupiga,haikuita mara mbili,baadaye ilipokelewa upande wa pili. “Haloo.” “Hans,” Mage aliita. “Naam Mage,vipi mpenzi?” “Upo wapi?” “Nipo Masaki.” “Naomba uje haraka.” “Nyumbani kwenu?” “Hapana,nipo njiani karibu na njia panda ya Masaki.” “Mbona kama unalia?” “Hans njoo kwanza.” “Haya nakuja.” “Kodi bodaboda.” “Sawa.” Baada ya kukata simu aliitupia kwenye kiti cha pili na kujilaza kwenye kiti baada ya kukiteremsha kwa nyuma ili kumsubiri Hans.

*** Cecy,baada ya kuachana na Colin alikwenda hadi nyumbani kwao. Baada ya kusalimiana na mama yake,aliingia chumbani kwake na kujifungia. Baada ya kuvua nguo zote alijifunga upande wa khanga na kujilaza chali kitandani na kuweka mikono nyuma ya kichwa kisha kutazama kwenye dari. Alitulia kwa muda na kuanza kuyakumbuka matukio yalitokea muda mfupi. Alijikuta akijilaumu kuingilia mambo yasiyomhusu, kwani ule ulikuwa ugomvi wa wapendanao, lakini kwa upande mwingine aliona kufanya vile ni kulipigania penzi lake.

Aliamini ndoa ya Mage na Colin haitakuwepo na ile ndiyo ilikuwa nafasi yake kukipata alichokipoteza. Alijiuliza kama ndoa ile itavunjika nani atakuwa mke wa Colin,kwake aliona ana nafasi ndogo hasa baada ya mama Colin kumdharau kutokana na umaskini wake lazima angemtafuta mwanamke mwingine kutoka familia yenye uwezo. Bado alitaka kujua sababu ya Mage kuuvunja uchumba ambao ulibakia siku chache kufunga ndoa kanisani.

Moyoni alijiapiza kama ndoa ya Colin na Mage itavunjika,basi ataipigania nafasi yake kwa nguvu zake zote. Mama yake alishangaa kumuona mwanaye yumo ndani muda mrefu,alipomfuata alikuta mlango umefungwa. Aligonga mlango huku akiita. “Cecy mbona umeingia ndani mwaka mzima kuna usalama?” “Ndiyo mama.” “Hebu toka basi.” Cecy alitoka nje,macho ya mama yake hayakucheza mbali na uso wa mwanaye na kugundua mabadiliko.

“Cecy upo sawa?” “Ndiyo.” “Hapana kuna kitu kimekutokea,si kawaida yako kuingia ndani moja kwa moja bila kunitania na kizungu chako cha kuombea maji.” “Ni kweli mama kuna kitu kimenitokea, kimenichanganya sana.” “Kitu gani?” Cecy alimweleza mama yake yote yaliyotokea wakati akitoka twisheni,mama yake alishtuka kusikia kampiga mchumba wa Colin. “Cecy kwa nini unatafuta balaa,unakumbuka mama Colin alituambia nini?” “Mama,mimi sijavunja ndoa yao bali wenyewe,kilichoniudhi ni kashfa aliyokuwa akiitoa yule mwanamke.” “Colin kasemaje?” “Amesema amechanganyikiwa kwani maamuzi yalikuwa ya ghafla ila alisema atanitafuta.” “Mmh! Sawa,basi kaoge ule.” “Sawa mama.” Cecy alipitia ndoo ya maji na kuelekea bafuni kuoga na kumuacha mama yake akimtazama na kutikisa kichwa,aliamini vita ya mapenzi ni nzima kuliko ya kumsaka gaidi mapangoni.

*** Colin baada ya kuachana na Cecy na kukodi gari lililompeleka hadi kwao,aliteremkia nje ya geti na kuingia ndani kwa miguu. Mama yake alikuwa wa kwanza kumuona akiingia sebuleni,lakini uso wake haukuonesha furaha kitu kilichomshtua na kuhoji. “Colin,baba vipi kwema utokapo?” “Kwema si kwema.” “Una maanisha nini?” “Nitakwambia naomba kwa sasa niache nikapumzike kwanza.” “Kuna nini? Mbona unanitisha?” “Mama naomba uniache kwanza.” “Mage yupo wapi?” “Sijui.”

“Colin ni majibu gani hayo?” mama alishtushwa na majibu ya mwanaye. “Mama yangu nipo chini ya miguu yako, naomba uniache kwanza.” “Mmh! Sawa.” Mama Colin aliachana na mwanaye aliyeelekea chumbani kwake,moyo wake ulimsukasuka,alichukua simu kumpigia mama Mage kutaka kujua kuna nini kimetokea. Baada ya simu kuita kwa muda, ilipokelewa upande wa pili. “Haloo dada.” “Za saa hizi?” “Nzuri,lete habari.” “Mage yupo hapo?” “Mmh! Toka atoke juzi sijamuona kwani vipi?” “Nimemuona Colin akirudi peke yake huku uso wake ukionesha kuna kitu si cha kawaida,nimemuuliza kuhusu Mage, amesema hajui.”

