Hadithi: Sitaki tena

Hadithi: Sitaki tena

Ilipoishia...
Mara nikaona karatasi pale
Mezani imefunikwa kwa hofu
niliyokuwa nayo nikaiwahi haraka
haraka kwenda kuichukua lakini
kabla sijafika pale ndo nakaribia
tu mara..
'
Endelea.....
Nikasikia kama sauti ya mtu
anabisha hodi,haraka haraka
nikaikodolea saa yetu ya ukutani
ikanionesha ni saa Tisa na robo
usiku, nikawa najiuliza.,
"....Huyu ni nani anayebisha hodi sa hivi..!"
Sikuitikia ile hodi nilichokifanya
nikaichukuwa ile karatasi na
kuanza kuisoma.,
"...MWANANGU WA PEKEE
LEVINA, KWANINI UNATAKA KUNIUA BILA YA KOSA
LOLOTE?.., NIMEHANGAIKIA
MAISHA YAKO KWA MDA
MREFU MPAKA
SASA.,NIMESIKITIKA SANA
KUKUTA TIKETI YA NDEGE CHUMBANI KWAKO NA SAFARI
NI KESHO,BILA HATA
KUNIAMBIA CHOCHOTE
MWANANGU..?MPAKA
NIKAAMUA KUCHUKUWA
UAMUZI HUU WA KUJIUA NITANGULIE MBELE YA HAKI,
NAKUTAKIA MAISHA MEMA,
Mimi MAMA YAKO,
Mama Levina."
"..No..! No..! No..! Mama..!
Kwanini umewahi kufanya hiivyooo...!"
Nikajikuta nauvua moyo wa
kikatili na kuanza kumuonea
huruma tena Mama huku
nikielekea mlangoni kwa yule mtu
aliyekuwa anabisha hodi, "...Hapa mezani nimekuta kikopo
cha sumu ya panya na hii
karatasi, yeye Mama atakuwa
wapi sasa..?"
Kabla sijaufungua mlango
nikalipenyeza jicho langu kwenye tobo la kuwekea ufunguo.,
"...Mungu mkubwa.,huyu ni
Mama yangu kabisa, ona na
kanga nilizomnunulia kipindi
kileee ni hizi hizi...!"
Sikutaka hata kuuliza ni nani kwani sauti nilikuwa siiskii lakini
kwanilivyokuwa nimemchungulia
dhahiri atakuwa ni Mama yangu,
"..Itakuwa alienda chooni kipindi
kile nilivyoenda chumbani..? Lakini
ile sumu na barua kwanini aliamua kuandika vile..? Inamaana
anajua picha lote
litakavyokuwa....?"
Ni kati ya maswali niliokuwa
nikijiuliza bila kupata majibu
kwani ni kweli choo chetu kimejengwa nje ya nyumba na
yule niliyemchungulia ni Mama
yangu kabisa.,
Nikachukuwa vile vitu nilivyokuwa
nimeshika ambavyo ni kamba
kubwa nene pamoja na Panga kisha nikavitupia uvunguni mwa
kochi ili Mama asijue lolote kisha
nikarudi pale kwa ajili ya
kumfungulia.,kadri nilivyokuwa
nashika kitasa ndivyo nilikuwa
naona mlango unazidi kuwa mgumu nikausukuma kwanguvu
kuelekea ndani nilipo, mara
nikasikia kishindo cha mtu
amedondoka mbele yangu,
"...Mamaa...! Mamaa...! Ni wewe
Mama.....!" Niliugeuza ule mwili nakuanza
kuutingisha maskini ni kweli
alikuwa Mama japo Mwili ulikuwa
umeshabadilika na kuwa mweusi
kama mkaa,huku damu yake
ikibadilika na kuwa maji kama kamasi ikiteleza kutokea
masikioni,puani na Mdomoni,
Ngozi yake ilijikunja sana lakini
halmashauri yangu ya kichwa
ikafanya kazi fasta na kujua kuwa
huenda alikunywa ile sumu kidogo halafu akaenda chooni
wakati anarudi ikamzidia.,
Bila kupoteza mda nikauvuta ule
mwili nakufunga mlango kwa
ufunguo halafu nikamburuza
mpaka sebuleni kisha nikaingia chumbani na kutoa Biblia.,
"Eeeh Mungu Baba muweza wa
yote...! Natubu mbele za haki
najua kama mimi ni Mwana
mkosefu kwa kitendo nilichofanya
na nitakachoendelea kukifanya ila naomba kusamehewa...Amina.."
