Hadithi: Sitaki tena

Hadithi: Sitaki tena

Nilijikuta nachukua kile kikaratasi
na kumpatia afande Jesca
nikiamini kuwa hajui kusoma
kwani huwa mara nyingi
akitumiwa ujumbe kwenye simu
yake huwa ananitafuta nimsomee.. Alikichukuwa kile
kikaratasi akakigeuza geuza kisha
akanirudishia..
"Acha upuuzi wako nenda kwa
wenzako sawa?"
"Sawa" nilimuitikia lakini kishingo upande huku akili yangu
ikinituma nielekee chooni
nikakimalizie kukisoma,taratibu
nikaongoza hadi chooni
nikakifungua kwenye gauni
kilipokuwa na kumalizia kukisoma, enhe ikawaje vilee.,
"lakini msamaha wenyewe
utalenga wale wenye ulemavu
nilichokifanya ni kutoa ada yangu
yote niliyotumiwa shilingi laki mbili
na kuwaonga polisi kisha wakalipitisha jina lako kwenye
orodha ya watakao kuwa huru"
Hapohapo nikakichukuwa
Kile kijikaratasi na kukichana
chana kisha nikakitupia katika
tundu la choo,nikitoka na furaha ya hali ya juu huku nikijiona
mshindi,
'
BAADA YA WIKI MOJA
-
Ikiwa ni asubuhi na mapema
tukiwa tumejipanga mstari
halmashauri ya kichwa changu
kikawa kimeshafanya kazi
nakutambua ni kitu gani kilituleta
katika eneo lile., Kama kawaida ya afande kimbele
mbele afande Jesca alikuwa tayar
akiwanyosha watu mistari huku
akiwapiga na kuwafokea wale
waliojifanya ni wabishi,
Tayari maafande takribani nane walikuwa mbele yetu huku mkuu
wa gereza akiwa kashikilia karatasi
bila kuchelewesha mda akaongea
kilichotuleta eneo lile na kuanza
kutuita majina naweza kusema
sikuamini kilichotokea kuwa kama ndoto kwani ni kweli na mimi
nilikuwa katika ile orodha ya
walioachwa huru,
"nashndwa kujua nimfanyie nini
huyu kaka 'Gervas'..
Gervas...! Gervas...! Nakupenda na Nitazidi kupenda daima"
nilijisemea kimoyomoyo huku
nikipiga ishara ya msalaba na
kukusanyika na wenzangu huku
tukitokea lango kuu,
****

Gari aina ya Land Rover yenye
namba T643 ABK iliyokuwa
imebeba magunia ya mpunga
kutoka Tunduma kuelekea Dar es
salaam huku ikiwa imepakiza
abiria wa nne tu,wawili wa kiume na wawili wa kike.. nikiwamo
katika hilo gari kwa mwendo wa
taratibu huku nikiwa na mawazo
mengi yalionijaa akilini mwangu
ikiwa ni pamoja na hofu juu ya
safari kama tutafika salama, mda huo ilikuwa imeshatimia saa 2
usiku,tulikuwa tunakaribia kufika
Iringa., mawazo gongana
yaliniandama ndani ya kichwa
changu hasa kwa kuzingatia kuwa
bado nilikuwa sijajiamini kwa kile kilichonitokea kama kweli niko
huru ama la.!
Huku nikiendelea kuwa katika
dimbwi la mawazo usingizi
ukanipitia.
"Lete Jeki fasta...waambie na hao wadada washuke huko..!"
sauti ya dereva wa ile gari
akiongea na mwenzake ndiyo
ilinishtua sana kwani gari lilikuwa
limeharibika kilomita chache
kabla hatujaingia Iringa.. Baridi lilikuwa kali sana,nilihisi
kama mwili umeganda sikuwa na
nguo yoyote ya kubadilisha,hivyo
sikuwa na jinsi zaidi ya kujilaza
pembeni ya lile gari huku
nikitetemeka mdomo na meno yakiumana kama nimepigwa
ganzi..
Nikiwa pale chini natafuta tena
usingizi huku dereva akiendelea
kutengeneza lile gari., kwa
mbaaali niliona mwanga mkubwa ukitumulika huku unasogea
taaratibu, akili yangu na wale
wenzangu haikuwa mbali kwani
lilikuwa ni gari lakini ilipofika
karibu yetu dereva wetu akawa
ameipungia mkono isimame kwa ajili ya kuomba spana.. ilisimama
kisha wakashuka wanaume
watano waliokuwa wamevalia
makoti meusi huku mikononi
wameshika panga na bunduki
wakitufuata eneo tulilokuwa.. "Wote mikono juu"
Na ole wake mtu asimame au
aongee hata neno moja.."
aliongea mmoja wa wale
wanaume aliekuwa anasura ya
kikomavu iliyojikunja kunja mithili ya mchekeshaji wanaomwita
'King'wendu', huku kavalia
miwani meusi na mdomoni
akivuta sigara na kutupulizia
moshi..tukiwa bado tupo pale
chini tukitetemeka na kuogopa pia tulikuwa kama tumeshajitolea
kwa lolote litakalotupata..
Ghafla milio ya risasi ikaanza
kurindima kuelekea kwenye
matairi ya lile gari letu
yakapasuka yote manne kisha wakamchukuwa dereva na
wenzake wakawachinja mbele ya
macho yangu kisha wakaondoka
na kuniacha na mwenzangu
niliyetokanaye gerezan, Roho ya
Ujasiri,ukatili na ukakamavu niliokuwa nayo toka nipo
kifungoni ilinisaidia sana kwani
sikuogopa hata kidogo
kilichonitokea mda mfupi uliopita
nilimchukuwa mwenzangu na
kutokomea naye msituni.. Nikiwa nimemshika mkono
mwenzangu Pendo tulikuwa tayari
tumeingia msitu wa Ruaha ambao
kiukweli ulikuwa ni mkubwa sana
na uliojaa na miti
mirefu,hatukuweza kuogopa kitu kwani maisha ya gerezani
yalikuwa tosha kwa mimi na
Pendo kuwa wajasiri,wakatili na
wakakamavu mda wote,
"Nimechoka.,nimechoka siwezi
kuendelea tena Pendo..tupumzike hapa.." Nilimwambia pendo huku
nahema nikitokwa jasho usoni
kwa mwendo tuliokuwa
tunatembea haraka haraka
hakika ulikuwa ni mwendo mrefu
sana., "Sasa ukiendelea kudeka deka mi
nakuacha, au unapenda kubakia
hapa porini?" alisema Pendo kwa
ukali kudhihirisha kuwa alikua
amechoshwa na kitendo cha mimi
kupumzika.,Nilijikaza na kuinuka tayari kwa kuendelea na safari
lakini..
"Pendo.! Pendo.! Mama yangu
wee mguu wangu..! Nilijikuta
namuita Pendo asiondoke kwani
mguu wangu kwa upande wa nyuma ulikuwa umeshachanika
na damu nyingi zilikuwa
zikinitiririka., Pendo hakuwa na
jinsi kwani aliona kubaki na mimi
katika ule msitu
kungemchelewesha kufika kwao kwani safari yake ilikuwa inaishia
Dodoma.,
"Pendo..! pendo..! Usiniache
pendo..! ntabaki na nani tena
Pendo..!"
aliniacha nikiwa katika hali mbaya huku machozi yakinitoka,na
kukata tamaa,nakuona bora
ningemsubiri Gervas aje
kunichukuwa.,ulikuwa tayari ni
usiku sana nahisi ilikuwa imetimia
kwenye saa nane au tisa kwani giza tororo ndilo lilitawala sana,
Nikiwa bado katika dimbwi la
mawazo na hasira nyingi pale
chini huku milio ya wanyama
wakali ikipaza huku na kule,
Ghafla nikaanza kusikia mshindo wa kitu kama kinakuja tena kwa
kasi ya ajabu, kadri mlio
ulivyokuwa unazidi kuwa mkubwa
mapigo yangu ya moyo yalizidi
kunipelekesha.nilihema mpaka
nikajihisi nimeishiwa pumzi sikuwa na lakufanya zaidi ya kujitoa kwa
lolote litakalonipata kutokana na
mguu kuumia vibaya kutokana na
kujiumiza na kipande cha bati
kwenye gari wakati tunakimbia
kujiepusha na yale majambazi waliotuteka kulee..
