LazaroSMtindi
Senior Member
- May 6, 2008
- 100
- 9
JokaKuu,
Nafikiri ni kweli aliwaita wana Kyela kuchangia na kuna watu wengi tu wamechangia.
Ila niliambiwa hata huo mkutano ulivurugika baada ya kushindwa kuelewana juu
ya nani akabidhiwe hizo fedha kati ya kundi la mbunge na lile la DC.
DC akapewa za kwake na mbunge naye akapewa za kwake.
Nafikiri ni muhimu kuhakikisha hayo makundi yanakufa maana yanayumbisha watu bila sababu za msingi. Kwenye masuala ya pesa transparency ndio dawa yake. Hao wanaosema unakula pesa wape wao ndio washike hizo pesa au ndio wawe waangalizi wa hiyo account na maneno yote ya pembeni yataisha hapo hapo.
It is a fact kwamba katika hili seke seke la Mwakyembe/Rostam media imepasuka kati kati.Udhihirisho ni jinsi waandishi wenyewe wa habari walivyokunjana mashati kwenye press conference ya Mwakyembe pale Durban Hotel.Hivi kuna Wandishi wateule wa Dr Mwakyembe?
It is a fact kwamba katika hili seke seke la Mwakyembe/Rostam media imepasuka kati kati.Udhihirisho ni jinsi waandishi wenyewe wa habari walivyokunjana mashati kwenye press conference ya Mwakyembe pale Durban Hotel.
Siasa za Kyela ni kaaazi kweli kweli...ila mimi namshauri RC angeachana na ubunge...maana hawezi.ajitahidi sana RC ili asije akakosa vyote.Dr nae ajaribu kuacha dharau kwa anayoshauriwa...pia apunguze jazba...hekima na busara imtawale maana huwezi jua anaweza kuja kuwa mgombea......2015 nani anajua??
Makubwa haya. Hata Mkuu Mtanzania unaingia kwenye UDAKU? WanaJF tunataka utupe dataz, issues, reasoned arguments. Unachosema hapa ni simulizi za vijiweni ambazo tutazisoma UWAZI, IJUMAA, NYUNDO, SANI na magazeti mengine ya udaku!
Mtanzania
Kwa kweli unafurahisha sana katika arguments zako kuhusu Kyela. Kwako ni kujitahidi uj8ionyesha wanakyela hawna wanalolifanya zaidi yahao watu wako hao wawili unaowatetea kwa nguvu zote kupitia kibwagizo cha ukabila.
Pengine nianze na huyo DC kwa kukuliza maswali yafuatayo;
1. Hivi alipotimuliwa U-DC wakati wa Mkapa nayo ilikuwa ni sababu ya majungu na ukabila wa watu wa Kyela!
2. Je alipofunaniuwa na mkewe hata akasimamishwa na RC Mwakipesile kumkaimisha DC wa Ileje tena kwa kumuapisha, na maelezo yake kwamba mwenzetu kapata ajali ya ndoa; haya nayo yalifanywa kutokana na majungu na ukabila wa watu wa Kyela!
3. Je unaelewa hao wafanyakazi wa Kiwira aliowahadaa ndio waliovujisha siri ya DC huyo kuhongwa VX (japokuwa unapotosha hapa kwamba niliandika kuwa wafanyakazi hao masikini wamemhonga DC vx) kwa shilingi laki sita? na habari ilipotoka kwenye vyombo vya habari hakukanusha!
4. Hivi kukaa naye ofisini akakupa maelezo yake ndio kumuelewa sawa sawa kwamba alikuwa mchapa kazi, na kwamba watu anaofanya kazi nao kila siku hawamfahamu sawa sawa ile wewe uliyeoko UK!
Pili ni huyo diwani wako unayedai anaandamwa kwa sababu ya ukinga wake, hivi Kyela kuna Mkinga mmoja tu! Na kama ana madhambi ikiwemo nyumba yake kutumika kuharibu watoto wa shule pale mjini, watu wasiseme kwa sababu itakuwa ni ukabila!
Je unao ushahidi gani kwamba Dr Mwakyembe alituma vijana wake wamuorodheshe huyo Diwani kwenye tuhuma za wanaofanya biashara ya viungo vya albino? Wakati hata taarifa za hizo kura hazijatolewa mwenzetu wa UK umezipataje au ndo majungu yenu na wewe na huyo rafiki yako DC aliyeondolewa!