Nilipomaliza nikaingia chumbani
kwangu na kuchukua Gunia
kubwa na koleo kisha nikalipitia
lile panga pale uvunguni sebuleni
na kuuburuta ule mwili kuelekea nje ya nyumba yetu,nawaombeni
sana wasomaji mnisamehe kwa
nilichokifanya mbeleni,
Nikauburuta ule mwili mpaka
karibu na eneo lilipokuwa na
kaburi la Baba,nikaulaza na kuchukuwa panga langu kisha
nikaanza kutenganisha upande
mmoja mmoja nikianzia na
mikono,Shingo na miguu yote
miwili hakika sikuwa levina yule
mlokole bali nilikuwa Levina Mkatili tena mnyama kama simba
Dume tena yule anayoogopewa
na kila mtu duniani.,Nilichana
kitambaa cha nguo yangu na
kujifunika usoni kisha nikaanza
kumkatakata Mama eneo la usoni ili nipoteze ushahidi kama ikija
kujulikana,nahisi damu ilikuwa
imeganda kwani sikushuhudia
hata chembe ya damu ikimtoka.
Nilipomaliza nikachukuwa viwiliwili
nikaanza kudumbukiza kwenye ule mfuko kisha
Nikachukuwa koleo nakuanza
kuchimba kashimo kadogo kwa
ajili ya kumfukia ili niendelee
kupoteze ushahidi kabisa, nikiwa
ndo namalizia kuchimba mara simu yangu ikaita,
"...haloo..! Aaah Gervas"
"...enh Mmefikia wapi..?"
"...Mama tayari nimemwacha na
mtu na keshokutwa safari
itakuwepo usijali mpenzi wangu..!" "...Okey, msalimie sana Mama
yako mwambie bado
namkumbuka na kuna zawadi
yake tayari nimemwandalia..,"
"...Usijali Gerva,amekusikia..!"
Nikakata simu nakumalizia kuchimba pale fasta fasta
nilipomaliza nikashindilia na
kokoto zilizokuwa karibu.,kisha
nikaingia ndani kwa mbwembwe.
"...Zoezi la kwanza limeisha na
bado Mama yake Gervas, atanitambua huko tunapoenda..!"
Nilijisemea kimoyo moyo huku
nikijiamini kwa kile nilichokifanya
mda si mrefu,nilipofika sebuleni
nikapiga magoti na kuomba tena.,
"...Najua jamii yote itachukizwa nami, lakini mtetezi wangu ni
wewe Baba uliye juu mbinguni..,
Eeeh mwenyezi Mungu mlaze
Mama yangu Mahala pema
peponi,Amina.."
Nilipomaliza kusali tu ghafla nikaanza kujihisi mabadiliko
makubwa kwenye mwili wangu
sana sana eneo la tumbo, niliumia
sana,nilijikaza bado ikawa haisaidii
uchungu ulinizidia mpaka nikajihisi
mimba inataka kuchomoka,nilishindwa kuvumilia
nikaanza kugala gala pale chini
lakini nikawa kama ndo
nalichochea tumbo liendelee
kuuma,miguu ikavimba kwa
haraka nikawa najiburuza sasa kuelekea chumbani..,kwa
maumivu yaliokuwa yamenizidia
mpaka nikajikuta nimeingia
chumba cha Mama ambaye tayari
nimeshamuua,kwa kujikokota
taaratibu mpaka eneo la 'dressing tebo' huku nikitafuta dawa yeyote
ya kutuliza maumivu,nikajishikiza
kwa mkono mmoja huku mkono
mwingine ukiwa unafungua droo
za lile 'dressing tebo'..
"....Mamaaaaaaa..! Mamaaaaaa...! Mamaaaaa...! Mi sijakuua Mama
ulikunywa sumu mwenyewe
Mama...!"
Sura yangu ilikuwa imekutana na
kioo cha ile 'dressing tebo' ghafla
ikatokea sura ya Mama katika kile kioo, Nilichanganyikiwa na kujiona
zaidi ya kichaa kwani usiku ule ule
nilitokomea kusikojulikana huku
nikiwa mtupu nimevalia 'nait dres'
na nywele zikinivuruga,
Kulipokucha asubuhi kila mtu alikuwa akinishangaa kwani
nilikuwa tayari majalalani
nikiokoteza vyakula vichafu,
ukinisogelea utakuwa unatafuta
balaa na Mimi kwani nikaa si
Levina tena., "Ng'aaam...! Ng'aaam..! Piiiiiipi..!
Pipiiii...! Oya pisha njia gari inakasi
hiyo we fala nini..? Embu pisha
nitakuitia Mama yangu aje
akugonge..?"
Nilikuwa tayari chizi kwani Mikononi nilikuwa nimeshika
mifuniko ya ndoo huku
nikiendesha kama gari nazunguka
zunguka wapita njia
wakinishangaa..
"...Gervas panda twende wewe...konda wadai nauli haoo..!"
Uchizi wangu uliendelea na
ilipofika mda wa usiku sana,Vijana
kama sita hivi nafikiri walikuwa ni
majambazi kwani walikuwa na
makoti makubwa huku wamekunja sura zao walipita
eneo nililokuwa nimejibanza na
kujikunyata pale jalalani.
"....Oyaa masela eenh..!"
"...washkaji huyu chizi vipi..,embu
mchekini..!" "...Oyaa hapa si Marekani.?"