“Mmh! Lazima watakuwa wametibuana,sasa Mage yupo wapi?” “Hapo ndipo pananichanganya,nilipotaka kumchimba sana Colin,ameniomba nimuache kwanza apumzike.” “Mmh! Lazima watakuwa wametibuana tu.” “Kwa hiyo hajafika?” “Bado,akifika atanieleza tatizo,nitakujuza kila kitu.” “Sawa dada.”

Mama Colin alikata simu,alipogeuka alimuona mwanaye amebeba vitu akitoka navyo nje,hakujua amebeba nini. Alisubiri muda kidogo upite ili akaone mwanaye amechukua nini na anapeleka wapi. Colin baada ya kuachana na mama yake alikwenda chumbani kwake,alipofungua mlango wa chumba chake macho yake yalikutana na picha kubwa aliyoibandika muda mfupi kabla ya kuelekea Bagamoyo akiwa na Mage katika pozi zito la mahaba. Picha kubwa aliyoibandika ukutani ambayo mwanzo aliiona ni sehemu ya kuongeza furaha ya moyo wake,lakini siku ile ilikuwa chukizo la moyo wake,alipanda kitandani bila kuvua viatu na kuibandua na kuitupa chini huku akiitemea mate. Alifungua kabati na kutoa picha zote alizopiga na baadhi ya nguo za Mage alizikusanya na kutoka nazo nje kwenda kuzichoma moto.

Itaendelea
 
ILIPOISHIA:

Picha kubwa aliyoibandika ukutani ambayo mwanzo aliiona ni sehemu ya kuongeza furaha ya moyo wake, lakini siku ile ilikuwa chukizo la moyo wake, alipanda kitandani bila kuvua viatu na kuibandua na kuitupa chini huku akiitemea mate.

Alifungua kabati na kutoka picha zote alizopiga na baadhi ya nguo za Mage alizikusanya na kutoka nazo nje kwenda kujichoma moto. SASA ENDELEA… Alipofika nje alizikusanya sehemu moja na kuzimwagia mafuta ya taa na kuzitia moto, mama yake alitokea kwa nyuma yake. Alipotupa jicho aliona moja ya picha ya Mage ikiteketea na moto pia nguo za mkwewe mtarajiwa.

“Colin! Unafanya nini?” alimuuliza kwa sauti mwanaye. Colin hakujibu kitu,aligeuka kumtazama mama yake aliyekuwa ameshashika mkono kiunoni. “Colin mwanangu una nini mbona unachoma picha na nguo za mchumba wako?” “Mama uliponichagulia mchumba ulifanya uchunguzi kwanza?” “Wa nini?”

“Kama ana mpenzi anayempenda kuliko mimi.” “Mage hakuwa na mpenzi,kwa nini unaniuliza hivyo?” “Ndiyo maana nikakuuliza,ulifanya uchunguzi kabla ya kumchagua kuwa mkweo?” “Ndiyo,kwani vipi?” “Tulitaka kujenga nyumba kwenye kiwanja cha watu.” “Una maana gani?”

“Mage ni mchumba wa mtu.” “Una maanisha nini kusema hivyo?” mama Colin alishtuka kusikia habari ile. Colin alimweleza yote yaliyojiri Bagamoyo walipokaa siku tatu mpaka kumteremsha njiani na kumtupia mfuko wake. Lakini hakumueleza jinsi Cecy alivyo ingilia ugomvi ule na kipondo alichompa Mage. Mama yake alibaki macho yamemtoka kama kaona meli ikitembea barabarani. Alishusha pumzi nzito na kubakia akimuangalia mwanaye na asipate la kusema. *** Hans alifika na bodaboda sehemu aliyoelekezwa na Mage,aliliona gari limepaki pembeni. Alimuomba dereva wa bodaboda amshushe,aliteremka na kumlipa hela yake na kuchepua mwendo hadi kwenye gari alilolikuta limefungwa vioo vyote. Aligonga kwenye kioo na kumfanya Mage anyanyue kichwa kuangalia,alimuona Hans, alifungua mlango. Hans alishangaa kumkuta Mage macho yamemuiva kwa kulia. “Vipi mpenzi?” alishtuka kuiona hali ile.

“Hans mpenzi umekuja?” “Ndiyo mpenzi wangu,mbona unalia?” “Hans nimekaza moyo ili niumeze mfupa nisikupoteze mpenzi wangu.” “Una maanisha nini?” “Hii si sehemu sahihi ya mazungumzo, endesha gari tuondoke,” Mage alisema huku akihama kwenye usukani kumpisha Hans.

