Hadithi: Sitaki tena

Hadithi: Sitaki tena

Yaani umetukosesha uhondo kwa kweli mi nimwifuatilia tangu mwanzo mbona tunaisoma wengi jamani
 
Kwa kuwa hadithi hii imepata wasomaji wachache basi naomba nisitishe rasmi kuiendeleza, na tutaendelea na hadithi yetu ya Play Gal.
Naomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Tupo wengi wengine tunasoma kimyakimya mweee
 
Ah tunasoma kimya kimya mkuu,ni nzuri usituache
 
Sawa. NAOMBA NIENDELEE,
ILA NINGEPENDA KUONA MUITIKO WA WATU AMBAO TUNAKWENDA NAO SAMBAMBA, HIVYO SIO MBAYA UKIMALIZA KUSOMA STORY UKADONDOSHA HATA LIKE, HII ITANIFANYA NIJUE KWAMBA WAPO WANAOSOMA.
Thanks
Pamoja sana....
 
Ilipoishia...

"...Inamaana aliyekufa ni Baba
Gervas..?"
"...yeah...! ndo huyo huyo na mi
niko njia moja kuelekea pale...

-
Endelea...

Kila nikipiga akili ni jinsi gani nitaingia nyumbani sipati
jibu..,haraka haraka halmashauri
yangu ya kichwa ikafanya kazi
fasta.,
"...'enewei' hii pesa niliyotaka
kumpa yule Dokta wacha niinunulie kanga nivae..!"
Njia hii niliyotumia ndo ilikuwa
sahihi kwani niliweza kuvaa kanga
na kujifunika mpaka eneo la
usoni na kuacha kijisehemu
kidogo tu cha kutolea macho, Watu walikuwa ni wengi sana
eneo lile nilijipenyeza mpaka
kwenye mlango wetu nakuingia
ndani.,nikamkuta Mama akiwa hoi
pale kitandani.,
"...Mama vipi bado tu umelala..!" "...Ndio mwanangu ntaenda wapi
na hali yangu kama
unavyoniona..!"
"...Unajua Nje kuna Msiba.....?"
".....Ntajulia wapi tena mwanangu
kama unavyoniona miguu imenijaa vidonda na ndo inavimba
kila mda...kwani msiba wa
nani...?"
"Mama..!,Baba Gervas hatunaye
tena..!"
"...Levina unasemaaa...?" Maskini sikujua kama ile taarifa
niliyompa juu ya msiba itamletea
madhara kwani nilishangaa Mama
akianza kujiuma uma meno kisha
akatapa tapa nakutoa mapovu
mdomoni kana kwamba anaugua kifafa,baada ya mda tena
nikamwona akinyong'onyea huku
anavuta pumzi kwa tabu pale
pale nikamuwahi na kuukutanisha
mdomo wake na wangu kisha
nikaanza kumpuliza ili naye apate pumzi kidogo.
Baada ya mda akarudi katika hali
yake kisha..,
"...Levina nipe maji..?"
" pumzika kwanza Mama.!"
"...Naskia kiu Mwanangu nipe hayo Maji..?"
Nikawa mbishi kumpa maji kwani
daktari alishaniambia
Ninapomuona Mama katika hali
ile nisithubutu kumpa kitu
chochote mpaka baada ya masaa. ~ BAADA YA MIEZI 4 ~ Tayari tulikuwa tumeshasahau
habari za msiba wa Baba
Gervas,kwani mpaka msiba
unaisha sikuweza kuiona hata
sura ya Gervas,..
"Au pengine alibanwa na shule au... aliogopa kuja kwasababu
anatafutwa na Mapolisi...?"
Ila kwa upande wa Mama yangu,
hali yake bado ilikuwa ikibadilika
siku baada ya siku, Mpaka mimba
inamiezi minne bado niliendelea na biashara yangu ya kujiuza
mwili kwani sikupata njia nyingine
mbadala wa kujikimu na maisha,
mtaa wote kila mtu alikuwa
akikerwa na tabia yangu ya
kutembea na waume za watu na hata Mama yake na Gervas
alikuwa mmojawapo aliyenichukia
sana na hata baada ya mumewe
kufariki.,
Ndipo nikapata wazo la kumrudia
Mungu. "...Bwana Yesu asifiwe..!"
"..Amina karibu binti..!"
"...Mchungaji..! nipo hapa mbele
yako kutubu zambi zangu zote..!"
"...Unaitwa nani Binti..?"
"Levina...!" "...Sogeza kichwa chako
karibu..,Fumba macho...!"
"...Baba katika jina la Yesu..! Weza