"...Fala nini..?"
"...Masela mi nina nyege sana
kama vipi njooni basi..!"
Niliwaita wakanifanya kitendo
kibaya wote wale huku nikifurahia kwa kile kitendo.
"...kama vipi na kesho mje basi..!
Au siyo masela..?"
Nikatoka eneo lile nikiwa na
mimba yangu huku nikijitembelea
kusiko julikana usiku ule, hata nilipowaona polisi sikuogopa
kabisa,
"...We binti chizi nini? Unafata nini
hapa Polisi..?
Nilijikuta nimeingia kituo cha polisi
huku nikiwa sina hata chembe ya woga..!
"...Kwani masela nyie vipi? Mi
muuaji Mmesikia..? Mimi ndo
niliomuua Baba Ali, Pendo na
hata Mama yangu nimemuua
mimi..!" "....Afande John, unarisikia hiri
ritoto rinavyoropoka..? Binti
unaitwaga rinani?"
"...Mi naitwa Levina.,oyaa kwanza
nipe bangi nitoe stimu..!"
"...Haroo hiri siro ri revina tunaroritafutaga..?"
"...Hamuwezi kunitafuta nyie
mabwege labda mumtafute
Afande Deus..!"
"Nani...? embu riingize rokapu
ritatusaidia kumpata huyo revina..,nakujua juu ya rimkuu
rifande Deus..!"
* * *
Levina tayari chizi na kaingia
Polisi bila kujijua,itakuwaje?
* * *
Vipi Gervas akija kujua
atamsaidia?
* * *
Itakuwaje mwili wa mama
yake Levina ukijulikana?
Inaendelea
 
Ww mnafiki sana, unajifanya kupinga post za pono kumbe ndo mwangaliaji mzur wa pono kwenye simu yako Valentina
 
Mtunzi: Andy

Ilipoishia.,
"...Nani...? embu riingize rokapu
ritatusaidia kumpata huyo
revina..,nakujua juu ya rimkuu
rifande Deus..!"
-
Endelea...
"...Mamaaa nakufaaaaa..!
maama..! Uuuuh...! Uuuh..!
Nilishtuka kitandani nikiwa sijielewi
na siamini kwa kilichonitokea
kama kweli ni ndoto au la!..,jasho
jembamba lilikuwa likinitiririka,Nikawa mzito kuamka,
nikaanza kupapasa papasa
kitanda changu,nikaivuta saa
yangu fasta ikawa inanionesha
kuwa imetimia kama saa mbili na
dakika ishirini asubuhi, sikuamini macho yangu mpaka pale
nilipofungua dirisha ndo nikajua
kuwa ni kweli asubuhi,Nikatoka
spidi mpaka sebuleni huku nikiwa
nahema juu juu nikamkuta Mama
akiwa amelala pale pale sebuleni nilipomuacha jana usiku baada ya
kumpa uji wa ulezi,
Nikamwangalia huku machozi
yakinitoka,
"...Mama.? Mama...?"
Akashtuka pale kutoka usingizini, "...Mwanangu Levina vipi tena
mbona unalia mwenyewe...?"
Nikampa mikono ishara kuwa
asimame kisha nikamkumbatia
kwa nguvu huku nikiwa na hisia
kali nyingi moyoni, "....Nakupenda sana Mama
yangu...!"
"....Mbona hata na mie
nakupenda pia mwanangu...!"
Nikatoka pale nakurudi tena
chumbani huku nikitetemeka na kutojiamini kama kweli niliokuwa
namkumbatia na kumsemesha ni
Mama kweli au la..!
"...Hiiiiiivi Kwanini huwa
naandamwa na ndoto za ajabu
ajabu hivi..? Eeh Mungu weza kuniepusha na ndoto mbaya
kama ya leo usiku...!"
Nikachukuwa Biblia yangu na
kalamu kisha nikaanza
kulichambua Neno la Mungu
taratibu., Ndani ya lisaa nikawa
nimeshamaliza kulichambua hivyo
nikamtengenezea Mama uji wa
ulezi kisha nikamwekea.,
"...Mama utakunywa uji upo pale
kwenye chupa, Mi naelekea kumchukua rafiki yangu Jammy
tutakuja naye baadaye..!"
"...Sawa Mwanangu uwahi kurudi
tu..!"
"Hilo tu...? Wala usijali kabisa
Mama yangu. Nikavaa nguo fasta kisha safari ya
kumtafuta Jammy ikaanza.
Jammy au kwa jina lake kamili ni
Jamila yule ambaye zamani sana
alikuwa rafiki yangu kipindi kile
nafanya biashara ya kujiuza mwili na ndiye aliyekuwa akinishikia
pesa zangu.Nilimkuta
nikamwelezea matatizo yangu na
sababu kubwa ya kusafiri na
kumuacha yeye na Mama
yangu,Kwakuwa Jammy hakuwa na sehemu maalumu ya kuishi
hivyo nikamwomba sana aishi na
Mama yangu na ipo siku ntakuja
kuwachukuwa acha kwanza
niende kuandaa Mazingira huko
Marekani. "...Mama nakimbia Morogoro
nitakaa kama wiki Moja
nitarudi,kwa hiyo utakuwa na
huyu rafiki yangu Jammy..!"