Hivi ni kwa lipi hasa Dr Mwakyembe amuandame huyo diwani wakati hata huo udiwani aliupata kupitia mgongo wake kutokana na kutokubaliwa na wakazi wa kata hiyo ya Kyela Mjini ambayo ghata hivyo wakazi wake wengi ni mchanganyiko!
Kupitia hoja zako ni wazi unayo ajenda yako dhidi ya wilaya ya Kyela hivyo ni vema ukawa muwazi, watu wakakuelewa na si kuwapaka matope wanakyela pasipo sababu za msingi.
Wana Kyela walioko Dar ambao wewe unawaita kuwea mtaji wa Dr Mwakyembe wanafanya mengi makubwa kwa ajili ya wilaya yao na si kuendekeza majungu kama ufanyavyo. Wakazi wewe unaziona habari za mafuriko ya Kyela kuwa za kutafutia misaada, wenzio wanayachukulia mafuriko kuwa janga hivyo wanapeleka misaada ya hali na mali kwa wahanga kama ilivyokuwa mwaka jana.
Mtanzania huna uchungu wowote na Kyela kama unavyotaka watu wakuelewe, una interests zako, time will tell.
Mtanzania,
Mkuu wangu unataka kugombea Ubunge Kyela au?..
Maanake hata sielewi kinachofanyika hapa. Mwaka juzi tu nilikuwa Dar kulikuwa na mkutano wa Wakerewe sikuenda lakini walikuwa na hoja kama hizi, sikuona issue hiyo ikifikia mahala popote magazetini...
Zaidi ya yote haya nilishuhudia mikutano mingi ikiandaliwa kutokana na makabila, dini na kadhalika jambo ambalo binafsi lilinisukuma kujiuliza kama Tanzania tumeanza kugawanyika kwa makundi ya dini, makabila, jinsia na kadhalika.
Matatizo ya Kyela yapo Tanzania nzima na wala sii ajabu isipokuwa Rostam kaamua kumfuata Mwakyembe hadi chumbani kwake.
Binafsi sioni tatizo kabisa la Mwakyembe kuzungumzia Ufisadi nyumbani kwake au kuwataarifu wananchi wake waliomchagua kile kinachoendelea, tatizo ni Rostam kumfuata Mwakyembe hadi nyumbani kwake, kuweka sikio dirishani kujua kinachozungumzwa..
Na hapa JF kinachoendelezwa ni - Sauti ya Rostam...
Jamaa ni msanii wa kutupwa. Juzi kaitisha mkutano wa vijana wanaochangishana wanaitwa vijana wa Vikoba. Akaanza kuwaambia atafungua bank, atamwita Mengi na Mengi ana uwezo hata wa kuchangia milioni 100.
Baadaye akawaita wale washirika wake pale mjini na kuwauliza waelezee wanachokijua. Wakaanza kusema mipango ndio iko hatua za mwisho na ujinga mwingine mwingi tu.
Mtu unabaki kujiuliza, hawa ndio wasomi wa nchi hii, kwanini wanakuwa wahaba wa ukweli?
DC aliyeondoka ndiye alikuwa na wazo la kuunda bank ya wilaya lakini hakuungwa mkono. Sasa mheshimiwa anajifanya hilo ndilo lengo lake.
Kama atatekeleza ni vizuri, ingawaje kwa jinsi wanavyoongea, unajua ni usanii tu kwa ajili ya mwaka kesho.
Mkuu LazaroSMtindi,
Labda uniambia nilichoandika hapo juu kwa vipi ni UDAKU? Ukitaka naweza kukuandikia mpaka na tarehe kilitokea nini.
Kulikuwa na mkuatano wa wana Kyela ambao ulikuwa ufanyike Dar kwa ajili ya kuchangia kujenga shule. Kulikuwa na mkutano wa maandalizi ambao ulifanyika ili kupanga vizuri namna ya kuendesha hiyo fund rising. Hapo ndipo palipotokea matatizo. Ujumbe kutoka Kyela ambao uliongozwa na mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela na DED, ulikutana na baadhi ya wana Kyela wengi wakiwa ni wale wajumbe wa KDF.