kumfungulia binti huyu
njia..,muachanishe na nguvu zote
za ajabu zitakazompinga..,Baba Mwenye majina Mengi..Yehova
Baba.., Masiha...kwa nguvu na
utukufu wako nakemea Mapepo
wote wanaomzunguka...kwa jina
la Yesu..!"
"...AMINA.....!" Baada ya hapo mwili wote
ukasisimka na sikuamini maishani
mwangu kama ipo siku ntakuwa
vile..,Nikawa mlokole safi
asiyemjua mwanaume,mara kwa
mara Mchungaji alikuwa akija nyumbani kumuombea
Mama,mpaka ikafika kipindi
akapata nafuu kidogo naye
akawa anaweza kutembea japo
kidogo..
"...Oya unamnyaka yule Malaya wa pale..?"
"Si yule aliyekuwa anatembea na
waume za watu..?"
"...aaahaa unasemea Levina..?"
"...Exactly..!"
"Enhee kwani amefanya nini..?" "...Si kameokoka eti..!"
"....Oya kausha...! kausha..! Acha
kunivunja mbavu mwana..!"
Nilidharauliwa kila kona
niliyopita,kwani ni kweli nilikuwa
nime'change' kuanzia Mavazi,Nilikuwa
Levina mimi wa kutembea na
Biblia mda wote kuhubiri neno la
Mungu mtaa kwa mtaa.,
"...Ushindwe katika jina la Yesu...!"
Nilikuwa mkali kukemea mapepo pale wanaume walipokuwa
wakinitaka kimapenzi., * * * * "..Hodi...! Hodi..!"
"Karibu... Levina embu nenda
kafungue mlango naskia kama
mtu anabisha hodi..!"
Ile nafungua tu mlango nakutana
uso kwa uso na sura niliyokuwa nikiifahamu.,kwani alikuwa
amevalia kisasa, suruali ya jeans
inayong'aa, tisheti nyeupe
iliyoandikwa kwa herufi kubwa
'BACK FROM US'..huku mwili
wake uking'aa kwa cheni alizojizungushia kuanzia
mikononi,shingoni mpaka
pembeni mwa mifuko ya kwenye
suruali yake,hakika alipendeza.,
"...Oooh..! Gervas...!"
"..Levinaaa...! c'om n hug em'..!" Sikumuelewa vizuri alichoongea
ila kwa vitendo alivyoonesha
viliingia kwenye hisia zangu
nakutambua kuwa anahtaji
nimkumbatie.,
"Ooh...baby..! baby..! baby..! R u aukey..! Haw abau ua Mama..!"
Niliambulia kusikia neno Mama
lakini nikamwelewa
anamzungumzia Mama.,
"...Mmmh yule pale sebuleni
mzima tu..! Pole kwa msiba..!" "...Naaah Naaah usijali Levy.., t
was da past...!"
"...Unasema.?"
Nilimuuliza kwani sikuwa
namuelewa kabisa
anachozungumza kwani alikuwa akichanganya lugha, nikamwacha
pale akiongea na Mama kisha
nikakimbia chumbani kwenda
kubadilisha nguo
"..Shikamoo Mama..!"
"Marahaba Mwanangu Gervas mzima wewe.?"
"Mimi mzima tu..sijui nyie
mnaendeleaje..!"
"Tunamshukuru Mungu..!"
"..kumebadilika sana hapa hata
na kwetu pia kidogo nilishapasahau...Mama nilishindwa
kuja kwenye Msiba kwani
nilikatazwa na ndugu kutokana
na ilee kesi ya levina..."
"Aaaaahhh ok, ok, ni kweli..!"
"....Hata hivyo hakuna kilichoharibika nimekuja kuangalia
kaburi la Baba pia nimeomba
misa kesho asubuhi tutasali pale
nyumbani...!"
Nilivyorudi nikamkuta bado
Gervas anaongea na Mama..., Baada ya mda Mama akaelekea
chumbani na kuniacha pale na
Gervas.,
"Enhee...! Niambie Gervas za
kutususa tangu ulivyoondoka...?"
".....Hapana Levina mimi sijawasusa ila tangu nilivyoondoka
na mzee kipindi kilee sikuweza
kupata njia yoyote ya mawasiliano
na wewe, Niliumia sana moyo
japo hutaniamini kwa hilo..!"
"....enhee nakusikiliza....!" "....Baba akaniacha na kurudi
huku bongo, nilikaa miezi mitano
bila ya kuwa na mawasiliano
yoyote na nyumbani, sikuweza
kuwa na mchumba yeyote kwani
niliamini wewe ndo wangu wa ndoa.,"