"....Kuna nini tena Mwanangu
huko Morogoro....?" "....Mama kuna dili Nono hilo we
subiri nikirudi ntakufanyia
maajabu mpaka ushangae...!"
"....Haya Mwanangu usisahau
zawadi..!"
"...Sema kingine Mama hilo tu...?" Kamwe sitakuja kumuua Mama
yangu nampenda sana,inanibidi
nguvu zote nizielekezee kwa
Mungu ili aniepushe kabisaa na
ndoto za ajabu kama ya leo usiku
niliyoota. Nikaingia ndani na kutoka na
kijibegi changu huku nikimwambia
Jammy anisindikize,nikamfata
Mama na kumkumbatia.,
"....Byee Mama....!"
Nikatoka pale huku namsihi Jammy anisaidie sana kuishi na
Mama yangu pia ahamishe vitu
vyake vyote na ahamie nyumbani
kwetu leo leo. * * * * Tayari ilikuwa imetimia saa sita
kama na dakika arobaini nikiwa
njiani na Jammy akinisindikiza
mpaka 'aiport'..Ndege ilikuwa
inaondoka saa tisa na
nusu,nikawa na hofu kweli ya kuchelewa,
"...Tukodishe teksi nini Jammy...?
Maana naona kama foleni
inasumbua..?
"....Ni sawa tu Levina...!"
Tukashuka kwenye Dala Dala fasta na kuchukuwa teksi
iliyotutoa kutokea pale Tazara
mpaka uwanja wa ndege, kidogo
tusingewahi kwani saa Nane
kamili imetugongea ndio tunaingia
uwanja wa ndege.. "...Chukua pesa yako hii hapa
fasta fasta...!"
Nikamlipa yule dereva teksi pesa
yake na kukimbia sehemu ya
kuingilia, ile tunafika tu tunakuta
wanaosafiri ndio wanaweka mizigo yao kwenye lifti ya mizigo
huku pembeni wakichekiwa
passpoti zao, haraka haraka
nikajisachi nakutoa pasipoti yangu
kisha nikaishika
mkononi ,nikamwachia simu Jammy na vijihela kidogo kisha
nikaagana naye akarudi zake.,
"...Kwa heri Jammy.,take care
sweety..!"
Nilijikuta naongea kiingereza cha
kujiuma uma pale mbele za watu na mimi nisijeonekana mshamba
eneo lile.
Kwa mbali nikamwona Mama
Gervas ndio anapita kukaguliwa
na tayari alikuwa anaelekea
sehemu ndege ilipo, Sikuwa na wasiwasi wowote kwani tulikuwa
tumeandikiwa kukaa siti moja
wote kwenye tiketi,Nikiwa na
shauku ya kuingia ndani ya
ndege,Hatimaye ile foleni
ikasogea na sasa ikafika zamu yangu kutoa ile pasipoti,yule mtu
aliyenihudumia akaanza kama
kuweka wasiwasi kwangu,Akawa
ananiangalia mara mbili mbili
huku anatingisha kichwa chake
kuonesha kuna kitu kinamtatiza juu yangu,
"...Unaitwa nani...?"
"..Levina Christian.."
Nilimjibu bila kuonesha woga
wowote.
"....Hii picha hapa kwenye Pasipoti ni yako...?"
"...Ndio ni mimi kwani vipi
mkuu...?"
"...Embu kaa kwanza pembeni
nimalize kuwahudumia hawa nina
wasiwasi na wewe... Nimekutafuta mda mrefu sana bila ya
kukupata...!"
Mwili wote ukawa kama
umepigwa ganzi,ghafla nikajikuta
haja ndogo ikitaka kunitoka pale
pale nikajihisi kama nina mkosi hapa duniani,nilitamani nichukue
Biblia niombe pale pembeni lakini
ikashindikana kwani nilishaipaki
ndani ya begi na begi langu
lilikuwa tayari limeshapitishwa
hivyo nikawa nipo tayari kupelekwa popote,huku
nikijiamini mtetezi wangu yu hai
na anaweza yote kwa yule
amuaminiaye.
Yule mhudumu aliendelea
kuhudumia wengine huku akinitia gadhabu na kushindwa kujua
nitoroke pale au?
"....sijui nimkimbie....? Lakini kama
ninakosa mbona hawajanifunga
chochote mikononi au hakuna wa
kunilinda...?" Alipowabakiza watu wachache
yule mhudumu aliyekuwa
amevalia mavazi ya kiaskari lakini
yalikuwa katika rangi ya bluu
kama wale askari wa uhamiaji,
akamwomba mwenzake awamalizie huku akinifuata
taratibu eneo nililokuwa nimetulia
namsubiria.
"...Twende paleee Mara moja
Levina..!"
Nilishangaa napelekwa sehemu nisiyoifahamu kisha tukaingia
chumba kidogo kilichokuwa
hakina hata mtu, akaiweka
bastola na pingu zake vizuri, kisha
akafunga ule mlango na ufunguo
kwa nguvu akanigeukia huku amekunja sura.
".....Nimekwishaa Levina mimi
leo....?" isikute ana undugu na
'Baba ali' au 'Baba Pendo....?"
"...Levina Christian...?"
"...Naam ndio mimi..!" Nilimjibu bila kuonesha woga
wowote,lakini moyo ulikuwa
hauna nguvu huku mdomo
ukinitetemeka kwa hofu.
"...Kwanza samahani sana kwa
kukupotezea mda.. Lakini bado kuna dakika thelathini ndio ndege
iondoke usijali kwa hilo
utaondoka tu...!"
Nikashusha pumzi na kuwa na
uhakika wa safari sasa,nikajiweka
sawa huku nikishika shika kitumbo changu kilichokuwa na
mimba kama ya miezi minne na
nusu hivi.
"...Mimi ni askari mpelelezi siku
nyingi na mara nyingi huwa
napewa kazi ya kukagua pasipoti za watu hapa..! Pasipoti yako
kwanza imenitisha sana na
nimekuwa na wasiwasi mkubwa
juu ya hilo...!"
Akazidi kunichanganya huku
akiniacha nisielewe anamaanisha nini..?
"...Niambie ukweli wako kutoka
moyoni nami nitaweza
kukusaidia...!"
"Ukweli gani huo tena..?"
"...Ulishawahi kufungwa gerezani Levina...?"
Aliposema hivyo nikaanza
kuingiwa na woga zaidi lakini
nikajiamini..!"
"...Ndio wakati mtoto
nilihukumiwa kifungo...!" "...Hapo hapo nikashangaa yule
askari akinikumbatia na kisha
akatoa Machozi.
"...Nakupenda sana mdogo
wangu, Mimi naitwa Magdalena
Christian au Mage kama walivyonizoea hapa,Na mimi ni
Dada yako kabisa wa damu japo
Mama alinitelekeza nikiwa mdogo
sana nikiwa na miaka minne
tu,Niliokotwa na wasamalia wema
na kunipeleka kituo cha Watoto yatima hadi nilipofikia miaka saba
nikampata mtu wa kunisomesha
na kuniendeleza..Nililelewa na
kusomeshwa na Mzungu ( Mark
Lowlery ) anayeishi hukoo Canada
kwa sasa lakini amenisaidia na anaendelea kunisaidia na huwa
nawasiliana naye karibu kila siku
mpaka hivi sasa,na hata Canada
huwa naenda kila baada ya miezi
miwili na yeye huwa anakuja
hapa. Nilijitahdi kusoma mpaka nikapata kazi hii,
"....Aaaaaaah My God.. Kumbe
nina Dada...?"
"....Yeah.,Ndio Mimi Dada yako
'Mage'..Kupitia kazi niliyonayo
nilikutafuta kwa mda mrefu bila ya mafanikio Mpaka niliposikia
ulikuwa Jela,Bado nikawa siamini
kama ni wewe.,"
"...Nilikuwa ni Mimi Dada..!"
"...Jamani marehemu Baba
tulishamzika siku nyingi sana..! Vipi Mama yangu mzima uko..?"
Huku akitoa machozi yalionifanya
nisisimke na mchozi kuanza
kudondoka taratibu.,
"...Mama mzima yupo
nimemuacha na rafiki yangu Jammy...!"
"Nilisikia kuwa ulitoka pale
gerezani na rafiki yako sijui
anaitwa 'Pendo'?..
"...Ndio Dada nilitoka naye
tukapata lifti then tulitekwa tukakimbilia msituni tukapoteana.
"Pole sana mdogo wangu vipi na
Morogoro ulifata nini tena..?
Morogoro nilienda kwa ndugu
yake na Rafiki yangu anaitwa
Baba Ali' Ulishawahi kulala pale..?"
Sikuwa na wasiwasi wowote kwani
nilijivunia niko na Dada yangu
tena wa damu hivyo nilimjibu
vyovyote kwa kujiamini.
"...Nililala pale kwa 'Baba Ali' kesho yake nikaondoka nakuja
Dar..".
"...Levina mdogo wangu..?"
"...Abeee Dada Mage..!"
"...Poleee sana nasasa ndio
unaelekea kuozea gerezani..! ...Nakuomba tena haraka sana
unipe tiketi na Pasipoti yako na
kuanzia sasa upo chini ya ulinzi.."
"...Vipi tena Dada Mage..?Si
umesema wewe ni Dada yangu
wadamu...?" Unahadhi ya kuwa na Dada kama
mimi? Embu angalia..!"
