Haya Samwel tumekusikia, Mwakyembe kweli hana nyumba maana ile ya pale muungano kijijini ulimjengea wewe. Kwako nyumba lazima ujenge mjini, acha hizo.
Natudia mwandishi haalikwi kwenye matukio ya hadhara kama mikutano, niliuliza kuhusu matukio machafu yanayotokea Kyela lakini waandishi wa kyela hawaandiki kwa sababu tu yanawahusu, tuite maswahiba. Kwa mfano wakati wanafunzi wa Shule ya Msingi Kyela wanalawitiwa na wafanyabiashara walimezea pamoja na uwt kuwapa taarifa, wenzao walitoka mbeya wakafichua wahalifu wakapelekwa mahakamani, hivi napo walipelekwa na Mwakyembe! Inapofikia mpaka mzazi analia na kueleza wazi kwamba "mtoto wangu anaf..." bado mwandishi unafumba macho lakini kila siku wanakuona umeganda kwenye gari la DC kama wewe ndo dereva, unadhani wananchi watakuhitaji tena!!!!
Kuelezea kwamba nyumba ya wageni ya diwani wa mjini ilitumika kulawitia watoto hao, mtu anakimbilia hoja dhaifu eti Nsesi mkabila, hata katika uchafu kama huo tena ulioripotiwa kwenye magazeti hadi watuhumiwa kufikishwa mahakamani tunataka kupotosha umma kwa kisingizio cha ukabila, ajabu sana.
Wafanyakazi kiwira wanadhulumiwa na wawekezaji feki, hao hao waandishi wa kyela wako kimya, wanaofuatilia na kuripoti kila siku ni hao hao wa kutoka mbeya, jee huko nako wanaongozana na Mwakyembe! Wakati wananchi wanakabiliwa na matatizo hayo mazito na wanawapelekea taarifa wako kimya ila wanawaona muda wote wako kwenye gari la DC, unategemea wananchi watawakimbilia nani!!!!.
Jamani mwandishi wa habari ni sauti ya wasio na sauti, kama hutekelezi hilo wananchi watakaa mbali na wewe, suala hapa sio jina tu mimi mwandishi. Kama kweli mko karibu na mambo ya kweli basi elezeni wanachokisema watu wa kawaida kuhusu hao waandishi. Katika maandamano yale waseme hawakualikwa na ni masuala mengi tu ya wananchi hawaelezwi.
Kyela hivi sasa kuna mafuriko, mbona hatusomi habari zao zinazoelezea kinachoendelea kila siku, na badala yake ni waandishi hao hao wa mbeya ndio wenye kuziandika, hivi napo walipelekwa na Mwakyembe! Hivi kwao habari ni za Dr. Mwakyembe tuu! Hizo za wananchi ndio sio habari!
Kama kweli mnaojadili humu mna uchungu na Kyela tuepuke kila jambo kulifanya la kisiasa, twende kwenye issues badala ya majungu.
Litakuwa jambo la msingi iwapo kutakuwa na michango yenye kuonyesha ufumbuzi wa matatizo yetu, kuliko kijifanya kila mmoja bingwa wa kukosoa.
Ombi langu ka JF ni kuwatupia jicho pia waandishi wetu hapa nchini, hivi kweli wanajishughulisha na matatizo ya wananchi au kwao habari ni wanasiasa, habari zao kubwa ni zipi, za wananchi au propaganda za siasa!
Ushauri kwa mnaowatete hao waandishi kwamba walizuiwa, waelemisheni, watoe kipaumbele kwa matatizo ya wananchi, kwamba waelewe kuwa wao sio waheshimiwa bali ni "Voice of the Voiceless." Wajifunze kwa wanzao wa Mbozi.