Hapo ndipo kulitokea kutoelewana na kurushiana maneno juu ya nani atunze pesa ambazo zingechangwa. Viongozi kutoka Kyela wakisema hizo pesa ni kazi maalumu na ziwe chini ya DED wakati wale wa Dar wakisema ziwe chini ya KDF. Hao jamaa wa KDF wakasema hawawezi kuruhusu hizo pesa zitunzwe na mwizi huyo DED. Huyo DED ndio kwanza alikuwa na mwezi mmoja Kyela, lakini tayari wakamwita mwizi.
Mpaka mkutano ukavunjika na hawakuelewana. Ilikuwa DC, mbunge na mwenyekiti wa halmashauri waongee na vyombo vya habari kesho yake kuhusu wito huo wa kuchangia shule. Baada ya kutoelewana hapo DC akaondoka kurudi Kyela kwa kisingizio cha RC kufiwa na mamake. Ujumbe wa Kyela wakakusanya pesa walizochangiwa na mbunge naye akaendelea kukusanya alizochangiwa kupitia KDF.
Hicho ndicho nilichoandika kwa kifupi sasa kama ni UDAKU niambie ni udaku vipi?
Mkuu, hoja zako mara nyingi ni nzuri sana, lakini linapokuja suala la Kyela unageuka kuwa extremely irrational. Kwa sisi tunaofika Kyela mara kwa mara kwa shughuli za kikazi, tunashindwa kuona lengo lako maana, utake usitake, Kyela imebadilika sana chini ya Dk. Mwakyembe. Ndo maana wengine wanakuelewa vingine kuwa lengo lako labda ni kugombea ubunge 2010! Lakini Mkuu, unaweza kuwa na azma hiyo bila kudisdtort ukweli! Muulize mwandishi wa habari yeyote wa Mbeya worth the title, atakueleza kuwa Kyela ina mabadiliko katika shule, miundombinu (barabara, madaraja na umeme) na hata mwamko wa wananchi. Nikisema mengi utaanza kusema nimehongwa! Ndo tulivyo!
Mkuu, hilo la michango ya Dar es Salaam nalijua, kwa vile mimi nilihudhuria vikao vyote! Kwanza, ziara hiyo ya DC, DED na Mwenyekiti wa Halmashauri ilifanyika wakati Mbunge yuko Dodoma, Bungeni! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Juhudi za DC kupata pesa kutoka kwa wana-Kyela zilikwama kwa sababu tatu kuu: 1. Yeye ni mtumishi wa Serikali Kuu, akiishiwa fedha aende Serikalini si kwa wananchi! Sasa akipewa fedha na wananchi, akaila, wananchi watamwajibishaje? 2. Kwa nini alifanya ziara ya kukutana na wananchi wa Kyela bila Mbunge wao ambaye wanaweza kumwajibisha? 3. Kwa nini chombo ambacho wana-Kyela wengi (wanaojua kuchanga fedha na siyo kupiga domo tu), yaani KDF, hakiombwi kufanya kazi hiyo ya harambee?
DC alikosa majibu! Vilevile, ndani ya wana-Kyela, kulikuwepo na "wanusa mambo" ambao walijua kuwa DC huyo kastaafishwa, kilichokuwa kinasubiriwa ni kutangazwa tu! Hivyo, baadhi yetu tukaona zoezi hilo lisiendelee!
Mbunge alipoingia Dar siku mbili baadaye, akaombwa asaidie. Mwakyembe hakusita, akaingia kazini na kesho yake tukapata pledges za sh.20 milion/= kutoka Post Bank, NHC, TBA na NMB kutokana na influence yake. Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake tumpe!
Sasa hayo unayoyasema Mkuu ya "kutoelewana" hadi kumwita DED mwizi, yanatoka wapi? Wana-Kyela wengi walikuwa vilevile wanamwuliza DC, kwa nini mfunge safari ndefu ya wiki moja na kutumia zaidi ya sh. milioni 5 kwa posho na mafuta ya gari, wakati wangeweza kupiga simu tu KDF wachangiwe? Mkuu, tusimwonee Dk. kwa sababu tu hawezi kukujibu! Dk. Mwakyembe atakumbukwa: ameweza kutekeleza yale ambayo kayafanya katika mazingira magumu sana aliyowekewa na watawala kwa kumwacha Mwakipesile Mbeya kama RC! Mwakipesile anayo rekodi ya muda mrefu ya ukorofi na visasi visivyoisha. Akiwa Mbunge wa Kyela, Mwakipesile alikuwa hakai meza moja na DC, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mbunge aliyemtangulia (Kasyupa), na Mhandisi wa Wilaya! Ubabe wake unatokana na kazi yake ya mwanzo kabisa, UPOLISI! Mimi mwenyewe hapa, pamoja na uandishi wangu wa habari, alishanitamkia kunizaba vibao nikiendelea kumdodosa! Hiyo ndo NGUVU MPYA!