Akachomoa kitambulisho chake
cha kazi na kunioneshea..Maskini
kumbe alikuwa haitwi Mage,jina
lake ni Gracia. "....Ooooh..! My God....!
Nimekwisha Levina mimi
nateketea sasa..,
Alichukuwa pingu zake na
kunifunga?
Twende Polisi mbwa wee., Damu nzito kuliko Maji na leo ndio
utaeleza Mauaji yako
ulioyafanya..?" ******* * * * *
Levina kakutana na mkosi
mwingine na safari hii ni ukweli
siyo ndoto tena na safari
imekufa?
* * * *
Itakuwaje Mama Gervas
akifika peke yake Marekani bila
ya Levina?
Itaendelea
 
Dah!nilikuwa naiota jamani usituweke muda mrefu wadau wa hii story tupo wengi
 
Ilipoishia...
.....Alichukuwa pingu zake na
kunifunga?
Twende Polisi mbwa wee., Damu
nzito kuliko Maji na leo ndio
utaeleza Mauaji yako
ulioyafanya..?"
-
Endelea....
Nilijihisi mimba inataka kunitoka
kwani tayari nilikuwa nimefungwa
pingu mikononi mwangu huku
tunatoka nje..
"...Dada Mage niachie...
nakuomba sana Dada...?" "...Nimeshakwambia siitwi 'Mage'
na Mie siyo Dada yako
mpumbavu nini...! Unaakili kweli
wewe...?"
Nilijikuta naishiwa nguvu huku
nikipata uchungu ghafla wa hii mimba yangu...
"....Nakuomba unionee huruma
jamani Afande...!"
"....Ulivyoua hukuona huruma...?
Then unataka leo mimi ndio
nikuonee huruma wewe....? Mpumbavu sana tena sana we
Levina....!"
Yale maneno yaliingia moja kwa
moja kichwani mpaka nikajihisi
kizungu zungu huku nikimtolea
macho, Akiwa anahangaika kufungua
mlango ule wa kutokea.,Nilifura
kwa hasira nikajikuta naivaa ile
sura yangu ya kikatili pale pale na
kuachana na ulokole kwa mda,
Nilimvizia afungue tu ule mlango,Mungu si Athuman
punde alishikilia kitasa ili afungue
mlango ile tunataka tu kutoka
papo hapo nikajiangusha chini
huku nikiacha wazi eneo langu
lote la kuanzia mapajani, kiufupi lile gauni langu lilinifunika kiasi
kwamba tumbo langu lote likawa
wazi hivyo dhahiri kama
mwanamke kweli atanionea
huruma na ile mimba niliyokuwa
nayo., "....Mamaa yangu tumboo..!
Tumboo langu afande....!"
"....Tuuuumbo...? Embu twende
huko na utakoma huko
nitahakikisha unajifungulia
gerezani...! Au unataka nikutoe hiyo mimba.. eeennhh...?"
"....Hapana Afande fungua tu huo
mlango unipeleke unapotaka...."
Aliongea kwa hasira lakini
hazikunitisha,nikajifanya mjinga ili
nimpime nijue atanipeleka kweli au la.!kitendo cha kuinama na
kunivuta nisimame juu huku
nikiwa na pingu hapo hapo
nilimvaa na zile pingu shingoni
mwake nikamkaba nazo mithili ya
yule mwanamieleka 'undertaker' akizidisha nguvu zake lakini mi
sikujali kwani niliamini kichwani
mwake ni lazima atakuwa anajua
kweli tumbo lilikuwa likiniuma,
kumbe kwangu mie ilikuwa ni
mbinu tu! "....una...a...ta...k...a ku....nifanya
ni....ni...?"
Aliongea kwa sauti ya kujiuma
uma kwani tayari nilikuwa
nimemthibiti vilivyo,Kitendo cha
yeye kuachia mikono na kutafuta bastola yake pembeni ya suruali
ilikuwa kosa kwani pale pale zile
pingu zikawa tayari zinamalizia
kazi yake maana zilikuwa
zimeumana na koo lake na
kung'ang'ania kwa nguvu zote... "...Un...aaa...n..iu..aaaa
Leeee...vinaaaaa...!"
"....Kufa tu wewe si umesema sio
Dada yangu..? ...kwanini unataka
kunikatishia ndoto zangu....?
Shwaiin mkubwa we....!" Niliongea kwa sauti ya kikatili na
ubabe huku yule afande
akitapatapa mbeke ya macho
yangu huku na kule kuonesha
kwamba anakata roho.,
alifurukuta kwa nguvu halafu akaanza kulegea huku macho
yake yakibadilika rangi na kuwa
nyekundu na mishipa ikimtoka
eneo la shingo yake hakika
sikuogopa kwani nilishazoea
kuua.,Pale pale nikachukua ile bastola pembeni ya mfuko wa
suruali yake,nikaichomoa na
kuikoki kisha nikamuingizia
mdomoni mwake na
kuifyatua.,Nilijitenga mbali sana
na damu kwani ingekuwa rahisi kushikwa endapo ningekutwa na
damu kwenye nguo..nikahakikisha
amekufa kabisa,haraka haraka
nikamsachi mifukoni mwake na
kuupata ufunguo,nikauchukua na
kujifungua pingu kisha nikachukuwa tiketi yangu na
pasipoti ambavyo tayari alikuwa
ameshanipora.
