Mbeya wamtahadharisha Kikwete
Baada ya habari hiyo kuchapishwa, wananchi hao walitaka kufahamu mwenye mamlaka na nguvu ya kumvua ubunge mbunge wao waliyemchagua kwa asilimia 93, kwamba ni wabaya wake, Rais, Spika au wapiga kura wake ambao ni wao wananchi wa jimbo la Kyela?
Masahihisho hapo, Kyela iligawanyika katikati kati ya Dr. na Mwakipesile. Baada ya uchaguzi wa CCM ni kama Dr. hakuwa na upinzani tena.
Hilo la asilimia 93 japo ni sahihi lakini kwa mazingira ya Kyela nafikiri haina maana hiyo mwandishi anayotaka kuonyesha.
Hata mwaka 2010 Kyela itagawanyika katikati na tegemeeni mapambano makali sana kutokea huko.
Dr. Mwakyembe ana advantage kwasababu ni mbunge na anaweza kuzunguka jimboni bila kuambiwa anafanya kampeni. Tatizo kubwa zitakuwa zile ahadi zake za 2005 ambazo kwa sehemu kubwa hakuna kilichofanyika. Pia ni kama Dr. hajui kutengeneza marafiki, maana watu wengi waliomuunga mkono 2005, sasa wamejikata taratibu kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya dharau (elimu), kutokushaurika na kukosa uongozi wa pamoja. Kiujumla dharau ndio weakness kubwa ya Dr. Kuna jamaa aliwahi kuniambia, inatosha kukaa na Dr. wiki moja tu kuweza kugundua weaknesses zake nyingi sana hasa dharau na usanii wa kusema mambo ambayo anajua wazi hawezi kufanya.
Kwa habari tulizo nazo wengine, jimbo la Kyela litakuwa gumu sana 2010 tofauti na watu walioko mbali na Kyela wanavyofikiri. Nafikiri hata Dr. kalitambua hili na mambo mengi yanayotokea sasa kwa sehemu kubwa ni siasa za Kyela. Dr. kafanikiwa kupitia magazeti ya Dar kuwafanya wengi walioko mbali na Kyela waamini atashinda kirahisi Kyela. Ukweli wa kule wilayani unaonyesha atakuwa na kazi ngumu sana.
Muda wote watu walidhani ni mpambano mwingine kati ya Dr na mwakipesile, lakini kwa taarifa za uhakika ni kwamba ni kama 100% Mwakipesile hatagombea ubunge Kyela. Hiyo inatoa nafasi kwa sura mpya kuingia kwenye ulingo. Dr angeweza kumshinda Mwakipesile kirahisi sana maana angemhusisha na ufisadi wa akina Lowassa na Rostam.
Kingmaker wa siasa za Kyela ni pamoja na prof. Mwandosya. Ila prof ni mjanja sana, hawezi kutumbukiza kichwa chake moja kwa moja. Anashirikiana na makundi yote hata kama ni kwa maneno tu. Naamini hataweza kumuunga mkono Dr moja kwa moja na atawaachia wana Kyela waamue. Anachoweza kufanya ni kumsaidia resources na kisha kuwaacha wana Kyela waamue.
Dr. Mwakyembe ana wafuasi wengi miongoni mwa wana Kyela wenye uwezo wanaoishi Dar, wakiongozwa na Kifukwe, yule aliyekuwa Yanga. Kule Kyela wanaitwa mafia wa Dar, hao ndio tegemeo kubwa la Dr. Wana mbinu nyingi, wana pesa, wana uhusiano wa karibu na Mengi. Kundi hilo hilo ndilo lilisaidia kwenda kuficha wajumbe kule Rungwe mwaka 2005 kabla ya mkutano mkuu wa uchaguzi. Kuna uvumi hili kundi ndilo limesababisha DC wa Kyela kuondolewa. Hivyo nategemea Dr. atakuwa na access ya pesa ma media ili kushinda Kyela. Tatizo lake ni kwamba wengi wa watu kwenye hili kundi hawajafanya chochote cha maana Kyela. Kwa Kyela ni kama watalii tu wanaofika Kyela na magari yao makubwa na wapambe lakini hawana muda kabisa na matatizo ya Kyela isipokuwa pale wanapokuwa na interests zao. Pia wameanza kugawanyika maana kwa mfano Mwanjala ambaye ndiye alikuwa kinara wa kubeba na kuhonga wajumbe kwa ajili ya Dr. sasa kakosana naye na ameamua yeye mwenyewe kugombea ubunge 2010. Hili kundi linakumbukwa kwa kusaidia kuanza kwa kanisa la Morovian la Kyela. Waliweza kuua njama za Rungwe kuzuia Kyela wasianzishe kanisa lao. Kuna watu bado wanawakumbuka vizuri kwa hilo.
Kundi lingine lenye nguvu ni la wale wastaafu mbalimbali ambao sasa wamejenga Kyela na kuishi Kyela. Hawa hawana uhusiano mzuri na Dr. Hili lina watu waliokuwa kwenye nafasi za juu upande wa jeshi la wananchi na polisi na foreign. Kundi hili ni pamoja na Apson mwenyewe, lina uhusiano wa karibu sana na Mwakipesile. Ni katika watu waliomshauri vizuri Mwakipesile kwamba asigombee maana ataadhirika vibaya. Hawa wanaijua Kyela vizuri sana ila sidhani kama wana influence kubwa vijijini. Wao wanaona wana influence lakini mimi nina wasiwasi kama influence yao itakuwa kubwa. Wakiungana kumuunga mtu mwingine basi atakuwa na advantage ya pesa na ushauri lakini pia atakuwa na disadvantage ya kuwa linked na mafisadi ili hata kama yeye hana uhusiano wowote na ufisadi, bado aunganishwe na Rostam kupitia hao wastaafu.
Ikifika 2010 kumbuka maneno ya hapo juu. Kyela ni katika majimbo ya kuyaangalia sana 2010. Watu wanaweza kuja kuwa shocked kuona Dr. kaangushwa na watafikiri Rostam kafanya kazi yake, kumbe ni mambo ya Kyela na siasa za Kyela.