“Mmh! Safari ya wapi,nyumbani?” alimuuliza huku akimtazama usoni. “Nyumbani siendi sasa hivi mpaka tumalizane na wewe.” “Sasa twende wapi?” “Sea Cliff Hotel.” “Hakuna tatizo.”

Hans aligeuza gari na kuelekea Masaki, muda wote Mage alikuwa amejilaza kwenye siti baada ya kuilaza kwa nyuma. Hans alisimamisha gari kwenye maegesho ya Hoteli ya Sea Cliff. “Bebi tumefika,” alimshtua Mage aliyekuwa amefumba macho. “Kachukue chumba kabisa,” Mage alijibu bila kufumbua macho. “Sawa.”

Hans aliteremka na kwenda kulipia chumba kisha alirudi kumweleza Mage. “Tayari.” Aliteremka na kufunga gari lao kisha waliongozana hadi ndani ya chumba walichokikodi. Mage alipofika alijilaza kitandani huku macho akitazama juu na mikono aliilalia kwa nyuma. Pembeni ya macho yake michirizi ya machozi iliendelea kuteremka na kulowesha shuka. “Vipi bebi?” Hans alizidi kushtuka. “Hans sijui nikueleze nini uelewe,najua jamii itanitenga kwa ajili ya uamuzi wangu wa kuvunja uchumba,wapo watakaoniona sina akili lakini anayejua mapenzi ataniunga mkono. Nimekubali kubeba lawama zote za wanadamu lakini niufurahishe moyo wako. Sijui nitakaporudi nyumbani mama atanipokeaje,naweza kutengwa na familia kwa uamuzi wangu huu.” “Kwani huyo jamaa umeshamwambia ukweli?” “Siku tatu nilizokuwa naye Bagamoyo nilizitenga mahususi kwa ajili ya kumueleza taratibu kuuvunja uchumba wetu rasmi. Ningeweza kumwambia tu,lakini naheshimu mapenzi yake kwangu.” “Amepokeaje?” “Ilikuwa kazi kwelikweli,alichachamaa mpaka kutishia kutoa mtu roho,siyo siri alikuwa amekufa,ameoza.

Nina wasiwasi akawa mwendawazimu au kuchukua uamuzi wa kujinyonga.” “Mi nafikiri mshale umerudi porini haujapotea,Mage nakuapia kwa Mungu hutoujutia uamuzi wako. Kama ulivyojitoa kwangu nami nitazidisha mapenzi mara mia ya mwanzo. Nina imani ulikubali kuolewa kwa shinikizo,lakini moyo wako bado ulikuwa kwangu,nami naamini hivyo. “Hii ni nafasi nyingine ya kuidhihirishia dunia kuwa mimi na wewe tulizaliwa ili tuwe mwili mmoja. Mage nashukuru kuuponya moyo wangu uliokuwa na maumivu ya muda mrefu,kulishwa nisicho kitaka,lakini kwa sasa nakula ninachokitaka.”

“Hans naamini unanipenda zaidi ya kunipenda ndiyo sababu ya mimi kukubali kurudi kwako,wasiwasi wangu mkubwa ni familia yako. Hans nitakufa na mtu kila atakayetia mkono katika penzi letu,sitajali ni nani,” Mage alitoa mkwara mzito.

“Mage nitalipigania penzi letu,nakuahidi hakuna atakayeingilia penzi letu,nakuahidi mapenzi ya peponi. Nitayafuta machozi yako kwa kitambaa cha upendo,” Hans alisema huku akimfuta machozi. “Hans nimejilipua,ukinitenda umenimaliza,” Mage alisema kwa sauti ya kilio huku akijitupia kifuani kwa Hans. “Nakuhakikishia na harusi yetu haitachukua muda mrefu.”

“Kweli Hans?” alimuuliza huku akiyatoa macho yake yaliyojaa machozi kumtazama Hans. “Toka uliponitamkia matumaini ya kurudi kwangu nilikwenda mbali zaidi ya maandalizi ya ndoa yetu. Nilikuwa nasubiri kauli yako ili nikueleze hili.” “Wazazi wako je?” “Niliwaeleza wakasema hawawezi kunichagulia tena.” “Huoni kama ule wasiwasi wao juu ya kifo cha mkeo utazidi na mimi kuonekana ndiye mhusika?” Mage aliingiwa wasiwasi.

