Hadithi: Sitaki tena

Hadithi: Sitaki tena

Hongera levina kwa kumuua baba Ali ingawa ndio unarudi jela tena
 
Ilipoishia..
....uku mwili wangu ukiwa
hautamaniki..
-
Endelea..
"...Ingia kwenye gari mpumbavu
wee..!"
Aliendelea kunikaripia yule polisi
ambaye sikumfahamu kwa jina
lakini lafudhi aliyokuwa akiongea
ilinifanya niamini kabisa atakuwa ni muhaya tena yule wa kule
Bukoba ndani ndani
(Vijijini),Tukiwa ndani ya ile gari
aina ya 'One Ten' huku nikiwa
nyuma na askari mmoja na yule
mwingine akiwa anaendesha gari, Ujasiri wangu feki niliuweka
pembeni hivyo nikawa ni mtu wa
kutoa machozi na kujiuguza
sehemu zilizoonesha kuumizwa
katika mwili wangu,njia nzima
mpaka tunaingia Kibaha nilikuwa mtulivu bila kusemeshwa kitu
chochote na yule polisi,Tulipofika
maeneo 'Mbezi' yule polisi
akafungua kinywa chake na
kuniuliza,
"Unasikia njaa..?" "Kimya..!"
"Dereva embu pitia pale 'Mnama
Restaurant' tupate chochote..."
Maswali aliyoniuliza na maongezi
aliyokuwa akiongea na dereva
ndo kati ya vitu vilivyoanza kuuchanganya ubongo wangu..
"Mbona kabadilika tena huyu
polisi..? Asije kuwa wananifanyia
njama kama Baba Ali..?
Kwanini wameniagizia chakula
kama kweli nina hatia?..sijui nimuulize kosa langu ni lipi hapa
hapa..?"
Nikiwa bado nimekaa katika kiti
cha mgawaha mmoja pale mbezi
nikiwa mimi na polisi wawili
mmojawapo ndo yule aliyekuwa akinishikia bunduki na ndo
aliyenifunga pingu,
"Wewe muuaji unakula nini?
"Hapana..., Sili chochot..." kabla
sijamalizia kusema nilishtukia
napigwa na kitako cha bunduki na yule yule polisi..
"Usitufanye siye wapumbavu,
kuua uue..! Tunakuonea huruma
japo na wewe upate chochote
unatuletea 'usenge' au
umeshazoea maharage ya Gerezani nini...?"
Nilijikuta nanywea na kuwa
mdogo na kukubali kula chakula
kama walichoagizia wao ambapo
walikuwa wakila wali nyama..
Ndani ya nusu saa nikarudishwa tena kwenye lile gari lakini safari
hii nilishangaa hawakunifunga
tena pingu mikononi hivyo
nikabaki na maswali mengi sana
kichwani..
* * * *

Mawasiliano ya mimi na wale
askari bado hayakuwa mazuri
kwani hadi tunapita kimara
hakuna hata mmoja
aliyenisemesha zaidi ya yule
mmoja kukaa karibu na mini nisiweze kutoroka huku mwingne
akiwa dereva ndani ya ile gari...
Mawazo yalitawala sana kichwa
changu huku nikijiona si mtu tena
wa kuonana na mama yangu
wala Gervas..,nikiwa bado niko kwenye dimbwi la mawazo huku
tukiingia kwenye foleni ya mataa
pale ubungo ghafla macho yangu
yakaamia kwenye gari la pembeni
yetu aina ya 'suzuki' hasira
nilizoshikwa nazo ghafla ziliwafanya hata abiria waliokuwa
ndani ya daladala ambayo ilikuwa
nyuma ya ile gari niliokuwa
nimeikodolea macho waweze
kunishangaa,hilo sikulijari kabisa
maishani mwangu kwani Levina mi aibu ilishanitokaga siku nyingi
ukianzia pale shuleni kwa kina
Gervas waliponigalagaza wale
wanafunzi,pia katika basi
nililokuwa nimeshushwa hvyo
ukinishangaa mi ntakuona mtu wa ajabu sana.,
Akili na mawazo yakiwa bado
ndani ya kale ka suzuki ambapo
macho yangu yalikutana uso kwa
uso na mama ambaye sitakuja
nimsahau hata nife, hakuwa mwingine bali ni yule mama
aliyenipeleka polisi kwa mara ya
kwanza na ndiyo aliyefanya
maisha yangu yapo hivi mpaka
sasa..,
"lazima nife mimi au wewe" Nilijisemea kimoyomoyo huku
nikimtolea macho yalioambatana
na mchozi ulioanza kuniteremka
kwa ghadhabu niliyokuwanayo,
kilichofuata ni kuhema haraka
haraka huku pua zangu zikianza kujaa makamasi kama mtu
aliyepatwa na mafua ya
ghafla..kama kawaida yangu
sikutaka kuchelewesha mda..