"...Ya kweli hayo Gervas.?"
"...Kweli Levy.,ilifika kipindi
nikapata kazi katika kampuni
moja huko ya kutengeneza
pombe kali aina ya 'HAMMIER WHISKY' nikawa nafanyakazi
huku najisomesha,kila siku
nilijitahidi sana angalau nipate
kusikia sauti yako lakini
ilishindikana..!"
"..Kwanini ilishindikana..?" "...Levy ...kila nikiwapigia simu
wazazi wangu japo nipate
kuongea na wewe wananiambia
nikuache haunifai na nisiwe na
wewe tena kwani umebadilika
sana na unatembea na kila mtu hapa mtaani..!"
Nikashusha pumzi huku machozi
yakinilengalenga kwa huruma
nikaendelea kumsikiliza Gervas.,
"...enhee ikawaje...?"
"...Mimi na wewe Levy tumetoka mbali na elewa kuwa nakupenda
na nitazidi kukupenda milele,
sijataka kuwasikia wazazi wangu
hata pale waliponiambia kuwa
umebadilika, Baba yangu alifariki
akiwa bado anakuchukia, Mama yangu pia mpaka sasa
anakuchukia kwani
nilivyomwambia kuwa nahtaji
kukuona leo alinijia juu na
kuchukia sana...! Levy..., Embu
niambie kweli unanipenda....?" Nilikaa kimya huku naitazama
mimba yangu na mwili kunisisimka
na ulokole wangu kuuweka
pembeni kwa mda....,
".....Levy hata kama mimba si
yangu mi niko tayari kwenda kuishi na wewe huko Marekani,
hiyo mimba mi nitalea....Elewa
kuwa bado nakupenda..."
"...S...a..a..a..wa..! Na Mama je? "..Kwani Hamna ndugu wa
kumuacha na Mama yako...?"
"...kama unavyoniona Mimi ndo
kila kitu kwa Mama..!"
".,Kwahiyo hutaki kwenda kuishi
na mimi au hunipendi..?" Alianza kuzungumza kwa sauti ya
ukali Gervas akanifanya
nitetemeke na kujikuta nikitoa jibu
haraka haraka...
"...Sawa Gervas nimekuelewa na
nitajitahidi tutakuwa pamoja..!" Hakuna mwanaume ambaye
amekaa moyoni mwangu kama
Gervas na hata kama angekaa
miaka Mia ndo akarudi bado tu
ningempenda kwa dhati, Juhudi
nyingi alizonionesha toka kipindi niko Gerezani mpaka nilipo ni
jambo la kumshukuru Mungu
kwakweli..Nilimalizana na Gervas
kisha alichoniambia kuwa kesho
yake atakuja kuniaga kwani Ofisi
ilimpa ruhusa ya siku tano tu za kukaa hapa. * * * * Asubuhi na Mapema nikiwa
nafanya usafi wa hapa na pale
huku Mama nikimwacha sebuleni
akizubaa mwenyewe,Nilifanya
usafi fasta fasta kisha nikaingia
ndani kumuogesha Mama yangu na baada ya hapo nikaingia
bafuni,na kutoka nikiwa safi kisha
nikavalia gauni langu refu huku
pembeni nikiwa na Biblia na
kalamu nikilichambua Neno la
Mungu.Nikiwa bado naendelea kusoma Biblia Mara nikasikia hodi
inapigwa mlangoni.,
"Karibu...! aaaah..! Gervas karibu
mpaka ndani...!"
"..Hata siyo mkaaji kwani nina
mda mchache na hapa Naelekea Mjini kidogo nikamfanyie
'Shopping' Mama kisha nitarudi
jioni sana..!"
"...Kwani safari ni lini..?"
"...Yani hapa unaponiona Tiketi
nilishakata zamani ya 'go an return' kwahiyo usiku kwenye saa
8 leo hii ndio nitaondoka..!"
"...aaah sas..."
Kabla sijamaliza kumuuliza
akadakia na kuendelea
kuzungumza., "...Wacha nimuage Mama then
utanisindikiza ndio utajua kila
kitu..!"
Akaingia mpaka sebuleni akakaa
kisha nikaenda chumbani
kumuitia Mama aje amuage.., ".....Mama kwaheri mi usiku wa
leo narudi Marekani..!"
"...Mbona haraka haraka
Mwanangu...,Mi nikajua upo hapa
hata kamwezi kamoja ndio
urudi..!" "Hapana Mama natakiwa haraka
sana Shuleni pia Kazini
ninapofanya kazi wananihtaji
sana..!"
