Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Upandikizaji wa figo (renal transplant) sasa hivi unafanyika hapa hapa nchini kwetu. Na tuko mbioni pia kuanza upandikizaji wa maini (liver transplant). Huko nyuma tulilazimika kuwapeleka wagonjwa wanaohitaji huduma hii nje ya nchi, hasa India kwa gharama kubwa ya fedha za nje za USA dollars. Wagonjwa wengi walikosa huduma hii kutokana na gharama hiyo kuwa kubwa.
Upandikizaji huu huhitaji ndugu wa karibu wa mgonjwa kumchangia figo moja mgonjwa. Hakuna madhara yo yote ya kiafya yanayotokana na kuchangia figo kama ilivyo kwenye kuchangia damu.
Jamii inatakiwa ielimishwe hivyo. Kwamba hakuna madhara ye yote ya kiafya yanayotokana na uchangiaji figo. Cha muhimu ni kuwa anayechangia awe ni ndugu wa karibu wa mgonjwa yaani watoto wake, au kaka au dada wa mgonjwa tu. Hawa ndiyo wenye uwezekano mkubwa wa tissue za miili yao ikiwemo hiyo ya figo kuwa compatible kwani wana share vinasaba (DNA) vingi kwenye tissue zao. Mtu baki tu ambaye siye ndugu wa damu hawezi kuwa compatible ku donate figo kwani mwili wa mgonjwa utaikataa ( reject) hiyo figo kwa vyo vyote vile.
Sasa taarifa ya leo ya habari ya ITV imepotosha kuhusu uchangiaji huu wa figo. Imetoa taswira kuwa vijana wanaochangia figo hupata madhara makubwa ya kiafya. Imeogopesha vijana kuchangia figo. Hii itafanya huduma hii ya upandikizaji wa figo kukwama kwa kukosa donors.
Ila kwa upotoshaji huu, wa kulaumu siyo ITV au vyombo vingine vya habari bali ni wizara ya afya imeshindwa kufanya uhamasishaji sahihi kwa umma kuhusiana na huduma hii ya renal transplant. Uuzaji au ununuzi wa figo ni kosa la jinai kisheria duniani kote. Hili vijana wanatakiwa kulijua, kwanza ni kinyume na sheria na pili kisayansi mchangiaji ni lazima awe ndugu wa karibu kinasaba ili upandikizaji huo kuwa na mafanikio. Hata mke au mume hawezi kumchangia figo mke au mume wake kwani vinasaba vyao ni tofauti kwani hawana undugu wo wote wa damu.
Ni vyema sasa wizara ya afya ikatoa ufafanuzi sahihi kwa vyombo vyote vya habari na sehemu mbali mbali kuhusu huu uchangiaji figo ili kuondoa hii taharuki inayoendelea kwa sasa ya utoaji figo na uuzaji figo hasa kwa vijana ambao ndiyo wachangiaji wakubwa.