"Bunduki kitu gani wacha
anifyatue tu lakini kwa huyu adui yangu siwezi kamwe kumuacha.."
Nikatoka spidi katika lile gari
nililokuwa huku nikimwacha yule
askari akinilenga huku
akinikimbilia lakini hilo sikulijari
ndani ya sekunde chache nikawa nshafungua na kuingia kwenye ile
suzuki na ku loki milango yote
tayari kwa kumvagaa yule mama
aliyekuwa akiendesha peke yake
ndani ya kale kagari..,
Nilitumia kucha zangu na meno kama filamu zile za kutisha
'VAMPIRE' kuisambaratisha
kwanza sura ya yule mama kisha
nikachukuwa mtandio wake
aliokuwa nao amejifunga
mabegani na kuuvingirisha shingoni mwake tayari kwa
kumnyonga,akiwa bado
anakurupuka na kutapatapa pale
gari zilikuwa tayari zimeruhusiwa
na trafiki na wale polisi niliokuwa
nao tayari niliweza kuwaona wakiwa nje wanataka kuingia
ndani nilipokuamo,sikujua hata
siku moja kuendesha gari lakini
nilisikia kwa wenzangu tu kuwa
kunakitu kinaitwa gia kipo kama
rungu pia kingine kinaitwa krachi kipo miguuni, sikulielewa hilo
lakini nilijikuta nimekanyaga chini
bila kujua kama ndo breki au ndo
hiyo krachi kisha nikalishikilia
rungu na kulisogeza kisha
nikashangaa kuona gari ikitoka tena kwa mwendo wa kasi
pale,nikiwa huku nimekaza ule
mtandio shingoni mwa yule mama
huku upande mmoja nikishikilia
msteringi nilijikuta nimevamia gari
za watu wengine waliokuwa mbele yangu na kusababisha ajali
mbaya pale huku umati wa watu
ukifurika katika lile eneo
kushuhudia ile ajari.,
Watu walikuwa ni wengi sana
mpaka nikachanganyikiwa japokuwa nilijihisi mwili wote
haufai kwa maumivu, ile gari
niliokuwa nayo ilikuwa
imeharibika vibaya baada ya mda
mchache nilihisi kuna watu nje
wanavunja vioo vya gari wanataka kuingia ndani katika kuangalia
vizuri macho yakamwona yule
polisi alionifikisha hapa nilipo..,
"Levina...! Levina...!Jisalimishe
mwenyewe unajitafutia matatizo"
Yale maneno ya yule polisi aliyokuwa akiniambia,
hayakuniingia akilini mwangu
kabisa niliona kama anampigia
mbuzi gitaa ili acheze.,yule mama
sikujua kama alikuwa amekufa ila
nilimwacha pale akiwa anahema kwa kasi ya juu huku akiwa
hajitambui wala hajiwezi hata
kunyanyuka,haraka haraka
nikafungua mlango upande wa
nyuma kisha nikatoka spidi huku
nikiuacha umati wa watu ukiwa haujui nini kinaendelea kutokana
na lile tukio..
Spidi niliyotoka nayo pale huku
watu wachache wakinishangaa si
kwasababu nimeponea
chupuchupu kwenye ile ajali bali pia waliniona kama mtu
aliyechanganyikiwa kwa jinsi nguo
zangu zilivyokuwa hazitamaniki
kwa uchafu tena ule uliokolea
damu katika ile suruali aina ya
trakisuti ilivyobadilika rangi nyekundu iliyokuwa imetapakaa
damu na kuwa kama nyeusi
nyeusi,
Sikumuogopa hata mtu nilizidisha
mbio huku nikielekea barabara ya
kwenda mwenge, kelele za wapiga debe pale ubungo
ziliongeza hisia zaidi ndani ya
kichwa changu kwani kitendo cha
kugeuka nyuma ilikuwa kosa
kubwa sana kwangu kwani
niliamini na kujua tu lazima umati mkubwa wa watu uwe
unanikimbiza nyuma yangu huku,
nikiwa nasonga mbele haijapita
hata hatua ishirini mara kundi la
watu wengine wakawa tayari
wametanda mbele ya macho yangu..
. * * * *
Baada ya yule polisi kunishika
ndani ya basi akanifunga pingu
baada ya pale akatikisa kichwa
chake kuashiria kuwa
ananifahamu akaniita na jina
"Levina...!" "kwanini umeua tena?"
"Au unapenda kwenda gerezani
tena"
Hayo ni kati ya maneno
ninayoweza kuyakumbuka kwani
yalinifanya niishiwe nguvu na kudondoka mpaka nikapoteza
fahamu,ninachokumbuka
nilishtuka na kushuhudia
nikipepelewa na yule polisi huku
nikiwa kwenye gari ambayo
sikuitambua vizuri kwa nje kwani alikuwa amenilaza ndani ya lile
gari na mikononi mwangu bado
nilikuwa na pingu hivyo nilipopata
usingizi akaendesha gari mpaka
nakuja kushtuka tumeshafika Dar
na nilikuwa nikiota ndoto tena matukio ya ajabu ajabu kama lile
la kumuua yule Mama na
kuharibu vibaya lile gari lake pia
kufukuzwa na umati mkubwa wa
watu pale ubungo..