"......Haya Baba safari Njema huko
uendako pia usitusahau Mwanangu uwe
unatukumbuka..."
"...Sawa Mama usijali ntaendelea
kuwakumbuka huko niendake
Mama...!"
Najua Gervas aliongea kwa makusudi ili Mama asiweze kujua
mpango wetu wa mimi na
Gervas.Tulitoka pale moja kwa
tukawa tunaekea nyumbani
kwao...,
"...Hapana Gervas mi sifiki kwenu Mama yako namuogopa sana...!"
".....Niiiiiiiiiini..?"
"....Gervas nielewe kwa hilo pia
usijali Mama yako niko naye
pamoja..!"
".....Levy ninachotaka ni twende nikakukabidhi kwa Mama sababu
leo hii natangulia Mimi then
nitawaachia Mipango yote ya kuja
we na Mama yangu si ndio?"
"....Sawa Gerva lakiini..!"
"Hakuna cha Lakini..., si umeshajua Mama yako mtu wa
kumwacha naye?"
"...Ndio nimeshajua....!"
Nikamuitikia kwa woga huku
nikiwa sijitambui nitamwacha vipi
Mama yangu. * * * * Ni Wiki moja imeshapita tangu
Gervas aondoke na
kuniacha,Nilijutia kumdanganya
hata Mama yake Gervas kuwa
sipo na Mama yangu naishi peke
yangu,Mpaka sasa Mama Gervas anajua kuwa Mama yangu aliugua
sana nikamsafirisha Moshi
nyumbani na kwa bahati mbaya
akafia hukohuko hivyo sasa hivi
naishi peke yangu., Siku
aliyoondoka Gervas alinipatia Dola thelathini pamoja na simu
huku akinisisitizia tufanye haraka
mi na Mama yake tuwe
tumeshaondoka.
Namkubali Mungu na nipo naye
Daima lakini kila nikimfikiria Gervas nakuwa katika wakati
mgumu,kwani Mama yake Gervas
hanipendi kabisa na mimi niko
tayari hata nimuache Mama
niondoke na Mama Gervas
nikaishi na Mpenzi wangu Gervas.,Siku moja tukiwa katika
pilika pilika za kuhangaikia Viza ya
kusafiria pale ubalozi wa
Marekani.,
"...Hivi wewe Levina na tumbo
lako na umalaya wako unaenda kwa nani...?"
"...Mama.,siku hizi nimeokoka na
nimemrudia Bwana Yesu hivyo mi
si Levina yule wa zamani..!"
"...eti Si Levina wazamani
nyooooooooooooooo...Na huko tuendako..? Walahi nitahakikisha
unarudi huku huku Malaya
mkubwa wee
'x@sh@hhzzzzzshhh'..."
Aliachia sonyo kali mpaka kila
mtu aliyekuwepo pale alishangaa,Sikuweza kumrudishia
zaidi ya kumwachia Mungu na
kuendelea kuvumilia kwani ndoto
yangu ni kuishi na Gervas
maishani mwangu. ~ BAADA YA WIKI MOJA ~ Furaha ilinitawala moyoni kwani
tayari tulikuwa tumeshapata Viza
na tiketi tukawa tumeshaweka
booking, Ndege ya shirika la
'EMIRATES' ndo tuliotarajia
kwenda nayo ikianzia safari yake hapa kisha kupitia 'Kenya' na
kituo cha pili kitakuwa 'Dubai'
kwa ajili ya kubadilisha ndege
itakayotupeleka mpaka
'Stockhom' halafu itaelekea
uwanja wa 'Amsterdam' pale Uholanzi kubadilisha tena ndege
ya kuelekea moja kwa moja
mpaka 'Maryland' ikipitia kusini
mwa 'Canada' na huko ndo
tutajua ni jinsi gani tutafika kwa
Gervas ambaye anaishi jimbo la 'Detroit..'
Si furaha tu niliyokuwa nayo bali
pia na huzuni huku nikiwa
sijitambui Mama yangu
nitamwacha na nani.....?
Gervas alikuwa akinipigia simu karibu kila siku huku akinisisitizia
kuwa nikienda huko sirudi kwani
ndo tunaanza Maisha..Sikuweza
kuihofia mimba niliyokuwanayo
kwani alishaniahidi kumlea mtoto
ntakayemzaa.. Safari hii halmashauri yangu ya
kichwa ilinituma vibaya kwani
nilijikuta nikitupa ulokole wangu
pembeni na kuanza kufanya
mambo kinyume na yale ambayo
yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.. * * * * Siku zilizidi kupungua hadi ikafikia
siku Nne zimebaki huku nikiwa
sijielewi kama safari kweli ipo au
la !,nikawa kama mtu
aliyechanganyikiwa kwani hali ya
Mama yangu ilikuwa inabadilika badilika sana haipiti siku bila
miguu yake kumvimba na ndio
hapo hapo presha inamuanza na
kuzidia lakini roho ya kikatili
ikanitawala kuna kipindi
Nilithubutu hata kumshindisha Mama yangu njaa karibu kila siku
hiyo yote ni kuhangaikia
safari...,Mama yake Gervas bado
aliendelea kunichukia lakini hilo
sikulijali zaidi ya kumvumilia
nakuona ipo siku atabadilika huko tuendako.
Roho ya kikatili iliendelea
kunirudia tena kila mda na kila
siku tena nilikuwa na roho mbaya
kama ile ya kule msituni
nilipomuua 'Pendo' na ile ya Morogoro pale Nilipomuua 'Baba
Ali'
Mama yangu nikawa simpikii
chakula zaidi ya kumnunulia
vijichipsi vikavu siku nyingine
nampa chai iliyokorogewa chumvi na hamna wala kitafunwa cha
aina yoyote ili mradi tu ajaze
tumbo siku ipite.,
Mara zikasalia siku mbili ikabidi
nijipendekeze kwenda kwa Mama
Gervas kujua safari itakuwaje hiyo keshokutwa ikifika,
"....Shikamoo....!"
".....Sihitaji shikamoo yako kama
chakula ile.., Enh upo tayari we
malaya usio na hata chembe ya
aibu..?" ".....Nipo tayari ila..."
"....ila nini......?"
"......Safari si keshokutwa mchana
Mama..?"
Nilijikuta nambadilishia mada bila
ya yeye kujitambua kisha nikamuaga akiwa amefura kwa
hasira,huku akinisindikiza kwa
fyonyo kali kuonesha kuwa
hanipendi kabisaa.,
".....Na hapa usije.., Tutakutana
'Airport' hiyo keshokutwa we malaya.!"
Akaniaga huku Moyoni nikiwa
sina raha ya vitu vitatu,kwanza
nitawezaje kuishi naye huyu
Mama Gervas huko niendako? Pili
itakuwaje hii mimba kwani ndio kwanza ina miezi Minne na Nusu,
Tatu nitamwacha mwacha vipi
Mama yangu na hali yake ile?
"....aah liwalo na liwe....."
Nikajisemea kimoyo moyo huku
nikijongea nyumbani kwetu, safari hii nilimuonea huruma kidogo
Mama kwani ilipofika usiku tu
nilimtengenezea uji tena ule wa
ulezi hadi akanishangaa,
alipomaliza kunywa tu,
"......Ahsante sana Mwanangu uji mtamu, umenikumbusha mbali
mno...!"
".....Usijali Mama nakupenda.."
Nilimjibu kinafki huku nikilitambua
kuwa sasa simpendi Mama hata
kidogo na hii yote ni kwasababu ya safari..,
Ulipofika mda wa kulala
Nilimwacha Mama akiwa
amejiegemeza kwenye kochi tena
akiwa amepitiwa na usingizi,
nilishangilia ushindi kimoyo moyo huku nikiamini mpaka kesho
itakuwa imesalia siku moja tu.
Nikaingia chumbani kwangu tena
kwa kunyata nikafungua Biblia
yangu na kuanza kuomba,
"....Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba unisamehe sana kwa
kitendo nitakachofanya hivi
punde...! Kisha nikamaliza kwa
kufanya ishara ya msalaba."
Nikafunika ile Biblia,kilichofuata
nikachukua panga na kamba nene ndefu na kurudi tena
sebuleni kwa kunyata lakini
nilipofika tu sebuleni sikumkuta
Mama pale nilipomuacha,hofu
ikaanza kunitanda,nikahisi moyo
wangu umepasuka huku na kule nikitoa macho kumtafuta Mara
nikaona karatasi pale Mezani
imefunikwa kwa hofu niliyokuwa
nayo nikaiwahi haraka haraka
kwenda kuichukua lakini kabla
sijafika pale ndo nakaribia tu mara.. * * *

Ni kitu gani kitatokea?
* * *

Je., Mama yake Levina
atakuwa wapi? Itaendelea
 
Back
Top Bottom