“Nilijua hilo litatokea lakini nimewaeleza mimi ndiye niliyekufuata japokuwa wewe haukuwa tayari kurudiana na mimi hasa baada ya kukutosa kukuoa pia familia yangu kukuingiza kwenye matatizo. Nashukuru walinielewa.” “Mmh! Sawa,kwako umemaliza sijui kwangu mama atapokeaje.” “Atakuelewa kwa vile anajua penzi letu lilivyokuwa,naamini moyo wake utafurahi kumpata mkwe sahihi.” “Mmh! Tutaona.” Walikwenda kuoga kisha walipata vinywaji na kufurahisha nafsi zao. Walipanga kuondoka pale saa sita usiku. *** Muda ulizidi kukatika bila Mage kuonekana kitu kilichozidi kumtia wasiwasi mama yake na kujiuliza atakuwa amepitia wapi. Mawazo yake yalimpeleka labda yupo kwa shoga yake Brenda. Lakini aliamini kama aliondoka nyumbani siku tatu zilizopita,alitakiwa afike nyumbani kwanza ndipo aende kwa shoga yake. Alipiga simu ya Mage haikuwa hewani kitu kilichofanya azidi kuingiwa wasiwasi,aliamua kumpigia simu Brenda. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kushindwa kuelewa kuna nini ikiwa simu ya Mage haipatikani na simu ya shoga yake haipokelewi. Akiwa katika ya mawazo,simu iliita, aliichukua haraka na kuipokea. Imepigwa na nani?


Itaendelea
 
Asante sana mkuu bucho.....sasa umetumwa na mizambwa au umeamua kumalizia mwenyewe
 
ILIPOISHIA


: Alipiga simu ya Mage haikuwa hewani kitu kilichofanya azidi kuingiwa wasiwasi, aliamua kumpigia simu Brenda. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kushindwa kuelewa kuna nini ikiwa simu ya Mage haipatikani na simu ya shoga yake haipokelewi. SASA ENDELEA… Akiwa katika mawazo,simu iliita. Aliichukua haraka na kupokea,ilikuwa inatoka kwa Brenda. “Haloo mama.” “Brenda,kwema?’

“Kwema mama,samahani simu ilikuwa mbali kidogo nimekuta umepiga,unasemaje mama?” “Mage amefika huko?” “Sijamuona,kwani amerudi?”

“Nasikia amerudi toka saa kumi na moja lakini mpaka sasa sijamuona na simu yake haipatikani.” “Umemuulizia shemeji Colin,si ndiye aliyekuwa naye?” “Mmh! Ipo kazi.”

“Kwa nini unasema hivyo?” “Basi ngoja nimpigie Colin alinieleze Mage kaenda wapi.” “Itakuwa vizuri.”

Baada ya kukata simu,alimpigia Colin nayo haikuwa hewani kitu kilichozidi kumuweka njia panda asijue nini kinaendelea,aliamua kumpigia mama Colin simu ilipokelewa.

“Haloo shoga kuna habari gani maana mimi mwenyewe moyo hauna raha,toka Colin kafika kajifungia ndani,kuna habari gani huko?” mama Colin alipokea na kuanza kumwaga maneno.

“Dada mbona umezungumza mengi,huku mpaka muda huu Mage sijamuona wala simu yake haipatikani. Nimemuulizia kwa shoga yake hajafika,simu ya Colin haipatikani,kuna nini katikati mbona sielewi, Colin yupo?”

“Ndiyo.” “Naomba kuzungumza naye.” “Sawa.”

Mama Colin alimpelekea simu Colin aliyekuwa amejilaza akitafakari kilichotokea. Mpaka muda ule alikuwa akiona kama ndoto yenye ukweli. Alijiuliza maandalizi yote na matangazo ya sherehe ya kukata na shoka atafanya nini,atawaeleza nini jamaa zake waliojitolea kusimamia sherehe ya harusi yao kwa gharama zao kubwa.

Rafiki zake wa nje ya nchi aliosoma nao Ulaya nao alijiuliza atawaambia nini ikiwa tayari walikuwa wameshona suti kwa ajili ya sherehe ile na walikuwa tayari kuja nchini ikiwa pamoja na kukodi vyumba kwenye hoteli za nyota tano na malipo yalikuwa tayari yamelipwa.

Kila alivyofikiria alikosa jibu,alitamani hata kumshawishi Mage akubali amuoe hata kwa mkataba wa mwezi mmoja ili jamaa zake wakiondoka waachane lakini wakiwa wamehudhuria sherehe yake iliyopangwa kutekekeza mamilioni ya shilingi.

Pamoja na kuujua msimamo wa Mage,bado aliamini kupitia wazazi wao anaweza kukubaliana nao. Lakini wazo la kuendelea kumbembeleza aliona kama ni kujidhalilisha, alikumbuka kitu. Alinyanyuka kitandani na kwenda kwenye kabati,kabla hajashika, mlango uligongwa,alipaza sauti kuuliza. “Nani?”

“Mimi,” ilikuwa sauti ya mama yake. “Naam mama,unasemaje?” ”Hebu fungua mlango.”

Alirudi hadi mlangoni na kufungua mlango, alionekana amechoka sana kitu kilichozidi kumuumiza mama yake. “Mama Mage anataka kuzungumza na wewe.” “Kuhusu nini?”

“Inasemekana toka ulipoachana naye hajarudi nyumbani na simu yake haipatikani, Colin mwanangu usiwe umemuacha wewe mtoto wa watu akaenda kujinyonga?”