"Mungu wangu kumbe yote yale ilikuwa ni kama ndoto..!"
Nilijikuta nausemea moyo huku
nikishusha pumzi kubwa..
"Uuhh...! uuhh...!"
Taaratibu nikiendelea kuhema
kwa nguvu na hasira kali., "Hapa ni wapi?"
Nilijikuta nikimuuliza swali yule
polisi aliyenitoa kule Chalinze na
ndiye alikuwa amenipakia baada
ya kuzimia pale Chalinze..
"Hupaswi kujua..unapaona pale?" "Nikakaa kimya.."
Huku nikiona kibao kimeandikwa
mbele yangu.., 'CENTRAL POLICE'
Nilitamani kutoroka pale lakini
nisingeweza kwani mda wote
nilikuwa na pingu mikononi. "Levina...! Embu niambie ukweli
hizo damu katika hyo suruali
ilikuwaje?"
Nikawa najiuma uma nashindwa
nimpe jibu gani kwani ni kweli
nimeua lakini nikisema ajue itanigharimu sana maishani
mwangu..
"Afande hizi ni damu za kawaida
tu ambazo nilipitia buchani
kuchukuwa nyama na kupeleka
nyumbani nilipokuwa kule Morogoro..!"
Nilijikuta namdanganya lakini
kiukweli alionesha kuchekeshwa
na mimi sana mpaka
nikamshangaa..
"Levina acha kunichekesha we mtoto...,
Mbona kule nilipokushusha
kwenye basi nilikuuliza swali kama
hili na ukaniambia kweli umeua
ila kwa bahati mbaya..?"
"Mi mi...? Labda utakuwa ulisikia vibaya
afande...."
Nilijitahidi sana kujikaza na
kubadilika lakini yule askari
hakuridhika na majibu yangu,na
kwa safari hii hakuwa mkali wa kunipiga bali nilimshangaa pia
kwa kuongea na mimi ndipo
akataka kuniambia ukweli sababu
kubwa ya kunichukuwa na
kunileta mpaka maeneo haya
kituo cha polisi endapo tu nitamjibu maswali yake kikamilifu,
huku tukiwa tumeliangalia lango
la kuingia polisi...
"Sitapenda nikuingize tena pale
polisi najua utateseka sana mpaka
uje kutoka tena mdogo wangu..,Ila kitu kimoja
ninachotaka kuongea na wewe ni
unipe jibu moja tu ili niweze
kukusaidia..
"Huko ulipotoka umeua?"
"Sijaua na naogopa sana kuua maishani mwangu..!"
Nilimjibu mara ya pili lakini kwa
sasa nilianza kuonesha
kauoga,kwani nilianza kuingiwa
na hofu huku nikitoka jasho
jembamba mwilini mwangu na niliamini kabisa ntakuwa
nategwa..
"Mimi nataka kukusaidia Levina
lakini unakuwa mbishi si ndio..?"
Alianza kubadilika yule afande
huku akinikodolea mijicho na kunionesha ufunguo wa zile
pingu kuwa kama nitakuwa
mkweli atanifungua pingu kisha
nitakuwa huru na salama,kitendo
kile kikanifanya uzalendo uanze
kunishinda na kujikuta namjibu anavyotaka..
"Ni kweli nimeua lakini si kwa
kukusudia.."
"Umeua..? ..Nani uliyemuua
Levina?"
"B...aa..a..a..b..a.. A...l..i.." Nilitaja jina kwa kujiuma uma pale
pale yule afande akabadilika
ghafla na kugeuza ile gari kisha
safari ikaanza lakini sikuweza
kujua ni wapi nilipokuwa
napelekwa zaidi ya kushuhudia akitoka kwa mwendo wa kasi
huku nikiwemo ndani ya lile gari
lake... *************** * * *
Levina anapelekwa wapi? * * *
Je., ukweli gani aliokuwa nao
yule afande...?
 
Mwendo wa kasi aliotoka nao
yule afande haukuwa wa
kawaida, kwani nilijikuta
nabilingita ndani ya lile gari lake
huku mikononi pingu zikinishika
vilivyo.. Nilichoweza kuambulia kujua ni
pale tulipokatisha maeneo
yalionesha kuwa na maduka
mengi huku daladala nyingi zikiwa
na mstari mwekundu katikati na
maandishi yaliosomeka 'ubungo - k/koo, hvyo halmashauri yangu
ya kichwa ikanituma moja kwa
moja na kujua tayari nimeingia
maeneo ya kariakoo,nikiwa ndani
ya gari huku yule afande
akiliendesha gari mithili ya mtu aliyeliiba lile gari au kuna mtu
anamfukuzia nilishangaa pia
kulipita tena kwa kasi eneo lile
ambalo nilishawahi kukaa
rumande kipindi kile cha kesi
yangu si kwingine bali ni kituo cha polisi cha 'MSIMBAZI'
Safari ilizidi kusonga mbele kwani
tulikuwa maeneo kidogo
ninayoweza kuyatambua
Kama vile tulikuwa kiprefti cha
kamata lakini maswali mengi kichwani mwangu yalinizidia bila
ya kuwa na jibu..