Hatimaye nikaanza kutambua kitu
kilichokuwa kinakuja kwani
mwanzoni nilijua labda atakuwa
Pendo amerudi kuja kunichukuwa
lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa mnyama mkubwa mweusi
aliyefanania na nyati ila alikuwa
akija kwa mwendo wa taratibu
huku akinifuata katika eneo
nililokuwa nimekaa..mwili
ulinitetemeka sana hofu kubwa ilitanda ndan ya kichwa
changu,nilitetemeka sana huku
mchozi ukiwa unanitoka
ukiambatana na mkojo kwa
kasi,maumivu ya ule mguu
yakatoweka kutokana na kile kilichokuwa mbele yangu..
"jamani..! jamani..! jamani..!
Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!"
Nikiwa bado nalia pale ghafla.. INAENDELEA...
 
akitoka hapo porini salama, nahic lazima atarudi tena gerezani kwa kesi ya mauaji
 
Ilipoishia.,
-
"jamani..! jamani..! jamani..!
Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!"
Nikiwa bado nalia pale ghafla..
'
Endelea.,
-
Ghafla nikamulikwa mwanga
mkubwa nikaangaza huku na
huku nikaweza kuwaona watu
wakiwa wamenizunguka..
"Wewe ni nani.? Na unafanya nini
hapa?" aliongea mmoja wa watu wale waliokuja pale nilipokuwa
baada ya kupiga makelele kwa
kuona mnyama akinifuata kumbe
hakuwa mnyama wa kunidhulu
bali alikuwa ni ng'ombe
aliyechelewa kuingizwa bandani na katika lile eneo walikuwapo
wanaishi watu.,
"Naitwa Levina nimetokea mbeya
ila gari yetu ilipata ajali tukawa
tumevamiwa na majambazi hivyo
nikaamua nikimbilie huku msituni..kwani hapa ni wapi?"
niliwajibu hapo hapo huku
nikishusha pumzi na kuwauliza
swali bila hata ya kuonyesha
woga wa aina yoyote,
"Hapa ni kijiji cha LIAMKENA tupo katikati na hili pori la msitu wa
Ruaha., Haya mbebeni tumpeleke
nyumbani na wewe John swaga
huyo ng'ombe turudini
nyumbani" aliamrisha mmoja wao
kwa sauti ya juu., Safari ya kutoka katika ule msitu
mpaka kuingia katika kijiji cha
'Liamkena' usiku wa manane
ilifanikiwa kwani nilipofika tu
wakaanza kunitibia kidonda
changu kwa kutumia dawa za kienyeji huku wanakijiji wengine
kutoka katika kijiji kile wakija
kunishangaa si kwakuwa nilikuwa
natisha bali walistaajabu
kuokotwa usiku wa manane
kwenye ule msitu ulioaminika kuwa na wanyama wakali tena
wengi,
Ndani ya siku mbili nikawa tayari
nimeshazoea mazingira uku akili
yangu nashauku kubwa
nikiielekezea nyumbani na jinsi gani ntampata Gervas na
kumshukuru kwa yote
aliyonitendea.,
Hali ya kidonda changu haikuwa
mbaya kwani kilianza kufunga
taratibu, ila wanakijiji walipenda niendelee kubaki mpaka nipone
kabisa jambo ambalo lilipingana
na halmashauri ya kichwa
changu,
Ilipofika saa tano usiku huku kijiji
chote kikiwa kimerindima kwa giza nene,sikuwa na hata chembe
ya usingizi, jicho langu liliweza
kupenyeza kupitia katundu
kadogo kadirisha kalichokuwa
kametengenezwa kwa kutumia
miti, niliweza kujua mara moja sehemu ya kutokea hivyo
nikachana kipande cha gauni
langu na kukifunga katika eneo
lakidonda changu kisha
nikachukuwa mishale na upinde
huku upande wa kulia kwangu nikashikilia panga tayari kwa
kuingia tena msituni huku
nikitafuta barabara ya
kutokea,nilifanikiwa kutoroka na
kuingia msituni,akili yangu na
mwili wangu vikawa kama vimeshapigwa ganzi kwani sikuwa
muoga hata kidogo,nilitembea
taratibu lakini nikaona kama
nachelewa hivyo nikaanza
kukimbia wakati nakimbia niliweza
kusikia kama kuna watu wananikimbiza nyuma yangu
kama sivyo basi ntakuwa
nimeingia katika ulimwengu wa
wanyama pori tena wale wakali
nikasimama na kujificha nyuma ya
mti kisha taratibu nikachomoa mshale japo nilikuwa sijui
kuutumia lakini niliweza
kuuelekezea upande wa ile
sehemu niliyotoka na kuhisi kile
kitu kitakuwa kinatokea upande
huo, Niliunyosha na kufanikiwa kuuachia,nikasikia sauti ya kike..
"Nakufaa mama niokoe..
Ooh.! Uuh.! Uuh.!" ghafla
ikafuatia mshindo kuashiria kile
kitu kimeanguka chini baada ya
kuachia mshale wangu wenye sumu kali, bila kuwa na woga kwa
kunyemelea nikaanza kufata lile
eneo kumtambua yule mtu, huku
nikikaribia pale nimeshika panga
langu akatokea fisi maeneo ya
karibu nikamfyeka akawa amekufa,nikaendelea na zoezi
langu la kutambua ni kitu gani
kitakuwa mbele yangu, sikuwa na
tochi,ila nilipoukaribia ule mwili
niliupapasa lakini bado
haikusaidia kumjua ni nani lakini ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini
ambao kwa namna moja au
nyingine sikuweza kuutambua
mara moja, kwa ushupavu wa
halmashauri ya kichwa changu
ikanituma nichukuwe panga na ku Nichukuwe panga na kuchana
kipande cha nguo yake,nikafanya
hvyo kisha kile kitambaa
nikakificha katika pindo la nguo
yangu ya ndani halafu safari
ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala
kumuogopa yeyote hatimaye
baada ya kukimbia mda refu
nikahisi kama kitu kigumu
nakanyaga chini,furaha na amani
vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo
katika barabara ya lami,akili ikawa
katika kukisia ni upande gani ndo
utakuwa unaelekea Dar na
upande gani utakuwa unarudi
Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la
kwanza,nikashindwa
kulisimamisha nikaamua kusubiri
gari nyingine,kwani sikuwa hata
na nauli hvyo nikaamua nijifiche
niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo.,
Baada ya kukaa pale takribani
lisaa moja na nusu bila ya kuona
gari lolote hatimaye nikaliona gari
kubwa likiwa linakuja kwa
kujikongoja., "Kama kufa wacha nife tu.,lakini
hili gari siliachi.." nilijisemea
kimoyomoyo huku nikijiweka
tayari kwa kurukia lile gari aina ya
roli,huku mikuki na mishale
pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika
karibu yangu kikawa kosa kubwa
sana kwangu kwani ndani ya mda
mchache nikawa tayari nipo
nyuma ya lile lori lililokuwa
limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao
nikaingia mpaka mule ndani ya
lile lori kwa nyuma ambapo
sikumuona mtu yeyote kisha
nikarudishia mlango na kujilaza
kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda,
"Sijui ndo litaishia morogoro au
ndo la Iringa hili gari?" hayo ni
kati ya maswali yaliyokuwa
yameandama ndani ya kichwa
changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu
kidogo, ghafla gari likasimama
kwa mbali nikahisi sauti ya watu
wanajibizana kwa nje.,
"Hapana mkubwa mzigo wetu
hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa
tutakuwa tumefika maeneo ya
mizani,
"Embu fungua nyuma tuhakikishe
maana tani zimezidi na kama
hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini"
Wakiwa bado wanabishana pale
tayari kwenye gari nikawa
natetemeka mwili mzima huku
nywele zikinisimama na akili
ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao
siwezi kwani ni kweli kulikuwa na
mbao nyingi kiasi kwamba nilipata
kanafasi kadogo sana ka kujificha,
"Mungu saidia.! Mungu saidia.!
Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba
nisiweze kukamatwa kwani nia
yangu nikufika Dar,
Mda si mrefu nikaskia
mungurumo wa gari kuwashwa
kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya
nikajihisi ni mtu tofauti sana
duniani tena aliye na bahati
mbaya kupelekwa gerezani lakini
aliyejawa na bahati nzuri uraiani,
Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza
kushuhudia tena kwa mara
nyingine kuki kuchwa kwani
mwanga ulikuwa umeshatoka
kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo
likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na
makelele ya watu ndio
yalichochea hisia zangu,niliweza
kutoa jicho langu kupenyeza
kwenye kauwazi ka mlango
nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata
wazo la kuangalia kile kipande
cha nguo nilichokikata kule kwa
yule mtu msituni alikuwa ni nani,
Taaratibu mkono wangu ukaanza
kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani
nikakichukuwa kile kitambaa na
kukiangalia.,
"Mamaa..! mamaa..! nimeuwa
tena mungu wangu..!
Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!"
Kumbe kile kilikuwa nikipande
cha nguo cha rafiki yangu
niliotokanaye gerezani 'Pendo'..
wakati nikiendelea kutoa sauti kali
nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia
mlango unafungulia eneo
nililokuwa..,
"Sauti inatokea humu ndani
bwana, tena ni sauti ya kike."
aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya
lile lori nililokuamo ndani.,
"Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema
ameua,embu mkamateni
tumpeleke polisi.."
Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa
natetemeka sana huku nikiishiwa
na pumzi,nahisi mapigo ya moyo
yalizidiwa kasi kwani nilijihisi
napata joto ghafla huku kijasho
chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili
ya maji yakifata mkondo wake,
sikuwa na jinsi tena kwani
niliamini ndoto zangu za kuwa
uraiani zimekwisha na sijui
ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena
gerezani,
Huku kojo likiwa linanimwagika,
ukakamavu na ujasiri wote
ukinitoka nilijikuta natoa tena
sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani
msinikamate.."
Huku nikinyosha mikono yangu
miwili kuelekea ile sehemu
niliyoamini ni mlango,taratibu
nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu.. Itaendelea kesho...
 
Story: Sitaki Tena - 01 (season 1)

Mtunzi: Andy Ryn ( Chief)

Nakumbuka Levina mimi nilikuwa na miaka
12,wazazi wangu walikuwa wakinipenda
sana na walipenda kuniacha huru hata pale
ninapokuwa nacheza na rafiki zangu michezo
mbalimbali,nilikuwa napenda sana kucheza
michezo tofauti na wenzangu c unajua tena utoto,na mchezo mkubwa niliokuwa naupenda ni
huu wa rede (ule wa kukwepa mpira
unaporushiwa).
Siku hiyo nikiwa mimi na rafiki zangu
tunacheza,sikuamini macho yangu na ni vigumu
kuamini mpaka sasa kwa kile nilichotenda kwani badala ya kuuokota mpira nirushe kwa ile
haraka niliyokuwa nayo ndani ya ule mchezo
nilijikuta naokota jiwe bila kujitambua nilichokuwa
nimeokota huku nikidhani kuwa ni mpira na
kumrushia Jeni na kwa bahati mbaya lilimpata Jeni
kichwani na kuzimia palepale.. Juhudi zilifanywa haraka haraka na majirani huku mimi nikiwa
pembeni cijui cha kufanya mchozi ukinitiririka
huku kijasho chembamba kikipenyeza katika
paji la uso wangu kupitia shingoni huku lile jasho
likichochea mkojo ulioanza kunitoka taratibu
palepale huku nikitazama kinachoendelea.. "Panda na wewe twende.. Nimesema panda huko
usikii.?"
Aliongea na mimi mama mmoja kwa ukali huku
akinitolea mijicho kana kwamba labda alikuwa ni
mtoto wake lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa ni
mpita njia aliyekuwa shuhuda wa lile tukio. Nilipanda taksi pamoja na wale majirani iliyokuwa
imekodiwa haraka kwa ajili ya kumkimbiza
Jeni hospitali.. kadri tulivyokuwa tunakaribia
hospitali ndivyo mapigo yangu ya moyo yalinienda
kasi mithili ya yule mwanariadha wa jamaika
anayeitwa 'Bolt'... Huku nikiomba miujiza yeyote itokee ili Jeni apone turudi nyumbani, niliendelea
kulia tena kwa sauti ya juu huku kamasi likinitoka..
Tulipokaribia kufika hospitali nilisikia mama mmoja
aliyekuwa
pembeni yangu akimshikilia Jeni..akitikisa kichwa
huku akimwambia dereva apunguze mwendo kwani haina haja tena kuwahi huku akimsisitizia
kuwa mtu waliyekuwa wakimuwaisha
ameshapoteza maisha..
"Jeni amekufaaa.. Amekufaaa.. Hapana.. hapana..
Mama yangu weeee...mama..baaabaaa uko
wapi jamanii mama yangu weee..." Nikazidisha kupaza sauti kwa kulia niliposikia yale
maneno..
Sikuweza kuamini kama kweli Jeni amekufa mpaka
nilipoona tunaelekea mochwari ndipo nilipoamini
Jeni alikuwa tayari keshapoteza maisha kutokana
na kupoteza damu nyingi zilizokuwa zikimtoka eneo la kichwani na puani.
"Umeshaua..? Ndio umeuwa naongea na wewe
kinyago uliyefanya makusudi haya..!”
Aliongea yule mama..
"Sijau.. Kabla sijamalizia kujibu nikashangaa
napigwa kofi kubwa la usoni mpaka nikajihisi kizunguzungu, huku akiendelea kuniambia..
“tena ishia hapohapo mwanaidhaya mkubwa
wewe na tunakupeleka polisi moja kwa moja
mbwa we ukaozee huko huko ndio utanyoka...!"
Taarifa za mimi kufanya lile tukio tena kwa bahati
mbaya lilitawanyika Mtaani kote na hakuna hata mmoja aliyeweza kuamini kwani taarifa hata
zilipofikiwa wazazi wangu nao hawakuweza
kuamini kilichonitokea walikuja pale kituoni japo
kunitoa kwa dhamana lakini ilishindikana kwani
huwa hakuna dhamana kwa kesi yoyote ya
mauaji.. Nilishiwa nguvu,na kulegea viungo vyote na kusababisha kupoteza fahamu kutokana na
kukataliwa dhamana..
BAADA YA SIKU (NNE).4 Sikuweza kupata hata lepe la usingizi takribani siku
mbili kutokana na kulia sana,kichwa kiliniuma
sana..nakumbuka ilikuwa asubuhi na mapema pale
askari alipotuamrisha tupande gari la polisi kutoka
pale kituo kidogo cha polisi kurasini na kuelekea
kituo kikubwa cha polisi pale MSIMBAZI KARIAKOO.. Safari ilianzia kituo kidogo cha Kurasini
nilipokuwa nimechanganywa na wenzangu
niliowajua pale pale na wao waliletwa pale kwa
makosa tofauti tofauti, huku tukikatiza Sheli ya BP
mpaka raundi about ya Kamata,sehemu zote
tulizopita bado machozi yalikuwa yakinitoka huku yakiandamana na mafua Makali yalionipata pale
kurasini kituoni, kwikwi ilibana sana na haikuwa
kwasababu ya kiu ya maji bali ilikuwa ni kwikwi ya
kulia kwa mda mrefu..
"Embu nyamaza hukoo.. Haupo kwa baba yako
wala mama yako..Tena unyamaze..??” Aliongea kwa hasira askari mmoja alioonesha
kukasirishwa na kitendo changu cha kulia mda
mrefu bila kunyamaza..