“Mama mimi na wewe tunataniana hasa katika jambo zito kama hili? Inaonekana tukiwa ndani ya uchumba Mage alikuwa na mpenzi wake. Ni wazi lilikuwa shinikizo toka kwa mama yake ili nimuoe lakini ukweli umejidhihirisha,maji hayachanganyikani na mafuta.”

“Hebu kwanza zungumza na mama Mage.” “Mama nitaongea naye nini?” “Ulichonieleza.”

Colin alichukua simu ya mama yake ambayo ilikuwa wakati huo imekata na kupiga,baada ya muda ilipokelewa upande wa pili. “Haloo dada.”

“Hapana ni mimi Colin.” “Ooh! Baba za siku mbili?” “Nzuri,shikamoo.”

“Marahaba.” “Naam mama.” “Eti baba,mwenzio yupo wapi?”

“Sijui,” alijibu kwa mkato. “Kwa nini unasema hujui wakati mlikuwa wote siku tatu.” “Mama,nimeachana na Mage baada ya kunifukuza ndani ya gari lake kama mbwa.”

“Wee! Kwa sababu gani?” mama Mage alishtuka. “Ana mtu ambaye ndiye aliyemuingiza dunia ya mapenzi na kunitamkia kuwa amevunja uchumba wetu.

Kumbembeleza kwangu kumekuwa kero kwake na kuamua kuniteremsha njiani kisha kunitupia mzigo wangu huku akinitolea maneno ya dharau kuwa yupo mwanaume wa ndoto yake.” “Yupo wapi baba,yule mwanaume alimtenda.” “Basi ameamua kurudi huko.”

“Sasa atakuwa amekwenda wapi?” “Si kwa mpenzi wake,” Colin alijibu kwa kifupi. “Lakini baba linazungumzika,mimi ndiye mzazi wake.”

“Ni kweli wewe ndiye mzazi wake lakini moyo wa uamuzi anampenda nani unabakia kwa Mage.” “Basi baba,niachie kazi hiyo.” “Wala usisumbuke,mwachie uamuzi wake, mapenzi hayalazimishwi japo kaniweka katika wakati mgumu maishani mwangu.”

“Baba…baba..naomba usifike huko nimekueleza niachie mimi naomba kuzungumza na mama yako.” Colin alimpa simu mama yake aliyekuwa amesimama pembeni yake akiwa amepigwa na bumbuwazi kutokana na kauli za mwanaye.

“Haloo dada.” “Dada kwanza nisamehe sana kama kweli asemayo Colin ni kweli,yaani nilidhania utani kumbe kweli. Dada naomba uniachie suala hilo.” “Sawa,nikutakie usiku mwema.” *** Saa sita usiku,Mage aliingia ndani ya sebule ya nyumbani kwao,alishangaa kumkuta mama yake yupo kwenye sofa akiwa amepitiwa usingizi. Alimsogelea na kumbusu shavuni kitu kilichomfanya mama yake ashtuke. Mbele yake alikuwa amesimama mwanaye Mage.

Kabla ya kusema lolote,aliangalia saa kubwa ya ukutani iliyomuonesha ni saa saba kasoro usiku. Hakuiamini,aliangalia ya mkononi iliyokuwa sawa na ya ukutani,alimuangalia mwanaye kuanzia juu mpaka chini kama ndiyo siku yake ya kwanza kumuona kitu kilichomshtua Mage. “Vipi mama?”

“Unatoka wapi?” mama yake alimuuliza kwa sauti kali huku akinyanyuka kwenye kochi. “Kwani vipi?” Mage alijifanya kushangaa. “Nijibu unatoka wapi muda huu?”

“Niliporudi nilipita kwa shoga yangu.” “Nani?’ “Debora,humjui.” “Kufanya nini?”

“Mama mbona maswali mengi?” “Kwa nini unanitia aibu,Colin umemfanya nini?” “Kama alivyokuambia kwa vile alichokueleza nilisha kueleza muda mrefu si kigeni kwako.” “Kwa hiyo umerudiana na Hans?”

“Ndiyo mama,ndiye chaguo la moyo wangu.” “Wewe si ulikuwa unasema humpendi tena na mapenzi yako yote kwa Colin,imekuwaje sasa?”

Itaendelea
 
Wakili wa moyo 41

ILIPOISHIA:

“Kwa hiyo umerudiana na Hans?” “Ndiyo mama ndiye chaguo la moyo wangu.” “Wewe si ulikuwa unasema humpendi tena na mapenzi yako yote kwa Colin?” SASA ENDELEA… “Mama ningempenda Colin kama Hans asingekuwepo,kama matatizo yangemtokea nimo ndani ya ndoa nisingeweza kutoka. Lakini amerudi wakati sijaolewa,sina budi kumpokea,mama Hans nampenda zaidi ya kupenda nipo tayari anioe bila mahari.” “Mage mwanangu nitaweka wapi sura yangu?” “Ukiwaogopa walimwengu huwezi kufanya jambo la kimaendeleo,watasema mwanzo lakini mwisho watanyamaza na kusahau.”

