Hadithi hii inatufundisha nini?

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Alikuwepo jamaa mmoja kijijini aliyekuwa mwema na kupendwa na watu wote. Aliwajuwa watu wote. Alimsaidia kila mtu kwa uwezo wake. Watu wote walimjuwa. Alikijijuwa kijiji chote, kila kipembe, kila mtaa, kila barabara, kila uchochoro.

Baada ya muda Mungu alimjaalia upofu, akawa haoni kabisaa. Lakini upofu haukua tatizo kwake kwani alikijua kijiji chote, hivyo aliweza kuenda huku na kule bila ya msaada hata wa bakora.

Siku moja, usiku wa giza totoro, hakuna mbalamwezi, alitoka akiwa amechukua kandili na kuanza kutembea mitaani. Mtu mmoja aliona mwanga, akatoka nje na kumfata. Alipogundua kuwa ni yule kipofu kwanza alicheka, kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwaaa!

Mimi nilidhani ni mtu amepotea au amepotelewa, kumbe wewe! Unatembeaje na kandili huku ukijuwa kuwa huoni?, aliuliza yule mtu.

Kwa nini bwana kipofu alitembea na kandili usiku wa giza ilhali yeye haoni?

Kama utapata jawabu alilojibu yule bwana kipofu, utakuwa umeelewa fundisho la hadithi hii. :confused2:
 
Huyu ni mtu aliyekuwa tayari kusaidia wengine hivyo kwa kuwa kulikuwa na giza alibeba taa ili watu wapata mwanga
 
MBONA mmehama Point ''' huyu jamaa alikijua kijiji vizuri hata fimbo akawa hatumii, kutokana na kukijua kijiji hata pindi umeme ukatikapo anajua....ndio maana akabeba kandili ili wengine waone!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom