STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,075
- 17,237
Story: Sitaki Tena - 01 (season 1)
Mtunzi: Andy Ryn ( Chief)
Nakumbuka Levina mimi nilikuwa na miaka
12,wazazi wangu walikuwa wakinipenda
sana na walipenda kuniacha huru hata pale
ninapokuwa nacheza na rafiki zangu michezo
mbalimbali,nilikuwa napenda sana kucheza
michezo tofauti na wenzangu c unajua tena utoto,na mchezo mkubwa niliokuwa naupenda ni
huu wa rede (ule wa kukwepa mpira
unaporushiwa).
Siku hiyo nikiwa mimi na rafiki zangu
tunacheza,sikuamini macho yangu na ni vigumu
kuamini mpaka sasa kwa kile nilichotenda kwani badala ya kuuokota mpira nirushe kwa ile
haraka niliyokuwa nayo ndani ya ule mchezo
nilijikuta naokota jiwe bila kujitambua nilichokuwa
nimeokota huku nikidhani kuwa ni mpira na
kumrushia Jeni na kwa bahati mbaya lilimpata Jeni
kichwani na kuzimia palepale.. Juhudi zilifanywa haraka haraka na majirani huku mimi nikiwa
pembeni cijui cha kufanya mchozi ukinitiririka
huku kijasho chembamba kikipenyeza katika
paji la uso wangu kupitia shingoni huku lile jasho
likichochea mkojo ulioanza kunitoka taratibu
palepale huku nikitazama kinachoendelea.. "Panda na wewe twende.. Nimesema panda huko
usikii.?"
Aliongea na mimi mama mmoja kwa ukali huku
akinitolea mijicho kana kwamba labda alikuwa ni
mtoto wake lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa ni
mpita njia aliyekuwa shuhuda wa lile tukio. Nilipanda taksi pamoja na wale majirani iliyokuwa
imekodiwa haraka kwa ajili ya kumkimbiza
Jeni hospitali.. kadri tulivyokuwa tunakaribia
hospitali ndivyo mapigo yangu ya moyo yalinienda
kasi mithili ya yule mwanariadha wa jamaika
anayeitwa 'Bolt'... Huku nikiomba miujiza yeyote itokee ili Jeni apone turudi nyumbani, niliendelea
kulia tena kwa sauti ya juu huku kamasi likinitoka..
Tulipokaribia kufika hospitali nilisikia mama mmoja
aliyekuwa
pembeni yangu akimshikilia Jeni..akitikisa kichwa
huku akimwambia dereva apunguze mwendo kwani haina haja tena kuwahi huku akimsisitizia
kuwa mtu waliyekuwa wakimuwaisha
ameshapoteza maisha..
"Jeni amekufaaa.. Amekufaaa.. Hapana.. hapana..
Mama yangu weeee...mama..baaabaaa uko
wapi jamanii mama yangu weee..." Nikazidisha kupaza sauti kwa kulia niliposikia yale
maneno..
Sikuweza kuamini kama kweli Jeni amekufa mpaka
nilipoona tunaelekea mochwari ndipo nilipoamini
Jeni alikuwa tayari keshapoteza maisha kutokana
na kupoteza damu nyingi zilizokuwa zikimtoka eneo la kichwani na puani.
"Umeshaua..? Ndio umeuwa naongea na wewe
kinyago uliyefanya makusudi haya..!”
Aliongea yule mama..
"Sijau.. Kabla sijamalizia kujibu nikashangaa
napigwa kofi kubwa la usoni mpaka nikajihisi kizunguzungu, huku akiendelea kuniambia..
“tena ishia hapohapo mwanaidhaya mkubwa
wewe na tunakupeleka polisi moja kwa moja
mbwa we ukaozee huko huko ndio utanyoka...!"