"Hivi we mtoto husikii..? Kwani sisi ndo
tumekutumauue..?" aliendelea kunikalipia yule
askari. Mpaka tunaingia pale kituoni MSIMBAZI macho yalikuwa mekundu na yamenivimba sana
huku sauti ikinikauka kutokana na kulia kwa mda
mrefu.. *** *** Tukiwa katika basi lenye namba PT 10319 ambalo
lilikuwa likikatisha mitaa ya kariakoo likiwa
linatokea kituo kikubwa MSIMBAZI huku nikiwa
katika orodha ya mahabusu waliokuwa
wamewekwa pale MSIMBAZI kituoni kuelekea
mahakama kuu pale KISUTU kwa ajili ya kusikilizwa kesi yangu kwa mara ya kwanza. kila moja wetu
akiwa amefungwa pingu mikononi .,
nywele pamoja na nguo zangu zilikuwa chafu sana
kutokana na uchafu wa pale kituo cha Kurasini na
msimbazi. Huku basi la polisi likiwa linakata kona
ya kuingia mahakamani , nikiangaza huku na huku labda naweza kumuona hata mama au baba,ghafla
nikamuona mama
kajifunika kanga upande mmoja wa paji la uso
wake kuashiria kuwa alikuwa ameumia upande
mmoja wa uso wake,nilijikuta nikipigwa na afande.
"Embu tembea hukoo... Unashangaa shangaa nini? Kwani hujui kama hapa ni mahakamani...?"
Tukiwa mstari mmoja tulishuka na kuelekea
kwenye vyumba ila mimi niliingizwa chumba
maalumu kilichoandikwa maneno makubwa
mlango wa kuingilia "CRIMINAL ONLY" kwa haraka
haraka sikuweza kutambua lile neno linamaana gani kwakuwa ndo kwanza nilikuwa niko form
one ila niliweza kuambulia neno moja tu
lililoandikwa "ONLY" kwani nilipenda sana
kuangalia ile
tamthiliya ya kifilipino iliyokuwa inaitwa 'only you'
nikijua inamaanisha 'Wewe Pekee..'sikuwa mbali na fikra zangu kwani kile chumba kilikuwa peke yake
kwa ajili ya kesi za mauaji kama yangu ndo huwa
zinasomwa hapa. Nikiwa na mawakili wangu
nisiowafahamu ila niliamini tu baba ndo aliwatafuta
kwani alikuwa akiongea nao kabla sijaingia mule
ndani. Chumba kilikuwa kidogo sana na watu walimiminika wakiwa ni pamoja na majirani,ndugu
na marafiki huku kesi ikitaka kuanzwa kusomwa
niligeuka nyuma nikajikuta nakutana jicho na
mama mmoja..kwa hasira na jazba niliokuwa nayo
nikajikuta Natoa fyonyo kali na la kupaza sauti ya
juu..Wote mle ndani wakawa kimya ghafla wakinitazama,
"xé@shh.. Mbea mkubwa we..!”
Kisha nikamtemea mate huku hasira zikinipanda
kutokea miguuni kuelekea kichwani na
mikononi, nilijikuta nataka kumpiga lakini mikono
yangu ilikuwa na pingu hivyo hasira ikazidi mara mbili huku nikihema kwa kasi ikiambatana na
makamasi yaliokuwa yakinichilizika mithili ya
umande unapokutana na majimaji au konokona
anapokuwa anaachia kofia yake..nikanyanyua
Mguu wangu wa kulia tayari kwa kumtupia mateke
yule mtu..nikawa tayari nimeshathibitiwa.. hakuwa mwingine bali alikuwa ni yule mama tuliepanda
naye taksi kumuwaisha Jeni hospitali yule
aliyekuwa akinisema ovyo kwenye gari pia ndo
alienipeleka
Kunikabidhi polisi..nikiwa naendelea kumtolea
macho huku nimekunja uso wangu kwa hasira mithili ya bi kidude akiwa jukwaani anaimba..
nilijikuta napokea vibao c kutoka kwa yule
mama bali alikuwa ni askari aliyekuwa akifuatilia
tukio mule ndani.,
"Hata kesi haijaanza umeanza kuonyesha we
nunda eenh... hatimaye hakimu aliingia Na lazima utaozea jela tu wewe.."
Maneno yale yalivuta hisia nyingi sana ndani ya
kichwa changu,mwili ulininyong'onyea
ghafla,niakanza kutetemeka japo nilikuwa mdogo
kiumri lakini nikawa tayari nimeshakomaa kifikra
na pia jasiri ndani ya mda mfupi.. ****** Mda wa hakimu kuingia mule ndani ulifika,hakuwa
mtu wa masihara hata kidogo kwani
aliingia haraka haraka na kuuliza jina langu kamili
kisha akaandika andika pale kwenye kitabu
alichokuja nacho na kisha akaniambia kuwa
inabidi nirudi tena ndani kwani kesi yangu bado ipo kwenye upelelezi hivyo nitarudishwa tena pale
mahakamani baada ya wiki 3 au 4.. Nguvu zilizidi
kunipotea,akili nayo ilishajichokea, Nilitoka pale
kwa ghadhabu huku askari akiwa nyuma yangu..
nilikuwa na hasira na vitu vitatu, kwanza sijapata
fursa ya kuongea na wazazi wangu kwa mda mrefu kwani kwenye kesi kama hizi mtuhumiwa
huwa hana hata ruhusa ya kuongea na mtu
yoyote, pili nilikuwa na hasira ya kuhairishwa kwa
kesi yangu na tatu ni hasira ya yule mama
aliojifanya yupo mstari wa mbele katika kunifuatilia
kujua mwisho wangu.. "Ole wake siku nikitoka..?"
nilijikuta najisemea kimoyomoyo huku dukuduku
likiwa limenijaa moyoni..
"Ipo siku tu.. Atanijua mimi ni nani..?"
nikapanda basi la polisi tayari kwa safari ya
kurudishwa tena rumande.. INAENDELEA
Let me know ukipost next episode. mimi nimeipenda hii Car From Japan Grand Giveaway 2017
 
Ilipoishia..
,
bado haikusaidia kumjua ni nani
lakini ulikuwa ni mwili wa mtu
pale chini ambao kwa namna
moja au nyingine sikuweza
kuutambua mara moja,
kwa ushupavu wa halmashauri ya kichwa changu ikanituma
nichukuwe panga na ku..
-
Endelea.,
-
Nichukuwe panga na kuchana
kipande cha nguo yake,nikafanya
hvyo kisha kile kitambaa
nikakificha katika pindo la nguo
yangu ya ndani halafu safari
ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala
kumuogopa yeyote hatimaye
baada ya kukimbia mda refu
nikahisi kama kitu kigumu
nakanyaga chini,furaha na amani
vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo
katika barabara ya lami,akili ikawa
katika kukisia ni upande gani ndo
utakuwa unaelekea Dar na
upande gani utakuwa unarudi
Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la
kwanza,nikashindwa
kulisimamisha nikaamua kusubiri
gari nyingine,kwani sikuwa hata
na nauli hvyo nikaamua nijifiche
niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo.,
Baada ya kukaa pale takribani
lisaa moja na nusu bila ya kuona
gari lolote hatimaye nikaliona gari
kubwa likiwa linakuja kwa
kujikongoja., "Kama kufa wacha nife tu.,lakini
hili gari siliachi.." nilijisemea
kimoyomoyo huku nikijiweka
tayari kwa kurukia lile gari aina ya
roli,huku mikuki na mishale
pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika
karibu yangu kikawa kosa kubwa
sana kwangu kwani ndani ya mda
mchache nikawa tayari nipo
nyuma ya lile lori lililokuwa
limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao
nikaingia mpaka mule ndani ya
lile lori kwa nyuma ambapo
sikumuona mtu yeyote kisha
nikarudishia mlango na kujilaza
kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda,
"Sijui ndo litaishia morogoro au
ndo la Iringa hili gari?" hayo ni
kati ya maswali yaliyokuwa
yameandama ndani ya kichwa
changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu
kidogo, ghafla gari likasimama
kwa mbali nikahisi sauti ya watu
wanajibizana kwa nje.,
"Hapana mkubwa mzigo wetu
hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa
tutakuwa tumefika maeneo ya
mizani,
"Embu fungua nyuma tuhakikishe
maana tani zimezidi na kama
hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini"
Wakiwa bado wanabishana pale
tayari kwenye gari nikawa
natetemeka mwili mzima huku
nywele zikinisimama na akili
ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao
siwezi kwani ni kweli kulikuwa na
mbao nyingi kiasi kwamba nilipata
kanafasi kadogo sana ka kujificha,
"Mungu saidia.! Mungu saidia.!
Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba
nisiweze kukamatwa kwani nia
yangu nikufika Dar,
Mda si mrefu nikaskia
mungurumo wa gari kuwashwa
kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya
nikajihisi ni mtu tofauti sana
duniani tena aliye na bahati
mbaya kupelekwa gerezani lakini
aliyejawa na bahati nzuri uraiani,
Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza
kushuhudia tena kwa mara
nyingine kuki kuchwa kwani
mwanga ulikuwa umeshatoka
kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo
likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na
makelele ya watu ndio
yalichochea hisia zangu,niliweza
kutoa jicho langu kupenyeza
kwenye kauwazi ka mlango
nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata
wazo la kuangalia kile kipande
cha nguo nilichokikata kule kwa
yule mtu msituni alikuwa ni nani,
Taaratibu mkono wangu ukaanza
kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani
nikakichukuwa kile kitambaa na
kukiangalia.,
"Mamaa..! mamaa..! nimeuwa
tena mungu wangu..!
Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!"
Kumbe kile kilikuwa nikipande
cha nguo cha rafiki yangu
niliotokanaye gerezani 'Pendo'..
wakati nikiendelea kutoa sauti kali
nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia
mlango unafungulia eneo
nililokuwa..,
"Sauti inatokea humu ndani
bwana, tena ni sauti ya kike."
aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya
lile lori nililokuamo ndani.,
"Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema
ameua,embu mkamateni
tumpeleke polisi.."
Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa
natetemeka sana huku nikiishiwa
na pumzi,nahisi mapigo ya moyo
yalizidiwa kasi kwani nilijihisi
napata joto ghafla huku kijasho
chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili
ya maji yakifata mkondo wake,
sikuwa na jinsi tena kwani
niliamini ndoto zangu za kuwa
uraiani zimekwisha na sijui
ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena
gerezani,
Huku kojo likiwa linanimwagika,
ukakamavu na ujasiri wote
ukinitoka nilijikuta natoa tena
sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani
msinikamate.."
Huku nikinyosha mikono yangu
miwili kuelekea ile sehemu
niliyoamini ni mlango,taratibu
nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu tu nikawa
tayari nipo mikononi mwa raia
nisiowafahamu lakini walikuwa ni
wanaume wamevalia sare ambazo
sikuweza kuzitambua mara moja
huku juu wakiwa na mashati meupe na wengine masweta
mekundu kutokana na hali ya
baridi kali lililokuwa limezunguka
maeneo haya,
Ilikuwa ni mchana tulivu kwani jua
lilikuwa si kali sana kutokana na kaubaridi katika huu mji,wale
wenye hasira wakaanza
kunishambulia kwa kunipiga
makofi huku wengine
wakinishambulia kwa matusi
makubwa ya nguoni huku wakiniburuza mithili ya mzoga
aliyeoza anayeenda
kutupwa,nilipiga kelele lakini
haikusaidia nilivutwa sana na wale
vijana..
"Wauaji kama nyinyi ndo tunaowatafuta" aliongea mmoja
wa wale watu huku wakiwa
wamenichania vipande vya nguo
yangu, nilikuwa sina tena ujanja
na pia kulikuwa hakuna tena
muujiza utakaotendeka kwangu ili niweze kujikomboa katika mikono
ya wale watu nisiowafahamu
walioonekana makatili wasio na
huruma hata kidogo.,
Waliniburuta kwa mwendo mrefu
sana,huku umati wa watu ukifurika kunishuhudia,
walipokezana kunishika na
kunivuta,huku nikiwa bado nalia
na kung'ang'ania nisiweze
kupelekwa kituoni,
Nikiwa naendelea kulia huku nguvu zikiniishia na kuacha
wafanye wanachokitaka,nikahisi
pumzi zimeniisha kwani kwa sasa
nilikuwa nahema juu juu huku
damu zikinimwagika pembezoni
mwa mdomo wangu, maji machafu pamoja na matope
vilitawala mwilini mwangu huku
sura ikiwa imenivimba sana,
niliamini hata nikiendelea kulia
haitasaidia chochote,na pale
malengo yangu yalikuwa yamefikia tamati kwani nilikuwa
nikipelekwa polisi,
Tukiwa njiani mwa safari huku
kipigo kikinizidia katika mwili
wangu huku macho yangu
yakiangaza huku na kule kupata japo msaada wowote ndipo
yakakutana uso kwa uso na kibao
kilichoandikwa,
'TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL'
Halmashauri ya kichwa changu
ikafanya kazi fasta hapo hapo nakugundua kuwa wale si raia
wakawaida kama nilivyodhani bali
walikuwa ni wanafunzi katika kile
kijiji tena katika shule anayosoma
Gervas japokuwa sikumuona
katika wale watu waliokuwa wakinipiga lakini niliamini lazima
alikuwa akisoma katika shule ile
kama alivyonielezea hapo awali
kwamba anasoma shule ya
wavulana tupu iliopo Iringa na
inaitwa 'Tosamaganga' hayo yote aliniambia kipindi kile nipo
gerezani,
"kabla hamjanifikisha huko
kituoni naomba mniitie Gervas
Phota nimuage"
Niliposema hivyo tu wale jamaa waliokuwa wamenishikilia
wakaniacha ghafla kwa mshangao
huku wengine wakiamini huenda
nilikuwa nimejifanyisha nimeua ili
niweze kuonana na Gervas na
wengine wakijiuliza nimemjuaje Gervas? Wakanikazia macho,
"Gervas.? Mbona sisi hatumjui"
Walinijibu huku wengine
wakinicheka na kunisonya kwa
dharau,
"We dada una mashetani au kichaa enhh.. Unamuitaji nani?"
jibu alilonipa mmoja wa wale
watu lilinifanya niingiwe na woga
huku meno yakiumana nakuhisi
labda Gervas alinidanganya
anasoma shule hii lakini haiwezekani.,
Hasira zilizidi kunipanda kwani
kipigo kiliongezeka mara mbili ya
pale huku damu nyingi
zikiendelea kunimwagika, ghafla
nikasikia kama mlio wakengele ukipigwa pembeni ya shule huku
watu waliokuwa wamevalia kofia
wakiwa wako na virungu
mikononi wakinifuata pale
nilipokuwa nimeburuzwa na wale
wanafunzi,hofu ilizidi kutanda kwenye ubongo wangu,mwili
ulininyong'onyea kuona wale
watu wamevalia sare kama polisi,
kila walipokaribia lile eneo ndipo
nilitamani nife hapohapo,nikiwa
nagala gala pale chini huku wale wanafunzi wakianza kutawanyika
kwa kuwaogopa wale watu huku
wakiniacha peke yangu nilianza
kujisogeza kwa mwendo wa
taratibu huku nikitumia magoti na
makalio yangu kujisogeza mpaka nikaona chupa ya soda,nikaivunja
ili niweze kujiua kabla ya wale
askari hawajanifikia, nikiwa nataka
kuanza zoezi la kujiua mara yule
askari akawa ameshanikaribia na
kunipokonya ile chupa., "niache nife..,niacheni jamani..!
Nikiwa nimeshakata tamaa tena
ya kuishi,kwa haraka nikaweza
kuyakodoa macho yangu na
kumuangalia mtu aliyenipora ile
chupa niliyokuwa nimeivunja vunja na kuacha ncha kali
nikitaka kujiua,nikaangalia mara
mbili mbili nikagundua kuwa yule
hakuwa askari polisi kama
nilivyodhani bali alikuwa ni mmoja
kati ya wale walinzi wa ile shule waliokuja kutawanya na
kuwakamata wanafunzi sugu
waliokuwa nje ya shule mda wa
masomo,
"Pole sana binti angalia sana siku
nyingine watakuja kukubaka wale wanafunzi wavuta bangi wale...!"
nilishangaa sana yule mlinzi
kunipora kisha akaniacha na
kuendelea kuwafukuza wanafunzi
wengine,nilijawa na nguvu na
furaha ya ajabu nakujiona ni mtu wa bahati tena ya mtende, watu
wengi walinishangaa sana hilo
sikujali kwani maisha ya kupigwa
kama yale nilishayazoea tangu
kipindi kile nipo Gerezani.
