Ilipoishia...
....Eeeh Mwenyezi mungu why
me..? Why me...? why me..?"
Nilianza kutoa machozi huku
nikimshuhudia Mama Gervas
akiondoka kwa kunizomea..
-
Endelea...
Nikaanza kutetemeka nisijue
nitaambiwa nini
pale,wakatizamana kisha
nikawaona wakiongea kwa sauti
ya chini chini huku wakitingisha
vichwa vyao. "...Ok., You can go...!"
Sikuamini yale maneno
nilioambiwa kwani niliambulia
neno 'go' tu kisha wakanikabidhi
ule ufunguo wangu,nadhani
hawakuwa wanaelewa maana ya yale maandishi,
Nikatoka pale spidi huku
nikimfuatilia Mama Gervas kujua
kakatizia wapi, Mara nikamwona
akiwa na Wasaidizi wakimbebea
mizigo yake huku wakiingia jumba kubwa lilioandikwa mbele kwa
maandishi makubwa,
'VAN LANTEER HOTEL' sikutaka
hata kujua maana kwani neno
'hotel' lilitosha kwangu kujua pale
ni wapi, Taaratibu nikajongea mpaka mapokezi na kuonesha
tiketi yangu ya ndege na Pasipoti
kisha yule muhudumu akawaita
wenzake wakachukuwa kibegi
changu na kuniongoza mpaka
chumbani. ".....Umenusurika we mbwaa
eenh..? Na unabahati mi nilitaka
urudishe Tanzania kabisa kuliko
kufuatana na wewe Malaya
mchafu...!"
".....Mama elewa kuwa nami ni binadamu na nina haki zote...!"
"....Haki....? Unahaki gani wewe
zaidi ya kufanya umalaya wako
uende ukamuambukize
mwanangu magonjwa yako ya
ajabu ajabu...?" Alinipokea kwa matusi mpaka
kufanya wale wahudumu wa pale
hotelini wamshangae kwa
maneno yake japo
hawakumuelewa lugha
anayozungumza. Kilikuwa ni chumba kikubwa cha
vitanda viwili ndani yake kukiwa
na kila kitu,
Sikuwa mtu wa amani mda wote
wa usiku niliolala pale hotelini na
Mama Gervas, alizidi kuwa mkali kama mbogo mpaka nikatamani
asubuhi ifike haraka tuendelee na
safari yetu.
".....Zima hiyo taa nimesema....?
Mda wote umekaa na hilo li Biblia
lako unajifanya eti umeokoka....! Wakuokoka utakuwa malaya
wewe eenh...?"
Nilizima ile taa kuepusha
lawama,ikanibidi nipige magoti na
kuanza kusali kwa sauti ya chini
chini, ".....Eee Mungu Baba ahsante kwa
wema wako wote ulionitendea,
Baba nakuja mbele yako
nikitanguliza maombi yangu
kwako.., Weza kuniokoa na
kuniepusha kwa mabaya yote yanayo...."
Nikiwa naendelea kuomba pale
chini nikamshuhudia Mama
gervas akiamka na kuwasha taa.
"....Hivi we mpumbavu...? We ndo
wakuninyima usingizi kwa mikelele yako....? Eeennh....?"
Nilimshuhudia akiwa amefura
hasira huku mishipa ya usoni
ikimsimama,kisha akanivua ile
nguo niliyokuwa nimeivaa (night
dress) nikabaki utupu kama nilivyozaliwa, Mama Gervas
alikuwa kabadilika sasa kwani
aliniburuta usiku ule mpaka
bafuni na kunilaza kwenye 'karo'
la kuogea kisha akafungulia maji
akatoka zake nje,akiwa anatoka tu nilimsemesha,
".....Nimekufanya nini Mama
Gervas....! ...Nisamehe kama
nimetenda kosa kwako..!"
Akiwa kaniacha bafuni pale
kwenye 'karo' la kuogea Mara akarudi na kijikaratasi kisha
akafungua na kutoa vitu kama
unga unga.,Nilikuwa naskia kwa
watu tu lakini sikuwahi kuwekewa,
ulikuwa ni 'upupu' ule
unaowasha mwili mzima na sasa ulikuwa umechanganyika na maji
niliyokuwemo ndani yake.
