Madhara ya Kisukari na Namna ya kuyaepuka: Ugonjwa wa Figo

Dr Adinan

Member
Jul 11, 2021
14
20
Habari yako ndugu. Karibu tena, tunaendelea na makala zetu kuhusu madhara ya kisukari.

Kisukari huharibu figo kwa namna mbili: namna ya kwanza ni madhara ya moja kwa moja yatokanayo na uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.

Tulijifunza kwamba kisukari husababisha shinikizo la damu kuwa juu katika kutokana na kuharibu mishipa ya damu kwenye figo.

Cha kuzingatia ni kwamba madhara yote haya yanayotokea kwenye figo yanaweza yasiwe na dalili yeyote mpaka pale ambapo madhara yamekuwa makubwa na kuelekea kwenye figo kufeli. Lakini habari njema ni kwamba, madhara yote haya yanaweza kugundulika na kupunguza hatari ya figo kufeli kama utafanya vipimo sahihi kwa wakati sahihi na kuchukua hatua stahiki.

Tafiti mbali mbali zinashauri mgonjwa wa kisukari kufanya yafuatayo ili kuepuka au kupunguza hatari ya kupata madhara kwenye figo.

1️⃣ Dhibiti sukari kwenye damu yako kadri uwezavyo.

2️⃣ Pata kipimo cha HBA1C angalau mara mbili kwa mwaka, mara nyingi zaidi ikiwa dawa yako itabadilika au ikiwa una hali zingine za kiafya.

3️⃣ Hakikisha unafahamu kiwango chako cha presha ya damu. Angalau shinikizo la damu yako liwe chini ya 140/90 mm/Hg.

4️⃣ Weka uwiano wako wa uzito na kimo katika wastani unaoshauriwa kiafya.

5️⃣ Fahamu na dhibiti kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu.

6️⃣ Epuka kiwango kikubwa cha chumvi- hasa ile ya kuongeza mezani.

7️⃣ Kula matunda na mboga zaidi.

8️⃣ Fanya shughuli zinazotumia nguvu ya mwili kama vile mazoezi.

9️⃣ Fuata maelekezo ya matumizi ya dawa zako.

Fahamu zaidi kuhusu madhara mengine na namna ya kuyaepuka! Endelea kufuatilia makala zangu.
 
Back
Top Bottom