Huku nikiwa nimelowa damu na kuchanika karibu nguo yote
nliokuwa nimeivaa, nliweza
kujikokota chini chini mpaka eneo
la nyuma na ile shule kisha
nikaegemea chini ya mti mkubwa,
kwa uchovu na maumivu niliyoyapata yalinifanya nianze
kunyemelewa na kausingizi
japokuwa kulikuwa na baridi kali
sikuwa na jinsi yoyote
yakukabiliana nalo,
"Twende bwana au unapenda kubaki hapa porini..? Mi
nakuacha...Hapana.,
Pendo usiniache..! Pendo
usiniache...! Usiniache..!
Usiniache...! Usiniache..!
Peeeendooooooooo.......!" Ghafla nikashtuka nakuanza
kuhema kwa kasi huku
nikitetemeka Levina mimi kumbe
ilikuwa ni ndoto tena nilikuwa
nikiota nipo na marehem pendo
kule msituni,usingizi ukanikata nakuanza kuangaza kila upande
nakuona giza limeanza kutanda
lakini upande wa mbele yangu
kulikuwa na taa kali zilizomulika
ile shule, nikaanza kusogelea
taratibu kwa kuzunguka yale majengo yaliokuwa yamewekewa
uzio huku nikitafuta lango la
kuingilia, hatimaye nikagundua
geti lilipo,walinzi takriban watatu
walikuwa wametanda pale lango
la kuingilia hivyo nikatafuta eneo la choo kwani niliamini kukijua
choo itakuwa ni njia nyepesi ya
kuingia ndani ya ile shule, haraka
haraka macho yangu yakaweza
kuona wanafunzi wakiongozana
wakiingia kwenye jengo lingine lililoonekana si kubwa sana kama
majengo mengine huku wakiingia
na kutoka, haraka haraka kwa
ujasiri na kwa shauku niliokuwa
nayo ya kutaka kupambana
mpaka nimuone Gervas nikawa na nguvu ya ajabu yakuweza
kuruka ukuta japokuwa haukuwa
mrefu sana ndani ya dakika
chache nilikuwa tayari nipo
kwenye kale kajengo kalichokuwa
na vyoo vingi vyote vikiwa na milango nikaingia choo
kimojawapo na kujifungia huku
nikishuhudia hamna mtu ndani,
harufu kali ya kinyesi na mikojo
katika vile vyoo nilipokuwamo
ndani havikunizuia hata kidogo kuondoka mule ndani,niliweza
kutulia kimya huku nikiombea aje
kati ya Gervas au mwanafunzi
yeyote nimuulizie Gervas, mpaka
nikajishangaa kwa jinsi nilivyokuwa
sina woga wowote, Ghafla nikasikia sauti ya kama
mtu anakuja,nikazidi kukaa kimya
ndani ya choo huku nikijiuliza
ntaanzaje mara ile sauti ya mtu
akiingia na kuanza kukojoa
mlango wa pembeni yangu, nikafungua mlango wangu
taratibu na kuanza kunyata
kuelekea mlango aliokuwepo
huku akili ikinituma nimuwahi na
kumnyamazisha kabla hajashtuka
na kuanza kupiga kelele, " Shhh..usiniogope wala
usikimbie..Naitwa Levina
natokea..."
Kabla sijamaliza kujitambulisha
yule mwanafunzi akawa
ameshanitambua.. " We si yule dada ambaye
nimetoka kuskia stori yako sa hivi
kwa wenzangu kuwa umepigwa
na kukuburuzwa mchana kutwa
pale nje na umeokolewa na
walinzi..?" "Ndio mimi ila nipo hapa kwa
msaada mmoja tu, unamfahamu
Gervas Phota..?"
"Namfahamu na ninasoma naye
lakini yupo Chumbani anaumwa
leo siku ya pili yupo kitandani.." "Tafadhali nisaidie kwa hili nenda
kaniitie mwambie Levina, nipo
hapa hapa chooni kwenye
mlango huu nawasubiria
mtanikuta.."
Ndani ya mda mfupi nikawa tayari nimeshayazoea mazingira ya kile
choo ikiwa ni pamoja na harufu
kali ya mule ndani, niliweza
kujifungia mlango mmojawapo
kwa mda mrefu tangu nimefika
bila ya hata mtu yoyote kujua, mara nikasikia sauti ya watu
wanaongea kwa nje huku sauti
kama niliyokuwa naifahamu
nilianza kuingiwa na furaha na
amani isiyokuwa na kifani kwani
niliamini Gervas ndiye mkombozi wangu na anayepajua mpaka
nyumbani kwetu kwani nilikuwa
nimeshapasahau hadi jina la
mtaa,sikutaka kujitokeza hvyo
nikavuta subira huku nikiisikia ile
sauti kwa umakini taaratibu nikaweza kuitambua kuwa
haikuwa sauti ninayoifahamu hata
kidogo na hata maongezi
waliokuwa wanaongelea
hayakuwa yakiunafunzi hivyo
halmashauri ya kichwa changu ikapambanua fasta na kujua kuwa
wale watakuwa ni walinzi kwani
walikuwa wanaongelea mambo ya
kifamilia na kikazi tena kazi ya
ulinzi, moyo ulianza kuniripuka
kwani walikaa mda mrefu huku wakipiga story na hata wanafunzi
walipokuja nilisikia wakiwaamkia
na kujisaidia na kuondoka
zao,kwa ujumla nililegea sana na
akili ilishaanza kuchoka,nikiwa
bado nipo nao wale walinzi chooni huku wakinogewa na stori
ila mlango nilikuwa nao tofauti
bila ya wao kujua ghafla nikasikia
sauti kali iliyotokea upande wa nje
huku ikilitaja jina langu.,
"LEVINAAAA...! LEVINAAA...! LEVINAAA...!
" YUPO MLANGU UPI
UMESEMA..?"
Nilitamani niweze kutoka lakini
haikuwezekana kutokana na wale
walinzi kukaa mda mrefu wakipiga stori, hakika ile sauti
ilikuwa ni ya Gervas akiongea na
mwenzake huku nikihisi
ameshakaribia kuingia mule
chooni,ghafla nikasikia ukimya
umetanda halafu yakafuatia maswali kutoka kwa wale walinzi
wakimuuliza Gervas,
"Levina..! Levina ndo nani? Na
mbona mwenzako amenyoosha
kidole mlango huo ambao
umefungwa..? Kuna nani...?"
-
************************* *** Je? Ndoto za Levina kumpata
Gervas zitatimia? *** Itakuwaje akikamatwa wakati
ile ni shule ya Wavulana tupu?
Inaendelea
 
Ilipoishia..

"Ni..mi..mi.. Ndo
nimemu..uaaaaaaa Peeeeeendo...
-
Endelea...
Nilijikuta nimeropoka kila kitu
huku kwa ghafla yule mzee
akamuwahi kumshika mke wake
kisha akanigeukia na kuniuliza
tena.,
"Binti ulikuwa unasema?... Samahani sana sijakusikia vizuri
nilikuwa namuwekea karibu na
mdomo mama yako mfuko aweze
kutapika..."
Aliongea yule mzee bila ya
kuonyesha wasi wasi wowote kama kuna neno baya ambalo
Levina mimi nimeropoka,
"Nilitaka kukupa mfuko huu hapa
mkubwa nimeona huo mdogo
hautatosha kwa maana mama
anatapika sana.." Nilimjibu kwa kuzuga huku
macho nimeyaelekezea chini kwa
aibu kubwa niliokuwa nayo pale,
nikajifanya kihere here kwa
kumpa maji yakunywa yule mama
aliyekuwa anatapika ambaye ni mama yake na Pendo,
Mzee alinishukuru sana kwa
wema wangu japokuwa ukweli
nilibaki nao moyoni,
"Umesema binti unaelekea wapi?"
Aliniuliza yule mzee na kwa mda ule tulikuwa tukiendelea kupiga
story za kawaida kuhusiana na
maisha njia nzima japo ukweli
kuhusu pendo nilikuwa nao
moyoni.,
"Naelekea Dar es salaam kutafuta kazi"
"Kazi gani binti yangu?"