Mkuu, nimalizie kwa kusema kuwa yote niliyoyasema hapo juu unaweza kuyahakikisha kwa Mwenyekiti wa Halmashauri (0754 630946); Mkurugenzi wa Kyela (0754738468) na Mbunge wa Kyela (0754284130).
LazaroSMtindi,
Mwanzoni si ulianza kwa kusema ni udaku? Ghafla unathibisha kile ambacho niliandika toka mwanzoni.
Rudia maandishi yangu hapo juu, hakuna niliposema Dr. Mwakyembe alikuwepo kwenye huo mkutano wa usiku. Soma tena hutakuta nilipoandika kwamba Dr. Mwakyembe alikuwepo hapo. Najua Mbunge alikuwa bungeni.
Nilishangaa ulipoandika ni udaku na ndio nikakueleza ukweli wote. Tatizo langu kubwa ni hiyo migawanyiko. Simlaumu mbunge pekee lakini yeye ni mhusika kwenye hiyo migogoro ambayo inawafanya watu wachague upande mmoja. You are either with us or with the terrorist.
Hayo mambo mengine yote ya Kyela nayajua na hata namba zote za wahusika ninazo. In fact hata mheshimiwa ana namba zangu na akitaka kuwasiliana na mimi anaweza tu kama alivyokuwa anafanya huko nyuma.
Kuna misinformation kubwa sana inatokea kutoka kwa hao mnaowaita waandishi wa maana kutoka Mbeya, ndio maana wakati mwingine nalazimika kusahihisha mambo.
Ningetaka kuandika ya Dr. Mwakyembe, mkuu utashangaa nayajua mengi mno. Ila sitaingia huko hata siku moja labda mpaka nikimwona yeye mwenyewe ndio nitamwambia mkuu mbona hapa ilikuwa hivi au vile na kwanini? Lakini haya mambo ya migogoro na misinformation inayofanywa kwa makusudi, nitaendelea kuyaandika.
Tatizo kubwa watu wengi wanamfahamu Dr. Mwakyembe yule wa Richmond na kamati yake ambako alifanya kazi nzuri sana, hawamfahamu Dr. Mwakyembe yule mwingine wa Kyela na madudu yake mengine. Anapofanya mema tunamsifia lakini akifanya mabaya pia tunaandika pia.
Mimi sijawahi kuwa rafiki wa Mwakipesile na in fact mwaka 2005 aliniandama sana akifikiri naenda kugombea ubunge Kyela. Akaja Mwakyembe na tukashukuru kwamba angalau sasa tumepata mtu ambaye anaweza kuwaunganisha wananchi wote kwa faida ya wilaya yao. Kwa mawazo yangu, Dr. hakuitumia vizuri hiyo nafasi na sasa mambo mengine anayofanya hayana tofauti sana na aliyokuwa anafanya Mwakipesile. Hapo ndipo wengine tuna matatizo napo.

Hayo mambo mengine yote ya Kyela nayajua na hata namba zote za wahusika ninazo. In fact hata mheshimiwa ana namba zangu na akitaka kuwasiliana na mimi anaweza tu kama alivyokuwa anafanya huko nyuma. Ukiniambia mimi niwaulize waandishi wa Mbeya kuhusu Kyela, utakuwa unafanya utani. Najua yanayotokea Kyela kwa ukaribu mno labda hata kuliko watu wengi tu walioko hata Mbeya. Hata ujenzi wa hizo shule najua ukweli wake wote. Wacha leo tusiliongelee hilo.
Kuna misinformation kubwa sana inatokea kutoka kwa hao mnaowaita waandishi wa maana kutoka Mbeya, ndio maana wakati mwingine nalazimika kusahihisha mambo.