"Samahani afande.."
"Samahani ya nini? Na unataka
nini tena?"
Majibu yake bado yakanifanya niishiwe nguvu.,
"Nahtaji kujua tunaelekea wapi?"
"Nyamaaaazaa..!,Tena kimya
nisikusikie tena ukiongea..!"
Ilinibidi niwe mpole huku
nikishindwa kujielewa na kujiona sina umuhimu tena hapa
duniani,na sasa nilikuwa tayari
kwa lolote litakalonikuta mbeleni.,
"Bora hata akaniue nijue moja
kuliko kuendelea kuteseka namna
hii" Niliusemea moyo maneno ya
ajabu,mda wote moyo ulikuwa
ukinienda tena kwa kasi ya ajabu
huku kichwa kikiniuma sana
nafikiri yote ni kwasababu ya
kuwaza sana,Mara tukasimama eneo kama nilikuwa nalifahamu
kisha yule afande akachukuwa
funguo zake na kunifungua ile
pingu,
"Twende.."
Mara nikashangaa kushuka naye huku kanishika mkono,lakini
nikawa bado na wasi wasi kwani
ile nyumba mbele yangu kama
naifahamu japokuwa ilikuwa
imepakwa rangi,niliendelea
kumshangaa yule afande kunizungusha nyuma ya ile
nyumba na kukutana na kaburi
kubwa likiwa limeng'arishwa kwa
kuezekwa marumaru nyeupe
zilizong'aa mithili ya kioo,huku
katikati kukiwa na picha kubwa.. "Uuuuwiii..! Uuuuwiii...!
Uuuuwiii...!Baaaba umeniacha...!
Najua mimi ndo
chanzo..,Nisamehe baba yangu...!
Baaaaaaaabaaaaaaa...!!"
Nililia sana na kwa sauti ya juu huku nikiamini ile picha ni ya
baba yangu na pale tulikuwa
eneo la nyumbani kwetu
japokuwa hakukubadilika
sana,sauti ya juu niliokuwa nikilia
iliwafanya majirani kuja kushuhudia pale huku mlango wa
nyuma ukifunguliwa..
"Maaaamaa..! Maaamaa...!
Mnisamehe miiimi..."
* * * * *

Afande Deus ndo jina lililokuwa
likitambulika sana kazini
alipolitumikia jeshi la polisi, weusi
na urefu ukichangia kuwa na
mwili mkubwa ni kati ya vitu
vilivyomfanya kuogopeka katika jamii haswa ukizingatia ukali
aliokuwa nao akiwa kazini,
hakuwa na cheo sana lakini
uonekano wake ulimfanya
aonekane kama mtu mwenye
cheo kikubwa, Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusindikiza watuhumiwa
wa kesi mbalimbali mpaka
mahakamani na kuwarudisha
tena rumande huku akisaidiana
na mapolisi wenzake,
Alianza ukaribu na Baba yake Levina toka kipindi kile cha kesi ya
Levina na hii yote ni kufanya
levina anakuwa huru,alijitahidi
sana mpaka kuwashawishi
wakubwa wake ili Levina awe
huru lakini ilishindikana na matokeo yake alisimamishwa kazi
kwa mda mrefu wakamfanyia
upelelezi ikaonekana hakuna
ukweli ndani yake hivyo baada ya
mda mrefu kidogo akarudishwa
tena kazini lakini haikuwa mwisho wa kuwa karibu na Baba Levina
kwani hata alipofunga ndoa
msimamizi wake alikuwa ni Baba
yake Levina na alizawadia gari
ndogo ya kutembelea, Tayari
walikuwa kama familia moja na hata Baba Levina alipofariki
afande Deus aliumia kweli kwani
alifanyiwa mengi sana ikiwa ni
pamoja na kununuliwa kiwanja na
kusaidiwa pesa kidogo za kujenga.
Afande Deus aliahidi hata siku Levina akiwa huru atamsaidia
kwani ilikuwa ni vigumu kumfatilia
tena Levina Gerezani akiwa kama
afande anayejulikana na aliyewahi
kusimamishwa kazi kwa kesi ya
huyo huyo Levina.. Akiwa bado kikazi na magwanda
yake ya kipolisi na bunduki yake
akitokea chalinze kuwasindikiza
wazazi wake waliokuja
kumtembelea Dar, alikutana na
rafiki yake waliyewahi kusoma pamoja ambaye ni trafiki, kwa
utani waliozoeana aliweza
kukagua mabasi mawili ndipo
akamgundua Levina alikuwepo
kwenye basi moja wapo.,lakini ili
kuua soo ilimbidi ajifanye mkali ili aondoke naye kiulaini...