"....Mamaaa ....Maaamaa Gervas
nawashwa....! nawashwaaa....!
nawashwaa Mamaaa....!"
".....Na hapa bado nilishakwambia Malaya kama wewe huwezi
ukawa na mwanangu, na hiyo ni
trela tu bado picha lenyewe...."
Niliwashwa sana huku nikipiga
makelele yasiyo na faida kwani
kile chumba kilikuwa hakitoi makelele ya aina yoyote, Nililia
sana kwa kuwashwa mpaka
nikajihisi mimba yangu inataka
kutoka,
"....Haya chukua uendelee kusali
sasa mie naenda kulala....!" Alirudi Mara ya pili mule bafuni
na safari hii alirudi na Biblia yangu
kisha akaitupia kwenye 'karo'
niliokuwamo,Nguvu zilikuwa
zimeniisha,niliwashwa mpaka
mwili ukavimba na kujiona umezoea ule muwasho, huku
nikiliegemea lile 'karo' na
kuitazama Biblia yangu ambayo
tayari ilikuwa imelowa sana na
yale maji.
Ilipofika asubuhi na mapema nikiwa nimepitiwa na usingizi
kwenye yale maji niliweza kutoka
pale kwenye karo la kuogea
mpaka chumbani huku
nikimshuhudia Mama Gervas
akiwa anajiandaa haraka haraka, "....Fanya haraka uko nakuacha
mie...!"
Sikumjibu chochote zaidi ya
kufungua kibegi changu na
kuchukuwa 'tenite' langu na
kuvaa,kisha nikarudi bafuni kuchukuwa Biblia yangu kwenye
'karo' huku ikiwa imelowa chapa
chapa,nikaichukuwa na kuipakia
kwenye kibegi changu hivyo hivyo. * * * * Safari ya kwenda uwanja wa
ndege ilikuwa
imetimia,Wahudumu ndo
walikuwa watu wakwanza
kutugongea wakitaka mizigo yetu,
walituchukuwa mpaka uwanja wa ndege lakini mda wote nilikuwa
kimya sikutaka kumsemesha
Mama Gervas lolote kwani
nilikuwa na hasira naye sana kwa
kitendo alichonifanyia jana usiku.
Ndege ya shirika lile lile la 'Emirates' ndio ilikuwa
ikitusubiria,kila mtu alikuwa
kwenye siti yake tayari kwa safari
ya kutoka pale uholanzi na
kuelekea Marekani tukipitia kusini
mwa Canada. Safari hii nilishangaa sana kwani
tulichukuwa mda mchache kama
masaa matano au sita kuingia mji
wa Maryland.,
Watu walikuwa ni wengi
wakiwasubiria ndugu na marafiki zao,
"....Umemuona Gervas yulee....!"
Alijiongelesha Mama Gervas kwa
kujifanya amesahau vitendo
anavyonifanyia,sikumjibu
chochote zaidi ya kukaa kimya nikimuangalia huyo Gervas kwa
mbali akitufata eneo tulipokuwa.
"...Shikamoo Mama... Za huko
utokako....?"
Gervas alimkumbatia kwanza
Mama yake na kisha akanigeukia,Nilishangaa Gervas
kutokunionesha furaha ya aina
yoyote kwani hakunikumbatia,
"....Mambo Levina....?"
Salam ile ilinifanya nianze
kuchanganyikiwa na kuhisi mengi kichwani mwangu lakini
halmashauri yangu ya kichwa
ikafanya kazi fasta na kujua kuwa
itakuwa ni uchochezi unaofanywa
na Mama yake nisiendelee kuwa
na Gervas. "....twendeni.. Mama twende
ingieni kwenye gari....!"
Tukatoka pale na kukatisha
kitongoji cha Baltimore kisha
tukautafuta Mji wa Detroit ambao
ndio alikuwa akiishi Gervas na kufanya kazi huko.
Tulipofika tu tulikuta
kumeshaandaliwa vyakula Mezani
japo hatukumuona mtu yoyote
aliyeandaa,Mda wote sikuwa na
raha kwani nilimkuta si Gervas niliyemtegemea,alikuwa kabadilika
sana huku mda wote akionesha
kuwa karibu na Mama
yake.sikwenda kuoga mda ule ila
Mama alienda kuoga na
aliporudi, "....Mama tukaribie tule jamani
chakula nilichokitengeneza
mwenyewe...!"