Ningetaka kuandika ya Dr. Mwakyembe, mkuu utashangaa nayajua mengi mno. Ila sitaingia huko hata siku moja labda mpaka nikimwona yeye mwenyewe ndio nitamwambia mkuu mbona hapa ilikuwa hivi au vile na kwanini? Lakini haya mambo ya migogoro na misinformation inayofanywa kwa makusudi, nitaendelea kuyaandika.
Tatizo kubwa watu wengi wanamfahamu Dr. Mwakyembe yule wa Richmond na kamati yake ambako alifanya kazi nzuri sana, hawamfahamu Dr. Mwakyembe yule mwingine wa Kyela na madudu yake mengine. Anapofanya mema tunamsifia lakini akifanya mabaya pia tunaandika pia.
Mimi sijawahi kuwa rafiki wa Mwakipesile na in fact mwaka 2005 aliniandama sana akifikiri naenda kugombea ubunge Kyela. Akaja Mwakyembe na tukashukuru kwamba angalau sasa tumepata mtu ambaye anaweza kuwaunganisha wananchi wote kwa faida ya wilaya yao. Kwa mawazo yangu, Dr. hakuitumia vizuri hiyo nafasi na sasa mambo mengine anayofanya hayana tofauti sana na aliyokuwa anafanya Mwakipesile. Hapo ndipo wengine tuna matatizo napo.
Nyie watu wa Kyela mna ubishi mwingi sana na mnautumia kama kivuli cha kujiamini. Hii ndiyo inakula kwenu kwa sana. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, kule Kyela kuna Cocoa, mchele na fruits kibao ambavyo vyote vina-fetch good prices kwenye markets zote, ndani na nje ya nchi. Lakini ukifika Kyela huwezi amini poverty level! Hivi kweli mnataka wanasiasa ndiyo wawaelekeze namna ya kufanya mkiwa na pesa zenu!? Mimi nashindwa kuelewa kama kuna mtu anasubiri ati mwanasiasa amwambie anunue bati na matofali kujenga nyumba ya kisasa!
Halafu hii tabia inayojengeka siku hizi, hasa hapa JF ya watu kuamini kuwa wanasiasa ndiyo watawaletea maendeleo, mimi siikubali hata kidogo. Watu tunatakiwa tupige kazi sana na kupasua vichwa tujue namna ya kupata fedha na si kusubiri politicians ati watusaidie. Pale tutakapoacha hizi dogma mbofu mbofu ndiyo tutaweza kuwa sawa na wenzetu majirani, Kenyans. Vinginevyo tutashangaa sana na tutashangaa zaidi.

Hapana Mwanjelwa,
Kama ni hivyo kwa nini wakati wanasaka huo ubunge au uongozi wanatanguliza swala la kuleta maendeleo jimboni. Kwa nini wananchi baada ya kuwasikiliza wanaamua kumchagua moja kati ya wagombea wengi na kuwaacha wengine. Kwa nini kila mara tunadai tujue sera za wagombea ama vyama vyao - kwa kifupi kwa nini kwenye jamii kunahitajika uongozi.
Mkuu Mwanjelwa, labda hatuelewi sana maana ya uongozi lakini popote pale katika jamii, maendeleo na ustawi hutegemea sana uongozi. Ukichagua uongozi bora una hakika ya kupiga hatua, na ukichagua kiongozi lege lege, ujue kabisa umelamba garasha. Uongozi bora unaendana na uwezo katika kupanga mahitaji, kutoa maamuzi mazito na kuyatekeleza.
Kosa tunalofanya Watanzania ni kutoangalia uwezo na sifa ya mtu binafsi tunayetaka kumpa uongozi. Tunatoa mwanya unaowawezesha wenye uwezo duni kabisa kujinadi chini ya kivuli cha chama au kutumia chama kuwanadi. Matokeo ya mtindo huu tunayashuhudia kwa wananchi katika nchi iliyojaa neema kama yetu kubaki katika umasikini wa kutupwa.
Kuchagua kiongozi kwa kupewa kitu kidogo au kwa kuangalia sura yake inavyopendeza ni laana kubwa kwa jamii ya Tanzania. Mtu anajitokeza na hana rekodi yoyote huko nyuma inayoonyesha alivyo mahiri katika harakati za kuwasaidia na kuwatetea wananchi halafu tunaanza kumtafutia visifa vya kuokoteza na kumpa uongozi !! Tutegemee nini ?
Kiongozi bora ndiyo chachu ya maendeleo na mafanikio.