Niliuchukuwa ule mwili wake na
kuuweka chini ya kameza mule
mule ndani kisha nikaufunikia na maboksi,nilipomaliza nikatoka nje
na kufunga ule mlango kwa
ufunguo kisha nikauweka
mfukoni na kuondoka., * * * * * ".....Najua sijachelewa sana lakini
mie nshakuwa mtoto wa mjini
hivyo njia zote nazijua....!"
Nilitoka kwa majigambo huku
nikijiamini safari yangu bado
ipo..nilipokaribia lile eneo la kuchekiwa pasipoti mara
nikamwona askari mwingine ndio
alikuwa anamalizia kufunga
mlango kuonesha kuwa watu
wamekwisha na mda wowote
ndege inaondoka, pale pale nikabadilisha mwendo na
kutembea mwendo kama
kumsindikiza bi harusi akiwa
kanisani au akiingia ukumbini
huku nimeshikilia tumbo langu
taaaaratibu... "....Askari.... Askari mnaniacha
jamani....!"
".....Ulikuwa wapi mda wote we
binti....?"
... Tumbo...! Tumbo linanisumbua
na hii mimba ndio kabisaaa..? "....Haya embu fanya fanya
haraka..,Pasipoti yako
imeshachekiwa pale..?"
"....Ndio afande..."
"...Na tiketi...?"
"Nayo pia vyote hivi hapa na mizigo yangu tayari
wameshapakia...."
Niliongea kwa kujiamini huku
nikiamini asilimia mia yule askari
hafahamu lolote pia mda ule
tulioondoka na yule askari yeye hakuwepo..,
"...'Host'! .....bado usifunge huo
mlango wa ndege kuna binti
anamimba huyu hapa
amechelewa kidogo...!"
Yule askari akawa anamwambia mhudumu wa ndege anisubirie.,
Mpaka napanda ngazi kwenye
ndege bado nikawa sijiamini amini
haswa kwa kitendo cha kumuua
yule askari pale pale uwanja wa
ndege., "...Mpumbavu sana wewe na
bora tungekuacha tu...!"
Ilisikika sauti pembeni yangu
nilipoingia tu ndani ya ndege
huku nikiwa nimemkabidhi tiketi
ya ndege yule mhudumu wa ndege,
"...Utakaa hapa..!"
Ahsante sana,
Nilijikuta peke yangu kwenye ile
siti,sikutaka kuuliza chochote zaidi
ya kukaa kimya peke yangu nikishusha pumzi.
"...Ulikuwa wapi we mshenzi
enh..!"
"...nilikuwa ch..."
"...Sasa kama hapa tu unaonesha
uvivu wako je ukifika huko? mwanangu si atakuwa analala na
njaa...?"
Alikuwa ni Mama Gervas akitokea
lango la chooni akiwa amefura
kwa hasira huku abiria wote
wakimshangaa kwa maneno anayotoa.,sikumjibisha hata neno
nikakaa kimya,safari ikaanza ya
kuondoka katika ardhi ya
Tanzania na kuelekea Marekani. * * * * Mpaka tunaingia Dubai bado
nilikuwa sijiamini amini kama kweli
ndo naelekea kwa Gervas au la!
Mawazo mengi
yalinitawala,nilijisalia kimyakimya
ndani ya ndege huku nikitubu makosa niliotenda,
"...Hakika kwa Mungu kuna
utukufu..! Eeeh Mungu wangu
weza kunifungulia njia zote..!
Baba weza kuniondolea mikosi
yote inayonikumba... Kwa jina lako nasema.. Ameni..!"
Ni kati ya sala nilizokuwa nikisali
kimyakimya bila hata ya Mama
Gervas kujua chochote.Mara kitu
kikadondoka eneo la chini yangu
kikitokea kwenye gauni niliokuwa nimevaa,haraka haraka
nikaangalia kwanza pembeni
yangu na kumuona Mama Gervas
akiwa kajifunika kitambaa kwenye
paji la uso akionesha kupitiwa na
usingizi.., Nikalipenyeza jicho langu fasta
eneo la chini kuangalia.
"....Mungu wangu si ule ufunguo
wa kulee uwanja wa ndege
huu...?"
Hofu ikaanza kunitanda kwani ni kweli nilipomuua yule askari pale
uwanja wa ndege nilimfungia na
ufunguo nikauweka mfukoni.
"...ayaiya...! iyaaa...! iyaaaa...!
iyaaaaa...!"