"Naenda kutafuta kazi za ndani"
Nilimdanganya sana kuhusu
maisha yangu kwa ujumla na
aliweza kuniamini kwa asilimia kubwa kuwa natokea Iringa
naelekea Dar kutafuta kazi za
ndani,
Ile roho ya kikatili,ilikuwa
imeshaanza kunikabili kwani
sikuwa hata na huruma ya aina yoyote..huku tukiwa tumeshasafiri
mwendo wa kama masaa manne
hivyo nikamwambia mzee kwakua
gari ilikuwa inapitia Morogoro
halafu ndo inaenda Dodoma
ilinibidi nimwambie mzee kuwa tukifika morogoro anishtue kwa
sababu nimeshapasahau
sitapakumbuka vizuri..
* * * * Ndani ya masaa kama sita huku
kausingizi kakinipitia mzee
alinishtua na kuniambia kuwa
tulikuwa tayari tupo maeneo ya
mzumbe tukikaribia kuingia
morogoro,hivyo niwe tayari nisilale tena, nilianza kujawa na
furaha isiyotabirika huku furaha
yangu zaidi nikiielekeza katika
mifuko ya ile traki suti niliyokuwa
nimeivaa na kuchomoa zile
karatasi za ramani kisha nikazing'ang'ania mikononi
mwangu nikisubiri niingie
Morogoro.. *** Hatimaye tukaingia ndani ya
mkoa wa Morogoro,kisha
nikamuaga mzee pale lakini
nilishindwa kumuaga mama
kwakua tayari alikuwa
ameshapitiwa na usingizi., "Usijali binti utafanikiwa nakutakia
maisha mema na ubarikiwe upate
kazi na uishi kwa amani huko
uendako.."
Yale maneno hayakuniingia akilini
hata kidogo kwani hayakuwa na ukweli wa aina yoyote pale ila
nikaamua nimuitikie tu kwa
kumridhisha yule mzee.,
"Ahsante sana mzee na poleni
sana kwa msiba uliowakuta"
Nilimwambia huku nikionesha tabasamu la huruma la uongo,
nikampa mkono kisha nikamuaga
kuelekea stendi ya upande wa pili
huku yule mzee akiamini kabisa
kuwa nlikuwa naelekea dar
kumbe naweka kwanza kituo.. *** Mda ulikuwa umeshatimia kama
saa nane mchana huku kukiwa na
hali ya uvugu vugu iliyojawa na
baridi lakini siyo kali sana kama la
Iringa kwani manyunyu yalikuwa
yakidondoka taaratibu kuashiria mvua inataka kunyesha,huku
nikiwa nimejikunyata mikono
yangu niking'ang'ania zile ramani
ndani ya mifuko ya
suruali,niliweza kutoa na
kufungua mojawapo ya ramani iliyokuwa inaelekeza kwa 'Baba
Ali' huku nikiiongoza
inavyoelekeza..
"Sasa, hapa ndo nimeambiwa
panaitwa 'Boma Road' na ramani
inaelekeza kota hizi hizi... embu ngoja nimuulizie huyu mtu.."
"Samahani kaka..Sijui
unamfahamu 'Baba Ali'..?"
Nilimuuliza mpita njia niliyeamini
kuwa atanisaidia kumpata mtu
ninayemhtaji., "Baba Ali..Baba Ali.. Yeeah,
nimemkumbuka anaishi maeneo
ya paleee juu tena mnene hivii
alikuwa anaishi na mke wake na
watoto lakini sasa hivi anaishi
peke yake?.." "Ndo huyo huyo..",nilimuitikia tu
huku nikiamini atakuwa ndo huyo
huyo kutokana na maelezo
aliyonipa Gervas.,
"Nyosha na hii barabara ukifika
pale njia panda anza kuhesabu nyumba ya kwanza mpaka ya tatu
ndo hapo hapo"
"Ok., asante sana.."
Furaha ilinizidia zaidi ya pale
nilipokua naelekezwa sikutaka
hata kugeuka nyuma akili yangu ikaelekea mpaka kwenye njia
panda na nilipofika kwenye lile
eneo nikaanza kuhesabu nyumba
ya kwanza mpaka ya tatu,
nikaingia ilikuwa ni nyumba
kubwa iliyojaa wapangaji mbalimbali nilipofika
nikapokelewa na majirani na
kuwaulizia 'Baba Ali' kisha
wakaninyoshea chumba
anachoishi na kuanza kugonga
hodi., "Karibu karibu.."
ilisikika sauti yakiume niliyoamini
ndo mwenyewe 'Baba Ali..'
"Wewe ndo baba Ali?"
"Ndo mimi karibu binti"
Niliingia ndani kwake japo alikuwa na chumba na sebule,ni kweli
sikuona dalili yoyote ya mke wala
watoto ,niliweza kumwelezea
matatizo yangu yote kisa cha mimi
kupelekwa gerezani na wema
wote alionitendea mdogo wake ambaye ni Gervas,misukosuko
yote hadi nilivyokwenda kwa
Gervas akanipa ramani mpaka
nimefika hapa, aliitikia kuwa
ilikuwa ni kweli alikuwa
akimfahamu Gervas kama ndugu na alikuwa akiishi na mkewe na
watoto lakini wameshaachana na
kuhusu kuelekea nyumbani kwetu
nisijali kesho yake atanipeleka
mpaka mlangoni kwetu, hivyo
akanizidishia furaha na msisimko ndani ya mwili wangu zile ramani
zikawa hazina tena maana
kwangu nikampa akazichukuwa
na kuzichanachana kisha akaenda
kuzitupa nje.
Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku hivyo akaniandalia maji ya
kuoga nikaenda kuoga niliporudi
nikakuta kashanunua chakula
(chipsi mayai) hivyo tukakaa
mezani na kula,baada ya hapo
akanielekeza chumba nitakacholala kisha taa zikazimwa
nikamwacha akijilaza kwenye
kochi pale sebuleni..
Ikiwa ni usiku wa manane huku
nikiwa nimejifunika shuka sio zito
sana huku nikiwa nimejikunja kwa kaubaridi kalichokuwa
kakininyemelea nilianza kuhisi
kama kuna mtu anahema
mgongoni mwangu tena kwa
pumzi ya hali ya juu,nilipaamini
sana pale na pia nilivyomuheshimu 'Baba Ali'
sikufikiria hata kidogo kama
anaweza kunifanya chochote,
kadri mda ulivyokuwa unaenda
ndivyo nilihisi kama mikono
inapenya katika makwapa yangu kisha inashika na kutekenya matiti
yangu huku ikiteleza kwa
kunipapasa pasasa ikihamia
taratibu katika sehemu zangu za
siri na kuanza kuzitekenya,
nilishtuka lakini kwa ujasiri niliokuwa nao sikutaka kupiga
kelele kwanza mpaka nimjue ni
nani anayenifanyia vile, sasa
nikawa napapaswa maeneo ya
mapajani kwangu huku yule mtu
akigeukia upande wa mbele yangu..
"Kohh..! kohh..! kohh..!"
Nikakohoa kwa nguvu japo yule
mtu ashtuke lakini hakutaka
kuniachia,
"Wewe nani? Naomba uniache..!" Niliamua kutoa sauti ya juu
kidogo huku nikiwa na hasira kali
na mishipa iliyonitanda
usoni,lakini haikusaidia kwani
kilichofuata nilihisi kama panga au
kisu kikiumana na sakafu kisha haraka taa ikawashwa..
"Heee Baba Ali..?"
Sikutaka kuamini hata kidogo
kwani ni kweli alikuwa 'Baba Ali'
juu ya kifua changu,
aliyejitambulisha na kunipa hifadhi hapa kwake ndo alikuwa akitaka
kunibaka..
"Shhh.. Nani Baba Ali..?
Tena ukome siku nyingine kuniita
hivyo,Gervas mie simjui na huyo
'Baba Ali' unayedhania ni mimi siyo na huko kwenu sikujui
malaya mkubwa we..!"
Yale maneno yalinichoma sana
sikuwa na jinsi kwakuwa alinishikia
panga na kunilazimisha kufanya
atakavyo hivyo akaniingilia kinyume na maumbile usiku
kuchwa huku akinisababishia
maumivu makali na damu nyingi
kunitoka mwilini mwangu.. Sikuweza kupata usingizi hata
baada
ya kunifanya atakavyo na
kuniacha
pale usiku ule
Kitandani nikiwa sijiwezi, nilimshuhudia
akichukuwa suruali yake na kutoa
noti
ya shilingi elfu moja na kunipatia..