Taarifa za mimi kufanya lile tukio tena kwa bahati
mbaya lilitawanyika Mtaani kote na hakuna hata mmoja aliyeweza kuamini kwani taarifa hata
zilipofikiwa wazazi wangu nao hawakuweza
kuamini kilichonitokea walikuja pale kituoni japo
kunitoa kwa dhamana lakini ilishindikana kwani
huwa hakuna dhamana kwa kesi yoyote ya
mauaji.. Nilishiwa nguvu,na kulegea viungo vyote na kusababisha kupoteza fahamu kutokana na
kukataliwa dhamana..
BAADA YA SIKU (NNE).4 Sikuweza kupata hata lepe la usingizi takribani siku
mbili kutokana na kulia sana,kichwa kiliniuma
sana..nakumbuka ilikuwa asubuhi na mapema pale
askari alipotuamrisha tupande gari la polisi kutoka
pale kituo kidogo cha polisi kurasini na kuelekea
kituo kikubwa cha polisi pale MSIMBAZI KARIAKOO.. Safari ilianzia kituo kidogo cha Kurasini
nilipokuwa nimechanganywa na wenzangu
niliowajua pale pale na wao waliletwa pale kwa
makosa tofauti tofauti, huku tukikatiza Sheli ya BP
mpaka raundi about ya Kamata,sehemu zote
tulizopita bado machozi yalikuwa yakinitoka huku yakiandamana na mafua Makali yalionipata pale
kurasini kituoni, kwikwi ilibana sana na haikuwa
kwasababu ya kiu ya maji bali ilikuwa ni kwikwi ya
kulia kwa mda mrefu..
"Embu nyamaza hukoo.. Haupo kwa baba yako
wala mama yako..Tena unyamaze..??” Aliongea kwa hasira askari mmoja alioonesha
kukasirishwa na kitendo changu cha kulia mda
mrefu bila kunyamaza..
"Hivi we mtoto husikii..? Kwani sisi ndo
tumekutumauue..?" aliendelea kunikalipia yule
askari. Mpaka tunaingia pale kituoni MSIMBAZI macho yalikuwa mekundu na yamenivimba sana
huku sauti ikinikauka kutokana na kulia kwa mda
mrefu.. *** *** Tukiwa katika basi lenye namba PT 10319 ambalo
lilikuwa likikatisha mitaa ya kariakoo likiwa
linatokea kituo kikubwa MSIMBAZI huku nikiwa
katika orodha ya mahabusu waliokuwa
wamewekwa pale MSIMBAZI kituoni kuelekea
mahakama kuu pale KISUTU kwa ajili ya kusikilizwa kesi yangu kwa mara ya kwanza. kila moja wetu
akiwa amefungwa pingu mikononi .,
nywele pamoja na nguo zangu zilikuwa chafu sana
kutokana na uchafu wa pale kituo cha Kurasini na
msimbazi. Huku basi la polisi likiwa linakata kona
ya kuingia mahakamani , nikiangaza huku na huku labda naweza kumuona hata mama au baba,ghafla
nikamuona mama
kajifunika kanga upande mmoja wa paji la uso
wake kuashiria kuwa alikuwa ameumia upande
mmoja wa uso wake,nilijikuta nikipigwa na afande.
"Embu tembea hukoo... Unashangaa shangaa nini? Kwani hujui kama hapa ni mahakamani...?"