'
~ BAADA YA MIEZI 9 ~

"Umesema kapanda basi lipi?"
"Sijui vizuri lakini likizo zote huwa
anapanda basi la 'HOOD'"
Haraka haraka,nikatoka mbio
kuelekea nyumbani nikampita
mama sebuleni akinishangaa ndani ya dakika tatu nikatoka
nikiwa nimevalia kiblauzi cha
mikanda cha pinki chini nikipigilia
kipedo changu cha jinsi huku
chini kabisa nikiwa nimevalia viatu
vyeupe aina ya 'makhirikhiri' usoni nikiwa na zile miwani kubwa za
kuzuia jua na hivi kamwili
kalikuwa kamesharudi,mtoto figa
ninayo,makalio ndo usiseme,
yaani daaah...! Natamani kama
ungeniona hivi? Kwani sikuwa tena Levina yule mliokuwa
mnamjua zamani,
Nilijipenda sana na hii yote ni
kufanya Gervas na jamii kwa
ujumla inione si Levina yule
waliyekuwa wanamjua kipindi kilee cha matatizo.,
Nikiwa ndani ya daladala
iliyoukuwa inatokea kariakoo na
kuelekea ubungo kumpokea
Gervas aliyekuwa amemaliza
masomo yake ya kidato cha Nne huko Iringa., Nikiwa nimekaa siti
ya pembeni na Mmama
nisiyekuwa namfahamu nadhani
ni kutokana na mavazi aliokuwa
amevalia aina ya 'baibui'..
Tayari ilikuwa ni alasiri kwani hata saa yangu ya pinki aliyeninunulia
afande Deus ilinionesha
imeshatimia saa kumi na robo na
Gervas alikuwa aingie mida ya saa
kumi na mbili kwenye na nusu.,
nikiwa tayari nipo kwenye foleni maeneo ya manzese huku
nikizubaa kwenye gari kutokana
na kuwa na mawazo na shauku
kubwa ya kumuona Gervas..,
"Hapo dada, hapo mjomba..."
Mama hapo... " Ilikuwa ni sauti ya kondakta akidai
nauli za daladala..
"kaka si nimeshakupa? Unataka
nini sasa?"
Alilalamika kwa konda yule mama
aliyekuwa pembeni yangu huku akioneshwa kuchukizwa na
kitendo cha konda kumdai nauli
mara mbili mbili,
Tukiwa ndo tunaingia ubungo
niliweza kumshuhudia yule mama
akitoa baibui yake katika paji la uso huku akisogeza simu yake
karibu na sikio aweze
kuzungumza na simu..
"kumbe namfahamu..!Mshenzi
mkubwa we unabahati sana...!"
Alikuwa ndo yuleyule mama niliyowahi kumuota namnyonga
na mtandio pia ndo yule aliyewahi
kuniharibia maisha yangu enzi
zile,
Sikutaka tena ugomvi kabisaa
kwani afande Deus alinisihi mambo mengi sana ya kujihadhari
nayo ikiwemo ugomvi usiokuwa
na maana.,Hasira na chuki
zilinishika lakini sikuweza
kukabiliana naye..,
Saa yangu ilikuwa tayari inaonyesha ni saa kumi na mbili
kama na dakika ishirini,Nikiwa
tayari nimeshaingia mule ubungo
ndani ya stendi ya mabasi.
Hatimaye basi la 'HOOD'
likaingia,watu ni wengi walioshuka,kila walipokuwa
wanashuka ndivyo mapigo ya
moyo yalikuwa yakinienda
mbio,ghafla nikahisi kama kuna
mtu ananigusa mgongoni
nikajikuta nageuka bila kuangalia na kumkumbatia..
"Waaaooo Gervas...!"
Maskini aibu kubwa ilinishika watu
wakabaki wakinishangaa kumbe
hakuwa Gervas.,bali alikuwa ni
Mama aliyejitambulisha kwa jina la 'Mama Ali' huku akiwa na
mtoto wake 'Ali' na vijana wawili
wakiume waliovalia miwani meusi
huku wakizunguka zunguka
kuashiria wanakuja kumpokea
ndugu yao., "Samahani binti mimi si Gervas.."
"Nimeshajua hata mimi nimekosea
ila naomba nisamehe"
"Hamna neno kwani huyo Gervas
ndo unamsubiria..?"
"Ndio mama..ni ndugu na pia jirani yangu wa siku nyingi.."
Nikiwa bado namjibu yule Mama
aliyejitambulisha kama 'Mama Ali'
mara nikamuona Gervas akishuka
bila kuchelewa nikamuwahi na
kumkumbatia,kisha wale vijana wakamuwahi na kuonesha
vitambulisho vya kazi zao
kilichofuata nikumshuhudia
Gervas akifungwa pingu mbele ya
macho yangu.