“Mage mwanangu naomba ukalale ili kesho tuzungumze vizuri.” “Sawa mama.” Mage alikwenda kulala na kumuacha mama yake akiwa bado yupo sebuleni. *** Mama Colin usiku ulikuwa mkubwa kwake, kila alivyojitahidi kulala,usingizi ulikataa. Aliamini kabisa Mage hana tatizo bali mwanaye ndiye aliyevunja uchumba na kusingizia Mage ana mwanaume mwingine anayempenda. Akili yake ilimpeleka kwa Cecy tu,msichana aliyemuona ndiye tatizo kwa vile tokea awali aliona dalili mbaya.

Alipanga kesho asubuhi kwenda kwa kina Mage ili aweze kuzungumza naye na akimwambia Colin ndiye aliyevunja uchumba basi breki yake ya kwanza kwa Cecy na kukitia moto kibanda chao na kumfanyia kitu kibaya ambacho hatakisahau mpaka kufa kwake.

Asubuhi alikuwa wa kwanza kufika mbele ya nyumba ya kina Mage na kipiga honi mbele ya geti. Baada ya kufunguliwa geti,aliliingiza gari ndani na kwenda kupaki kwenye maegesho. Aliteremka na kuelekea ndani ambako ilionesha bado wamelala baada ya kumkuta msichana wa kazi akifanya usafi, alipomuona alimkaribisha: “Karibu mama.” “Asante,mama yupo wapi?” “Bado yupo chumbani kwake.” “Kamwite.”

Msichana wa kazi alikwenda kumuamsha mama Mage,baada ya muda alitokea na kushtuka kumuona mzazi mwenzie asubuhi ile. “Karibu dada.” “Asante,mmeamkaje?” “Mmh! Tunamshukuru Mungu.” “Mage yupo?” “Yupo chumbani kwake.” “Ndiye kanileta asubuhi yote hii.” “Ngoja nikamwamshe.” “Sawa.” Mama Mage alikwenda chumbani kwa mwanaye na kumuamsha. “Vipi mama mbona asubuhi sana?” “Mama Colin anataka kuzungumza na wewe.” “Ha! Mbona asubuhi sana?” Mage alishtuka. “Kwani uliyofanya madogo?” “Mmh! Haya twende nikamuone.” Walitoka pamoja hadi sebuleni alipokuwa amekaa mama Colin. “Shikamoo mama,” Mage alimsalimia mama Colin. “Marahaba mwanangu,samahani kwa kukurupusha asubuhi.” “Bila samahani mama.” “Naomba tuzungumze kidogo.” “Hakuna tatizo.”

“Na mimi niwepo?” mama Mage aliuliza. “Kwanza naomba tuzungumze wawili kisha tutazungumza wote.” Mama Mage aliondoka na kuwaacha mtu na mkwewe,baada ya kubaki wawili mama Colin alimuuliza Mage. “Mage mwanangu,kuna tatizo gani kati yako na mwenzako?” “Hakuna tatizo lolote.” “Mbona anasema kuwa eti wewe umevunja ndoa yenu,ni kweli?” “Ni kweli.”

“Kama ni hivyo sasa mbona unasema hakuna tatizo?” “Ndiyo mama hakuna tatizo,ila ni kweli alichokisema Colin.” “Wewe na yeye nani kavunja uchumba wenu?” “Mimi.” “Kwa nini?”

“Mama kabla ya kuwa na Colin nilikuwa na mchumba wangu ambaye kipindi hicho alikuwa ameoa. Lakini kabla ya ndoa,alipata matatizo ya kufiwa na mkewe na kurudi kwangu. Kwa vile ndiye aliyekuwa chaguo la moyo wangu,aliporudi kuniomba niwe naye wala sikuhitaji ushauri nilimkubalia na ndiye nategemea kufunga naye ndoa na si Colin,” Mage alisema kwa kujiamini. “Mage,hebu kuwa mkweli naomba usinifiche,Colin amekufanya nini kilichokufanya kuchukua uamuzi huo?” “Kwa haki ya Mungu,kweli hajanifanya lolote baya.” “Hujamfumania na mwanamke?” “Walaa.” “Kwa nini unavunja ndoa yako? Mage nakuahidi kukupa chochote ukitakacho ili tu ukubali kufunga ndoa na Colin.” “Mama naomba kuwa mkweli wa moyo wangu,japokuwa bado mdogo mapenzi nayajua kwa vile yalinijeruhi. Ningeweza kuolewa na Colin jina,lakini mapenzi yangu yangekuwa kwa Hans. Lakini siwezi kufanya kitu kama hicho,sitaki kumtesa Colin bila sababu.” “Hans ndiye nani?” “Mwanaume wa ndoto yangu.”