Gervas alitukaribisha pale sebuleni
tupate chakula lakini sikuwa na
hamu kabisa ya kile chakula hivyo nikapakua kidogo sana
kumridhisha tu.
Ulipofika mda wa usiku
nilishuhudia Mama akielekezwa
chumba cha kulala kisha Mimi
nikaingia chumba anacholala Gervas na kulala naye,Niliingia
bafuni na kumuacha Gervas akiwa
pale chumbani anaangalia Tv.
Nilipotoka nikamkuta bado
hajalala hivyo nikachukua nguo
yangu ya kulalia tayari kwa kulala, nikaomba sala fupi kimya kimya
kisha nikachukua shuka nakuanza
kujifunika,
"...Gervas mpenzi..!"
"...mmhh...!"
"...Mi ndio nalala hivyo, lakini kabla sijalala nahtaji kujua kwanini
leo hujachangamka mpenzi
wangu eenh..!"
"...Levina...!"
"...Abeee...!"
"...Utaacha lini kuua....?" Hilo swali lilinitatiza nisijue nianzie
wapi kumjibu,
"....kwani nimemuua nani tena...?"
Akaangalia kwa pembeni kisha
akanitolea mafaili akidai kuwa
katumiwa kwa njia ya 'Fax' jana. "...Levina.., umemuua askari
uwanja wa ndege kisha
ukamfungia ndani humo humo
na ushahidi huu hapa unatafutwa
kuanzia hivi sasa....!"
Nilitetemeka na kushindwa kujua nianzie wapi huku machozi
yakinilenga lenga.
"...Levina...!Nakupenda na ndio
Mana nipo na wewe mpaka
sasa...!"
"....Ahsante Gervas nakupenda na wewe pia.. Ila kitu
kimoja..,Nakuomba usimwambie
Mama pliz...! Kwasababu si
unajua Wamama..?,anaweza
kumwambia Mama yangu
akachanganyikiwa...!" Nilimdanganya Gervas ili asije
akamwambia Mama yake kwani
angenibadilikia.
Moyo wa upendo kwa Gervas
ukazidi kunitawala katika nafsi
yangu,Nilipata usingizi wa raha sana usiku kwani nilijikuta
nikichukuwa mikono yangu
nakupenyeza katika kifua chake
kilichojaa nywele,taratibu
nikizishika shika kwa kuteleza
mpaka mabegani mwake,hakika Gervas alikuwa ana mwili mzuri,
nilijikuta nikilegea huku nikijigeuza
geuza huku na kule kumwachia
Gervas mwili wangu wote aufanye
anavyotaka,kwa kifupi niliufurahia
usiku mpaka inafika alfajiri Gervas alikuwa bado hoi na anataka
tuendelee.
"...Sweetie mi nipo kwa ajili
yako...!, Nenda kajiandae tu
uende kazini...!"
"Ok...!, Wacha nijimwagie maji fasta fasta niende..!"
Aliingia bafuni na kujimwagia
maji,kisha nikakimbia jikoni
kumwandalia chai angalau
kikombe kimoja na alipotoka
nikasaidia kumvalisha nguo kisha akanywa ile chai haraka haraka
nikamsindikiza mpaka nje na
kuondoka zake,Nilipoingia ndani
nikapitiliza na kuingia jikoni
nikamkuta Mama Gervas akiosha
vyombo huku akitengeneza kitu kama chai..
"....Mama shikamoo...!"
Hakuitikia akanitolea macho kisha
akapekuwa haraka haraka
kwenye eneo lililokuwa na
vyombo na kuchomoa kisu chenye ncha kali na kunifuata
huku akiongea kwa ukali..
"....Sali sala zako za Mwisho
malaya mkubwa we unaetaka
kuniulia mwanangu kwa ukimwi
uliotoka nao Tanzania...!" ************ * * * Mama Gervas atafanikiwa
kumuua Levina? * * * Levina anatafutwa na
Mapolisi kwa kuua polisi wa
uwanja wa ndege Tanzania na
Gervas analijua hilo je, Levina
atamatwa? Itaendelea