Tukiwa mstari mmoja tulishuka na kuelekea
kwenye vyumba ila mimi niliingizwa chumba
maalumu kilichoandikwa maneno makubwa
mlango wa kuingilia "CRIMINAL ONLY" kwa haraka
haraka sikuweza kutambua lile neno linamaana gani kwakuwa ndo kwanza nilikuwa niko form
one ila niliweza kuambulia neno moja tu
lililoandikwa "ONLY" kwani nilipenda sana
kuangalia ile
tamthiliya ya kifilipino iliyokuwa inaitwa 'only you'
nikijua inamaanisha 'Wewe Pekee..'sikuwa mbali na fikra zangu kwani kile chumba kilikuwa peke yake
kwa ajili ya kesi za mauaji kama yangu ndo huwa
zinasomwa hapa. Nikiwa na mawakili wangu
nisiowafahamu ila niliamini tu baba ndo aliwatafuta
kwani alikuwa akiongea nao kabla sijaingia mule
ndani. Chumba kilikuwa kidogo sana na watu walimiminika wakiwa ni pamoja na majirani,ndugu
na marafiki huku kesi ikitaka kuanzwa kusomwa
niligeuka nyuma nikajikuta nakutana jicho na
mama mmoja..kwa hasira na jazba niliokuwa nayo
nikajikuta Natoa fyonyo kali na la kupaza sauti ya
juu..Wote mle ndani wakawa kimya ghafla wakinitazama,
"xé@shh.. Mbea mkubwa we..!”
Kisha nikamtemea mate huku hasira zikinipanda
kutokea miguuni kuelekea kichwani na
mikononi, nilijikuta nataka kumpiga lakini mikono
yangu ilikuwa na pingu hivyo hasira ikazidi mara mbili huku nikihema kwa kasi ikiambatana na
makamasi yaliokuwa yakinichilizika mithili ya
umande unapokutana na majimaji au konokona
anapokuwa anaachia kofia yake..nikanyanyua
Mguu wangu wa kulia tayari kwa kumtupia mateke
yule mtu..nikawa tayari nimeshathibitiwa.. hakuwa mwingine bali alikuwa ni yule mama tuliepanda
naye taksi kumuwaisha Jeni hospitali yule
aliyekuwa akinisema ovyo kwenye gari pia ndo
alienipeleka
Kunikabidhi polisi..nikiwa naendelea kumtolea
macho huku nimekunja uso wangu kwa hasira mithili ya bi kidude akiwa jukwaani anaimba..
nilijikuta napokea vibao c kutoka kwa yule
mama bali alikuwa ni askari aliyekuwa akifuatilia
tukio mule ndani.,
"Hata kesi haijaanza umeanza kuonyesha we
nunda eenh... hatimaye hakimu aliingia Na lazima utaozea jela tu wewe.."
Maneno yale yalivuta hisia nyingi sana ndani ya
kichwa changu,mwili ulininyong'onyea
ghafla,niakanza kutetemeka japo nilikuwa mdogo
kiumri lakini nikawa tayari nimeshakomaa kifikra
na pia jasiri ndani ya mda mfupi.. ****** Mda wa hakimu kuingia mule ndani ulifika,hakuwa
mtu wa masihara hata kidogo kwani
aliingia haraka haraka na kuuliza jina langu kamili
kisha akaandika andika pale kwenye kitabu
alichokuja nacho na kisha akaniambia kuwa
inabidi nirudi tena ndani kwani kesi yangu bado ipo kwenye upelelezi hivyo nitarudishwa tena pale
mahakamani baada ya wiki 3 au 4.. Nguvu zilizidi
kunipotea,akili nayo ilishajichokea, Nilitoka pale
kwa ghadhabu huku askari akiwa nyuma yangu..
nilikuwa na hasira na vitu vitatu, kwanza sijapata
fursa ya kuongea na wazazi wangu kwa mda mrefu kwani kwenye kesi kama hizi mtuhumiwa
huwa hana hata ruhusa ya kuongea na mtu
yoyote, pili nilikuwa na hasira ya kuhairishwa kwa
kesi yangu na tatu ni hasira ya yule mama
aliojifanya yupo mstari wa mbele katika kunifuatilia
kujua mwisho wangu.. "Ole wake siku nikitoka..?"
nilijikuta najisemea kimoyomoyo huku dukuduku
likiwa limenijaa moyoni..
"Ipo siku tu.. Atanijua mimi ni nani..?"
nikapanda basi la polisi tayari kwa safari ya
kurudishwa tena rumande.. INAENDELEA