“Mmh! Nimekuelewa,basi Mage naomba ubadili uamuzi ili uolewe na Colin.” “Siwezi kuulazimisha moyo wangu,najua nawavunjia heshima,lakini nayaogopa maumivu ya moyo,niliumia sana wakati Hans ameoa. Kurudi kwake kwangu ni kutibu majeraha ya moyo wangu siwezi…siwezi kubadilika kwa vile nampenda sana Hans,” Mage alisema kwa sauti ya hisia kali. “Mmh!” mama Colin alishusha pumzi ndefu na kusema: “Nimekuelewa.” “Una la ziada?” Mage alimuuliza. “Mpaka hapo sina,nikuache upumzike.” “Sawa mama,msalimie Colin,naendelea kumuombea naye apate mke mwenye mapenzi naye ya kweli.” “Amen.” Mama Colin alimwita mama Mage amuage, baada ya kuja alimweleza: “Dada nikukimbie.” “Jamani,mbona haraka? Mmeelewana na mwanao?” “Tumeelewana na nimemuelewa vizuri sana.” “Basi nikutoe.” Waliongozana kutoka nje,walipofika nje mama Mage alitaka kujua kama mwanaye amebadili uamuzi. “Vipi amesemaje?” “Amesimamia msimamo wake,nami naheshimu alichokisema kwa vile amekuwa mkweli. Japo inauma lakini ndiyo ukweli wenyewe.” “Bado hatujakata tamaa,nitazungumza naye.” “Muache tu,kwa aliyo zungumza hata kwa mtutu wa bunduki habadili uamuzi wake.” “Mmh! Sawa,lakini Mage ni mtoto bado nina nafasi kama mzazi,” mama Mage alisema kwa sauti ya kukata tamaa. Waliagana na mama Colin,aliingia kwenye gari lake kurudi kwake akipata uhakika wa ndoa ya mwanaye kuvunjika.

*** Siku ya pili,Mage alimuamsha mama yake aliyekuwa bado amelala,baada ya kuamka alimuaga. “Mama nasafiri kidogo.” “Unakwenda wapi?” “South.” “Una maanisha Afrika ya Kusini?” “Ndiyo mama.” “Na nani?”

Itaendelea
 
bucho afadhali bana
Endelea endelea tena kidogo aise mbona unakatisha kama mizambwa bana
 
Last edited by a moderator:
Wakili wa moyo 42

ILIPOISHIA:

“Cecy hebu nisikilize.” “Ungekuwa na shida na mimi ungenifuata nyumbani kwetu.” Colin aliamini kabisa Cecy alikuwa amechukizwa na kitendo cha kumtelekeza na ahadi za uongo. Alitoka mbio kumuwahi Cecy nje, alimkuta amekaribia getini, akamfuata na kumshika mkono asiondoke. SASA ENDELEA… “Cecy najua nimekukosea,naomba unisamehe.” “Colin najua hunipendi bali mimi najipendekeza kwako,endelea na Mage wako.” “Hapana Cecy,nakuapia haki ya Mungu wewe ndiye moyo wangu,” Colin alipiga magoti mbele ya Cecy ambaye siku ile alionekana mrembo maradufu.

“Colin wewe ndiye wa kunifanya hivi au kwa vile mimi ni maskini,mbumbu sijui lolote? Asante,” Cecy alisema kwa sauti ya kilio.

“Ha..ha...Si..si…” Colin alinyamaza baada ya kusikia honi lakini alishindwa kunyanyuka kwa vile alikuwa bado kamshika mkono Cecy akimuomba msamaha. Geti lilifunguliwa na gari la mama Colin liliingia na kushangaa kumuona mwanaye amepiga magoti mbele ya binti mrembo.

Cecy alipomuona mama Colin akiteremka kwenye gari,alimsukuma Colin na kutimua mbio kwenda nje. “Cecy…Cecy rudi na..na..”

Cecy hakugeuka,alitoka hadi nje ya geti, bahati nzuri aliona Bajaj inapita, aliisimamisha na kupanda kisha alimweleza dereva ampeleke nyumbani kwao.

Colin alipotoka nje alikuta ameshaondoka. Alirudi ndani mbio na kumwambia mlinzi afungue geti,alipanda kwenye gari alilokujanalo mama yake na kumfukuzia Cecy kwa kuamini hasira za Cecy hazikuhitaji kupewa muda zaidi ya kutulizwa haraka,la sivyo atakosa Bara na Pwani.

Mama Colin,tangu afike alikuwa akijionea vioja asijue kumetokea nini na yule binti mrembo ni Cecy gani. Alimsogelea mlinzi na kumuuliza. “Eti yule msichana ni nani?”