"Kafanya nini tena..? Muacheni
jamani..,muaaaaaaaaacheni...!"
Nilihisi kama ndoto lakini ilikuwa
kweli Gervas kafungwa pingu bila
kujua kosa lake.,
"Geeervaaaaaas...!"
* * * *
Taarifa za juu ya kifo cha 'Baba
Ali' zilienea sana ikiwa ni kuanzia
Kwa majirani Mpaka kwenye
vyombo vya habari,siku ya Mazishi
'Mama Ali' alizimia mara mbili
ikiwa ni pamoja na kupata pigo la kuachwa na mtoto ambaye ni Ali
tena mdogo sana akiwa na miaka
4 tu,
Upelelezi juu ya kifo cha Baba Ali
ulifanyika kwa haraka zaidi na
kuanzia usaidizi wa Majirani ambao walimshuhudia mtu wa
mwisho aliyeingia ndani kwa Baba
Ali hakuwa mwingine bali ni
Levina japo majirani walimtambua
kwa sura tu na si kwa jina.,
Uchunguzi uliofanywa kwa kina ulibainika kukutwa na karatasi
mbili mifukoni kwa Baba Ali
ambazo zilifinyangwa sana na
zilionesha ramani ya anapoishi
Baba Ali ambaye si huyu
aliyeuliwa, Polisi walifanikiwa kumkamata
Baba Ali mwenyewe na
kumuweka hatiani kisha
akafanikisha mpaka jinsi ya
kumpata Gervas,hivyo polisi kwa
kusaidiana na Mama Ali wakawa tayari stendi ya ubungo
wakimsubiri Gervas,ambapo
ilisemekana ameshapanda basi
aina ya 'HOOD' hivyo kuanzia saa
kumi na mbili atakuwa
ameshafika Mama ali akisaidiwa na mapolisi wawili huku akishikilia
picha ya Gervas aliyopewa na
Baba Ali waliyemuweka hatiani
kule Morogoro,wakafanikiwa
kumpata Gervas., ************ * * *
Je.,Nini hatma ya Gervas?
* * *
Na Levina atakamatwa
kweli? Na itakuwaje akikamatwa?
'
Hii ndo season 2..
'
Inaendelea...
 
Nikajikuta navua viatu vyangu na
kuvishika mikononi huku nikiitupa
ile miwani kwani niliona haina
umuhimu tena kwangu,
Nilijitahidi sana nisiweze kupiga
makelele eneo lile, nikabaki nafuta mchozi tu huku
nikiwafatilia polisi kwa nyuma
nijue watampeleka
wapi,nikawaona wakiingia kituo
cha polisi pale pale
ubungo,nikashusha pumzi,kisha nikatazama ni jinsi gani naweza
kuongea na Gervas,nikiwa bado
najifikiria pale ghafla nikapigwa
kikumbo na Mama Ali.,
"Na huyu hapa tumchukuwe
aliniambia ni ndugu yake..!" "Nani..? Mimi...!,hapana...!, aah...!
aah..!"
Nilijikuta namkana Kama Petro
alivyomkana Yesu mara tatu,huku
nikijifanya kama simjui Gervas
kwakuwa nilikuwa tayari nilishalikoroga nilipomwambia
mwanzoni kuwa Gervas ni ndugu
na jirani yangu.,
"We binti.? Embu potea hapa
haraka...!"
Aliongea kwa sauti ya juu askari mmoja pale huku kanikazia
macho.
"Hapa leo siendi popote kama
kurudishwa gerezani wacha
nirudishwe mie na sio Gervas
ambaye hana hata hatia.." Nilijisemea kimoyo moyo huku
naongoza njia ya kutokea,
" Lakini haiwezekani narudi,
aah...! aah...!"
Nilijikuta narudi tena huku
nikiangalia saa yangu ikinionesha ni saa mbili kasoro usiku, hilo
sikulijali kikubwa ni jinsi gani
nitamtoa Gervas,Nikajikuta
halmashauri yangu ya kichwa
inafanya kazi fasta na kuchukuwa
simu yangu tayari kwa kumpigia 'Afande Deus'..,
"Haloo... Shikamoo Baba Deus..!
Nipo hapa polisi
"Wapi.? Na umefanya nini tena
Levina...?"
"Nipo hapa kituo cha polisi ubungo ndani ya stendi ya basi..."
Nikiwa bado naendelea
kumuelekeza Afande Deus
nilipo,nikashangaa ananikatia
simu..
Nilizidi kuumia moyoni kwani mi ndo nlikuwa mtu wa kumsaidia
Gervas ili aweze kutoka pale.,
Ilimchukuwa lisaa tu kwa afande
Deus kuweza kufika eneo
lile,nikamshuhudia akipitiliza na
kuingia ndani kituoni nadhani hakuniona vizuri nilipo hivyo
nikamfuatilia kwa nyuma,
"Jambo afande"
"Habari, kuna binti yangu yupo
humu ndani..?"
"Hakuna binti yeyote aliyeletwa leo humu....!"
Wakiwa bado wanajibizana
nikajitokeza kwa nyuma taaratibu
huku nikinyata.,
"Mimi hapa Baba...!"
"Twende nyumbani..!" Alinichukuwa kiaskari zaidi huku
nikitetemeka na kuelekea upande
aliokuwa amepaki gari
yake,nikaingia na kupanda gari
yake kabla hajaondoka
nikamwambia ukweli, "Baba...!"
"Unasemaje tena..?"
"Aliyekuwa amewekwa ndani siyo
mimi..?"
"Nani sasa..?"
"Ni Gervas..." "Naaaaaaaaaaaaaaaan.!"
* * * *
Nikiwa nimetulia kwenye gari
peke yangu huku nikimwacha
Afande Deus akirudi tena kituoni
kumalizana na mapolisi wenzake
kuhusu kutoka kwa Gervas,
haikuchukuwa mda nikamwona anarudi peke yake huku
akitingisha kichwa kuashiria kuwa
kashindwa kumtoa Gervas,
"Wamesemaje..?"
Nilijikuta naropoka nikitaka
kujua.. "Imeshindikana mpaka kesho
kwani ni kesi kubwa sana..!"
Miguu ilinilegea,mwili ukaingiwa
na ganzi,kichwa kikawa kizito mda
huohuo huku nisijue nini cha
kufanya, gari ikawashwa tayari kwa kwenda nyumbani.,
Baada ya nusu saa tukawa
tumeshaingia nyumbani kwani
njiani hakukuwa na foleni
kabisa,tuliweza kuingia nyumbani
kwakuwa afande Deus alikuwa na haraka akaniacha nje na kuniaga
kwa kuniambia kuwa kesho
asubuhi atadamkia kwa
Gervas,nikamuitikia na kuingia
ndani,
Nilipoingia ndani nikakuta hali si shwari kwani Mama alikuwa akilia
sana bila kujua nini tatizo,
"Au kwasababu nimechelewa
kurudi..?"
Nilijikuta najipa maswali yasiyo na
majibu, Nilijaribu kumnyamazisha lakini
ilinichukuwa mda mpaka
akanyamaza na kwikwi ikamuisha
kisha akanipa barua aliyokuwa
ameshikilia,nikaichukuwa na
kuanza kuisoma huku presha ikinipanda na kushuka,nikiwa
natetemeka..
Niliendelea kuisoma ile barua
huku nikihisi kichwa changu
kizito,huku ganzi ikinijaa
mwilini,kadri nilivyokuwa naendelea kusoma ndipo
kizunguzungu kikanizidia..,
"LEVINA CHRISTIAN"
Unahitajika Mahakama ya
mwanzo mkoani Mbeya haraka
upatapo barua hii.. Uchunguzi wa kina uliofanywa na
jopo la Madaktari kutoka Iringa
imebainika kuwa Marehemu
Pendo amefariki kwa kuchomwa
na kitu chenye ncha kali na mwili
wake kuokotwa porini huko Iringa,
Na siku alioachiwa huru gerezani
alikuwa na wewe Levina Christian
ambao wote mlikuwa wafungwa,
hivyo ukiwa kama mtu ambaye
uliongozana naye kutoka gerezani mara ya mwisho unahitajika na
mahakama haraka iwezekanavyo
kwa ushahidi juu ya kifo cha
Pendo Abel..."
Nilipomaliza tu kuisoma
nikamgeukia Mama nakuanza kwani alikuwa bado anaendelea
kulia tena kwa sauti ya chininini,
kichwa na akili yangu vikiwa
havifanyikazi, nilijihisi kujiharishia
huku nikiwahi kulibana tumbo
langu lililokuwa linaunguruma kwa kasi kisha nikamtazama
mama yangu.
"Nani ameileta hii barua..?"
"Vijana wawili waliovalia nguo za
kiraia wakiwa na gari..."
Sikuhitaji kujua la zaidi,nilichofanya ni kumuhadithia
Mama yote yaliyonikuta
kuhusiana na Gervas,
"Mama haiwezekani,inanibidi leo
leo tena sasa hivi nifanye juu chini
tena kabla hata afande Deus hajajua kitu chochote niwe
nimeshaondoka na kwenda
kulimaliza hili tatizo najua kesho
asubuh Gervas atatolewa kwahiyo
Mama nakuomba Gervas
usimwambie lolote juu yangu" "Mama nakuomba sana.,sana
tena sana..,
Hii barua na hata hizi taarifa
asizijue afande Deus,atashindwa
kunisaidia kumtoa Gervas..!"
"Mwanangu kwanini ni wewe tu jamani..?
.......Kwanini mikosi yote inakuja
kwako tu..?"