Nikauvuta na kuuchukuwa kisha nikaukagua vizuri, ulikuwa si
kama funguo za kawaida bali
ulikuwa tofauti kwani hata
maandishi yake yalikuwa
yameandikwa 'TZ ARPT 06' kila
nikiyasoma yale maandishi nazidi kuchanganyikiwa,lakini
halmashauri yangu ya kichwa
ikafanya kazi fasta kuwa niende
chooni nikaitupe,sikuchelewesha
Mda.
"...where is toilet..?" Sikutaka kuonekana wakuja
hata,palepale mhudumu
akanielekeza na kuingia huku
nikimwacha Mama Gervas akiwa
kapitiwa na usingizi,nilipofika tu
chooni kabla sijautupa ule ufunguo nikawa natetemeka
huku namuomba Mungu atende
miujiza usije onekana tena,
Kwa haraka niliyoingia nayo mule
chooni nilijikuta najisahau hata
kufunga mlango hivyo nikaufunga ile naumalizia kuufunga nasikia
kama kuna mtu ananiita.
"...Levina ...Levina"
"abee Mama..!
Sauti ya Mama Gervas ilikuwa
ikiniita kwani hakuna abiria yeyote aliyekuwa analijua jina langu zaidi
ya Mama Gervas mule ndani ya
ndege.
"...Hiiivi we mtoto? Kwanini
unaniaibisha kiasi hiki...? Hiyo
mimba yako ndo inakufanya hivyo....?"
"....Kwani nini tena Mama....?"
"...Unadhani hii ndege ya
marehemu Baba yako...?
Eeenh....! Twende ukaone upuuzi
ulioufanya...?" Sikudhania kama Mama Gervas
anaweza kuja chooni na kunitoa
tena akiwa ananivuta nywele
zangu mputa mputa ndani ya
ndege mpaka abiria wote wakawa
wananishangaa mimi na Mama Gervas,
"...Hapana...! Hapana....!
Hapana...! Hapana wala siyo
mimi...!"
Maskini ni ile siti niliokuwa
nimekalia ilikuwa imetapakaa damu nilivyokuwa
nimeegemea,kwa mshangao
niliokuwa nao nilijikuta ule
ufunguo unadondoka pale pale
kisha kwa haraka Mama Gervas
akauwahi kuuokota.. "...Na huu funguo wa nani?"
"...Wakwangu Mama....!"
Akauchukuwa nakuanza
kuukagua kagua,kisha nikamwona
kama ameshtuka ghafla.,
"...Umesema funguo ya nani?" "Ya kwangu Mama..?"
"....Mbona imeandikwa 'TZ ARPT
06'....?"
Aliposema hilo neno tu haraka
haraka yule mhudumu wa ndege
nikahisi kama ameshajua kila kitu kwani aliposikia tu Mama Gervas
akitamka namba za ile funguo
akatoka kasi na kuelekea kwa
marubani sikumwelewa ameenda
kufanyaje.,
"...We mtoto utakuwa jambazi wewe..! Hiivi kale kanyumba kenu
ndo muwe na funguo kama huu
uliotengenezea 'material' adimu
hivi..?"
Nikamyamazia aongee mpaka basi
huku akili yangu yote nikiielekezea kwa yule mhudumu., * * * * Ilituchukuwa kama Masaa saba
kutokea Dubai mpaka uwanja
mkubwa wa kubadilishia ndege
pale 'Amsterdam' uholanzi, Ule
ufunguo tayari ulikuwa mikononi
mwa Mama Gervas, tulishuka salama bila hata kuulizwa kitu
chochote kutoka kwa yule
mhudumu wa ndege, Na sasa
tulihitajika kupumzika kwa siku
moja hotelini kisha kesho yake
tutapanda ndege nyingine lakini ya shirika hili hili la 'Emirates'.
Tukiwa lango la kutokea huku
kila mmoja wetu akisubiria mizigo
nilishangaa mizigo yetu ya mimi
na Mama Gervas kuzuiliwa na
Askari wa usalama kama watatu huku wakiwa na bunduki zao
pembeni,
Hofu ikanijaa tena
Moyoni,walionesha kama sura za
kukasirishwa na kitu, wakanifanya
nikose Amani na kuanza kusingizia tumbo linaniuma..
"...Oooh Jesus...! My stomach
uuuh...! Uuuh...! Mummy pliz
help me...!"
"....shut up...! Tena ukome
kunililia hapa who is your mother....?"
Tayari Mama Gervas akawa
amenigeuka pale pale kisha
nikamshuhudia akitoa ufunguo na
kuwakabidhi wale askari,
wakauangalia mara mbili mbili kisha wakamruhusu Mama Gervas
aende ila mimi nibaki,
"....Eeeh Mwenyezi mungu why
me..? Why me...? why me..?"
Nilianza kutoa machozi huku
nikimshuhudia Mama Gervas akiondoka kwa kunizomea.... ********* * * *
Levina yuko tena hatiani kwa
kitu gani?
* * *
Je? Huu ndio utakuwa
mwisho wa safari ya Levina au? Inaendelea
 
Back
Top Bottom