“Hata sijui,alikuja na kuuliza kama upo, nikamwambia haupo,akaniuliza Colin, nikamwambia yumo ndani. Basi aliingia hata hajakaa,niliona akitoka mara nikamuona Colin akimkimbilia na kumshika yule msichana,akawa mkali. Nilishangaa kumuona akipiga magoti kumuomba msamaha.” “Nimesikia anamwita Cecy,ni Cecy yupi?”

“Mmh! Ndiyo leo namuona.” “ Sasa atakuwa amekwenda wapi?” “Hata najua! Labda atakuwa amemfuata huyo msichana.” Colin aliendesha gari kwa kasi kuitafuta Bajaj ambayo ilikuwa imeshapotea kuonesha Cecy alimwambia dereva aikimbize. Alikanyaga mafuta kuitafuta Bajaj kuelekea nyumbani kwao Cecy. Alipokaribia nyumbani kwao alimuona akiteremka kwenye Bajaj na kuingia ndani.

Colin alisimamisha gari mbele ya nyumba ya kina Cecy na kuteremka,hakufunga mlango alikimbilia ndani,Cecy alishangaa kumuona Colin pale,alimuuliza kwa sauti ya juu. “Colin umefuata nini hapa kwa masikini?” “Cecy mpenzi naomba unisikilize.”

“Nikusikilize nini,ni wazi nalazimisha mapenzi,nenda kwa Mage,mwanamke mwenye uwezo na elimu,niache mimi masikini nisiye na elimu.”

“Ukifanya hivyo utakuwa ukinifunga mikono na kunipiga,sitaweza kujitetea,naomba unipe nafasi.” “Umetudhalilisha vya kutosha kwa kutudanganya kuishi maisha ya peponi,leo yapo wapi? Najua una chaguo lako,naomba uondoke utuache na umasikini wetu.”

“Cecy najua nimewakosea lakini nami ni mwanadamu ninayehitaji kusamehewa kwa vile si mkamilifu.” Mama Cecy aliyekuwa nyumba ya pili akichota maji,aliporudi alishangaa kumkuta Colin kampigia magoti Cecy.

“Kuna nini?” aliuliza kwa mshangao. “Mama huyu si alikuja hapa kusema nini na alifanya nini?” Cecy aliuliza kwa sauti hasira. “Mama najua sikuwa mkweli lakini mpango wangu upo palepale.”

“Baada ya kukataliwa na Mage eeh?” Cecy alimuuliza huku amemshikia kiuno. “Hapana,majukumu yalinibana,mama naahidi nikitoka hapa kila nilichoahidi nisipofanya hivyo chukua uamuzi wowote.”

“Tuchukue uamuzi gani ikiwa hatukudai ni hiyari yako si lazima,” mama Cecy alisema. “Mama nilikuwa katika kipindi kibaya ambacho naamini ningelazimisha,ningeweza kuwatia kwenye matatizo.”

“Colin,maisha yetu ndiyo haya,hatuhitaji msaada wako,hatujaja kwenu kuomba msaada,hata masikini ana nafasi kwa muumba,” Cecy alisema huku machozi ya uchungu yakimtoka. “Cecy usifike huko,najua unanipenda. Nakuhakikishia kulipa upendo mara mbili.”

“Sihitaji,” Cecy alijibu kwa nyodo japokuwa moyo wake wote ulikuwa kwa Colin,alitaka kutikisa kibiriti kuona kama kimejaa.

“Cecy najua nimekukosea lakini amini huu ni wakati wako wa kuponya maumivu ya moyo wako.” “Cecy msamehe mwenzako,” mama Cecy aliingilia kati.“Basi amka,” Cecy alimnyanyua Colin ambaye alikuwa bado amepiga magoti kama muumini aliyekuwa akiungama dhambi kanisani.

Colin alinyanyuka na kukumbatiana na Cecy ambaye alijilaza kifuani kwa mpenzi wake, mama yake alikuwa pembeni,alitabasamu huku akiomba dua Colin amuoe Cecy ili kutimiza ndoto ya mwanaye. “Cecy nataka kukuhakikishia mbele ya Mungu,mama yako na mchana wa jua kuwa wewe ndiye mke wangu wa maisha.”

“Muongo Colin unanidanganya,” Cecy alisema kwa sauti ya kudeka. “Unataka nifanye nini ili uamini ninayosema.” “Nioe niwe mkeo.”

“Nakuhakikishia kukuoa uwe mke wangu na mimi niwe mumeo.” “Asante.”

“Naomba sasa hivi twende nyumbani nikamueleze mama mbele yako.” “Akikataa?”

“Hawezi,hii ni nafasi yangu ambayo hakuna wa kuiingilia,naomba uniamini.” “Mmh! Sawa wacha nikaoge ili tuondoke.” Colin alipewa kiti ili amsubiri Cecy aliyeingia ndani kubadili nguo,alitoka amejifunga upande wa kanga na kutoka kuelekea bafuni kuoga.
 
Back
Top Bottom