Aliongea kwa sauti ya kukwaruza
kuonesha kwamba amelia sana
na sauti inataka kumkauka.., "Mama Naumia na nitaendelea
kuumia.,Najua na wewe unaumia
lakini ninachokuomba uwe na
moyo wa subira nitarudi salama
tu wala usihofu?
"Sawa mwanangu..,ila chunga sana mwanangu.."
Haraka bila kupoteza mda
nikaingia chumbani kwangu na
kuvaa suruali yangu ya
jinsi,nikajivika tsheti yangu ya kijani
iliyokuwa na maandishi makubwa kwa mbele yaliyosomeka 'YOTE
MAISHA' chini nikadondoka na
raba za rangi ya kijivu,kisha
nikachukuwa kijibegi changu cha
mgongoni, nikatoka sebuleni na
kumuaga mama, "Chukuwa hii itakusaidia huko
ukipatwa na matatizo itakuepusha
nayo"
Alinivulia cheni yake ya dhahabu
kisha akanivalisha,
"na hii nauli itakusaidia uko uendako"
Akafungua upindo wa kanga yake
na kunipa kiasi cha shilingi elfu
sabini,
Haikuwa na jinsi ilinibidi
nichukuwe hivyo vitu kisha nikafanya ishara ya msalaba na
kuondoka zangu huku
nikimsisitizia Mama afanye juu
chini Afande Deus asijue chochote
na amdanganye vyovyote,
Sikuhtaji Mama anisindikize kwa usiku ule kwani nilijua kabisa
inaweza kutokea Afande Deus
akaja pale usiku kwa kushtukiza,
Nikiwa nje natoka naelekea stendi
ya mabasi japo nikaambulie gari
lolote,nikashangaa mwanga mkali wa gari ukinimulika
machoni,nikiwa najaribu kujizuia
na kulikwepa mara nikashuhudia
likisimama mbele yangu..
"Levina...! Levina...! Levina...!
Unaenda wapi usiku huu., Hapa huwezi kututoroka hata
mara moja,Na tupo hapa nje
tangu ulipoletwa na Afande
Deus..!"
Moyo ulilia paaah..! Kisha nikahisi
kama mlango unafunguliwa nyumbani nilipotoka,
"Kwani nyie wakina nani?"
"Huitaji kujua ila utajua ukifika
mahakamani kule mbeya"
Nikashuhudia afande mmoja
akishuka kwenye gari kisha akanifuata na kunifunga pingu
haraka akaniweka kwenye gari
aina ya 'Toyota land Cruiser'
nyeupe.,
Niliumia moyo,nguvu nilikuwa
tena sina nilipojaribu kuangalia nyumbani macho yalikutana na
Macho ya Mama yangu akiwa
amesimama mlangoni huku
macho yake yakionesha kuwa na
simanzi tele,mara gari ikitoka pale
kwa kasi ya ajabu.. "Mwanaangu....!"
Ndio neno la mwisho nililoweza
kuambulia kwa mama huku
akiniliza na kunisisimua mwili wote
kwani alinikumbusha aliniambia
hivyo kipindi kile nahukumiwa mahakamani.,
* * * *
Safari ilianza kuanzia Dar lakini
tulipofika Morogoro nilijikuta
Nalia sana kutokana na mauaji
niliyoyafanya ila nikajipa moyo na
tulipofika Iringa haswaa tulipofika
kijiji cha 'Liamkena' machozi mengi yalinitoka huku nikilia kwa
sauti ya chini chini na kwikwi kwa
mbali kila nikikumbuka mateso
niliyopata pale kwa wale
wanafunzi,pia nilipomua rafiki
yangu Pendo bila kukusudia, Nilipigwa na baridi lakini sikuweza
kulisikia nadhani hii ni kutokana
na kuchanganyikiwa kwanza ni
kuwaza itakuwaje kwa Gervas
asubuh pili huko niendako kutoa
ushahidi, Ilituchukuwa masaa kama kumi
na moja mpaka kufika Mbeya,
Tulifikia mahakamani moja kwa
moja kwani kesho yake ndo kesi
itasomwa ila nilishangaa
kupelekwa pale mahakamani asubuhi asubuhi, wale askari
wakanichukuwa hadi kwenye ofisi
nisiyoifahamu pale pale
mahakamani, nikiwa nashangaa
shangaa huku na kule ghafla
nikashangaa nasemesha kwa upande wa nyuma yangu..
"Hujambo binti..? Za masiku..?"
Alikuwa ni baba yake na Pendo
yule niliyomdanganya kipindi kile
kuwa nafanya kazi za ndani na
sasa alikuwa pale ofisini.. "Ba..a..a..a..a..b..a...Pe..ndo...Mi
sijamuua mtoto wako.. ******************** * * *

Mdomo wa kuropoka
umemponza tena Levina
itakuwaje..?
* * *

Je.,Gervas kashatolewa,na
Afande Deus atajua kuhusiana na
Levina? Itaendelea
 
asee majanga juu ya majanga, huyu kupona ni ngumu
 
Back
Top Bottom