"We malaya, chukuwa hii
itakusaidia japo ukapate chai"
Nilijikuta napandwa na hasira
kali,huku
nikihema haraka haraka pale bila
hata
kuongea chochote nikachukua ti sheti yangu na ile traki suti
nyeupe aliyoniachia Gervas kisha
nikamgeukia
na kumwambia..
"Ahsante sana kwa wema wako
ulionitendea" Kisha nikatoka nje,kupitia kwenye
kakorido ambapo pembeni
kulikuwa na beseni la vyombo
vichafu vya
majirani kwa bahati nzuri nikaona
kisu katika vile vyombo hivyo
halmashauri
ya kichwa changu ikafanya kazi
fasta,
nikakichukuwa na kurudi ndani
kwa kasi ya ajabu na kumkuta 'Baba
Ali' akiwa kainama chini uku
akifunga
kamba za viatu,nikamuwahi kabla
hajageuka na kuinuka na
kumchoma kisu cha mgongoni kisha
nikakichomoa haraka na
kumuwahi
tena kabla hajapiga kelele na
kumchoma tena maeneo ya
shingoni kisha nikachukuwa kitambaa na
kumjaza mdomoni ,hivyo
nikamshuhudia 'Baba Ali' akigala
gala
pale chini huku akitoa macho na
mishipa ya shingoni ikimlegea. Zoezi lililofuata ni kuingia mpaka
chumbani kwake na kutafuta hela
zilipo, nilitumia kama dakika tano
bila
ya mafanikio huku nikishuhudia
kuona madawa ya kulevya pamoja na
vitambulisho mbalimbali vya watu
tofauti feki hivyo nikagundua
kuwa
'Baba Ali' alikuwa ni jambazi tena
sugu lililoshindikana tena lilikuwa
likitafutwa, baada ya kutafuta
hela bila
ya mafanikio hatimaye nikazipata
pesa
nyingi sana kwenye kisanduku alichokuwa amekificha chini ya
kitanda, lakini mimi nilikuwa
nahtaji kama shilingi elfu hamsini
tu hivyo
nikazichomoa,
"Liwalo na liwe..!" Nilijihisi kama yule stelingi wa
muvi za
kichina 'Jet Li', kwakuwa ilikuwa
usiku
sana kama mida ya saa
kumi,niliweza kutoka pale bila hata ya kuonana na
majirani wowote haraka haraka
nikafuata ile njia niliokuja nayo na
kuondoka kuelekea msamvu
ambapo
ndipo ilipo stendi ya mabasi ya mikoani.,
**** Nikiwa tayari nimeshakata tiketi
katika
basi la Abood, safari ya kutoka
Morogoro kuelekea Dar ilianza
na
nilikuwapo ndani ya basi la kwanza
kabisa lililotoka sa kumi na moja
na
nusu, na tangu nilipoingia katika
basi sikuwa na wasiwasi wowote
kwani moyo wa kishujaa na kijasiri
ulikuwa
umenitawala, lakini sasa takribani
nusu
ya watu kwenye lile basi walikuwa
wakinishangaa huku wakiangaliana na
kutikisa vichwa vyao, nilishindwa
kujizuia nikajiangalia juu mpaka
chini..
"Mmmh...! mmmh...!"
Safari hii niliweza kuwah kujiziba mdomo ili nisiropoke jambo lolote
baya
kwani traki suti yangu yote ilikuwa
imejaa damu huku na mikono
yangu ikitapakaa damu mpaka
sehemu za usoni kitendo kilichofanya njia
nzima
abiria wanishangae kwa kuwa
vile..
Tukiwa tunakaribia kuingia
chalinze, basi letu likasimamishwa na trafiki
wawili mmojawapo akiwa ni askari
polisi,kwa mara nyingine moyo
ukawa
kama unawaka,nywele
zilinisisimka huku mdomo ukinitetemeka kisha
nikalitega sikio langu kwa upande
wa
nje kusikia maneno ya kondakta
wa
basi letu akiwa na trafiki., "Umesema mmepakiza abiria
wangapi?"
"Sitini na mbili tu"
"Hakuna waliosimama?"
"Hakuna"
"Usiniambie hakuna wacha nipande
niingie nijionee mwenyewe ndo
uniambie hakuna sawa?"
Maneno hayo yalinifanya nizidi
kulegea
kwani aliyekuwa anaongea na kondakta alikuwa hajavalia mavasi
meupe bali alivalia mavazi ya kaki
yale
yenyewe ya polisi huku akiwa
kashikilia bunduki akapanda
ndani ya basi huku akiangaza siti moja
baada ya
nyingine na alipofika kwangu..
"We vipi tena Mmepata ajali
wapi?"
"Hatujapata ajali yoyote huyo kapanda
basi hivyo hivyo..!"
Aliropoka dereva wa basi huku
akisaidiana na kondakta
wake kunimaliza..
"Haya shuka., shuka upesi chini.,we
dereva endeleeni na safari yenu"
Nilijikuta nipo mikononi mwa yule
polisi haraka akiniwahi kwa
kunifunga pingu baada
kushushwa chini na kuacha basi likiendelea na safari..
"Mungu wangu...! Mungu
wangu...!
mbona umeniacha..? Mbona
wanitenda
hivi....!" Nilijikuta nikiandamwa na mikosi
na kumshushia lawama Mwenyezi
Mungu
alieniumba na kujiona sifai kuishi
katika dunia hii, huku nikiwa chini
ya ulinzi pale barabarani,Yule askari
polisi
akaniangalia juu mpaka chini
akawa
anatingisha kichwa huku akicheka
kuashiria kama mtu anayenifahamu
sana..
"Levina..?"
Sikuamini amini kama jina hilo
atakuwa
amelitaja yule askari au ameambiwa na
mtu kuwa naitwa Levina,nilihisi
kama moyo ukinipasuka
ghafla,hivyo nikawa
sina tena jinsi kwani nikawa
nimeshapatikana, lakini swali lililoniumiza kichwa ni kwamba
nipo
pale kwa kosa lipi la mauaji?
"maskini isikute baba yake 'Pendo
ndo kamtuma huyu
polisi..? ....Au., nilivyomuua 'Baba Ali taarifa
zimemfikia
huyu polisi..?"
Nikiwa bado najiuma uma pale
huku
akili ikiwa haifanyi kazi kabisa,ghafla
nikamuona yule polisi kabadilika
zaidi ya pale kwani sura yake
ilikunjamana
ghafla huku akinifokea..
"Kwanini umeua Tena..?" Lile swali lilinifanya nilegee na
kudondoka mpaka chini kwani
nilikuwa sina nguvu tena ya
kusimama huku nikishindwa kujua
kipi cha
kufanya pale chini... "Au unapenda kwenda tena
gerezani.,
naona safari yako nyingine sasa
imefika..?"
"Hapana nisamehe afande
sijakusudia nii...l..ii...piii...ti...wa...,tu..na
shetani..?"
Kabla sijamalizia kujitetea
nilishangaa
kuinuliwa kwa kushikwa shati kwa
nguvu kisha kilichofuata ni kupigwa
vibao na mitama huku
nikishindwa
hata kujizuia kutokana na zile
pingu nilizokuwa nimefungwa
mikononi., "Kaka mkubwa, wacha nimpeleke
kituoni Dar huyu mpumbavu ana
kesi
kubwa na nitampigia simu afande
Geofrey aje msaidiane hapa.."
Nilijihisi kama mtu asiye na bahati hapa duniani,maumivu
aliyonisababishia
'Baba Ali wakati akiniingilia
kinyume na
maumbile ukiongezea maumivu
aliyonisababishia huyu polisi vilinifanya
niumie sana moyoni,huku mwili
wangu
ukiwa hautamaniki kwa
majeraha..
******* * *
Levina amekamatwa kwa
mauaji
yapi, ya 'Pendo' au 'Baba Ali..? Inaendelea...
 
Back
Top Bottom